Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Naitwa king kong wa tatu nafanya kazi hapa kiwanda cha urafiki kama mlinzi salamu zangu za kwanza namtumia mod invisible,paw,maxence za pili namtumia member mwenzangu king kong feis buku bila kumsahau mwali na husninyo club raha leo shooooooooooooooow!
 
Halaf kipindi hiki kiliendeshwa na mwanamama mmoja mwenye sauti ya malezi kwa watoto sijui alikua anaitwa nani? Alikua akisimulia hadithi za kuvutia, alikua akianza na maneno, "PAUKWA..., hapo zamani za kale palikua na..."[/QU hadi machozi yanlenga lenga kwa kunikumbusha yazamani. Akhsante
 
majira
pwagu na pwaguzi
mahokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
mama na mwana na hadithi za ua jekundu
matanagzo ya: sikiliza bwana umeme

wimbo:
kuleni chakula bora cha kuujenga mwili
na kujenga nyumba bora pakulala pawe safi....
Kuleni kuku mayai mboga samaki maziwa.......
 
Wakati umewajia wa salam za wagonjwa hoplini leo tunawapa pole,ajuae bwana mungu kwa mzima kuwa mfu mgonjwa kuwa salama leo tunawapa pole..MALIZIA
 
"...swahili lugha ya taifaaa ya taifaa..
na visiwani oohh swahili lughaa ya taifa..
..swahili luughaaa.."

huu wimbo ulikua wasindikiza kipindi flani murua sana...
 
Kipindi icho tuko wadogo mzee j.2 ananituma nikamlete magazeti mzalendo na sundaynews tulikuwa tunayanunua mwenge gazeti unalipata kwambinde foleni yakufa mtu.Enzi izo mambo yalikuwa mazuli sana.
 
"...swahili lugha ya taifaaa ya taifaa..
Na visiwani oohh swahili lughaa ya taifa..
..swahili luughaaa.."

huu wimbo ulikua wasindikiza kipindi flani murua sana...
na vijijini oh ni kiswahili chatumika..
 
Kumekucha mamakumekucha! Majogoo vijijini yanawika wazalendo wa mjini tukafanye kazi sasa,oh oh mama tusong mbele.
 
Namkumbuka sana Ahmed Jongo, Ben Kiko, Malima Ndelema, Richard Leo, Salim Mbonde, et al. By that time RTD ilivutia sana.

unamkumbuka mwandishi wa rtd toka kigoma alikuwa anaitwa Tumbo Risasi??
 
Kwa upande wa vipindi nilipenda sana Chaguo la msikilizaji j3 hadi ij sa8 mchana, mama na mwana j1 sa9 alasiri, Salaam za wagonjwa j2 sa4 asubuhi, Igizo la Twende na wakati wakiwemo kina Kidawa j4 sa3 usiku.

yaap mkuu! Umenikumbusha mbaaali sana
 
Mchezo wa radio wenye maadili ya kutosha saa 2:30 usiku kama sikosei hivi!
TWENDE NA WAKATI mixer ka mdundo fulani hivi nduuu! nduuuu! nduuu!
nilikuwa skai mbali na radio ya mkuliwa
NATIONAL!

eti watoto wa leo wanasimuliana kwao wana flat tv wakat enzi hiyo kitu cha mkulima kipo classic
 
Kumbe nawe ulikuwepo enzi za cheichei shangazi studio akiwemo mwanamama ELISIA ISABURA. Aisee kitambo sana.

hivi yule aliyepiga ngoma ya taarifa ya habari anaitwa nani vile?
 
Mnaikumbuka 'mikingamo', 'club raha leo show' pia mchezo wa kuigiza wa kiinua mgongo ukichezwa na mzee jangala kikidhaminiwa na dar brew watengenezaji wa pombe safi kibuku (enzi hizo lkn)

nakumbuka enzi hizo waigizaji maarufu ni akina mzee jangala, mzee mundu, pwagu na pwaguzi
 
Back
Top Bottom