Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

  • Jamani external service na Legandary Edda Sanga, ilikuwa burudani
  • Watangazaji wa kike na sauti murua, thank God wengine bado wapo: Alacia Maneno, Christine Chokunegela, Betty Chalamila n.k

  • Julius Nyaisanga (RIP) wakati anaripoti sherehe mbalimbali utapenda
  • Misakato
  • Mazungumzo baada ya habari
Betty Chalamila ndio Betty Mkwasa unajua
 
Namkumbuka Julius Nyaisanga (uncle J) alikuwa anasoma taarifa ya habari vizuri sana na alikuwa anatangaza kipindi kingine sijui kilikuwa kinaitwaje! anayekumbuka atukumbushe jamani.
 
naona atakuwa Michael Katembo
Nashukuru sana ndiye huyo alikuwa kiburudisho tosha kwenye hiki kipindi. RTD wameondoka wengi tuliowapenda kama Ben Kiko, Michael Katembo na wengine. Ila Dada Sango na kaka Kipozi wapo ila Kipozi alipewa ujiko wa siasa ikawa siyo fani yake. He did not deserve to be there. Kama wangempenda wangempa Mkuu Radio ya nchi (hivi ipo?) or something else. I do not think he is a politician. Nimeishi nao Dom I know them a bit if not more.
 
Hivi mama debora mwenda wa kipindi cha mama na mwana alishakufa au?? Nlikua sibanduki redioni kila jpili saa 8 mchana kusikiliza kipindi cha mama na mwana hadithi za kina adili na nduguze
Haikuwa jumapili, bali Jumamosi, Jumapili muda hiyo nadhani kulikuwa na kipindi cha dini ya Kikristo (kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe) kisha kilifuatiwa na Cheichei shangazi
 
Ivi yule jamaa wa mazungumzo baada ya habari na maneno hayo alikuwaga nani maana alikuwa na maneno kuntu sana yule jamaa! Yuko wapi na anajishughulisha na nini?
Mara nyingi alikuwa Abdul Ngalawa, ndio hasa alikuwa mtaalamu wa hiyo kitu
 
Your correct. Nakumbuka nilivyunja mlango wa redio upande wa kuwekea kanda......niliweka kanda, kumbe haijakaa vizuri mie nikang'ang'aniza kufunga mlango, kutahamaki mlango umevunjika, kipigo nilichokipata kutoka kwa mother sitakaa nisahau
Kumbe na wewe wa zamani? Radio kipindi hicho ilikuwa ni asset kubwa sana, sio kila nyumba ilikuwa na radio,
 
  • Thanks
Reactions: ram
Kuna kipindi likuwa lazima tusikilize shuleni, kile cha masomo sikumbuki kinaitwaje ila mnasikiliza mwanzo mwisho baadae mwalimu anaanza kuuliza maswali kutokana na kilichofundishwa.
Kipindi cha wakati wa kazi, kilikuwa marvelous hiki kilikuwa kinawahoji wafanyakazi wa mashirika mbali mbali jinsi wanavyofanya kazi, so ilikuwa ni rahisi kujua mashirika yanafanya kazi gani, changamoto wanazokutana nazo n.k
Aisee una kumbu kumbu sana!halafu wakati huo magazeti ya kiswahili ni uhuru,mzalendo na mfanyakazi kila jumamosi na pia kiongozi,....Daily news na sunday news ni ya maboss...,ukilipata uhuru unaburudika na chakubanga,polo,bushiri na Chupaki,na enzi ile ukiwa na lips kubwa wanakuita chupaki,siku hizi lips kubwa ni "Fasheni" kwa wadada wa dot com.
 
Mzalendo wa jumapili ndio kulikuwa na yule kakamiye
 
Michael Katembo
Nashukuru nimemkumbuka. Imagine tulikuwa tunachora picha ya mtu bila kumwona. Nilichora picha ya michael katembo kama mtu mwembamba, mrefu halafu anavaa suruari za kubana na ana uso mrefu. At least uncle J nilibahatisha kuona picha yake kwenye gazeti alipokuwa ITV. Hivi kuna mtu aliweza ona picha ya Katembo? Tupia basi.
 
Haikuwa jumapili, bali Jumamosi, Jumapili muda hiyo nadhani kulikuwa na kipindi cha dini ya Kikristo (kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe) kisha kilifuatiwa na Cheichei shangazi
jumapili sa nane mchana nakumbuka ilikuwa NIPE HABARI,kikitangazwa na mkurugenzi DAVID WAKATI...ndio kipindi pekee ambacho Wakati alikuwa anatangaza,ukimsikia sauti yake mara nyingi itakuwa kuna jambo zito la kitaifa.
 
Namkumbuka Julius Nyaisanga (uncle J) alikuwa anasoma taarifa ya habari vizuri sana na alikuwa anatangaza kipindi kingine sijui kilikuwa kinaitwaje! anayekumbuka atukumbushe jamani.
Nyaisanga hakuwa sana kwenye Habari, habari kama ni nzito sana yenye umuhimu basi Jackob Tesha ndio anachukua jahazi, za kawaida ni wakina Charles Hilali, Abdul Ngalawa, Halima mchuka nk

Nyaisanga alikuwa sana kwenye vipindi vya Makampuni mbalimbali, kama Bima nk, na pia alikuwa mzuri sana kwenye vipindi vya miziki kama Misakato, club raha leo show, akiwa n Enoch Ngombale

Na kwenye Zilipendwa alikuwa mzee mwenyewe Ngombale
 
Wakati umewadia wa salamu za wagonjwa hospitalini leo tunawapa poleeee....

Shambani shambani shambanii.....
Mazao bora shambaani.

Baadhi ya vinyimbo[emoji115][emoji115][emoji115] navikumbuka
 
Back
Top Bottom