Tujitahidi kuwa waangalifu sana huko makazini zama za sasa vijana wamejaa majungu na wivu kushinda wazee

The best way is to Sly like a Fox & Trust nobody.
 
WELL SAID MKUU

Umetueleza jambo moja very sensitive, maisha ya sasa tumezungukwa na chuki, roho mbaya, unafki, ubinafsi na majungu. Roho zote hizi mbaya mzizi wake ni WIVU na kutakiana mabaya.

Kijana hakikisha hauna marafiki ambao hauna connection nao ya kueleweka. Hasa hawa uliokutana nao kazini au vijiwe vya pombe- Ulabuni na mtaani unapo kaa. Usipende kukaribisha marafiki hao nyumbani kwako, waishie kupaona kwa mbali, ikibidi kama nyumba ni ya kwako waambie umepanga, na wala usipende kushea nao mipango, mikakati na mafanikio yako. Hakika hao ndio watakao kukaanga mapema zaidi.

Mtu anakuja kwako kukutembelea kama mshkaji halafu huyo huyo anakuchora mambo yako anapeleka maneno kazini kuwa huyu jamaa anabonge la nyumba kajenga kwa mshahara upi? kanunua gari amemfungulia mkewe biashara anaishi vizuri kwa mshahara upi huyu lazima anakula rushwa au anapiga hela sehemu sio bure.....

Mambo ya kazini jitahidi yaishie kazini, mambo ya nyumbani na mtaani yaishie huko yasiende kazini. Kata huo mnyororo wa mahusiano kabisa. Kataa kabisa marafiki wakazini kuja nao mtaani. Hawa watu uliokutana nao kazini SIYO MARAFIKI ZAKO mmekutana pale kwaajili ya kazi ukitaka kuamini hao siyo marafiki zako mmoja wenu abadili kazi, aachishwe kazi, au ahamishwe eneo, Uone kama ukaribu na mawasiliano yataendelea kuwepo.

Kama unafanya ujenzi au biashara usipeleke marafiki wakazini wakapajue. Tena kwenye biashara wakijua ni biashara yako hawatanunua vitu kwako wataenda kununua kwingine, kwako utaona wanauliza bei wana sepa.

Na usikubali kujenga nyumba mtaa mmoja na wafanyakazi wenzako hiyo ni mbaya kinoma, kama huamini fuatilia uone majungu wanayopigana walio jenga hivyo.

Rafiki yako wa kweli ni yule ulietoka nae utotoni mpaka leo uko nae karibu (japo kuwa nao baadhi wanakuaga wasaliti na wapuuzi) Kama huna huyo achana kabisa kushobokea watu ulio kutana nao wakati umeota ndevu, au maziwa...hao watu watakukaanga vibaya.. huto amini. Jenga urafiki na mtu ambae unaona ana akili nzuri kama ya kwako au kuzidi ya kwako ila asiwe wa kazini kwako.

Chunga sana...Mmbaya wako siku zote hatoki mbali, Mchawi huwa harogi mbali.. Hakikisha unatokomeza masnitch wote usio waelewa katika hatua za mwanzo sana, usiruhusu mtu akujue jue ovyo ovyo, wala asikuzoee ovyo. Utaishi kwa raha sana na mambo yako hawata kuchawia.
 
Kaka umenena vyema zaidi, hakika ungekuwa karibu yangu ningekununulia bucket moja ya Windhoek.

Hawa hawa niliowachukulia kama marafiki wamegeuka maadui, kisa tunetofoutiana katika mshahara na posho kadhaa tu.
 
Kaka umenena vyema zaidi, hakika ungekuwa karibu yangu ningekununulia bucket moja ya Windhoek.

Hawa hawa niliowachukulia kama marafiki wamegeuka maadui, kisa tunetofoutiana katika mshahara na posho kadhaa tu.
Kaka nashkuru sana huu uzi ulio anzisha ni zaidi ya bucket.. ninafahamu saana haya mambo ya kazini na nimeyapitia sana pia, yamenijenga.
 
Inaonekana na wewe ni miongoni mwao wale wanako vihelehele wa Bosi,Kwan kutoboa kimaisha lazima uwe mnafiki?😲

Moja ya kiongozi mkubwa aliwai kusema bila unafiki /kujipendekez hutoboi'
Haikupita muda nikafanyiwa huo unafiki na nikafukuzwa kazi na mwajili maana sinaga mambo za kujipendekeza alafu nafanya kile nachokiamini.

Napenda kazi ila sio kupelekeshwa!. Kama utakuwa mtu smart tegemea majungu sana mkuu.
 
Yes! Baba yangu ni mfano hai, alikuwa smart, si mtu wa majungu au kusengenya, akafanyiwa vitimbwi na kuikimbia kazi aliyoisotea kusoma pasipo kupenda. Nimelia, huenda nisingeishi maisha niliyoishi.
 
wenye shida ni hao maboss au waandamizi wanaokaa kufanyia kazi majungu.

ukiwa boss wa namna hii kuwasilisha uwezo wako 100% huwa ni changamoto sana.
 
Mipaka

Mipaka


Mipaka

Hamuweki mipaka na ndicho kinachowaponza.


Mfanyakazi mwenzio nyumbani kwako anafata nini na huumwi hoi hoi wala hujafiwa?????

Urafiki wa pika pakua...... bata batani na mfanyakazi mwenzio wa nini?????

Maisha yako binafsi yanamhusu nini????
 
Kabisa
 
Kikulacho....

Hatari zaidi usiwaamini hata ndugu zako, kuna vita mbaya za kifamilia ndio zipo kwenye chati sasa hivi.
Mkuu nimeshtuka nikama unanisema mim.

Vita ya ndugu zangu ilianza kwa kunitupia makombira ya kuniangamiza baada ya kununua kajiusafiri.

Mara nikaanza kusenwa ooooh, anajifanya hana pesa anatunyima mbona kanunua gari.

Nyie ndugu Mungu atawalipa kwa roho mbaya zenu
 
Mbaya Wako - Les Wanyika (huu wimbo una ujumbe mzuri sana kuhusiana na mada husika.
 
ahsante sana mzee wetu Nyboma, Id yako imenikumbusha wimbo wa Nyboma na pepe kalle unaitwa Nina
Nina mosei yoo!! Ngai nalingi yooo..
Atabasali nyoso, Pasi na lula yooo..
Lelo nazuiyanga mobali,Fami esepeli.
Nalingoli bino'soni yoo de'puisa'lanca mamaeee...

Chorus:
Bong'o lango motema mokili e'shante o'
Tubelango masumu balimbisayo na nzambe,
Nzambelaka masiah papaa tobotaa........

Nina Mosey
 
ewaah, hii ngoma kali mnooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…