Asante ndugu Mgombezi,
Hilo ni Jambo Nyeti sana ambalo umeongelea ambalo litatoa ajira kwa vijana wa Kitanzania, WAKE kwa WAUME. Pia ndo njia pekee ya kupunguza mfumuko wa bei na kukuza uchumi wa kila Mtanzania.
Kila siku tunakula, na tunavaa. Tunakula Mpunga,Ngano, ugali, alizeti, ndizi, matunda na mengine useme..
Tunavaa Pamba,
Kondoo wa Hariri - Njombe
Bia - Shayiri west kilimanjaro, Mbulu, Nyanda za juu
Mafuta - Palm (Kigoma), Alizeti Singida
Mahindi yanaliwa na pia yanatengenezea cooking oil.
Kitimoto inaweza kuuzwa Ulaya
Sasa kwa nini watanzania tunakalia uchumi halafu tunakuwa masikini???
LIPO TATIZO
Tatizo ni utashi wa Kisiasa na Ulimbukeni.
Kila kitu hatuwezi, kila kitu mwekezaji.
Mfano kuna mashamba makubwa yaliyokuwa RANCH na NAFCO.
Hayo mashamba yamekuwa usingizi kwa muda mrefu na mengine wamegawana vigogo, mengine wamepewa wawekezaji (wakoloni).
Sasa hao wawekezaji wamewageuza watanzania watumwa ndani ya nchi yao. Imagine watu wanaajiriwa kama kibarua katika mashamba.
Ingekuwa vipi kama hao watanzania wangegaiwa kila mtu kuanzia heka 5 mpaka 10. Sidhani kama mtu anaweza kuhudumia heka 5 au basi sema heka 2 basi aidhuru.
Sasa kama mtanzania mmoja akigaiwa heka 5, akapewe hati miliki, anaweza kupata mkopo benki, akalima kwa tractor na pia akapata pembejeo. Kama hakuna mvua, kilimo cha umwagiliaji kifanye kazi. Hapo mavuno ni lazima, masoko ya mazao watafutiwe.
KASORO
Viongozi wengi wa Kisiasa ni wabinafsi, na 10% zinawanufaisha. Masilahi ya wananchi hayaangaliwi.
Wanawapa wawekezaji au wao wanajigawia mahekari kwa mamia wakati wananchi wanakosa angalao heka moja.
TUFANYEJE?
Haya mazungumzo tunayojadili hapa, tunayaandike kwenye magazeti na pia tuyawasilishe wizara ya kilimo, wizara ya ardhi, wizara ya uwezeshaji. na hata wanaharakati na taasisi kama kituo cha haki za Binadamu, haki elimu na vyama vya siasa.
Pia tuanze kujiandikisha, kiwilaya, kimkoa na kitaifa. umoja ni nguvu.
Asanteni, nawasilisha!!