Tujuzane madhaifu ya MO SIMBA AWARDS

Tujuzane madhaifu ya MO SIMBA AWARDS

McDonath

Senior Member
Joined
Jan 2, 2018
Posts
110
Reaction score
105
Habari za wakati huu wana jamvi

Jana kulikua na tukio kubwa sana la ugawaji wa tuzo za wachezaji waliofanya vizuri katika timu ya Simba Sports Club
Ikumbukwe tuzo hizi zinafanyika kwa mara ya pili kwa maboresho makubwa tofauti na za mwaka jana ambazo zilikua ndo za kwanza

Kwanza nichukue nafasi hii kuupongeza uongozi wa Simba na wale wote waliohusika na kuandaa tuzo hizi ili kutambua mchango wa wachezaji katika timu ya Simba SC

Lakini kama kawaida kila tuzo hazikosi kasoro isipokuwa kwenye tuzo zenyewe basi zitakua kwenye uandaaji wa tukio lenyewe

Binafsi kwenye tuzo naona waliopata walistahili lakini kwenye suala la aundaaji wa tukio ndo nimeona kasoro kidogo

1:Tuzo ya aina moja kwenye vipengere vyote.
Binafsi kwa ufuatiliaji wangu kwenye masuala ya tuzo sijawahi ona kila kipengere kina aina moja ya tuzo yaani tuzo ya mchezaji bora inafanana na goli bora na ya tuzo ya heshima?
Nadhani haya mambo yapo kwenye miziki na filamu.Nategemea msimu ujao tuzo kama ya mchezaji bora iwe hata na kisanamu cha mtu anapiga mpira kama Ulaya na kwingineko wafanyavyo hata kwenye vipengele vingine kuwe na utofauti wa aina ya tuzo.

2:Tatizo la Kiteknolojia
Hili nadhani ni tatizo ambalo kila mtu angeweza kuling'amua kwa jana maana kuna wakati utakuta ma MC wanaongea huku tunawekewa video ya goli la chama yaani ilikua vurugu,pia suala zima la picha za wachezaji wanaowania tuzo zilikua na ubora mbovu najiuliza walishindwa kuwaandaa wachezaji walioingia kwenye categories wakawapiga picha za HD ili wawe wanazidisplay pale kwenye screen?

Hayo ni miongoni mwa mapungufu niliyoyaona mimi jana kwenye tuzo za Mo Simba Award,Mbali na mapungufu hayo lakini lazima tukiri tuzo zile zilifana sana watu walipendeza,vituko vya hapa na pale.kila kitu kilikaa mahala pake mbali na mapungufu ya hapo juu ambayo najua wahusika watayafanyia kazi kwa msimu ujayo

Mwisho niwatakie kila la kheri Simba sasa natumani mnaelekea kweny suala la usajili na sherehe za siku ya Simba (Simba day)

Nawaamini mtafanya vizuri kuliko mwaka jana .
 
sisi yanga bado tupo na msemaji mkuu zahara
 
Mfungaji bora wa timu na mchezaji bora wa timu ameshindwa kuwa mshambuliaji bora, bado naona duble duble.

Niyonzima sawa hakucheza saana(japo kapombe wamemuweka), chama je, amekosekana hata katika wale wa3 waliokuwa wanawania tuzo ya kiungo bora.

Tuzo isiwe ndio kupeana tu, wapewe wanaostahiki hapa kwa boko ni kama wamempa tu sijui kwa sababu yao ipi.
 
mshambuliaji sio kufunga tu kaka
 
1. mchezaji ambaye hajawa NOMINATED kugombea tuzo ya Kiungo bora yupo kwenye tuzo ya mchezaji bora (overall)
2. mlinzi wa kushoto aliyecheza mechi karibu zote na kucheza vizuri tu hajawa NOMINATED ila mlinzi wa kulia aliyecheza nusu msimu yupo
 
mshambuliaji sio kufunga tu kaka
Sikatai hili, nakubaliana nawe mshambuliaji sio kufunga tu, ila sema wewe kwa kipi bocco alimzidi kagere kwa msimu huu, hiyo moja.
Pili! Hushangai mchezaji bora wa klabu, ambae nae ni mshambuliaji, awe mchezaji bora wa klabu ila si mshambuliaji bora, km bocco kamzidi kagere na kuwa mshambuliaji inakuwaje azidiwe na kagere kuwa mchezaji bora kwa ujumla.

Ushawahi kuona wapi T.O anakuwa kaongoza kitaifa ila kwenye shule yake yeye asiwe wa kwanza.
 
1. mchezaji ambaye hajawa NOMINATED kugombea tuzo ya Kiungo bora yupo kwenye tuzo ya mchezaji bora (overall)
2. mlinzi wa kushoto aliyecheza mechi karibu zote na kucheza vizuri tu hajawa NOMINATED ila mlinzi wa kulia aliyecheza nusu msimu yupo
Shangaa na wewe!! Mchezaji bora wa timu ambae ni mshambuliaji, ila si mshmbuliaji bora!!
 
Niliwaambia wadau kabla kwamba the so called uzalendo ndo utatumika kumpa Bocco badala ya Kagere kwenye ushambuliaji. Kiko wapi sasa?
 
Sikatai hili, nakubaliana nawe mshambuliaji sio kufunga tu, ila sema wewe kwa kipi bocco alimzidi kagere kwa msimu huu, hiyo moja.
Pili! Hushangai mchezaji bora wa klabu, ambae nae ni mshambuliaji, awe mchezaji bora wa klabu ila si mshambuliaji bora, km bocco kamzidi kagere na kuwa mshambuliaji inakuwaje azidiwe na kagere kuwa mchezaji bora kwa ujumla.

Ushawahi kuona wapi T.O anakuwa kaongoza kitaifa ila kwenye shule yake yeye asiwe wa kwanza.

Jibu ni rahisi tu, ni kwasababu wamepigiwa kura, ingekuwa wanaangalia number kusingekuwa na haja kuwapigia kura,
Simply kusingekuwa na haja ya kumshindanisha kagere na boko kwa kufuata maelezo yako. Kabla ya kulaumu haya mungeanza kulaumu mfumo uliotumika kuwapata washindi. Watu wameingia kwenye website wamepiga kura, majibu ya maswali yote ni hayo
 
1. mchezaji ambaye hajawa NOMINATED kugombea tuzo ya Kiungo bora yupo kwenye tuzo ya mchezaji bora (overall)
2. mlinzi wa kushoto aliyecheza mechi karibu zote na kucheza vizuri tu hajawa NOMINATED ila mlinzi wa kulia aliyecheza nusu msimu yupo
Uko sawa mkuu.. japo kuna mechi hasa round ya kwanza Zimbwe Jr alisugua benchi kwa Kwasi.
 
Kwanye washiriki wa tuzo ya beki Bora Kapombe hayuko uwanjani muda mrefu ...badala yake angekuwa mohamedi Hussein.
 
Back
Top Bottom