Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Kaka tetee you are my age mate! Kwa uwasilishaji wako hapa, siongezi kitu!
 
Daah,mi kipindi cha majira cha asubuhi kilikuwa kinaniboa nakosa amani!
Maana yakianza yale magona tu najua muda wa kuamshwa kwenda shule umekaribia nikicheck pembeni mdogo wangu anakata usingizi tu!!
Dah zamani raha sana
 
Majira, shambani, na nk. Umenikumbusha mbali sana mkuu! Maisha yalikuwa mazuri sana, watu walikuwa wanapendana, leo mwanadamu mpishie mbali baba lasivyo utajuuta kumfahamu.
 
Warudushe wimbo wa kumekucha wa MALIJANI ulituhimiza sana huku vijijini kufanya kazi za kilimo
 
ajuaye bwana Mungu kwa mfu kuwa mzima mgonjwa kuwa salamaa leo tunawapa polee


Hakuna wimbo wa RTD uliokuwa unasema "wafu watakuwa wazima, wagonjwa watakuwa salama, leo tunawapa pole." Okay? Litake radhi jamvi.
 
Kumbe dodoma haya mambo hawakuanza jana he he he asa wanaletewa maji wao wanakata wanatengeneza heleni na bangili,juzi watu wako kwenye utafiti wamechoma moto aseeee dodoma
 
Jamani mwenye ule muziki uliokuwa unalia kuashiria kuanza kwa kipindi cha michezo. Naomba anitumie au auweke hapa jukwaani. Nimeutafuta sana
 
Juma Killaza wa Cuban marimba Moro hiyo mji kasoro meli,jamaa alikuwa tajiri na alifariki kwa ajali
Mkuu inaonekana umechanganya majina kati ya Juma Kilaza na SALUM ABDALAH. Ni Salum Abdalah ndiye aliyekua tajiri (alitoka katika familia tajiri yenye asili ya Asia,ila mama yake ni mswahili) na alikufa kwa ajali ya gari mwaka 1965.Salum Abdalah alikua mwanzilishi wa Cuban Marimba Band na kisha kuanzisha band nyingine iliyojulikana kama Morogoro Jazz Band.
Mwanamuziki JUMA KILAZA alikuja kushika nafasi ya Salum Abdalah baada ya kifo cha Salum katika Morogoro Jazz Band. Yako mengi ya kusema Ila kwa leo naomba nikomee hapa.
 
Asanteni nimekwksha upata.
Mkuu kwa kukuongezea unaweza kuupata wimbo mzima mtandaoni (pengine kwa YouTube ) kwa kuandika COTTON CANDY-AL HIRT.Inaonekana RTD walitumia wimbo huu kutengeneza "jingle" ya kipindi.
 
Vipindi vingi vilikuwa bomba sana. Mie nilikuwa siendi kucheza kama kuna kipindi cha Super Tall Julius Nyaisanga RIP jamaa alikuwa mjuzi sana kwenye kupanga nyimbo za kizungu na za kicongo na nyimbo ikiisha anakutajia majina ya wana bendi wote.

Kulikuwa na kijaluba hiki kilikuwa kipindi cha kina mama na kilikuwa kikianza kwa kelele kelele za akina mama. Jamaa yangu mmoja alidai walikuwa wakipiga kelele kuhusu picchu zao huyu akisema yangu nyeupe, mwingine yangu nyeusi, mwingine yangu ya blue lol! Hahahahaha.

Nilijaribu sana kusikiliza kwa makini ili niwaelewe wale akina mama walichokuwa wanakisema lakini sikupata kitu.
 
shikamoni wakubwa me nilikua bado dogo sana babu yangu alifungulia sauti ya juu sana na radio kaiweka sikioni sipati picha zile speaker za Enzi zile na hiyo radio sikioni
 
duuuu sijui una list ya vipindi vyote mkuu maana umenitajia vingne nilikua mdogo Sana ndo navikumbuka leo hasa hyo namba 2 tulikua tunaimba na watoto we zangu
 
umenikubusha babu yng ilikuwa lzm asikilize osia wa bb wa taifa bila hvy ananuna
 
Nakumbuka kipindi cha dini ile asubui kikristo na kisha kiislam hapo nishaamshwa na mzee tuko shamban tunalima na ng'ombe maksai tangu saa kumi kasoro ikifika saa 2 hv tunarud nyumbani kuchukua jembe la mkono kwenda kupalilia mpaka mida ya saa 5 hivi asubui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…