Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Kaka tetee you are my age mate! Kwa uwasilishaji wako hapa, siongezi kitu!
 
Daah,mi kipindi cha majira cha asubuhi kilikuwa kinaniboa nakosa amani!
Maana yakianza yale magona tu najua muda wa kuamshwa kwenda shule umekaribia nikicheck pembeni mdogo wangu anakata usingizi tu!!
Dah zamani raha sana
 
Majira, shambani, na nk. Umenikumbusha mbali sana mkuu! Maisha yalikuwa mazuri sana, watu walikuwa wanapendana, leo mwanadamu mpishie mbali baba lasivyo utajuuta kumfahamu.
 
Warudushe wimbo wa kumekucha wa MALIJANI ulituhimiza sana huku vijijini kufanya kazi za kilimo
 
ajuaye bwana Mungu kwa mfu kuwa mzima mgonjwa kuwa salamaa leo tunawapa polee


Hakuna wimbo wa RTD uliokuwa unasema "wafu watakuwa wazima, wagonjwa watakuwa salama, leo tunawapa pole." Okay? Litake radhi jamvi.
 
Ben baada ya Tabora alikaa sana Dodoma. Alijenga na kuishi hapo hata baada ya kuretire. Ben ninachokikumbuka sana ni yeye kuugua kipindu pindu mwaka 1989. Alilazwa kwenye kambi ya kipindu pindu na alisema kosa ni kula samaki wa kukaanga wabaridi. Kumbuka miaka ya kata mbuga Arusha to Moshi. Alitangaza majira kuhusu watu wa Dodoma kukata mabomba na kutengeneza hereni na bangiri. Ukiona Bangiriiii nyeusi na hereniii zake ujue ni mabomba ya majiiii Dodomaaaa!!!!!!!!!!!
Kumbe dodoma haya mambo hawakuanza jana he he he asa wanaletewa maji wao wanakata wanatengeneza heleni na bangili,juzi watu wako kwenye utafiti wamechoma moto aseeee dodoma
 
Jamani mwenye ule muziki uliokuwa unalia kuashiria kuanza kwa kipindi cha michezo. Naomba anitumie au auweke hapa jukwaani. Nimeutafuta sana
 
Juma Killaza wa Cuban marimba Moro hiyo mji kasoro meli,jamaa alikuwa tajiri na alifariki kwa ajali
Mkuu inaonekana umechanganya majina kati ya Juma Kilaza na SALUM ABDALAH. Ni Salum Abdalah ndiye aliyekua tajiri (alitoka katika familia tajiri yenye asili ya Asia,ila mama yake ni mswahili) na alikufa kwa ajali ya gari mwaka 1965.Salum Abdalah alikua mwanzilishi wa Cuban Marimba Band na kisha kuanzisha band nyingine iliyojulikana kama Morogoro Jazz Band.
Mwanamuziki JUMA KILAZA alikuja kushika nafasi ya Salum Abdalah baada ya kifo cha Salum katika Morogoro Jazz Band. Yako mengi ya kusema Ila kwa leo naomba nikomee hapa.
 
Asanteni nimekwksha upata.
Mkuu kwa kukuongezea unaweza kuupata wimbo mzima mtandaoni (pengine kwa YouTube ) kwa kuandika COTTON CANDY-AL HIRT.Inaonekana RTD walitumia wimbo huu kutengeneza "jingle" ya kipindi.
 
Vipindi vingi vilikuwa bomba sana. Mie nilikuwa siendi kucheza kama kuna kipindi cha Super Tall Julius Nyaisanga RIP jamaa alikuwa mjuzi sana kwenye kupanga nyimbo za kizungu na za kicongo na nyimbo ikiisha anakutajia majina ya wana bendi wote.

Kulikuwa na kijaluba hiki kilikuwa kipindi cha kina mama na kilikuwa kikianza kwa kelele kelele za akina mama. Jamaa yangu mmoja alidai walikuwa wakipiga kelele kuhusu picchu zao huyu akisema yangu nyeupe, mwingine yangu nyeusi, mwingine yangu ya blue lol! Hahahahaha.

Nilijaribu sana kusikiliza kwa makini ili niwaelewe wale akina mama walichokuwa wanakisema lakini sikupata kitu.
 
shikamoni wakubwa me nilikua bado dogo sana babu yangu alifungulia sauti ya juu sana na radio kaiweka sikioni sipati picha zile speaker za Enzi zile na hiyo radio sikioni
 
Mchezo wa mzee Jangala ikidhaminiwa na pombe aina ya chibuku, nakumbuka nyimbo, idara yetu ya uhamiaji nalo jukumu kubwa saanaaaa kuwakaribishaa kuwasafirishaa na kulinda mipaka yetu[emoji441][emoji443][emoji443][emoji445][emoji445]

Watoto wasafi moyonii ni nyoota za macho ya wazaziiiiii[emoji445][emoji445][emoji445][emoji443][emoji443][emoji441]

Shamba aaanii shambaani shambaani mazaoo boora shambaani, haya twendenii shaambanii wananchi tukaalimeee [emoji443] [emoji444] [emoji446] [emoji447]

Wanawakee wa Tanzania wazuuuriii saaaanaaa, wanawakeeee tanzaniaa maendeleo tanzaniaaaa[emoji445][emoji443][emoji441][emoji443][emoji445]

Kuleni chakula boora cha kuujenga muili naku.... Pa kulala pawe boraa[emoji443][emoji445][emoji441]

Wakati umewadia wa salam za wagonjwa hosipitalinii leo tunawapa poleee, ajuaye bwana Mungu kwa mfu kuwa mzima mgonjwa kuwa salamaa leo tunawapa polee[emoji445][emoji445][emoji443][emoji445][emoji445][emoji441]

Wananchiiiii tujifunzeni ushirikaaaaa wananchi tujifunzeni ushirikaaaaa [emoji441][emoji445][emoji445][emoji445][emoji445]

Jamani vitaa imetangazwaa jamaaa wananchi wote tuwe imara, vijijini na mjini msisite kuwasema walanguzi[emoji445][emoji445][emoji445]


Matangazo sasa
1. Tumaa vifurushiii barua na pesa vitu mbalimbali vifike harakaaa tena kwa uhakikaaa, itumie sasaa shirika la posta na simu tanzaaaaniaaa ndio tegemeo letuu.

2. Hebu jitokezeee jioneshe simamaa mbelee za watuuu

3. Tairi general kutoka arushaaa tanzaaaaniaaa

4. Revolaaa revolaaaaa revolaaaaaa revolaaaaaaaa

5. Wee acha kula mali ya umma wee acha kujitafuna tafuna weeeee, wachaaaaaaaaa

6. Tumia chibuku ndio pombe bora, radha ya chibuku hujulikana, sifa moja na nyinginezo ni kulinda hadhi ya mnywaji

7. Komoooooaaaaa aaa komooooaaaa komoaaaa

8. Benki ya akiba ya posta ndio yako, benki ya akiba ya posta ni kwa watanzaniaaa woooote wakubwa kwa wadogo... Wananchi unaweza kufungua akaunti ya kawaaida, akaunti ya muda na akaunti ya muda maaalum.. Usingoje kesho ooo fungua akaunti yako leooo

Watangazaji hahaha Mama Deborah, Dominic Chilambo
Nimejikuta napata sweet memories tu
duuuu sijui una list ya vipindi vyote mkuu maana umenitajia vingne nilikua mdogo Sana ndo navikumbuka leo hasa hyo namba 2 tulikua tunaimba na watoto we zangu
 
umenikubusha babu yng ilikuwa lzm asikilize osia wa bb wa taifa bila hvy ananuna
 
Nakumbuka kipindi cha dini ile asubui kikristo na kisha kiislam hapo nishaamshwa na mzee tuko shamban tunalima na ng'ombe maksai tangu saa kumi kasoro ikifika saa 2 hv tunarud nyumbani kuchukua jembe la mkono kwenda kupalilia mpaka mida ya saa 5 hivi asubui
 
Back
Top Bottom