Tujuze umeanza kutumia JamiiForums tangu lini? Ni kipi kilichofanya ukavutiwa na JF?

2013 nilivutiwa na MKUU P.Mayalla, Joka Kuu, Elly bila kumsahau MKUU KIRANGA baadae nikawa nacheka na post za Mr.POPOMA as Genta
 
Umesema maneno mengiiiii ila hujajibu swali!???? LINI ULIJIUNGA NA JF!???
Mfano
Q 1: Lini Ujerumani ya Wanazi ilianguka
A: Baada ya kushindwa vita ya pili ya dunia
Q 2: Mwaka gani Ujerumani ya Wanazi iliangushwa
A: 1945

Swali limeniuliza lini, sio specifically mwaka gani. Well ilikuwa 2017
 
2013 nilivutiwa na MKUU P.Mayalla, Joka Kuu, Elly bila kumsahau MKUU KIRANGA baadae nikawa nacheka na post za Mr.POPOMA as Genta
Mkuu, humu vipo vichwa vingi sana! Pia, nami nilikuwa napenda sana kumuona Le Mutuz. Cha kufurahisha, akichangia chochote, hata kama uzi hajauanzisha yeye, wachangiaji wanahama kuchangia kilicholetwa, wanaanza kujadili yake, na kumjadili yeye binafsi.
Nikajifunza kitu kutoka kwake, uhimilivu wa maneno yasiyo na staha. Hachokozeki huyu mtu!. Nimesoma mahali kuwa anaumwa, amepelekwa hospitali ya Apolo India. Hebu tumuombee apate matibabu ya mafanikio, na apone haraka!
 
😃😃😂Story za Le Babaz nilikuwa nilikuwa Sina hobby nazo Sana.

NGUVU YA KIROHO by Pascall Mayalla
MUNGU HAYUPO by KIRANGA

Historia ya nchi yetu na siasa by Elly na JokaKuu

Elly hasa kwenye mambo ya dini.

Saizi JF tunatrend na KULA TUNDA KIMASIHARA.


Nakumbuka braza Pascal Mayalla alishawahi niambia mind set aiseeee nilimmaind vibaya nilitaka kumtukana badala yake nilijiondoa Jf nikabak msomaji.

Ila baada ya kusoma NYUZI ZA MR.POPOMA as GENTA nikajua ndani ya usiriasi Kuna utani.

Ndipo nakaanza kushinda Jukwaa la intelejensia😃
 
mie biashara tu JF imenitengenezea network kubwa zaidi kwenye biashara zangu kulinganisha na mitandao mingine
sikumbuki hata nilijiunga vipi
 
Nakumbuka kipindi cha nyuma hivi 2006 tulipata kupokea ujumbe shuleni (primary) kwetu walikuja wageni waka jitambulisho kua wao wana toka jambo forums na kuna vipeperushi viliachwa kwa walimu wetu lakini nikawa nakumbuka tu hile neno Jambo forum baadae 2010 wakat nime maliza olevel na tayari nilikua namiliki simu janja ndo nikaanza kutafuta jambo forums kuijua zaidi hii ika nipelekea kuijua sasa jamii forum(2010) ambapo nilikua naperuzi kama Guest user mpaka pale 2013 ndipo niliweza kujiunga Rasmi kama mwanachama wa huu mtandao since then sijawahi kuacha kuitumia JF kwa hakika JF ime nifunza mengi mengi sana.... pongezi nyingi zifike kwa Max na Mike Mushi kwa kuweza kuleta huu mtandao wetu pendwa.
 
Daaaah, kuna watu wanatoa mafunzo ya uvumilivu, na upambanaji! Huyu Genta, aweza kushambuliwa na watu kibao. Lakini hatoki kwenye mstari, na kila aliyemshambulia, anapata vidonge vyake stahili.
Kwa kweli, hapa JF kuna walimu wa kila aina! Ni zaidi ya shule hapa!
 
Sikumbuki lini ila kuna documents nilizisave za JF za 2008 wakati napitia news online...ilikuwa za ufisadi alioibua Dr Slaa.
 
Nilijiunga mwaka 2008, miaka 13 iliyopita.
 

Kwa sisi ambao tumetoka katika familia ambazo hazina utani utani hapo ngumi za uso fasta.😃
 
wakati huo tulitesa sana. kulikuwa na mwamba aliiitwa Malaria Sugu alikuwa kama kigogo wa twitter. sijui ilikuwaje yule mwamba
Wengine tulikuwa wasomaji tu Kama sehemu ya kupata habari tu😃
 
Le mutuz yule wa instagram?
 
ID YANGU YA KWANZA ILIKUWA 2010... nikasahau nywila na sikuweza kurecover.... ya pili 2015 nayo nilisahau nywila na hii hapa 2017
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…