Tujue moja: Nchi hii ajira kwa graduates zimeshafutwa!

Yaani kaka, hizo intern mimi binafsi nimetafuta hadi nimechoka cha ajabu wengine baadhi wanapata kirahisi(wenye conection na vigogo)
Sasa nataka nianze kuuza mitumba tu hii ndiyo biashara niliyoiona ninaweza kuifanya kwa mtaji mdogo na nikapata faida ajira hizo zishakuwa ngumu
 
Mkuu we anza na ulichonacho tu hata kama ni mtaji ni mdogo maana hawa jamaa ukisema uwasikilizie watakupa miyeyusho tu.
 
Hayo ni maneno wanayoambiwa watoto wa wanyonge tu,watoto wa wakuu wanamaliza vyuo kama kawa na kazi za vimemo wanapata kama kawa.

Watoto wa wanyonge wakajiajiri tu maana vitambulisho vyao vya umachinga viko tayari.
Inasikitisha kwa kweli,
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaaah hali ni mbaya kwa kweli.
 
kaeni hapohapo ukisubiria ajira ukija shtuka ni 2049 alafu unakufa....
Kuna mwenzenu amemaliza 6 mwaka 95 lakini had leo ni tapeli tapeli tu...na ukiangalia miaka hiyo fursa za wazi ni nyingi hasa kwenye mambo ya tech.....

huyo jamaa na musk wote walimaliza pamoja ila musk billionaire na yy tapeli tu....siri ni musk alikataa kuajiliwa akaenda kupambana Ila huyu mswahili akawa kila kazi anayopewa anasema mshara mdogo na hadi leo hajapata hicho anachokitaka we unategemea utajirike kwa mshahara?...ajira ni kifungo cha umasikini vijana.... what's wrong with us Africans???.....
 
Wao walibahatika, ukiwa unasubiri kubahatika, jishughulishe na kazi yoyote.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaaah hali ni mbaya kwa kweli.
Ukiwa na mtaji ni bora ukaangalia namna nyingne ya kuish changamoto ni kubwa
 
nasikia kuna madaktari kibao hawana ajira wapo tu mtaani
 
nyie ndio wanafiki wakubwa eti ajira ni kifungo cha umasikini, mbona kuna watu wanamaisha mazuri wapo kwenye ajira, hivi unazijua changamoto wanazopitia vijana walioamua kujiajiri? Kila mtu angependa kujiajiri lakini katika nchi hii bado hakuna mazingira mazuri ambayo yanaweza kuwawezesha vijana kujiajiri na kua na kiasi kiasi kikubwa cha kutoboa haswa kwa wanaoanza kwa mitaji midogo
 
Kikubwa kila mtu apambane kwa namna yake, hata ukitaka kuwa Tapeli sawa tuh tutakukuta Central....
 
Kwa hio wewe unamiliki viwanda vingapi mpk sasa?
 
Na zinazotangazwa kila leo ni nini? Serikali yoyote duniani haina uwezo wa kuajiri kili mhitimu, hata Tanzania haiwezi lakini kiwango cha kuajiri tulichonacho ni kizuri.
Unazingua. Ajira gani izo zinatangazwa. Kuna Jamaa alitufukuza kazi temple eti tukaombe ajira PSRS. Mpaka leo tupo tunachoma mahindi kitaa.
 
Kuajiriwa ni kujitia kitanzi cha kuwa na uchumi usiosogea kabisaaaa, labda kama umeanza tabia ya udokozi kwenye taasis ulioajiriwa hapo utatoboa lakini bila kuiba hutoboi, utakachokua unafanya ni kuamisha mikopo hadi unazeeka....Ni mawazo yangu lakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…