Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Kichwa cha habari kinasema enzi hizo alafu unaishia kutaja watu wa juzi as if matangazo ya redio yameanzia juzi.

Any way, ngoja tu wa enzi hizo tuwakumbushe.

Kulikuwa na jamaa anaitwa Michael Katembo...alikuwa anaendesha kipindi kinaitwa TUMBUIZO ASILIA, enzi hizo inaitwa RTD...jamaa ndio kama alikuwa kizazi kipya wa wakati ule.

Sikumbuki vyema mwaka aliofariki, lakini aliacha pengo kubwa sana RTD/TBC...huwa nimekuwa najaribu sana kusikiliza wanaojaribu kuvaa viatu vyake lakini wanaishia kuchemsha tu.....huwa namsikia Mzee Acheli Chilewa akijitutumua lakini wapi..

.......Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na tamasha la muziki uwanja wa Sheikh Amri Abeid....bendi mbalimbali zilikuwa zinashindana...shughuli ilipofika ukingoni, kuna jamaa akaenda mbele ilipokuwa inatumbuiza moja ya bendi, akachukua ngoma na kuanza kupiga...akapiga kwa muda alafu MC akasema "jamani huyo anayepiga ngoma ndiyo Michael Katembo" huwezi kuamini uwanja mzima ulizizima...ilimbidi akimbie kwa jinsi watu walivyoanza kumzonga.

....RIP Michael.
 
Mi enzi zangu nakua watangazaji waliokuwa wanatamba ni kama Aboubakar Sadick 'kwa fujo', Misanya Bingi, Abdala Majura, Nyaisanga, Rose Chitala, Amina Mollel, Mwaipaya, Kidbway (RFA), Soggy Doggy (RFA), Double G (RFA)
 
Amina mollel,dah huyu dada kwenye miwani ya maisha,nani zaidi,chombeza, yaani sauti yake nadhani hutataka redio ndani,ni maalum sana.
 
Jina sio geni lakini flavor yake kumbukumbu sina.
Itabidi mageeks wawe wanatuwekea na clips zao
kiaina.
Wasalaam

Mtangazaji wa zaman wa RFA alikuwa anaendesha show za burudan kwa ss nakifiri yuko clouds FM team ya wahariri
 
Dah binafsi namkumbuka reporter toka mbeya huyu jamaaa alikuwa na kiswahili kitamu sama na mwisho alikuwa akimalizia nikiripoti toka mbeya mimi ni mswima errrrrrrrrrrrrnest
 
nswima Ernest, peter makongolo na Martha ngwira niliwakubali sana hawa maripota
 
Idrisa Sadalla-Mbeya anaifagilia Tukuyu stars,Chisunga Steven Kigoma anaifagilia rtc Kigoma,Ben Kiko Tabora- Milambo,Abissay Steven Songea_Majimaji,Chilambo Dominic Mwanza alikuwa anaifagilia sana Pamba sports club wana tp lindanda kawekamo,ilikuwa raha sana kusikiliza radio kipindi hicho.
 
'You are listening to news bulletin from Radio Tanzaniaaaa, read by Jacobbbb Tesha'--- hapo ni taarifa ya habari external service !!!!
 
Fauziyat abood na Elizabeth chalamila(mkwasa) hawa wamama enzi zao walikuwa wanasauti za mvuto.
 
Back
Top Bottom