Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Nikipindi cha pili cha pili hapa wao sifuri sisi moja na utamsikia tukifungwa timu ya taifa alikuwa hata hasemi goooooooooooo utasikia washatufunga. namna gani hapa jamaa alitakiwa kutumia hata ulimi kuweka ule mpira kimiani. Ahmedi Kampira na mpira lalalalalalalalalaaaaa ah namna gani Juma Mgunda anashindwa kuona milingoti mitatu hapa.
Kwenye maguu kumi nane ana weka mpira ule Edward Chumila na na simba wanafanya mabadiliko namuona kocha mchezaji anaingia hapa heeeee he Chumila kwa guu lake la kushoto anapiga mpira ule anaingiza majalo moja pale ile inaitwa banana chop gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo a namna gani hapa mpira unagonga mtambaaaaa panya wasikilizaji ..................... nikikumbuka enzi hizo sipati jibu

Huyo alikuwa Ahmed Jongo.
Namkumbuka 1993, Yanga wametoka kutwaa ubingwa wa CECAFA, wakakutana na Simba.
Yanga wakapata bao la 2, Jongo anasema:
"Niliwambia kule Kampala, niliwambia kule Kampala,
Yanga si timu ya mchezo.
Ninachotaka kuwambia ni kwamba, Yanga wanapata bao la 2.
Said Mwamba Kizota anaifungia Yanga bao hapa"
 
Yusufu Omari Chunda alikuwa ripota wa Zenj, mkali wa Methali.
Kipind hicho, Super ligi(ya Muungano), Reli, kiboko ya vigogo, ya kina Athumani Msumali, Dancun Mwamba, Dancun Butinini, Mbuyi Yondani, David Mihambo, Gasper Lukindo, Fikiri Magoso.
Wakaenda Zenj kucheza na Black Fighters, wakapigwa. Sasa Chunda anaripoti:
"Kwani waswahili husema, Reli haivuki bahari, ikivuka, si reli hiyo, bali ni jinamizi. Huyu ni Yusufu Omari Chunda, michezo, Zanzibar"

au

"kwani waswahili husema, usihadaike na rangi, utamu wa chai sukari"
 
mmetukumbusha mbali sana enzi hzo redio kubwa ya mkulima inashaka stationi moja tu.EZEKIELI MALONGO mmemsahau jamani na uongo wake.
 
Nyani Ngabu,yeye ndo alitangaza live sherehe za uhuru wa Tanganyika 1961 ,sijui kapotelea wapi,mara ya mwisho nasikia mkewe alimpiga na mwiko baada ya kumbamba anachoropoa nyama kwenye sufuria.
 
Last edited by a moderator:
Hahaaaaaaaaa BAK una vituko wewe..Haya maneno hata mimi mpaka leo sijajua yalikuwa ni maneno gani aisee...Hiki ni kipindi nilichokipenda sana enzi hicho,hasa madoido na mikogo ya mtangazaji wake Abdallah Mlawa...Mkuu pia kulikuwa na kipindi cha Ngano za Muziki wakikumbuka hiki???,yaani hapa ilikuwa zakusanywa nyimbo zenye maudhui yanayoendana kisha latengenezwa/launganishwa bonge la stori


Swadaktaaaaaar....
 
Hivi ni kwanini Sued Mwinyi siku hasikiki na hasa kwenye mpira? Yule bwana anaweza sana kutangaza football bana


No Data no right to speak...
Ulisikiliza TBC Taifa majuzi kwenye mashindano ya soka kombe la Kagame?
Kwanza unazijua mitabendi za TBC Taifa?
 
hiv yule jamaa wa kipindi cha ngoma za asili aliitwa nan vile
 
Kweli zamani raha ivi watoto wetu miaka 20 ijayo watasimulia sifa za watangazaji wa sasa hivi kama hizi?
 
Mama na mwana na Debora Mwenda. Kilikuwa kipindi cha watoto lakini wakubwa walikuwa wanapenda kusikiliza.
 
Pasco Mbona hata Pascal Mayalla kajisahau kama na yeye alikuwa RTD Bila Kumsahau Mohammed Kisengo huyu nakumbuka alitangaza Kifo cha Marehemu Habib halahala...Nakumbuka Saa Mbili Usiku ''Habari zilizotufikia punde sasa hivi kwenye chumba cha habari ziasema Mwandishi wa Raisi Mwinyi amefariki Dunia baada ya Kukatwa Panga la nyuma ya helicopter mkoani Lindi Raisi alipokuwa anafanya Ziara kwenye mafuriko yaliyotokea Lindi na Mtwara'' Watu ziii tulibutwaa kifo cha Jirani yetu na tukifikiria jinsi ya aina hiyo ya kifo japo baadae yalisemwa mengi sana kuwa ni chezo walicheza aliposhka wakawa wanamuambia rudi nyuma rudi nyuma masikini akawa anasikiliza tu hadi panga likamkata kichwa uugh! na huo aliyekuwa anamuambia alimezewa japo na yeye yaliyomkuta alikuwa mtu mnene pia
 
Sarah Dumba

Fuziat Aboud - Mama na Mwana alikuwa na Sauti Nzuri kwenye Hadith.i Alikuwa Raia wa commro
 
alhamisi saa kumi na moja na nusu jioni palikuwa na kipindi cha misitu ni uhai...
Kwenye jingle ya kipindi utaisikia sauti ya Captain John Komba kabla hajamla pono na kuwa anasinzia Bungeni asubuhi, mchana, jioni.
Alikuwa akiimba na kusema:..

Watanzaniaaa Bara na Visiwanii
Tuyahifadhi ii mazingira yetuuu
Tangu zamanii tulipewa urithi
Tuikumbuke ee misitu ni uhai jaama...

RTD kuanzia vipindi, watangazaji, wasikilizaji woote tulikuwa timamu kichwani.
Tofauti na watangazaji kama hawa wa Clouds kama Gea Habib ambae katikati ya kipindi anamwambia mtangazaji mwenzie ''halooo oooh, shost akileta zake mchambe, mchambe mchaambe Babu nyoooo''

Sasa maneno hayo uliwahi kuyasikia kwa Siwatu Luanda, au kwa Aloisia Maneno, au kwa Eda Sanga, au kwa Salama Mfamao?
 
yaani RTD ilikuwa ni balaa.
Ukiachilia mbali watangazaji mahiri
pia pakawa na kipindi cha benki ya CRDB...
Jingle yake ilipigwa na Sikinde na kuna kipande murua anaunguruma Benovilla Antony anasema...

Watu binafsi na wakulimaa
Na wafanya biashara
Na vikundi vilivyoahinishwa
Mnaweza kukopa CRDB...

CRDB ni chombo
Kilichoundwa Madhubuti
Kinachotilia mkazo
Maendeleo ya Umma

Nani anamkumbuka mtangazaji aliyekuwa anaongoza kipindi hichi?
Kilikuwa kinaanza saa moja na robo mpaka saa moja na dakika 45 jioni.
 
Ambao hamjawataja hapa ni kama
Kauye Saidi
Halima Kihemba
Abasi Kihemba
Karim Besta
Suleiman Kumchaya
Ben Kiko
Abysai Stephen
Nechy Limo
Julius Nyaisanga
 
Back
Top Bottom