1 Taarifa ya habari na ile ngoma ya yule mzee asiyeona na ngoma kumi
2. Wakati wa kazi. "ujuzi niliupata hapa hapa kazini"
3. Hii ni kwaresimaa.
4. Lala salama.
5. Vipindi vya masomo ya shule za msingi tukikaa darasa zima watoto 40 na kusikiliza mwalimu wa redio. Wengine hata hiyo redio ilikuwa haisikiki vizuri lakini ilikuwa lazima mhu!
6. Kipindi cha wagonjwa. (Ajuaye bwana Mungu kwa mzima kuwa mfu, mgonjwa kuwa salaaaama leo tunatoa pole).
7. Mchezo wa Redio (Mkataa pema pabaya panamwita) Sikosi hapo. watu mnakaa kana kwamba mnawaona akina Jangala na wenzie na yule mwenye sauti kubwa na yule mama aliyekuwa na roho mbaya. Mtu unamchukia mtu hata bila kuona sura yake.
8. Mpiraa. Nakumbuka Yanga ilikuwa inacheza na Simba 74 tulipiga teke redio ya baba mimi na kaka yangu. Tulikula mkong'oto.
9. Hotuba za Mwalimu. Kila wakisema anaongea na wazee wa Dar ujue kuna kitu. Hapo hatutoki kama tupo likizo, wazee wote wa jirani wanakuja kwetu ili wasililize hotuba. Shuleni boarding kulikuwa na redio moja inazunguka kila bweni kila week.
10. Mchana na usiku mwema na miziki yake!! We acha akina Mbaraka Mwinshehe, Juma ******, Marijani Rajab, Western Jazz, Ndala Kasheba, Polisi Jazz, JKT, Tankat Almasi, Taarab nk. Samahani nimeandika mengi lakini ni kama therapy kutoa haya ya sasa kichwani. Big up mtoa mada.