Tukiacha Unazi tuwe wakweli, je ni nani anayechezea Brand ya Simba hivi sasa bila makubaliano ya kimkataba yenye uwazi na yanayoeleweka?

Huo mkataba uliona wapi? Na hiyo ela ndefu ni kiasi gani? Kusema ela ndefu bila kutaja figure maanake hauju lolote umehisi tu. Tuambie huo mkataba ulisainiwa lini na kiasi gani kililipwa. Ndio maana mleta mada kasema uwazi uwepo
 
Nafikiri wewe akili yako ni ndogo , mwaka. Juzi hii sabuni ilipokuwa inaingia mkataba pamoja Mo energy ulikuwa bado unanyonya
 
Mkuu kuna vitu ambavyo mnachanganya. Moo hajaja Simba kufanya hisani bali ni kufanya biashara na ndio maana ya mwekezaji. Hivyo kufanya usajili mzuri na kuweka mazingira mazuri ya timu ni moja ya majukumu yake ili apige pesa/ kupata faida kupitia uwekezaji wake. Unataka kusema kuwa kwavile mtu alikuwa hana uwezo wa kula, kulala na kuvaa vizuri kisha akatokea mtu akakupa kibarua cha kuwa unasafisha garden. Huyu mtu ikitokea anataka kukuingilia kimwili utakubali tu kwavile kakutoa kwenye hali mbaya si ndiyo?

Kitu kikubwa kwa Simba ni lile wazo la timu apewe mwekezaji, hilo ni wazo kubwa ambaye hata asingekuwa Moo leo hii angekuwepo mwingineyo ambaye pengine angefanya makubwa zaidi ya Mo kwenye upande wa mafanikio hatuwezi jua. Ila kikubwa kwa miwekezaji ni kufuata utaratibu sio kwavile anapesa basi ni kufanya atakavyo. Kumbuka Simba ni brand hivyo brand ya Simba ni kubwa kuliko mwekezaji. Kwanini mnawaza kinyonge hivyo wakati Moo anaitaka Simba zaidi ya Simba inavyomuhitaji Moo na ndio maana mchakato wa uwekezaji haikuwa wazi katika kuwapa nafasi wengine wanaotaka kuwekeza Simba.

Moo akiondoka Simba, Simba kama wataendelea na vision ile ile ya kumpa mwekezaji haipiti miezi miwili pasipo kupata mwekezaji mwingine. Je Moo akiondoka Simba anaweza kupata brand iliyokuwa kubwa kuzidi Simba ukiiweka kando timu ya Yanga?
 
Mo yupo Simba kiupigaji, yupo pale kuvuna tu, maana mashabiki wa Simba ni watu duni na upeo mdogo. Wao watakwambia wanapata vikombe vya ubingwa, sasa kwanini wahangaike kumsumbua Mo.

Akili zitawakaa siku wakikosa ubingwa.
Na gsm yupo yanga kwa lengo lipi
 
"Kwani wachezaji unawalipa wewe mshahara? Wewe umeichangia simba shilingi ngapi ili ijiendeshe? Tuachie timu yetu. Sisi tunachotaka ni makombe tu na ubingwa wa TPL!"

Alisikika shabiki mmoja hivi.
 
Huyo mwingine alikuwa wapi mpaka MO amekuza brand kwa pesa yake mfukoni?
MO aondoke aende wapi? Zile hisa zake amuachie nani?
Kama kuna mtu anawaza MO ataondoka basi atafute kazi ya kufanya?
 
Kwenu kosa la Mo ni kuwekeza Simba SC, hakuna kingine, ile Simba ilikuwepo pale miaka yote hakuna yeyote kati yenu aliekwenda kusaidia hata chapati moja asubuhi wachezaji wanywe na chai. Leo kaja Mo, klabu bingwa Afrika robo fainali, makundi imekuwa kawaida, ndio mnaibuka na kelele zenu.

Hiyo habari ya kubakwa sijui kufanywa hapa haihusiani kabisa, acheni kelele Mo afanye aliyokusudia kuyafanya Simba SC, maneno yake tunayaona uwanjani yakitendeka timu imebadilika sana toka aje na viwango Afrika imepanda, nyie na hizi kelele zenu mnaonekana kama wachawi tu msiopenda maendeleo ya watu.
 
Subiri uje kutukanwa
 
Kwamba utopolo ndio mnaupeo sana sio ,hapo huwezi walaum simba laam malaka za nchi wao ndo wamekubal yeye kukaa hapo kabla ya mo simba ulikua wap?
Utopolo mwaka Jana tu kwenye jezi wamepata mil 45 ,hao misukule hawana lolote ,jezi tu wanapigwa na GSM
 
Hapo huna la kujibu tena maana umetandikwa na facts
Daah nchi hii ngumu sana, hivi huoni mimi nilikuwa namuelewesha mdau hapo juu kuhusu concern ya mtoa uzi?
Huoni nimemalizia kuwa hata mimi sijui chochote?
Ukilaza huu ndio maana nchi haisongi..
Unazi unazi kila pahala.
 
Watu wa mpira muko vichwa ngumu, ni ushabiki tu. Mo hana mikataba, Azam hana mikataba, Harsi hana mkataba, muwe mnatizama na kwenu. Nakuzindua ili useme kama umewahi kuona mkataba wa Gsm


Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
Azam usifananishe na Simba na yanga ,ile ni timu ya familia
 
Huo mkataba uliona wapi? Na hiyo ela ndefu ni kiasi gani? Kusema ela ndefu bila kutaja figure maanake hauju lolote umehisi tu. Tuambie huo mkataba ulisainiwa lini na kiasi gani kililipwa. Ndio maana mleta mada kasema uwazi uwepo
Mkuu we ni mpumbavu ,hivi mikataba huwa inaonyeshwa?hapo umepewa facts Hadi waandishi wa habari wameitwa ,bado unataka uone mkataba we ni Kama nani uone kwenye bodi ya Simba,ingekuwa hivo basi wachezaji wangekuwa wanapost mikataba yao Facebook .Hivi hata mikataba ya serikali we unaziona ?hata ungeambiwa hela ni kiasi hiki bado utataka ushike shike Kama siyo feki ndo maana nimesema we ni mpumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…