Elnino it is well said... na mimi binafsi nakubaliana kwamba mtaji ni kitu muhimu sana.. ila niseme kuwa kuna mitaji ya aina mbili, mtaji pesa na mtaji muda... kuna watu wana pesa lakini hawana muda wa kufuatilia nini kinaendelea shambani.. kwa hiyo tukiunganisha nguvu mambo yataji-compliment..
El nino aidha umegusia suala kubwa sana-- UHAMASISHAJI.. nakumbuka malila alishawahi kuratibu CHAI DAY.. na kweli nikili kwamba kwangu ilikuwa ni mojawapo ya mkutano uliobadilisha fikra zangu katika kilimo.. maana kwa sasa nimepata shamba katika baadhi ya maeneo na ninawekeza fedha kidogo ya mshahara wangu katika kufanya shughuli za kilimo.
kwa hiyo basi napendekeza, kama kweli tupo serious napendekeza watu wafuatao tupange tukutane kwa sababu nimeona tuna interest za kilimo:
- Malila
- Elnino
- Mimi (Kanyagio)
- Mgombezi
- Maskini Jeuri
- NewMzalendo
- mwingineyo anayemaanisha (narudia tena anayemaanisha kulima)
tukubaliane tukutane lini na wapi.
nimetaja watu wachache kwa sababu ili mambo yaende ni lazima kuwepo na kikundi kidogo cha kujitolea kutengeneza msingi then kundi kubwa zaidi linashirikishwa.
ahsanteni sana