McDonath
Senior Member
- Jan 2, 2018
- 110
- 105
Habari za wakati huu wana jamvi
Jana kulikua na tukio kubwa sana la ugawaji wa tuzo za wachezaji waliofanya vizuri katika timu ya Simba Sports Club
Ikumbukwe tuzo hizi zinafanyika kwa mara ya pili kwa maboresho makubwa tofauti na za mwaka jana ambazo zilikua ndo za kwanza
Kwanza nichukue nafasi hii kuupongeza uongozi wa Simba na wale wote waliohusika na kuandaa tuzo hizi ili kutambua mchango wa wachezaji katika timu ya Simba SC
Lakini kama kawaida kila tuzo hazikosi kasoro isipokuwa kwenye tuzo zenyewe basi zitakua kwenye uandaaji wa tukio lenyewe
Binafsi kwenye tuzo naona waliopata walistahili lakini kwenye suala la aundaaji wa tukio ndo nimeona kasoro kidogo
1:Tuzo ya aina moja kwenye vipengere vyote.
Binafsi kwa ufuatiliaji wangu kwenye masuala ya tuzo sijawahi ona kila kipengere kina aina moja ya tuzo yaani tuzo ya mchezaji bora inafanana na goli bora na ya tuzo ya heshima?
Nadhani haya mambo yapo kwenye miziki na filamu.Nategemea msimu ujao tuzo kama ya mchezaji bora iwe hata na kisanamu cha mtu anapiga mpira kama Ulaya na kwingineko wafanyavyo hata kwenye vipengele vingine kuwe na utofauti wa aina ya tuzo.
2:Tatizo la Kiteknolojia
Hili nadhani ni tatizo ambalo kila mtu angeweza kuling'amua kwa jana maana kuna wakati utakuta ma MC wanaongea huku tunawekewa video ya goli la chama yaani ilikua vurugu,pia suala zima la picha za wachezaji wanaowania tuzo zilikua na ubora mbovu najiuliza walishindwa kuwaandaa wachezaji walioingia kwenye categories wakawapiga picha za HD ili wawe wanazidisplay pale kwenye screen?
Hayo ni miongoni mwa mapungufu niliyoyaona mimi jana kwenye tuzo za Mo Simba Award,Mbali na mapungufu hayo lakini lazima tukiri tuzo zile zilifana sana watu walipendeza,vituko vya hapa na pale.kila kitu kilikaa mahala pake mbali na mapungufu ya hapo juu ambayo najua wahusika watayafanyia kazi kwa msimu ujayo
Mwisho niwatakie kila la kheri Simba sasa natumani mnaelekea kweny suala la usajili na sherehe za siku ya Simba (Simba day)
Nawaamini mtafanya vizuri kuliko mwaka jana .