Tujuzane mbinu wanazotumia matapeli kuwatapeli wafanyabiashara za miamala ya kifedha

Tapeli dronedrake mzigoni 😁😁😁😁
 
Ilikua hivi, ni miaka kadhaa sasa Jamaa alikuja Dukani alinipa Pesa kama Milioni 1 nimuwekee katika Tigo Pesa..... akanipa nikazihesabu ila akaghairi akasema nimuwekee katika Zantel ilihali anajua kabisa Tanzania bara huku Zantel ni kupengere... nikamwambia hiyo sina.... akasema basi naomba hizi Hela... nikampa, mara Simu yake ikaita akapokea akasema HUYU ZANTEL HANA LABDA NIKUWEKEE KATIKA TIGO TU, akanirudishia zile Hela akasema weka katika Tigo tu.... laaahaulaaaaa!!!! Kumbe alishazibadilisha na alikua na Vibunda viwili... kimoja Elfu kumi kumi ambazo alinipa mwanzo na kibundq kingine kilikua Elfu mbili mbili nyingi ila zimefunikwa na Elfu kumi kumi nami sikuzihesabu.... nilivyomuwekea kumbe ana namba za Wakala, Nilivyoweka tu akazitoa muda huo huo.....
 
Duh 🙄
Duniani hakuna huruma
 
😃 😃 Hapana
Niyo mbinu ni active sana kwenye mitandao ya simu kama tigo,airtel na halotel ila voda ni ngumu maana voda ukikosea mualama wanakusubirisha hadi masaa 12 kukurudishia pesa yako.
Hiyo yote ni kuwa na uhakika kama kweli pesa imetumwa kimakosa ikiwemo kumpigia aliyetumiwa kimakosa.

Big up kwa vocodam.
 
Kuna hii tapeli anamtu mtu wa jiran sana na wakala
Anachukua simu ya wakala anaandika namba ya tapeli kisha anasave M.pesa au Tigopesa
then tapeli anakuja siku mbili tatu mbeleni na txt iliotumika ya M.pesa Anaedit muda na tarehe


Wakala ukiwa na haraka ukiifungua tu simu unaona imeandikwa mpesa..unampa pesa tapeli ....na ww unakuwa ushaenda kibla
 
Ni mpumbavu pekee ataibiwa kwa mbinu hii kwa sababu Salio baada ya mamala lazima libadilike
 
Hiii sululisho lake wakala mteja yoyote akitoa pesa kubwa inatakiwa ajilidhishe kama ni mhusika mwenyewe.kwa kuangalia utambulisho wa muamala tarehe saa na msg kama ameforwadiwa .
 
Hii pia nilipigwa bahati nzuri haikuwa kiasi kikubwa
 
sahihi kabisa
Mimi nafanya hii kazi ..nikiona mteja katoa kuanzia laki tano na kuendelea nachofanya na mwambia mteja sijaona msg yake..naomba simu yake nijiridhishe ..hapo nakagua tarehe utambulisho na msg kama sio ya kufowadiwa...then narudi kwa simu yangu kuangalia salio nililokuwa nalo mwanzo na lililoingia sahizi kama ni sahihi.ndipo nampa pesa yake.mara nyingine nikiwa na stress huwa nafunga frem naenda zangu home kulala ili kuepusha majanga zaidi.kazi hii akili yako ina bidi iwe hatua kumi ya mteja umzidi mteja akili.na usifanye mazoea na watejaa
 
Huyo kiboko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…