Tujue moja: Nchi hii ajira kwa graduates zimeshafutwa!

Tujue moja: Nchi hii ajira kwa graduates zimeshafutwa!

umusuntiwawe

Member
Joined
Jul 9, 2020
Posts
52
Reaction score
125
Miaka mitano hamna ajira kabisa wala kupandishwa mishahara wafanyakazi? Hebu vijana unganeni mumtoe huyu jamaa hata akiiba kura ingieni barabarani.

Hakikisheni utawala kama ule wa JK wa kuajiri kila mwaka madaktari na walimu unarudi la sivyo huyu jamaa atawaua maana hajali lolote bora mfe ila ndege zinunuliwe, bora mfe flyovers zijengwe. Hana mpango kabisa na nyinyi hata mkijipendekeza.

Juzi kati kuna shule ilitangaza nafasi ya walimu wawili wa hesabu, walienda 600 kwenye interview. Jamani hali ni mbaya kwa JK mambo hayakuwa hivi. Arts wenyewe kawapotezea mazima. Vijana na wakulima unganeni mumtoe huyu jamaa. He gona kill you, woga wenu ndo kifo chenu!
 
umusuntiwawe,

Nakumbuka shairi moja nililisoma nikiwa shule ya msingi linasema “Kama mnataka mali mtayapata shambani.” Nenda kavamie mapori upande mbegu mbalimbali utapata mazao kisha uuze upate ujira.
 
Na zinazotangazwa kila leo ni nini? Serikali yoyote duniani haina uwezo wa kuajiri kili mhitimu, hata Tanzania haiwezi lakini kiwango cha kuajiri tulichonacho ni kizuri.
 
Na zinazotangazwa kila leo ni nini? Serikali yoyote duniani haina uwezo wa kuajiri kili mhitimu, hata Tanzania haiwezi lakini kiwango cha kuajiri tulichonacho ni kizuri
zipi! Hizo mia tano kati ya efu 92. Nyie muwakejeli tu vijana matokeo mtayapata october! Jk aliweza kuajili wote hakuna aliyekuwa anabaki labda ukatae ajira mwenyewe
 
Tuangalie namna ya kufanya uzalishaji mali na huduma independently, tusitegemee sana ajira
Huu Ushauri Kawapeni Kina Omari Kigoda, Goodluck Mlinga, Ridhiwan Kikwete, Hussein Mwinyi, Godfrey Mgimwa na Kina Halima Bulembo.

Au Kawapeni Kina Januari Makamba au Nape Nnauye Washazoa Mitaji Wakajiajiri, Siyo Kukubali Kutembezwa Kwa Magoti Siku Ipite
 
tunataka tujue tu kama ajira zimeshafutwa awamu hii ya jamaa au lah!
Inshort kwa sasa zimefutwa,yuko bize na miradi mikubwa ya Stigler's,SGR,madaraja ambayo yanahitaji vibarua tu kwa sana.
 
Ajira za nin maisha mbona yanasonga kwan? Kunasehemu tulikubaliana na serikali kwamba baada ya kusoma itakuajiri.
Hayo ni maneno wanayoambiwa watoto wa wanyonge tu,watoto wa wakuu wanamaliza vyuo kama kawa na kazi za vimemo wanapata kama kawa.

Watoto wa wanyonge wakajiajiri tu maana vitambulisho vyao vya umachinga viko tayari.
 
Ajira ni utumwa sana jaribu kupambana utafurahia maisha ya kujiajir.
 
Na zinazotangazwa kila leo ni nini? Serikali yoyote duniani haina uwezo wa kuajiri kili mhitimu, hata Tanzania haiwezi lakini kiwango cha kuajiri tulichonacho ni kizuri.
Nimemsikiliza jamaa mmoja leo asubuhi kwmy Tv akiisifia awamu ya 5 anakwambia Magu tangu ameingia madarakani ameajiri madaktari 300(mia tatu tu),hahah nikasema tu hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom