Tujuzane: Je, ni samaki gani mtamu kuliko wote?

maji baridi ndo hawa wa kufugwa nyumbani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salam kwenu.

Si mjuzi sana katika nyanja hizi..hivyo naomba kujua

Je, ni samaki gani mtamu kuliko wote? Mtaje !
1. Changu
2. Sato
3. Kibua
4. Sangara
5. Kambare
6. Perege
7. Migebuka
8. Pweza
9. ________
Changu mwenye kidoti wenyewe wanamwita changu_doa
 
Salam kwenu.

Si mjuzi sana katika nyanja hizi..hivyo naomba kujua

Je, ni samaki gani mtamu kuliko wote? Mtaje !
1. Changu
2. Sato
3. Kibua
4. Sangara
5. Kambare
6. Perege
7. Migebuka
8. Pweza
9. ________
mbona umechanganya samaki wa baharini na maji baridi (ziwani)? Ladha yao ni tafauti.

Pia pweza siyo samaki.

Kwa baharini best quality ni jamii ya kingfish (nguru) - nadhani ndiyo akina 'tuna'. Nenda hoteli ukaulizie bei utaona.
 
Nafikiri samaki wa ziwa tanganyika, kwa mzunguko niliofanya hapa nchini ndo watamu zaidi ,mfano :Singa,kuhe ,migebuka nk
 
Huwa nasikia mgebuka ni mtamu sanaa. Sijawahi kumla nitamuonja siku moja nione.
Ila mgebuka wanasema wenyewe watu wa Kigoma upate yule fresh aliyetoka kwenye maji siyo samaki aliyekaa kwenye mafriji wiki
Mgebuka hana maajabu yeyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…