Tujiunge na kuanzisha JAMII FARM

Haa, this is lovely,

kwa kipindi kirefu watnzania tumekuwa tunaongea tu hatuchukui hatua, kama vile tulivyo kuw atunapiga kelele haaa tumechokaka na utawala, tunanyanyaswa, nchi ni msikini kwa kukosa uadilifu.... lakini wengi hawakupiga kura... hii inachukiza sana

sasa jamani mm nonya juu ya siasa kuingi humu, tuwe waangalifu sana, tukumbuke watu wasion huruma pia wamo humu, tuwe makini katika kudisign hii movement.

Arrangement za vikao nk kwa speed hii inaridhisha, aliyependekeza early Jan 2011, namuunga mkono, niko tayari kutoa kila support itakayohitajika kwangu ikiwa ndani ya uwezo wangu!

Kuna watu wananiudhi kweli humu ndani, wanosema katu haliwezekani, nawashauri kama hawaoni uwezekano basi wasuburi waone, na pia ndugu zangu comments zilizo negetive namna hii inaonyesha ni jisni gani tlivyo na kazi ya kuwaelewesha watz hawa, tunapaswa kuwa polite kwao na kuwaelekeza wataelewa tuu. Nakushukuru Mgombezi unavyowachukulia.... asante kwa upole na ukarimu kwa watu hawa.

Pamoja daima, wanaofikiria kuwa ujamaa uliokufa enzi sa Mwalimu ndo unjamaa wa leo imekula kwao, Niwaulize watuambie ni akina nani wanamiliki CRDB, TBL, TCC nk kama sio watu wengi (wanahisa) na hii ndo modern Ujamaa, kwa nini tusione haya mambo kwa mtizamo huu?

Mabepari walikuwa wanaupinga ujamaa lakini wao sasa hivi ndo wanaona unafaa kwa kuweka hisa kwenye masoko yao!!! sasa ss tunaweka hisa za mwanzo hapa jamvini!! kwa mfumo wa mawazo yanaojenga, tunakuwa taratibu hatimaye kufanya informal, Formal!!

Pesa ni watu na Watu ndo sisi
 

Asante Realtor

Ni kweli watu tunakuwa/wanakuwa na mawazo mengi juu ya kuanzisha biashara/project fulani; lakini huo utaalamu wa project proposal inawezekana ukawa adimu katikati yetu. Hivyo basi ndiyo maana niliamua kuleta hili kama wazo na hayo mengineyo yataendelea kuchangiwa hapa jamvini, kwani ninaamini hii itaweza kuwasaidia na wengine ambao wanaweza kuwa na mawazo lakini wasifahamu jinsi ya kuanza.

Kutokana na michango ya wadau wengi imeonekana ni vyema kukutana kwanza wale wote ambao tuna same interest juu ya Kilimo na Ufugaji; vile vile ambao tuataonelea ni vyema kuwa na ushirika huu. Hivyo basi mchakato wa kukutana unaendelea na tutapeana taarifa zaidi.
 
Wakuu ndo wengine tumeshtukia hii thread,tunaomba feedback ya huo mkutano na maazimio..
Tuko pamoja
 

Wakuu heri ya mwaka mpya, nawashukuru wote kwa michango murua, niombe samahani kwa kutoonekana ktk mjadala huu kwa muda, nilikuwa ktk utekelezaji wa maazimio ya Chai day tuliyowahi kufanya mwaka jana. Ktk chai day hiyo sisi kama vijana tulikubaliana kufanya large scale investment ktk land, na tumefanikiwa sana kwa mwaka uliopita. Nawahakikishia wanabodi uwezo huo wa kufanya mapinduzi tunao sana.

Hata sasa tunaendelea na utekelezaji wa maazimio yetu, hakuna hata mmoja aliye/anaye jutia kukutana kwetu. Kupitia mkutano ule ndio nikajua Wabongo hela wanazo,ila hawajui waweke wapi. Tulifanya jaribio la kuanzisha kijiji cha wafugaji na marafiki zangu, tumefanikiwa vizuri na hakuna aliyeibiwa, ila wote ni kicheko na kujilaumu kwa nini tumechelewa kuunganisha nguvu.
 

Naam naunga mkono hoja.
 

Hata sasa waoga wanaodhani haiwezekani wapo, ila tunaosema inawezekana tupo, usijali idadi yetu. Mimi naamini ktk vitendo huko field. Twendeni.
 
haya tunaanzia wapi,{location} when? estimated initial investment ,expected ROI.
Hata sasa waoga wanaodhani haiwezekani wapo, ila tunaosema inawezekana tupo, usijali idadi yetu. Mimi naamini ktk vitendo huko field. Twendeni.
 
wazo zuri. then a venue should be selected

siku hazigandi, mlioko dar mna nafasi nzuri ya kutafuta venue ili tuanzie hapo. Tahadhali, tulipoandaa chai day siku ya kwanza watu walikuja wengi na tukalipia ukumbi bila taabu, mara ya pili ilibidi kutoa mfukoni kwangu ili kujazia malipo. Sasa mahali pa kukutana ni muhimu gharama zikaangaliwa kabla.
 

Mkuu Malila nimeku-PM 2 days ago!

Naomba mliopo DAR kusaidia kutoa mapendekezo ya Venue pamoja na gharama zake.
 
Mkuu Malila nimeku-PM 2 days ago!

Naomba mliopo DAR kusaidia kutoa mapendekezo ya Venue pamoja na gharama zake.

Naamini nimejibu pm uliyonitumia, kuondoa utata narudia tena mkuu. Asante.
 
Mbona hakuna feedback ya kinachoendelea huko town? Au ndo yale yale ya kila siku wakuu? Hata kutoa pendekezo la ukumbi? Mimi niko nje ya Dar kwa sasa.
 
mimi napendekeza eneo la Milenium Towers,either pale Pembeni ya Break Point au Makumbusho ,Date and Time itabidi tukubaliane
 
Naomba tuwasiliane mie ni mtaalamu wa kilimo hili linawezekana kabisa na hasa sasa pamba inalipa mbaya
 
ndugu wanajamii tukubaliane lini tutakuwa na muda wa kufanya mkutano huo ,. then kila mtu aandae elfu kama elfu kumi mpaka 15 kwa ajiili ya gharama za ukumbi (inaweza kupungua au kuongezeka kutegemeana na idadi ya watu).. ukumbi upatikana tu.
 
Mkuu eneo au ukumbi unaopendekezwa uwe na walau parking ili wenye usafiri wao wasiteseke, suala la ulinzi liangaliwe pia,sio kama mlimani city.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…