Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Mnapotoshwa sana kuhusu Sadaka.Kufatia kuvurugika kwa maadili inaonekana kuna tatizo katika upande wa kiimani na kwa haraka naweza kufikiiria kuyumba kwa uchumi misikitini,kanisani na madrasa ambapo inawalazimu walimu, masheikh na waubiri kufanya kazi kwa kiasi kikubwa ili kujiihudumia.
Ukweli ni kwamba Ukitoa sadaka hupotezi ila unajivika vazi la imani kwa kupata rehema za mungu kwa kuwa unapowawezesha walimu neno la mungu litawafika wengi na hata dunia kuongoka vile vile nyumba za ibada zitakuwa kwenye hali nzuri kwa matokeo ya michango yenu ya sadaka.
Nawasilisha
Waumini wengi hawajui chochote kuhusu Sadaka, wamebakia kukaririshwa kwenda kutoa pesa na mali zao kwenye nyumba za ibada ili kutimiza malengo ya mwenye umiliki wa hizo nyumba za ibada huku wakidhania ndio wametoa sadaka, wamedanganywa kwa 100%.
Kukusaidia tu mleta mada hapa na wengine wengi ni hivi:
1. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Sadaka, michango na misaada. Sadaka ni mali ya Mungu (haijarishi unaitoa wapi), michango ni sehemu ya uwajibikaji kutimiza malengo ya mahali ulipo na misaada ni matendo ya haruma kwa wenye uhuhitaji.
2. Sadaka ni ibada kamili, ni lazima uitoe ukiwa na Imani kamili kwa yule unayemwabudu na utoe kwa utaratibu wa imani wa yule unayemwabudu. Kama unayemwabudu yuko ndani ya moyo wako, moyo wako utakusukuma pa kwenda kuitoa.
3. Sadaka inapaswa kutolewa kwa kupenda, na sio kwa kutishwa, kubembelezwa au kushawishiwa. Kiongozi wako wa kiimani anapaswa kukufundisha umuhimu wa kutoa sadaka kwa Mungu wako basi, mengine utajua wewe mwenyewe na Mungu wako. Ukiona kiongozi wako wa kiimani anakadhania sana kukutisha, kukubembeleza au kukushawishi kwa mitindo mbali mbali ili ulete sadaka kwake/kwenye nyumba ya ibada uliyopo, tambua huo ni utapeli wa kiimani kwa 100%.