Tujuzane aina ya manukato (perfume) unayotumia

soleil de jeddah by stephane humbert lucas
pata hii perfume utakuja kunishukuru
 
Nyingi zinazotajwa humu ni bei ghali, wale wenye maisha ya kawaida kama mimi nataka niwape perfume nzuri. Mchanganyiko ninaotumia mimi kila mtu lazima ausifie kuanzia masela ukija kwa wadada na wamama ndio balaa zaidi, almost wote ninaopishana nao lazima wasema nanukia vizuri. Nenda na elfu kumi yako kwenye duka la vipodozi then ulizia perfume inayoitwa Soft ambayo ni 4k au 5k kuringana na eneo utakaloenda baada ya hapo nunua spray inayoitwa Diable Blue kama ukikosa hii nunua spray inayoitwa Monaco. Amini usiamini huo mchanganyiko unatoa harufu nzuri sana.
 
Elfu Kumi, Unanukia Hadi Wanakusifia? Chai Hii 😀
 
nishawah kuchanganya ivo manz mmoja akanambia unanukia kimbuzi mbuzi,au nilikosea mixer
 
leo nimepuliza Lacoste White (for men) naona naopishana nao wanageuka kuniakiki kama ni mtanzania mwenzao au nimetokea kwenye nchi za Corona
Lacoste White ipo vizuri sana, harufu yake ni ile tulivu isiyo na makelele...

Mbadala wake hii unaweza jaribu Calvin Klein euphoria for men, au K-Men ya Dolce&Gabbana au Givenchy Gentleman au Mankind ya Kenneth Cole au pia Mont blanc Legend
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…