Kwa uowefu wangu katika samaki wote wanao patikana Tanzania. Samaki wa ziwa Tanganyika ni watamu zaidi.
1. MANJE huyu ni Samaki mtamu zaidi kupita wote. Samaki huyu ni nadra sana kuvulika kwani anao ujuzi wa kuruka kutoka katika mtego wa nyavu. Walaji wa samaki huyu hugobe kula eneo la Tumboni ambapo anakua amenona na ndipo patamu zaidi. Tatizo la samaki huyu nyama yake ina miiba mikali sana midogomidogo iliyo katikati ya minafu. Wataalamu humkausha kwa siku kadhaa na kufanya miiba ipotee. huyu ni mtamu kwa kuchoma. Ukifika Kigoma ulizia ukiwa na bahati sana utampata lakini hata wavuvi wanaweza kukaa miaka bila kumla.
2.SINGA Huyu ni samaki jamii ya Kamambale lakini sio Kambale. Huyu Samaki nampa namba mbili. ni mtamu sana na menona zaidi ya kitimoto, wengine humwita Zimamoto kwani ukiwa unamchoma zazima uwe na mkaa wa zaiada kwani moto utaimika kwa urojo wa mafuta. Kuwa makini unapo mla samaki huyu, wengi hujikuta wanaharisha kwa sababu ya kula mafuta mengi ya Samaki singa, sio kama hawajui la hasha ila unapo onja mnofu wa singa ni ngumu kukumbuka swala la kuharisha, kila ukieza unahisi bado haitoshi.
3.KUHE huyu ni samaki mtamu sana Pia anapatikana Ziwa Tanganyika. Ni mtamu ukimla akiwa amepikwa fresh. Huyu Samaki kwa namna alivyo mtamu Waha humuita Kuku wa Bahari au Kuku wa Ziwani. Waha wanao utamaduni kwa kumkirimu mgeni kwa kuku, sasa Samaki huyu huweza kutumika badala ya kuku pia. Kama uko Dar nenda Tegeta Nyuki utakuta waha wanauza Samaki wa Kigoma unawea kumpata Kuhe wa friji angalau utaonja utamu.
4.MGEBUKA huyu ni samaki mtamu ukimpata aliye nona. Kuna wakati wanavulika wasio nona na ladha inapungua.
5.SATO wa Mwanza hawa hao nawapa nafasi ya tano
6.SANGARA/NONZI na NTUBU wa Kigoma hawa nao wako vizuri sana. Nonzi ni safi akipikwa na NTUBU aliwe kwa kuchomwa, huyu Samaki anayo nudu kama ya ng'omba ina mafuta na rojo la utamu
7.Kungura huko Kigoma wanamla akichomwa ni mtamu kumla kwa Chapati