Tukibaki Hai, Tutasimulia

Tukibaki Hai, Tutasimulia

Tayukwa hii ushaisoma??? Ni nzuri sana japo ina matukio mengi mengi na episodes zake ni ndefu sana!! Ila nzuri mnooo
 
Well done. Vipi umeipenda? Umejifunza nn?
Nimeipenda sana hadi natamani Hata saii Steve aimalizie!!
Humu bwana mafunzo ni mengiiii.... kwanza The power of 💰💰💰💰💰 pili usnitch aisee trust no one...watu wako wa karibu usiowadhania ndio wanaokumalizaa chini chini..tatu ishi kivyakoo watu wasikujue kabisa au uwe na changing behavior wasikusome . Nne point yako ya weakness watu ndio wanaitumia kama strength yaooo... na mengine mengi mengi
 
Huu ni upumbavu kabisa kwann ulete story alafu iishie njiani kama hukutaka kuleta uache hakuna mtu wa kuja kukutafuta ulete story ni kiherehere chako tu
 
yani jaman hadi siku Steve arudi itabidi na mimi nirudie post yake ya mwisho kujikumbusha tulipoishia
Hahaha.. Mimi nitakumbuka tu kuwa Mitchelle yuko mikononi mwa Dr Lambert kwasasa Hana ujanja tena!! Afanye aje kuimalizia hii kwanza jamani !!
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 09


Na Steve B.S.M



New York Police Department, New York.


Saa tano ya asubuhi.



Mpelelezi alikuwa anahisi maumivu ya kichwa. Alifungua kikopo kidogo chenye vidonge vingi vyeupe ndani yake, akajiwekea vidonge vitatu kwenye kiganja chake na kuvibugia bila maji.

Tangu asubuhi ya mapema mpaka sasa, alishakunywa vidonge vinne vya kukata maumivu. Kichwa kilikuwa kinapoa na kurudi tena kwenye makali yake.

Akiwa amekaa, nguo alizovalia ni zilezile alizokuwa nazo kwenye kumbi ya kamari jana yake, alishika paji lake la uso akilijaribu kulikandakanda na vidole viwili, gumba na kinachofuatia.

Alijaribu kukumbuka nini kilitokea lakini hakupata picha kamili. Kitu pekee alichokumbuka ipasavyo ni yale yote yaliyoishia pale alipopanda gari lake tu. Baada ya hapo alikuja kukurupuka asubuhi baada ya kugongewa kioo na mtu anayehusika na 'parking'.

Kichwa chake, alichokuwa anahisi ni kizito, hakikumpa majibu aliyokuwa anataka. Baada ya kufikiri sana aliona ni bure. Aliamini mapigano yale, baina yake na wacheza kamari, ndiyo yalimuathiri kiasi cha kujikuta anapoteza fahamu.

Alijinyoosha mwili akiugulia maumivu ya viungo. Alishika simu yake akitazama jambo, punde mtu akaingia. Alikuwa ni yule bwana, mtaalamu wa michoro. Mkononi mwake ameshikilia bahasha.

Walipeana salamu kisha bwana huyo akampatia Mpelelezi bahasha ile alokuja nayo akimwambia ni ile kazi alompatia.

"Nadhani itasaidia kwenye upelelezi," bwana huyo alisema kisha akajiendea zake.

Ndani ya bahasha kulikuwa na karatasi tatu. Karatasi moja ilikuwa na mchoro halisi, uliochorwa kwa penseli ya mkaa, wakati zingine mbili zikiwa ni nakala vivuli.

Mpelelezi alitazama michoro hiyo kwa umakini, kwa kama dakika mbili hivi, kisha akavuta droo ya meza yake alimotoa bahasha moja yenye picha mbili.

Picha za Ferdinand.

Aliwianisha picha hizo kwa macho yake ya kazi.

Aliona kuna uwiano ndani yake.

Mabega ya mhusika, mtindo wake wa nywele na hata umbo la fuvu la sura yake vilikuwa vinafanana. Kwa sura ilikuwa ni wastani, ila umbo hili la mwili lilikuwa ni sawa sawia.

Aliziweka picha hizo mezani akiwaza jambo la kufanya.

Kichwa kilimuuma. Kila alipojifikirisha aliona anayatibua maumivu. Alitazama saa yake ya mkononi. Alikata shauri kwenda kujipumzisha.

Aliweka vitu vyake vizuri ndani ya droo alilolifunga na funguo baada ya kuvipiga picha na simu yake kisha akanyanyuka kiuzito toka kitini.

Hajapiga hatua, simu yake iliita. Alikuwa mtu wa kitengo cha taarifa na uchambuzi. Alimwambia ana taarifa kuhusu ile picha ya mwanamke alompatia.

"Njoo ofisini," Mpelelezi alisema akirejea kitini. Muda kidogo, mgeni wake alifika hapo. Alikuwa ni yuleyule aliyepewa kazi hiyo, afisa mnene anayevaliwa miwani.

Alimweleza mpelelezi kuwa picha ile ilikuwa ni ya binti wa huko California. Mwanafunzi wa chuo ambaye aliwahi kujimaliza uhai kwa kujinyonga miaka miwili iliyopita.

"Alijinyonga?" Mpelelezi alirudia kwa kuuliza.

"Ndio," alijibu bwana huyo kwa uhakika. "Kwa mujibu wa taarifa, alikuwa anasumbuliwa na sonona."

"Sonona?"

"Hakuwa mtu wa marafiki. Alikuwa anaishi peke yake. Muda mwingi alikuwa mpweke hata kwenye mazingira ya watu wengi darasani."

Mpelelezi aliitazama ile picha kwa kuirudia. Alimsihi afisa huyo aendelee kutafuta taarifa zaidi kumhusu huyo mtu. Endapo akipata familia au watu wake wa karibu itapendeza zaidi.

"Sawa, nitajitahidi," alisema bwana huyo akaaga. Kidogo mpelelezi akawa amesahau dhamira yake ya kuondoka. Alipata cha kuwaza. Alijiuliza nini mahusiano yaliyopo baina ya mwanamke yule anayemtafuta na huyu aliyejinyonga.

Kichwa tu kilimuuma.

Aliona ni kheri anakili taarifa hizi kwenye tarakilishi yake iliyokuwepo mezani, muda akili yake itakapotulia basi afanye jambo kwa umakini.

Akiwa ananakili, pia ameona atoe na zile taarifa kwenye droo apige picha na kutunza, simu yake iliita. Alikuwa ni mkuu wake wa kazi katika kitengo hichi cha upelelezi.

Alipokea akapewa taarifa kuwa anahitajika ofisini mwa mkuu maramoja. Aliacha kazi yake akaelekea huko.

Alifungua mlango wa kioo uliopachikwa cheo cha aliyekuwemo ndani: 'Chief of Detectives'. Macho yake yalitua kwa wageni wawili waliokuwa wamevalia suti nyeusi maridadi. Mmoja alikaa upande wa kushoto, mwingine akiwa amekaa upande wa kuume wa mkuu.

Kati ya watu hawa, mmoja hakuwa mgeni machoni mwake. Akili yake ilimwambia anamfahamu mtu huyo japo hakukumbuka alimwonea wapi.

Alisalimu kisha akaketi. Macho yalimtazama tena yule mwanaume ambaye si mgeni kisha yakahamia kwa mkuu wake, mwanaume wa makamo ya miaka hamsini, kichwa chake kina uwaraza mpana, nywele zikibakia juu ya masikio tu. Macho yake ya kahawia, uso wenye taya pana na sharubu nyeupe.

Mkuu alimtambulisha mpelelezi kuwa wale watu wawili walikuwa hapo ni wageni wake. Wapo hapo kwaajili ya kesi ya mauaji ya The DL.

Hakujua ni nini ila hapa ndo' Mpelelezi alijikuta anamkumbuka bwana yule aliyekuwa anamshuku anamfahamu muda wote huo.

Huyo bwana alikuwa ndiye yule aliyemsaidia kwenye mapigano kule kwenye ukumbi wa kamari.

Alimtazama tena.



SIKU YA NYUMA:


Gari 'tinted', aina ya Chevrolet Suburban nyeusi, iliyokuwa imeegeshwa katikati ya jiji la New York majira haya ya asubuhi, ilikuwa imebebelea watu watatu waliokuwa wamevalia suti nyeusi; mmoja alikuwa dereva, amekaa peke yake kiti cha mbele, wawili walikaa nyuma.

Kati ya hao wawili waliokuwa nyuma, mmoja wao hakuwa mgeni machoni petu. Kuna mahali tulipata kumwona.

Mwanaume huyo, kwa macho kamili, alimuarifu mwenziwe wa pembeni kwamba wamepata vielelezo vya kuanzia na amepanga ndani ya siku hiyo kuonana na mhusika uso kwa uso, ikiwezekana kufanya maandalizi ya makutano yao ya baadae.

Bwana yule mwingine wa pembeni, ambaye alikuwa mtulivu sana, mwanaume wa makamo ya miaka arobaini aliyevalia miwani isiyokuwa na fremu za kuonekana, macho yake ya kulegea yalikuwa yanatazama picha alizokabidhiwa.

Picha za Mpelelezi, akiwa katika mazingira tofautitofauti, zilikuwa pomoni, lakini pia picha kadhaa za Ferdinand.

Picha moja ilimwonyesha Ferdinand akiwa katika tukio lile la Afisa Parker kukutwa akiwa amekufa ndani ya gari mjini. Picha ya pili ilimwonyesha bwana huyo akiwa karibu na makazi ya Afisa Parker. Picha ya tatu ilimwonyesha akiwa karibu na moja ya kumbi za kamari.

Yule bwana, ambaye si mgeni, alieleza ya kwamba wakati wanamfuatilia Mpelelezi walibaini Ferdinand naye alikuwa kazini. Bila shaka alikuwa katika misheni inayohusu kesi yao ya The DL kwani wahusika alokuwa anawafuatilia ndo' wale wanaoshikilia kesi.

Lakini kwa tukio hilo, ilikuwa rahisi kumfuatilia bwana huyo, mara mbili, japo mara zote hizo hawakufanikiwa kubaini makazi yake halisi. Hawakufahamu namna alivyowapotea. Mara ya tatu, ndipo walitekeleza agizo la kumfyatulia risasi kama ilivyoamrishwa.

"Kulikuwa na haja gani ya kufanya vile?" Aliuliza bwana huyu aliyekuwa anatoa taarifa. Mwenziwe alimtazama kisha akaurudisha uso wake kwenye picha.

"Ni mbinu ya kumwondolea utimamu kwenye mipango yake," alijibu, akaongezea; "Shambulizi huathiri umakini wa mtu. Hatujui wamepanga nini. Kwa kupitia tukio hilo watajua wamefahamika hivyo watalazimika kuchukua hatua upesi. Upesi na uholela ni ndugu wa karibu. Tunategemea itakuwa kamari nzuri kuwapata wengine."

"Haudhani tukio hilo linaweza kuwafanya wakaongeza umakini kwenye kujificha?"

"Kati ya haya mawili, moja likifeli, lingine litazaa matunda ama yote kuzaa kwa wakati mmoja. Endapo wakiongeza umakini wakajificha zaidi, basi kazi ya mpelelezi itatupa nyavu. Kwa harakati zake, naamini kuna ambayo hatuyafahamu. Hicho ndo' tunakihitaji ... kwa picha hizi, ni rahisi kuaminika kuwa Ferdinand alihusika na mauaji ya Parker na pia kuthibitisha yu mbioni kumuua Mpelelezi."

Bwana huyo alimalizia kwa kutoa amri ya kazi, mwenziwe akashuka kwenda zake kisha yeye akaendelea kufanya pembuzi wa vile vyote alivyokuwa navyo mkononi.

Alishika 'microchip' na 'tube' yenye kimiminika cha kijani, akavitazama.

Vitu hivyo ndo' vile alivyopokonywa Ferdinand baada ya kupigwa risasi siku ile.

Alichomoa simu mfukoni mwake akapiga. Aliongea na simu hiyo gari likienda.


MUDA WA SASA:


Mpelelezi alitazama bahasha aliyokabidhiwa na mkuu wake wa kazi. Ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na picha za bwana Ferdinand, picha akiwa kwenye yale maeneo yanayoshukiwa kwa mauaji.

Akiwa anazitazama, mkuu wake alimweleza ya kwamba bwana huyo ndiye mhusika wa mauaji ya Afisa Parker na wageni hawa wamekuwa wakimfuatilia kwa muda sasa.

Aliamriwa kuwapatia mabwana hao yale yote aliyofanikiwa kujifunza kwenye kesi hiyo. Hilo ni agizo toka ngazi za juu za usalama.

Yaliongelewa mengi lakini Mpelelezi huyu alikuwa na maanani madogo sana. Mengine hakuyasikia. Mengine hakuyaelewa. Kichwa hakikuwa sawa. Kuna muda alihisi kelele tu masikioni. Alitamani muda uishe ajiendee zake.

"Mpelelezi, uko sawa?" aliuliza yule bwana mwenye uso mchanga. Mpelelezi alifunga macho yake kwanguvu akasema kichwa kinamsumbua kwa maumivu makali.

Katika hali hiyo, wale mabwana walisihi aweke sahihi kwenye makubaliano ya kazi ambayo walikuja nayo ili wapishe ratiba zingine kuendelea.

Kwa kutaka kupumzika, Mpelelezi aliridhia aliyoambiwa. Alipomaliza, alitoka akajiendea zake ofisini kwake alipokaa kwa muda mfupi kabla hajatoka kufuata gari lake.

Nje alikutana na yule bwana aliyempa mkono wa msaada jana yake usiku. Alikuwa amesimama kando ya gari yake akimngoja.

"Nimefurahi tumekutana tena," alisema bwana huyo kisha akatabasamu kwa mbali. "Natumai tutasaidiana na kwenye hili, sivyo?"

Mpelezi alimtazama bwana huyo kwa macho malegevu yenye uchovu. Alikuwa anajivuta akiufuata mlango wa gari lake

"Nilikuuliza wewe ni nani ukaniambia ni mwanasanaa wa mapigano."

"Unadhani pale palikuwa sehemu salama kueleza kazi yangu? Hata wewe usingeniambia kama ni mpelelezi!"

Mpelelezi alifungua mlango wa gari, bwana huyo akamzuia. Alimwambia hayupo katika hali nzuri ya kiafya, angeomba amsaidie kumwendesha kwenda nyumbani.

Mpelelezi alisita lakini kwa namna alivyokuwa anajisikia, na bwana yule akimsihi jambo aliloliona ni la kweli, alikata shauri la kuketi sehemu ya abiria akimpatia mgeni usukani.

Wakiwa njiani walizungumza mengi.

Mengi ambayo kama Mpelelezi angekuja kuulizwa hapo baadae, si ajabu asingekumbuka hata.


***


Brookhaven, New York.


Kitongoji cha Upton. Maabara ya Taifa.


Saa kumi jioni.



Dr. Lambert alijitahidi kutembea kwa upesi akitazama nyuma yake mithili ya mtu anayehisi kukimbizwa. Mkono wake wa kuume alikuwa ameukunja ngumi, akiutupa huku na kule kulifuata gari lake kati ya mengi yaliyoegeshwa hapa.

Alikuwa amevalia suruali ya kitambaa, rangi kahawia, na shati la sufi la mikono mifupi.

Alipojiweka kwenye gari, alihema kwa mikupuo kwanza kuikamata pumzi yake kisha akatulia akitafakari. Alihakikisha ame-lock milango na kufunga vioo vya madirisha. Alitulia humo kwa kama dakika nne hivi, tuli kama maji ya mtungini.

Kuna kitu kilikuwa kinamtatiza.

Alitazama kwenye vioo vya gari lake kama kuna mtu anakuja ama yu karibu naye. Hakukuwa na mtu. Alikuna kichwa chake chenye mvi akatulia.

Kidogo aliandika namba kadhaa kwenye simu yake akapiga. Simu ilipokelewa baada ya muda mdogo. Alikuwa ni mwanamke upande wa pili.

"Kwanini hamkuniambia?" alifoka. "Haya yote mlikuwa mnayajua lakini mkakaa kimya. Mnataka kuniweka kwenye hali gani?"

Mzee huyo aling'aka kwa namna gani usalama wa maisha yake ulivyokuwa hatiani.

Alieleza namna alivyohojiwa kwa masaa mawili na maafisa usalama, siku hiyo baada ya kazi, kwasababu ya kukamatwa kwa kemikali nyeti ambayo inaaminika imetoka kwenye maabara yao.

Alijipambanua kuwa hali si shwari. Kwaajili ya usalama wake, inabidi mawasiliano baina yao yasitishwe kwa muda ama itafutwe njia mbadala kwani baada ya tukio hilo watakuwa chini ya uangalizi mkali.

"Kila mmoja amehojiwa kwa nafasi yake," alipaza sauti. "Sifahamu wenzangu wamesema nini. Ofisi zetu zimekaguliwa na marejeleo ya kamera yamefanyika siku nzima. Kwa lolote likalonitokea basi mfahamu kuwa mkono wenu umehusika."

Alikata simu kisha akatoa 'line' aliyoitupa baada ya kuitafuna mara nne.

Alitazama tena usalama, alipoona ni shwari akaendesha gari kuelekea getini. Huko alikuta walinzi wawili wakiwa wamesimama, mmoja anaongea na 'radiocall' wakati mwingine akiwa anafanya ukaguzi.

Huyu anayefanya ukaguzi alisogelea gari akatazama dereva. Alipohakikisha ni mtu anayefahamika, alimpa ruhusa aende zake.

Kabla hajasogea mbali, yule mlinzi aliyekuwa anaongea na 'radiocall' alisimama njiani akawonyesha ishara ya kumtaka asimame!

Moyo ulimpasuka kisha ukaanza kwenda mbio.

Alimtazama mlinzi huyo akiwa anamjongea, bado anaongea na radio call yake.

"Ndio, afande ... sawa, over."

Mlinzi huyo alimtazama mwenzake akamtikisia kichwa kwa ishara kisha akamtazama Dr. Lambert kwa macho ya udadisi. Dokta alimuuliza kama kuna shida lakini hakusema neno. Uso wake ulikuwa umefinyana kwa ndita.

Alitupa macho yake huku na kule ndani ya gari la dokta huyo.

Alitazama kwa umakini sana.

Alipoona haijatosha, alimwamuru mzee huyo ashuke na kusimama kando.

"Ni vema mkaniambia shida ni nini, vijana. Pengine naweza nikawasaidia."

Bwana yule mwenye radio call hakutaka maneno. Alichofanya ni kurejea amri yake kwa mkazo kisha akasimama kwa lolote litakalojiri.

Dr. Lambert alitetemeka. Alikabwa na hofu kali. Alishuka kwenye gari, kama alivyoamriwa, akasimama kando akishuhudia. Aliweza kukaza mikono lakini ungetazama miguu yake ungeona namna gani inavyogongana.

Alihisi huu ni mwisho.

Walinzi waligawana majukumu kila mmoja akishika upande wake. Gari lilikaguliwa chini, kwenye viti na kwenye madroo yake. Hakukuwa na kitu.

Mlinzi yule mwenye radiocall alipata wazo fulani. Alifungua kile kidude kinachokaa juu ya kichwa cha dereva kikishushwa kusaidia kukabiliana na mwanga mkali wa jua unapomulika machoni.

Humo alikuta karatasi nyeupe zilizochoka, tano kwa idadi. Alizichomoa akasimama kuzikagua kwa macho makali.

Alizitazama karatasi hizo huku akiibia kumtazama Dokta. Alipomaliza, alisonga kando kidogo akawasiliana kwa kutumia radiocall yake. Dokta alimuacha na mlinzi mwingine.

Alipoongea kidogo, Dokta asisikie nini kinachozungumzwa, alirejea akasema,

"Tafadhali, dokta naomba tuongozane."

Dokta alihisi miguu yake inapoteza nguvu.


***
Duh! Ishanilevya sasa
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 10


Na Steve B.S.M




Dr. Lambert aliingizwa ndani ya jengo, akiwa ameongozana na walinzi wawili, mpaka kwenye ofisi ya mkemia mkuu.

Aliingizwa ndani ya ofisi wakati karatasi ile aloyokamatwa nayo akikabidhiwa mkemia mkuu kwa ajili ya utambuzi.

Alikaa hapo, chini ya ulinzi, kwa muda mchache kabla ya mkemia mkuu hajaungana naye kwaajili ya maongezi machache.

Mkemia huyo, mwanaume aliyechongoka mabega na uso, nywele nyeusi zilizokuwa shaghalabaghala na miwani kubwa ya macho, makamo ya umri wake ni arobaini na tano, alimtazama Dr. Lambert kwa macho yake mapole.

Alifikichafikicha mkono wake wa kushoto kama mtu anayenawa mikono. Alitengenezea miwani yake usoni alafu akashusha pumzi ndefu. Ni kama vile alikuwa anatafuta mahali pa kuanzia.

Walinzi walikuwa wamesimama wakiwatazama. Sio wale wa getini tena, ni wengine waliovalia suti nyeusi. Mmoja ana miwani meusi na kifaa cha mawasiliano sikioni.

Mkemia alimuuliza Dr. Lambert kuhusu taarifa zile kwenye makaratasi ambayo yametolewa katika gari lake.

Alimuuliza Dokta huyo ni vipi taarifa hizo zilikuwamo katika usafiri wake holela na nini zilikuwa lengo lake.

Dr. Lambert, akiwa anajitahidi mno kupambana na hofu yake, alieleza ya kwamba taarifa hizo ni za kitambo sana, hilo linaweza kuthibitishwa na ubora wa karatasi zenyewe, lakini pia hazihusiki na lolote lile kati ya yale yanayotuhumiwa na maabara na usalama.

Aliziweka karatasi hizo muda akiwa anapitia rejeleo fulani la kisayansi kisha akasahau kuziondoa hapo.

"Ni makosa tu ya kibinaadam. Hamna cha ziada."

Maelezo yake yote yalinakiliwa, pia yalikuwa yanasikilizwa na watu wengine wa usalama kwa upande wa pili.

Mkemia alirudia maswali yake kama kuna litakalobadilika lakini hakukuwa na jipya. Bado Dr. Lambert alishikilia hoja yake ileille.

Mkemia alipiga simu yake ya mezani, punde akafika mtaalamu mmoja wa maabara aliyempatia makaratasi ya Dr. Lambert na kumwambatanishia kazi ya kufanya.

Baada ya robo saa, bwana huyo alipiga simu. Alishamaliza kazi. Mkuu wake alisikiliza ripoti yake alafu akapiga simu kwa mkuu wa usalama.

"Hamna jambo."

"Kivipi?"

"Taarifa haziwiani ... hakuna ushahidi wa yeye kuhusika moja kwa moja na ile kemikali. Formula zilizopo kwenye karatasi ni tofauti kabisa na zilizotumika kutengenzea ile dawa."

"Kwahiyo nani anahusika?"

"Bado tunafanyia kazi, mkuu. Tukipata majibu tutakurejea."

"Sina huo muda! Unasikia? Huo muda wa kupoteza sina kabisa. Nataka kila kitu kumhusu huyo bwana mliyemkamata. Hata kama gharama yake ikiwa kubwa namna gani. Sijali!"

Maramoja lilitolewa agizo la kuambatana na Dr. Lambert mpaka nyumbani kwake kwaajili ya uchunguzi zaidi.

Wanausalama watatu wakiwa ndani ya 'SUV' nyeusi walishika barabara upesi na ndani ya muda mchache wakawa wametinga kwenye makazi ya mhusika wao.

Watu waliokuwa eneo hilo walitahamaki kumwona Dr. Lambert akiwa anasindikizwa na wanaume wasiokuwa na uso wa furaha, ndani ya suti nyeusi.

Walitazama, kwa macho ya udadisi, mpaka mwanaume huyo alipotokomea katika uso wao chini ya ulinzi mkali.

Dr. Lambert alifungua mlango wa makazi yake, na punde ulipokuwa wazi alibakia hapo akiwa na mwanaume mmoja huku wawili waliozama ndani wakifanya ukaguzi mkali! ... Macho yake ya kizee yalikuwa yanachungulia wanachofanya mabwana hao.

Walitupa vitu huku na kule. Walifungua hiki na kile. Waligusa hivi na vile. Hakuna kitu kilichoachwa salama. Hadi ukuta ulipondwapondwa kubaini kama kuna mlango wa siri.

Walipomaliza kila ncha ya eneo hapo sebuleni, wakafungua na chumbani pia kukagua. Zoezi lilikuwa ni lilelile. Hakuna walichokiacha salama. Ukaguzi ulikuwa mkali. Kama ungekuwa mtu anayekaa hapa, ungeumia kwa namna vitu vikitupwa na kuachwa shaghalabaghala.

Hawakujali!

Walimaliza zoezi hapo wasione jambo. Sasa ikabakia sehemu moja tu katika eneo hili, nalo ni chumba kilichokuwa kimejitenga.

Chumba kilichokuwa kina mlango rangi ya samawati.

Walitaka kuuvunja mlango lakini Dr. Lambert aliwasihi kutumia diplomasia. Uharibifu waliokuwa wameufanya hapo ulikuwa unatosha. Haikuwa na haja ya kufanya zaidi.

Aliwapatia ufunguo mabwana hao wakaingia ndani kwa fujo.

Ama! Walikuta maabara ndogo iliyosheheni vifaa lukuki vya kisasa. Walistaajabu kwa namna vifaa hivyo vilivyopangwa. Kila kitu kilikuwa katika stadi yake.

Walikagua eneo hilo kwa macho wakisogea huku na kule. Waliona pazia lililokuwa limefungwa, wakaliendea wapate kutazama yaliyomo humo, wakati huo mmoja akitoa taarifa makao makuu juu ya kile kilichokuwa kinaendelea.

Walifungua pazia wakarusha macho. Hakukuwa na kitu zaidi ya kitanda kidogo chembamba.

Walirejea upande waliotokea, wakaendelea kutazama na kukagua. Hapa hawakuharibu kitu hata kimoja, walihofia huenda ikawa ushahidi. Waliendelea kutazama huku wakingoja usaidizi wa kisayansi tokea makaoni.

Dakika zilisonga.

Joto liliongezeka.

Walitiririka jasho ndani ya suti zao.

Mmoja alikohoa, kidogo naye mwenzake akafuatia. Walikohoa kwa pamoja tena na kisha kila mmoja akakohoa kivyake.

Walikohoa zaid ya hapo. Zaidi na zaidi. Mwenzao aliyekuwa nje, pamoja na dokta, alihisi hali hiyo si ya kawaida upesi akaenda kuwajulia hali wenzake.

Aliwakuta wakiwa chini, wameshikilia shingo zao wanakohoa. Mishipa ya shingo imewasimama. Macho yao mekundu mithili ya nyanya mbovu!

Alijawa na hofu na butwaa. Alimshika huyu kisha yule akiuliza nini kimejiri. Alipaza sauti kumwamrisha dokta aje humo ndani kutoa msaada lakini hamna aliemuitikia. Alikuwa mwenyewe.

Alinyanyuka kwa hasira amfuate daktari. Kabla hajapiga hatua ya pili, akakohoa. Huo ndo' ukawa mwanzo wa balaa.

Alikohoa pasipo kukoma. Alikohoa mfululizo kama mwehu. Kila alipotaka kuongea ama kusogea, kikohozi kilimtamatisha upesi. Aliinama akikohoa koh-koh-koh! ... koh-koh-koh!

Kwa vikohozi hivi vya mfululizo, alishindwa kuhema vizuri. Taratibu alianza kuhisi kichwa kinamuelemea. Macho yanapoteza nguvu. Miguu inashindwa kubeba mwili.

Aliangukia magoti yake. Alitamani kuita dokta lakini kikohozi hakikumpa nafasi kamwe. Alitoa macho kama balbu ya solar, mdomo kama kapu.

Mwisho wake ulikuwa ni kudondoka chini, akatulia. Tuli.

Alitulia kama wenzake wawili waliomtangulia.

Kitambo kidogo, dokta aliingia akiwa amevalia mask nyeupe iliyofunika mdomo na pua yake. Aliwatazama watu wale watatu. Hawakuwa na fahamu ndani yao. Aliwaburuza, kwa nguvu zake za uzee, akawaweka pamoja.

Baada ya hapo aliendea sebuleni akabofya kitufe fulani kilichokuwapo ukutani.

Alitazama saa yake ya mkononi, akajisemea mwenyewe ya kwamba ana dakika chache tu za kuweka kila kitu sawa kabla eneo hilo halijafurika wanausalama na wanasayansi kutoka maabara ya taifa.

Alirejea kwenye maabara yake ndogo, akajifungia humo.


Baada ya Masaa Matatu:


"Kwahiyo hamjafanikiwa kupata kitu?" Bwana aliuliza kwa macho makali ndani ya miwani yake. Sauti yake ilikuwa kali na kavu mithili ya mtu anayekunywa vinywaji vikali.

Bwana huyu alikuwa ndiye yule aliyekabidhiwa picha za Ferdinand, Mpelelezi na kemikali ndani ya gari. Simu yake alikuwa ameikamata kwa hasira akis'kiza anayoambiwa na mtu wa ng'ambo.

Amesimama wima nje ya jengo refu la kahawia la McGowan. Mbali naye kidogo, kuna gari moja la wagonjwa linalowaka taa za bluu na nyekundu. Mbali na hilo kuna magari mawili 'SUV' meusi.

Jua lilikuwa lishazama. Taa zinawaka huku na kule. Giza linaelekea kukomaa.

"Tumefanya 'sampling' na uchambuzi wa kemikali zote, hakuna inayowiana na ile uliyotuletea, na mpaka sasa hatujapata kuona sababu haswa ya bwana Ferdinand kumiliki kemikali hiyo. Tunafanya tafi--"

Bwana huyo alikata simu akang'ata meno. Alisimama hapo akitafakari. Hakuelewa mambo haya yanayotukia. Aliweka simu yake mfukoni akalijongea lile gari la wagonjwa.

Nyuma ya gari hilo, walikuwa wameketi wale mabwana watatu, walinzi walioongozana na Dr. Lambert kwenye makazi yake. Mabwana hao walikuwa wametoka kupata tiba lakini bado hawajatengemaa. Miili ilikuwa dhaifu. Vichwa vizito vinawagonga. Mmoja wao alikuwa amevaa 'mask' ya kujipatia hewa safi toka kwenye mtungi uliokuwemo ndani ya gari hilo.

Walimwona mkuu wao wa kazi anakuja upande wao, upesi wakakaa sawa. Walijitahidi kwa ukakamavu mchache uliobakia mwilini mwao kuonyesha heshima yao.

Mkuu wa kazi alisimama kuwatazama maafisa hao kwa macho ya hasira. Alitamani kuwameza. Nao hawa maafisa walitazama kwa uoga, nyuso zao zikijawa na haya.
Kwa yale yaliyotokea, ilikuwa ni aibu kujitambulisha kuwa ni wanausalama.

"Hatukufahamu mkuu," mmoja alijitetea. Aliongea pasipo kumtazama mkuu wake wa kazi. Macho yake yalitazama chini lakini kwa tahadhari. "Hatukujua kama mule ndani kutakuwa na kemikali hatari. Tumekosea."

Mkuu hakusema jambo. Aliona ni bure. Alijiondokea akafuata gari lake. Aliketi kwenye kiti cha nyuma akiwaza mambo haya. Hakika yalikuwa yanamvuruga. Japo hamna kitu kilichopatikana lakini swala la maafisa wake kupoteza fahamu katika maabara ile ndogo ya Dr. Lambert kilimfikirisha.

Kwa kutumia simu yake, alitoa amri ya kuachiwa kwa Dr. Lambert kutoka kifungoni kisha akaagiza bwana huyo afuatiliwe nyendo zake kwa ukaribu. Endapo lolote likibainika basi apewe taarifa haraka iwezekanavyo.

Baada ya simu hiyo, alimwamuru dereva kuondoka eneo hilo.


***


Kesho yake, asubuhi ya mapema, jiji la New York liliamshwa na habari ya kutisha kwenye maredio, runinga, mitandaoni na magazetini!

Kila mmoja aliyepata nafasi yake alisoma habari hiyo akistaajabu juu ya nini kilichotokea. Lilikuwa ni jambo jipya katika jiji hili lakini zaidi lilikuwa ni la kuogofya.

Habari ziliripoti kuwa katika kitongoji cha Brooklyn, yalitokea mauaji ya kikatili yaliyotokana na na mlipuko mkubwa uliotokea majira ya usiku unaokaribia na alfajiri ndani ya moja ya jengo moja maarufu kwa wauzaji na wanunuaji wa madawa ya kulevya kukutania kwa ajili ya kufanyia biashara zao haramu.

Katika sakata hilo, ilisadikika watu zaidi ya kumi walifariki papohapo. Miili yao ilisambaratishwa na bomu pasiwepo hata vya kuokota vikazikwe kwa heshima ya utu.

Majirani, pamoja na manusura wachache wa tukio hilo, walieleza yale waliyoyashuhudia, na kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, taarifa zao zilirushwa hapa na pale, huku na kule. Sio tu ndani ya New York bali Marekani nzima!

Wachache waliobahatika kurekodi tukio hilo adhimu, waligeuka kuwa mali kwa video zao kusambaa kama moto wa nyika mitandaoni, na hata baadhi ya vyombo vya habari vyenye uweledi walizitumia video hizo kama nyenzo pekee ya kuonyesha kilichojiri.

Basi ikawa hapa na pale watu wakizungumza na kupiga soga. Pia huko mitandaoni, watu wakimwaga maoni yao juu ya tukio hilo. Mlengo mkubwa wa watu wakikemea udhaifu wa jeshi la polisi kwenye kudhibiti mitandao ya madawa ya kulevya pasipo kujali maafa wanayoyasababisha.

Kwa kupitia video hizo ambazo ziligeuka kuwa maarufu ndani ya muda mchache mno, polisi waliweza kubaini sura kadhaa za wahanga. Takribani watu sita waligundulika maramoja huku wengine, kwasababu mbalimbali aidha za mwanga ama mwelekeo wa kamera, haikuwezekana kutambulika kwa upesi. Ulikuwa unangojwa upelelezi zaidi kwaajili ya kutambua wadhfa wao.

Picha za wale waliotambulika zilisambaa kwenye vyombo vya habari, kila chombo kikitaka kuwa cha kwanza kwenye kuripoti taarifa motomoto kwa wateja wake. Picha hizo kutoka kwenye video, ziliboreshwa zikaonekana vema. Macho na pua. Midomo na nywele, pia maumbo ya mwili.

Miongoni mwa picha hizo, ilikuwa ni ya Ferdinand.

Muda kidogo, mkuu wa kitengo cha polisi cha New York alitoa tamko kwenye vyombo vya habari kuhusu hayo yaliyojiri. Alielezea muda wa tukio hilo na pia jitihada za polisi kwenye kulishughulikia haraka iwezekanavyo.

Aliwasihi wananchi kuwa watulivu huku jeshi la polisi likifanya kazi yake, lakini pia alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa dhati juu ya janga hilo ili kuwawajibisha wale wote waliohusika nalo kwa njia moja ama nyingine.

Wakati huo akiwa anatoa hotuba, mkuu wa kitengo cha upelelezi alikuwa yuko pembeni kidogo, yu 'bize' anahangaika na simu yake.

Bwana huyo alikuwa amevalia shati jeupe na kizibao cheusi kilichoendana na suruali yake. Upara wake ulifunikwa kwa kofia aina ya panama, rangi nyeusi yenye riboni nyeupe.

Alikuwa ameukunja uso akitazama simu hiyo kana kwamba kuna kitu kimeenda kombo. Aliibonyeza kwanguvu akiiweka sikioni, kisha aliitazama akaibonyeza tena na kuiweka sikioni.

Zoezi lilikuwa linajirudiarudia pasipo matunda. Alisimama akashika kiuno chake, akarudia tena zoezi hilo kabla ya kurejea kuungana na wenzie.

Lisaa limoja baada ya hotuba hii ya mkuu wa polisi, taarifa rasmi ilitolewa juu ya kutambua mabaki ya watu wengine waliokuwemo katika tukio la mlipuko. Watu wawili wa ziada, kwa kutumia mabaki yao madogo ya mwili yaliyofanyiwa uchunguzi, walibainika sura na wadhfa wao, upesi wakasambaa mtandaoni na kwenye vyombo vya habari.

Baada ya lisaa lingine, walibainika wahanga wengine waliobakia. Kwa kuwianisha vinasaba vyao na taarifa zilizotunzwa kwenye 'database' ya usalama na serikali, nyuso zao ziliwekwa bayana mmoja baada ya mwingine.

Shida ilikuja pale ambapo mmoja kati ya wale walioonekana katika ile video ya wahanga wa bomu iliyosambaa mitandaoni, hakutambulika!

Japo kila kielelezo kilikusanywa toka eneo husika na vikasanifiwa na wataalamu wa hali ya juu, hakukuwa na majibu yoyote yaliyokuja.

Bwana huyo si mwingine bali Ferdinand. Mwanaume ambaye alikuwa anasakwa na polisi kuhusu kesi ya mauaji ya The DL!

Jambo hilo lilileta utata na mkanganyiko kwa polisi. Mkuu wa kitengo cha upelelezi, katika muda wake mchache, alikutana na afisa wa usalama aliyekuwa kwenye makubaliano ya kushirikiana na Mpelelezi wake juu ya kesi ya bwana huyu anayesadikika kufia motoni.

Afisa huyo wa usalama, rahisi kumrejelea kama 'babyface', aliomba apatiwe mabaki yote ya mwili yaliyofanyiwa uchunguzi kubaini utambulisho wa wahanga wa ajali ile kwa ajili ya wao kwenda kufanyia tafiti zaidi, lakini katika hilo aliomba kuwe na usiri mkubwa.

Haikutakiwa taarifa hii kuwa bayana kwa umma.

"Ondoa shaka," mkuu wa upelelezi alimsihi. "Nitalifanyia kazi ndani ya muda mfupi."

Baada ya masaa mawili, afisa huyo wa usalama akawa ameshapata kila kitu alichokihitaji. Wakati huo wote mwenza wake, yaani Mpelelezi, akiwa hana ufahamu na lolote lile linaloendelea.

Simu yake ilikuwa inaita pasipo majibu. Mkuu wake ameshapiga mpaka amechoka sasa. Ana shaka hata habari hizi za mauaji ya bomu kama kweli zitakuwa zimemfikia.

Uchunguzi uliporejelewa kwenye maabara za usalama, ilikuja kubainika kuwa ni kweli Ferdinand alikuwamo katika eneo la tukio! Mabaki kadhaa ya mwili yalithibisha hilo pale yalipowianishwa na wasifu wa bwana huyo katika 'database' za ofisi ya usalama. Wasifu ambao, hamna chombo kingine chochote cha usalama walikuwa nao, isipokuwa wao tu.

Ingawa ilikuwa ngumu kuamini, lakini vielelezo vilionyesha kuwa Ferdinand amekufa.


***
Duh! Kivumbi cha kufa mtu![emoji2962][emoji1782]
 
Nimeipenda sana hadi natamani Hata saii Steve aimalizie!!
Humu bwana mafunzo ni mengiiii.... kwanza The power of [emoji383][emoji383][emoji383][emoji383][emoji383] pili usnitch aisee trust no one...watu wako wa karibu usiowadhania ndio wanaokumalizaa chini chini..tatu ishi kivyakoo watu wasikujue kabisa au uwe na changing behavior wasikusome . Nne point yako ya weakness watu ndio wanaitumia kama strength yaooo... na mengine mengi mengi
[emoji817] Hakika umeisoma na kuielewa.
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 13


Na Steve B.S.M



San Fransisco, California.

Saa tano usiku.


Mpelelezi alitazama saa yake ya mkononi kisha akatengenezea nywele zake kwa kiganja cha mkono wa kushoto. Nywele zilikuwa zimekaa vema.

Alikuwa amevalia suruali nyembamba nyeusi na viatu vyenye sori kubwa ngumu. Juu alivalia shati rangi ya machungwa na koti jeusi.

Ulikuwa ni wasaa wake murua huu. Wasaa wa kutumia pesa. Alikuwa amesimama karibia na sehemu ya kuegeshea magari, mkabala na jengo kubwa lenye maandishi makubwa meupe yaliyosomeka: San Pablo Lytton Casino.

Jengo hilo lilikuwa mahususi kwa michezo ya kamari. Humo ndani kulikuwa na mashine lukuki za michezo ya kubahatisha pamoja pia na watu wengi wakitumia fedha zao kwenye starehe.

Mpelelezi aliingia humo akatafuta sehemu ya kuketi, mbele ya mashine, kisha akaanza kucheza hapo akiwa anakunywa kahawa tamu na ya moto aliyoambatanishiwa na tiketi yake.

Alicheza na kunywa kidogo, akahisi simu yake inaita mfukoni. Akaipuuzia.

Aliendelea kucheza akiweka pesa kama mara tatu hivi, dude likizunguka na kuambulia patupu. Kabla hajaenda mzunguko wa mara ya nne, akachomoa simu na kutazama ni nani aliyekuwa anampigia.

Akakuta ni mkuu wake wa kazi. Tayari alishampigia mara mbili sasa.

Akawaza kidogo.

Akaendelea na mchezo wake akiipuuzia simu hiyo.

Alicheza kama michezo mitatu ya ziada, yote hakuambua kitu. Kila mashine ilipozunguka, ilikuwa ni patupu ikisimama.

Akashusha pumzi fupi. Hakuwa na mchezo mzuri hapa. Aliwaza huenda leo haikuwa siku yake ya bahati.

Basi akatoka hapo akielekea mahali kwanza apate kunywa kuweka kichwa chake sawa. Kiasi alichopoteza katika mashine hii kilikuwa kinatosha.

Alipanga akitulia kidogo, atarejea tena mchezoni japo kwa upande mwingine mbali na huu alotoka kuucheza sasa.

Aliagiza mvinyo akiwa amekaa mahali maalum ndani ya kumbi hii ya wastani, akawa anakunywa taratibu.

Taratibu huku akiipanga siku yake ya kesho pale patakapokucha.

Ilifikia muda akaacha kuwazawaza mambo ya kazi, akaamua kujipumzisha kwa kuiingiza akili yake katika starehe.

Akiwa anamalizia kinywaji chake, alibahatika kukutana macho kwa macho na mwanamke mrembo aliyekuwa amekaa kwenye moja ya meza ya kamari.

Mwanamke huyo alikuwa amevalia gauni jekundu lina vidotidoti vingi mithili vya almasi inayometameta.

Gauni hilo lilikuwa limemkaa vema katika 'English figure' yake matata.

Nywele zake zilikuwa ndefu nyeusi, kaziachia zikienda mpaka karibia na kiuno chake.

Macho yake, makubwa na malegevu, yalichorwa vema na msanii wa 'makeup'. Kope zake zilikolezwa rangi nyeusi na nyusi zake zilipunguzwa wingi zikitindwa kwa ustadi mkubwa.

lUso wake mwembamba ulipambwa na 'lips' zake zenye nyamanyama zilizometa kwa rangi ya 'pink'. Masikio yake yaliyochongoka yalitogwa na hereni murua yenye mikia mitatu iliyokuwa inaning'iniza vijitufe vidogo vyenye kumetameta.

Mwanamke huyo alikuwa amevalia viatu virefu vyeusi ambavyo havikuonekana mdomo wake kwani gauni lilikuwa refu.

Aliupandishia mguu mmoja juu ya mwingine alafu akapeleka uso wake pembeni, mbali na macho ya Mpelelezi.

Mpelelezi akamtazama mwanamke huyo kwa kitambo kidogo kisha naye akaendelea na yake. Akagiza kinywaji kilichofika si punde, akaendelea na ulabu wake wa wastani.

Muda kidogo, akayarudisha macho yake kwa mwanamke yule.

Hakuwapo.

Alirusha macho yake huku na kule pasipo kutumia nguvu. Hakumwona mwanamke yule. Akapuuzia na kuendelea kunywa. Kidogo akanyanyuka toka hapo akaendea meza moja waliyokaa wanaume wawili wakicheza kamari ya karata.

Akaungana na wanaume hao waliowekeana madau ya kawaida katika mchezo wao, haikuzidi dola hamsini kwa kila mtu. Wakacheza mchezo wa kwanza, Mpelelezi akashinda.

Alifurahi kurudisha kiasi fulani cha pesa yake aliyopoteza hapo awali. Alitumai kwa mchezo huu atarejesha hasara yake yote na faida juu.

Hapa ndipo anapendea kamari.

Wakacheza mchezo wa pili, akashinda tena. Moyo wake ukafurahi. Usoni mwake ungeona tabasamu pana, meno yote nje kana kwamba anafanya 'promo' ya mswaki.

Kabla hawajaanza mchezo wa tatu, mtu fulani akaja na kuketi pembeni yake. Mtu huyo alikuwa ameongozana na harufu tamu mno ya kuvutia.

Mpelelezi akashindwa kujizuia. Aligeuza shingo yake upesi kutazama.

Uso kwa uso akakutana na mwanamke yule aliyevalia gauni jekundu. Hakujua kwanini lakini alijikuta akisisimka. Ubaridi wa kipekee ulimpitia toka kichwani ukashukia mpaka miguuni.

Mwanamke yule akawa kama amejua hilo. Akatabasamu. Akazidi kuongeza uzuri wake maridhawa.

Mpelelezi akasema,

"Habari yako, mrembo?"

Mwanamke yule akajibu,

"Nzuri. Naona usiku wako ni mwema leo," alisema akitazama karata na pesa mezani.

Mpelelezi akatabasamu.

Alimjibu,,

"Naam. Natumai utakuwa usiku mzuri."

Mwanamke yule akatikisa kichwa na kumpongeza.

Alisema,

"Wewe si mtu wa San Fransisco."

Mpelelezi akamuuliza amejuaje hilo? Mwanamke huyo akamweleza kuwa ni mara yake ya kwanza kumwona katika ukumbi huo wa starehe.

"Ni kweli," Mpelelezi akakiri na kuongezea, "lakini mimi huwa najihisi mwenyeji popote pale ninapokuwa katika kumbi hizi. Haijalishi mji gani."

Mwanamke akastaajabu kiustaarabu.

"Kweli?"

"Ndio, kweli," Mpelelezi akamjibu kwa uhakika. Basi mwanamke huyo akamtaka aungane naye katika mchezo unaofuata. Alikuwa na hamu ya kuona uwenyeji wa Mpelelezi huyo.

Mchezo ukaanza.

Kila mtu alipata karata zake akiamini akizicheza vema basi ataweza kuibuka kinara, kazi ikabakia kwenye 'timing' na matumizi ya akili binafsi.

Kila mtu akacheza karata yake ya mzunguko wa kwanza. Kwa tahadhari tena, kila mmoja akacheza mzunguko wake wa pili.

Macho yalikuwa yanazunguka, kila mmoja akimtazama mwenzake usoni. Kila mmoja akijaribu kusoma saikolojia ya mwenziwe.

Kwenye hilo, Mpelelezi alikuwa bora zaidi, hata yeye mwenyewe aliamini hivyo.

Kwa kupitia macho ya kila mmoja, aliweza kubaini kinachoendelea katika vichwa vyao akapanga karata zake vema.

Wakaenda mzunguko wa tatu, sasa ikabakia mizunguko miwili ya mwisho. Mizunguko ya kuamua mshindi. Hapo Mpelelezi akapiga mahesabu yake kuwa kila kitu kipo sawa. Anachongoja ni muda tu ufike.

Muda ulipowasili, akajikuta akipigwa na butwaa. Hakuamini macho yake. Mwanamke yule mrembo alimaliza mchezo kwa karata yenye nguvu dhidi ya ile aliyokuwa ameishikilia kwa matumaini.

Akajiaminisha huenda ni bahati.

Wakacheza mchezo wa nne. Mwanamke akashinda. Wakacheza wa tano, mwanamke akashinda tena. Kila mara Mpelelezi alipojitahidi, kusoma akili ya mwanamke huyo alifanikiwa.

Lakini kila unapofika mwisho wa mchezo ndipo anajikuta alijidanganya. Hakujua kitu. Alichezewa shere.

Mwisho wa siku, akajikuta anapoteza pesa za kutosha. Kila alipotaka kucheza ajirejeshe mchezoni, akajikuta anapoteza zaidi.

Kuja kufahamu hamna matumaini tayari alishakawia.

Alimtazama mwanamke yule, asiamini yaliyotokea mbele ya macho yake. Hakuwahi kuchakazwa kiasi hiki. Achilia mbali kuchakazwa na mwanamke.

Alimuuliza mwanamke huyo,

"Wewe ni nani?"

Mwamamke akatabasamu. Akamkumbusha Mpelelezi kuhusu ugeni wake ndani ya jiji la San Fransisco. Alimuambia kama angekuwa si mgeni basi angeshamwepuka kucheza naye tangu mapema.

Mpelelezi akataka kujua nini siri ya mafanikio ya mwanamke huyo. Alijawa na hamu iliyoambatana na mshangao. Alisihi sana.

Mwanamke akamtazama na kumweleza kuwa kama angetaka hilo, basi waonane hapo kesho yake.

Majira kama hayo.

Baada ya hapo, akabusu hewa akimlenga Mpelelezi, alafu akaenda zake.

Ama!

Mpelelezi akamsindikiza kwa macho mpaka alipoyeya katika mboni zake.

**

Queens, New York. Olympus Printing Press

Saa Moja Asubuhi.


Hilda alitazama nyuma yake alafu akainamia meza ya Richie. Macho yake ameyakodoa. Uso wake umeparamiwa na mashaka.

Akauliza,

"Richie, hukuona 'calls' zangu zote?"

Richie, ambaye muda wote huo alikuwa anatazama tarakilishi yake kana kwamba hajamwona Hilda, akasafisha koo na kutengenezea tai shingoni.

Leo alikuwa amejinyonga koo.

Shati lake pana na jeupe lenye mikono mifupi lilimfanya aonekane kama mtu aliyeongezeka uzito.

Alisema,

"Niliziona lakini sikuona haja ya kupokea."

Hilda akatazama tena nyuma yake alafu akamsogelea Richie kwa ukaribu. Alivuta kiti akaketi.

Akasema,

"Richie, ungejua ni namna gani nilivyohangaika jana wala usingesema hayo maneno. Nilitaka kweli kuongea na wewe."

Richie akamtazama na kumwambia:

"Kama ungelitaka, tungeliongea tulipokuwa njiani. Nilikusihi lakini haukutaka. Hata nilipokugusia jambo lako bado ulienda. Nini kimekufanya ukabadili mawazo yako?"

Hilda akamshika mkono Richie.

Richie akas'kia baridi kali limempitia. Hakuelewa baridi hilo limetokea wapi kwa ghafla namna hiyo. Ni kana kwamba mikono ya Hilda ilitokea kwenye jokofu kuu la kisasa.

Hilda akasema taratibu,

"Richie, hamna chochote nilichofanya kwa lengo la kukuumiza. Laki ... Lakini, Richie, ulijuaje kuhusu haya mambo yote? Au kukulipia kwangu huduma ya 'speech-language pathologists' ili kurekebisha kigugumizi ulichonacho ndo' kulikushtua?"

Richie akatabasamu.

Akamweleza Hilda kuwa hilo sio jambo kubwa japokuwa lilizidi kumwaminisha juu ya upataji mkubwa wa pesa wa mwanamke huyo.

Akamweleza kuwa maongezi yote baina yake na boss amekuwa akiyasikia hivyo hamna cha kuficha. Anajua kila kitu.

Kwa kumwaminisha hilo, akamweleza Hilda mambo kadha wa kadha ambayo ana ufahamu nayo. Hilda akaondoa shaka kabisa juu ya ufahamu wa bwana Richie. Aliamini kwa dhati bwana huyo anajua kila jambo hivyo sasa anaweza kuwa huru mbele yake.

Hilda, akiwa amenyong'onyesha sura, akamweleza Richie kuwa jana usiku hakupata kulala kabisa. Hata kuna muda akiwa mwenyewe anapatwa na milipuko ya hofu.

Alisema,

"Richie, nahisi vibaya. Sikuwahi kukutana na mtu ambaye kazi yake nilikuwa naifanya. Nakuja kupata taarifa ni kifo chake tena akihusishwa na madawa ya kulevya. Kama haitoshi, bado naambiwa kazi itaendelea kama kawaida. Kazi ambayo hata sielewi haya ninayoyaandika na kunakili. Vipi tukija kuonekana ni washirika wa wahalifu?"

Macho ya Hilda yaligeuka kuwa mekundu na mabichi. Uso wake ulianza kubadirika rangi kufanania na nyanya iliyokwiva.

Aliendelea kuongea kidogo, mlango ukafunguliwa akaingia Bryson. Bwana huyo alikuwa amebebelea mkoba mkononi, mwilini kuna shati na suruali ya kitambaa rangi ya bluu.

Alisalimu akapita zake. Hilda alikuwa amempa mgongo hivyo hakupata nafasi ya kumwona usoni.

Kwasababu ya ujio huo basi, maongezi yao yakaishia hapo wakiahidiana kuonana baadaye.

Hilda akamtumia Richie baadhi ya kazi alizofanya, na mwanaume huyo katika nafasi yake akawa anazipitia.

Alipitia kazi hizo asielewe ni nini kilichokuwa kinalengwa. Taarifa nyingi zilikuwa za kisayansi zikiwa zimeambatana na michoro mingi ya kuonyesha 'chemical compositions'.

Michoro ambayo kwa Richie ilikuwa ni vitu vigeni.

Alifikiria na kutengeneza nadharia tofautitofauti kuhusu taarifa hizo lakini bado hakuona tija.

Mwishowe, baada ya masaa kadhaa, akapata mawazo mawili ya kuyatazama kwa jicho la tatu.

Moja, alifikiria huenda taarifa hizo za kikemia zinahusu mifumo ya utengenezaji wa madawa ya kulevya. Wazo hilo lilimjia sababu ya kutazama mahusiano ya mhusika, yaani Ferdinand, na kazi yenyewe.

Pili na mbaya zaidi, akawaza kutafuta majibu ya taarifa zile kwa kutumia watu wa nje. Yaani, watu baki ambao wana maarifa na nyanja hii ambayo kazi imetokea. Kumaanisha wanakemia.

Akiwa anawaza hili, picha ya mmoja wa rafiki zake aliosoma nao shule ya upili ikamjia.

Aliamini huyo atamsaidia kufungua hizi 'code' ili ajue kama yaliyomo yamo.

**
Oh!hooow!! Jaribio la kujiua na kuua wenzie
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 14


Na Steve B.S.M



Brookhaven, New York.

Saa tano asubuhi


Dr. Lambert aliufungua mlango akaingia ndani ya ofisi. Ndani humo kulikuwa na meza tano, kila moja ikiwa na kiti chake na tarakilishi zenye visogo bapa.

Akaendea meza moja, upande wake wa kusini, akatundika koti lake jeupe katika mgongo wa kiti kisha akaketi kwa kuutupa mwili.

Akashusha pumzi ndefu.

Akaunyoosha mgongo wake, ukalia kah-kah-kah kisha akashusha pumzi tena.

Alikuwa amechoka. Umri nao ulichangia. Kama si serikali kumwomba aongeze mwaka mmoja katika mkataba wake kwasababu ya umuhimu wake kazini basi angekuwa kijijini huko akitazama ng'ombe na kula pensheni, ama amekaa nyumba tulivu akicheza na wajukuuze.

Alibofya kibodi, tarakilishi ikawaka. Upesi akachezesha vidole vyake kunakili taarifa fulani katika mashine hiyo.

Vidole vilikuwa na wepesi sana. Macho yake yakitazama kioo, vidole hivyo vikachapa taarifa iliyotoka kichwani pasipo kusoma popote pale.

Akiwa anaandika hayo, mlango ukafunguliwa wakaingia wanaume wawili waliokuwa wamevalia makoti meupe kama lile la Dr. Lambert.

Wanaume hao walikuwa wanateta mambo yao lakini punde walipoingia ndani, kila mmoja akajigawa kuendea meza yake.

Mmojawao alikuwa ni kijana wa makamo ya miaka thelathini ya mapema wakati mwingine akiwa wa makamo ya miaka arobaini hivi. Ndevu zake amezichonga 'O' na kichwa chake hakina nywele hata moja.

Waliketi kukawa kimya. Kidogo, mmoja akaja na kuungana nao. Alikuwa ni bwana mfupi sana, mzee wa makamo ya miaka hamsini hivi. Nywele zake zilikuwa mchanganyiko wa nyeusi na nyeupe. Alisalimu kisha akaketi naye katika sehemu yake.

Bwana huyo alipokaa tu, mjadala ukaibuka.

Ulikuwa ni mjadala kuhusu mazingira yao mapya ya kazi baada ya taarifa ile ya kuvuja kwa data kutuhumiwa kutoka maabara hii.

Walijadili namna gani kazi ilivyokuwa ngumu wakisimamiwa kila eneo, lakini pia namna gani kamera zilizopachikwa kila mahali zinavyowanyima faragha zao.

Walienda mbali wakajadiliana juu ya mhusika wa hayo yote. Waliongea wakimwonea huruma bwana huyo punde atakapokamatwa.

Wakiwa katika mjadala huo, Dr. Lambert alikuwa kimya sana. Macho yake yalikuwa yanatazama tarakilishi huku vidole vikichapa kazi mfululizo.

Ni kana kwamba alikuwa katika dunia yake ya pekee. Hakuskia wala kujali kilichokuwa kinaendelea hapa.

Kidogo simu yake ikaita. Watu wote waliokuwa wanaongea wakanyamaza kutazama. Simu iliwakatisha. Dr. Lambert aliitoa simu yake mfukoni akaangalia nani anapiga.

Namba ngeni.

Mojamoja akili yake ikampeleka kwa mwanamke Mitchelle kwani ndiye mtu pekee ambaye ana hizi namba zake anazozibadili mara kwa mara. Kiuhalisia, mwanamke huyo ndiye anayempatia namba hizo hivyo kumtafuta ni jambo la wakati tu.

Hakupokea, alichofanya alizima sauti kisha akairejesha simu mfukoni. Mazingira hayakuruhusu.

Simu ikaendelea kuita kwa kunguruma huko mfukoni mpaka ikakata. Wale wengine ndani ya ofisi wakaendelea na shughuli zao, kila mmoja akiwa na yake.

Simu ikaita kwa mara ya pili. Muda huu ni Dr. Lambert pekee ndiye alikuwa anajua kwani sauti haikutoa. Simu ilitetemeka ndani ya mfuko wake akivumilia kana kwamba hamna kitu kinachotokea.

Alivuta muda kidogo, kama dakika tatu, kiendelea na kazi yake alafu ndo' akaamka na kuelekea zake nje.

Akiwa anakatiza, bwana yule mfupi aliyekuwa wa mwisho kuingia ofisini alimtazama akamuuliza kama kila kitu kipo sawa. Dr. Lambert akatikisa kichwa.

Alisema,

"Hamna shaka."

Akafungua mlango na kwenda zake.

Akatembea upesi kuimaliza korido, ndani ya muda mfupi akawa amefika mbele ya mlango wa choo. Akatazama kushoto na kulia kwake, kulikuwa salama. Hakukuwa na mtu hapo ispokuwa kamera tu.

Akaingia ndani.

Humo ndo' palikuwa sehemu pekee ambamo hamna kamera.

Dr. Lambert akaingia ndani ya kijsehemu kidogo cha kujisaidia haja kubwa, huko akatoa simu yake mfukoni na kupiga.

Alijiaminisha humu yu salama.

Simu ikaita kidogo kisha ikapokelewa. Ilikuwa ni sauti ya kike kwa upande wa pili. Sauti ya Mitchelle.

Mwanamke huyo alimkumbusha Dr. Lambert kuhusu makubaliano yao ya msingi. Alimtaka dokta amtumie dawa na nyaraka muhimu haraka iwezekanavyo. Afanye atakavyojua lakini siku hiyo ama ijayo isipite pasipo yeye kupata mahitaji yake.

Lakini atazipataje?

Dokta alisema,

"Sifahamu ulipo. Uliniambia utanitaarifu lakini ukakaa kimya."

Mitchelle akampatia anwani yake, pia akamsihi autume mzigo huo kwa njia ya DHL. Aliamini ataupata kwa upesi na kwa usiri anaoutaka.

Dokta akaridhia kila jambo, lakini ndani yake alikuwa na shaka. Alihusha pumzi fupi, akasema,

"Mazingira yangu ya kazi yamekuwa magumu sana hapa karibuni, Mitchelle. Ulinzi umekuwa mkubwa sana kuingia na kutoka. Hata humu ndani, hamna kinachofanyika pasipo kuonekana na kamera lukuki.

Kule nyumbani napo walibeba kila kitu muhimu nilichokuwa nahitaji, hivyo utakapoona nasuasua basi fahamu mazingira ni magumu."

Mitchelle hakutaka kuelewa.

Alisema,

"Dokta, unakumbuka makubaliano yetu ya kazi? Tulikubaliana kazi itafanyika kwa namna yoyote ile, kiangazi ama masika, na hiko ndo' kinanifanya nikulipe maelfu ya madola kila uchwao. Unavyoniambia mazingira magumu, nashindwa kukuelewa, dokta. Kwahiyo mimi naishije?"

Dokta akakosa cha kujitetea. Akabakia kimya, moyo wake ukiwa unaenda kwa kasi. Uso wake umeparamiwa na mashaka na maulizo.

Mitchelle akamalizia kwa kusema,

"Nangoja. Kaa ukijua namaanisha hilo."

Kisha akakata simu.

Dr. Lambert akafuta jasho kwenye paji lake la uso. Akaketi juu ya choo cha kukaa kilichokuwa pembeni yake.

Akaketi akiwaza.

Mazingira ya hapa yalikuwa yako kimya sana. Dokta alipotelea kwenye mawazo akitazama namna gani anaweza kufanya.

Kila alichowaza kichwani kiligoma na kuishia kufeli. Hakuona njia kwa sasa. Kila alipofikiria ulinzi ule wa kamera na wana usalama, alichoka kabisa. Alihisi kichwa kinapasuka.

Alinyanyuka na kutoka humo alimo, akaufuata mlango wa kutoka ndani ya choo.

Akaukuta mlango ukiwa wazi.

Alisimama hapo akajiuliza kama mlango huo hakuufunga alipoingia ndani. Hakukumbuka vema lakini hisia zake zilimweleza kuwa aliufunga mlango huo. Hakuwahi kuingia ama kutoka chooni akauacha mlango wazi.

Kwa ukimya uliopo ndani ya vyoo, aliamini hakukuwa na mtu aliyeingia wala aliyekuwamo humo isipokuwa yeye mwenyewe tu.

Akaelekea ofisini upesi.

Humo akakakuta wenziwe wote kasoro mmoja. Yule mwanaume mfupi hakuwapo. Moyo wake ukamjaa shaka.

Akauliza,

" Ameenda wapi huyu jamaa?"

Hakuna aliyekuwa anajua. Walijibu hapana wakiendelea na kazi zao. Walionyesha kutingwa na kazi nyingi.

Dokta akiwa amesimama hapo, kidogo mlango ukafunguliwa akaingia bwana aliyekuwa anamuulizia.

Akamuuliza,

"Ulikuwa wapi?"

Bwana huyo akastaajabu na hilo swali. Aliyatoa macho yake akimtazama dokta.

Akamuuliza,

"Bwana, kuna tatizo?"

Dr. Lambert akamtazama pasipo majibu. Wakatazamana kwa kama sekunde tano kama majogoo waliohitilafiana.

Bwana huyo akasema akiwa anaendea kiti chake,

"Niliitwa na mkuu ofisini."

Akaketi na kumtazama dokta.

Akamuuliza,

"Ulikuwa una shida na mimi?"

Dokta hakujibu. Alifuata meza yake akaketi.

Alitazamatazama hapo kwa muda mchache kabla hajashika tena tarakilishi yake kuendelea na kazi. Muda si mrefu akawa amemaliza.

Akatoka kwenda kujipatia chakula cha mchana.

***

San Fransisco, California. Chuo kikuu cha Stanford.

Saa saba mchana


Mpelelezi alikuwa amekaa kwenye moja ya viti vya chuma vilivyokuwa nje ya ofisi ya 'Dean of Students' wa chuo hiki.

Mkononi mwake alikuwa ameshikilia simu, akiipekua taratibutaratibu kusogezea muda.

Bwana huyo alikuwa amevalia suruali nyeusi, ile aliyovaa jana yake, kiatu kilekile lakini juu akiwa amebadilika. Alivalia shati la kahawia la mikono mifupi, mkononi ana saa yake ya kila siku.

Kidogo, bwana mmoja, mtu mzima wa makamo ya miaka thelathini na tano, akatokea akijia ofisi hii. Bwana huyo alikuwa katika mwendo wa ukakamavu. Juu amevalia shati na kizibao cha sweta rangi ya damu ya mzee.

Uso wake wa wastani ulibebelea miwani safi ya macho. Pua yake ndefu, mdomo wake una 'lips' nyembamba.

Kwa kumtazama, Mpelelezi akaamini kuwa huyu ndiye aliyemfuata. Upesi akanyanyuka na kumsalimu kisha akajitambulisha.

Dean akamkaribisha ofisini kwake.

Waliingia, Mpelelezi akahudumiwa kwa kahawa nzito ya moto kusindikizia maongezi yao.

Pasipo kupoteza muda, Mpelelezi akaeleza haswa kilichomleta hapo. Mguu wake ulilenga kupata taarifa kumhusu mwanamke ambaye alisoma hapo akaishia kujiua.

Alimkabidhi Dean picha ya mwanamke huyo pamoja na majina yake matatu. Akamwambia ampatie yale yote anayoyajua kumhusu mlengwa huyo.

Dean alipotazama picha na kuskiza alichoambiwa, akatengenezea kwanza miwani yake usoni. Akatulia kidogo kabla hajafunguka kumwambia Mpelelezi kuwa mwanamke huyo alipata kusoma hapo miaka mingi iliyopita lakini hakumaliza masomo yake akajiua.

Mwanamke huyo kwa sifa alikuwa ni mtu wa kujitenga akibahatika kuwa na rafiki mmoja tu. Rafiki ambaye wengine walistaajabu kumwona ni namna gani alifaulu kuwa karibu na mwanamke huyo.

Mbali na hayo, Dean akamwambia Mpelelezi namna gani mwanamke huyo alivyokuwa mwerevu mno darasani. Ingawa alikuwa ni mtu wa kujitenga sana, akijiepusha na makundi ya majadiliano, bado alama zake zilikuwa juu mno.

Alimpatia Mpelelezi rekodi ya kitaaluma akaitazama na kukiri yale anayoambiwa ni kweli. Mitihani pekee ambayo mwanamke huyo alifeli, ilikuwa ni kwa kupata alama B. Mengine yote yalikuwa ni A na A+.

Dean akasema,

"Kwa mwanafunzi mwenye alama hizi katika kozi yake hii, ana 'future' ya kuaminika. Ni ajabu mtu kama yeye kuyatoa yote sadaka kwa kujiua."

Mpelelezi akauliza,

"Kuna kingine cha ziada?"

Dean akamwambia hana jambo la zaidi ya hayo, mengine anaweza kuyapata kwa msimamizi wa hostel ambamo binti huyo alikuwa akiishi.

Akampatia mawasiliano yake, Mpelelezi akaelekea huko. Ndani ya muda mchache akawa yu pamoja na mwanaume aliyevalia kapelo nyekundu yenye chapa ya chuo cha Stanford.

Bwana huyo mzee mwenye kijitambi kilichoshikiliwa na 'form six' nyekundu yenye chapa ya chuo, alikuwa na masharubu meupe na mwanya mpana.

Alimkaribisha Mpelelezi akimweleza amepata taarifa zake toka kwa Dean. Akamwahidi kumpa ushirikiano wake wa dhati.

Akamweleza Mpelelezi juu ya namna alivyomjua mlengwa wao kisha akamsaidia kupata namba ya simu ya yule ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu. Aliamini huko atapata vya ziada ambavyo wao hawavifahamu.

"Lakini," bwana huyo alisema, "kifo cha huyu binti kilinigusa sana. Namna alivyokuwa anaishi na wenzake, hakuwa mtu wa makuu na kujivuna, na sikuona akiuchukulia upweke wake kama ulemavu. Naamini alikuwa anafurahia kuwa peke yake zaidi. Nina mwanangu mwenye sifa hizo.

Yeye hupenda kujitenga akiutumia muda wake mwingi chumbani. Mwanzo nilikuwa na mashaka sana lakini nilikuja kugundua kuwa, kwa upande wake alikuwa sawa kabisa."

Bwana huyo akamalizia akisema,

"Mara kadhaa nilikuwa namwona akitabasamu awapo mwenyewe au awapo na kitabu. Tabasamu lile la dhati. Lakini ilikuwa aghalabu kumwona akifanya hivyo akiwa na watu wengine isipokuwa rafiki yake tu."

Mpelelezi akamalizana naye na kuondoka zake.

Aliita Uber ikaja ndani ya muda mfupi. Akajiweka viti vya nyuma, safari ikaanza.

Akiwa humo, akajaribu kupiga simu ya mwanamke yule rafiki wa mlengwa wake. Simu ikaita kisha ikapokelewa.

"Nani?"

Sauti ya kiume ilimuuliza, akastaajabu.

Alikata akaitazama namba hiyo kwa uhakiki. Akabaini ilikuwa sawa kabisa. Akapiga tena.

"Wewe nani?"

Sauti ya kiume ikamuuliza. Sauti ileile ya mwanzoni.

**
Duh![emoji848][emoji53] Kafukua kaburi
 
BONUS YA MWISHO


TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA.




Alipohakikisha mwili huo uliolala chini hauna uhai, akatazama mazingira ya eneo hili kwa ajili ya usalama.

Palikuwa kimya sana.

Mbali na hilo, vitu vilikuwa shaghalabaghala. Meza na viti viko bidubidu!

Kiti kimoja kilikuwa kimevunjika mguu wake wa mbele.

Kwa mazingira hayo, Mpelelezi akabaini kulitokea na purukushani eneo hili. Purukushani iliyosababishwa na mtu kupambania uhai wake.

Lakini kwanini mwanamke huyu kauawa? Swali hilo lilimkabili kichwa.

Kila alipoyatazama mazingira tangu mwanzoni mpaka hivi sasa, aliamini kabisa kifo cha mwanamke huyu kinamhusu yeye, kesi yake ama vyote.

Swala la kuona gari lile karibu na mazingira yake ya makazi na kisha kuliona hapa likiwa limeacha maiti nyuma, lilimwondolea shaka kuwa hili ni swahibu lake.

Lakini kwanini mwanamke huyu kauawa?

Alitaka kuamini kifo cha mwanamke huyo ni kutokana na kumiliki taarifa muhimu ya kiupelelezi, lakini nani alikuwa anajua?

Nani alifahamu kuwa yeye anakuja hapa kiasi kwamba akawahiwa hivyo?

Alianza kujenga mtandao wake kichwani tokea mwanzo mpaka mwisho.

Moja akawatuhumu wale watu wa chuoni, Stanford University, lakini alipokumbuka ya kwamba watu hao hawakuwa na taarifa yoyote kuhusiana na makazi ya huyu mwanamke, akapuuzia shauri hilo.

Pili ... Hapa akasita.

Akarudi nyuma kwenye mawazo yake.

Aliwaza.

Mtu aliyefanya haya alikuwa ni yule ambaye anajua yeye alipo kwani alipitia kwanza kwake kabla ya kuja hapa.

Je, ni nani huyo zaidi ya mkuu wake wa kazi?

Mkuu huyo alikuwa anafahamu makazi ya mwanamke huyu? Hapa hakupata jibu.

Akakumbuka simu ya Babyface.

Akakumbuka maneno ya mwanaume huyo kabla hajakata simu.

Hapa moyo wake ukapiga 'alarm'.

Kuna mambo yakamshawishi kichwani mwake kumhusu bwana huyo.

Lakini kwanini wafanye hivyo ingali jambo lao ni moja la kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya The DL?

Hapa upande mmoja wa akili yake ukamkumbusha ni namna gani kesi hiyo ilivyofanywa kuwa siri na mkuu wake, watu wakimtafuta mtuhumiwa pasipo kusema kusudi nyuma yake.

Lakini kama lengo lao ni mtuhumiwa, kwanini wahusike na mauaji ya ngazi inayoweza kuwasaidia kufika huko?

Ama tayari walishapata taarifa waliyokuwa wanatafuta?

Kama wameshapata kwanini wammalize mwanamke huyu?

Ilikuwa ni swali baada ya swali. Kichwa cha Mpelelezi kiligeuka kuwa uwanja wa fujo.

Mawazo yanatoka na kuingia.

Anawaza na kuwazua. Anajiuliza na kujijibu mwenyewe.

Akiwa anaogelea katika dimbwi hilo, mara akasikia sauti ya mlango ukifunguliwa.

Upesi akatoa bunduki yake ndogo mfukoni.

Aliishikilia bunduki hiyo kwanguvu kwa mikono yake miwili.

Macho yake yalikaa atensheni. Mwili wake aliusogeza kando akajibania kwenye ukuta akitulia tuli.

Masikio yamesimama wima kama mbwa anayeskiza hatari.

Kidogo, akasikia mwanaume anaita jina,

"Ronelle!"

Akarudia tena kuita na ghafla akasikia kishindo cha miguu kikivuma.

Kishindo hicho kilipokoma, kikafuatiwa na sauti kali ya mwanaume akilia.

Akimlilia Ronelle.

Mpelelezi akachomoza pale alipokuwa amejificha, akamwonyeshea mwanaume huyo mdomo wa silaha.

Akamwamuru,

"Simama juu, weka mikono wako nyuma ya kichwa upesi!"

Mwanaume huyo alikuwa amepiga magoti pembezoni mwa maiti. Mikono yake imejaa damu. Macho yake yanachuruza machozi.

Alikuwa ni bwana mwembamba kwa umbo, nywele zake kahawia iliyofifia. Mashavu yake hayana nyama, ni fuvu za chini ya macho zimesimama.

Meno yake yamekaa kwa ustadi mzuri isipokuwa chonge moja iliyopinda.

Alihofia sana kumwona Mpelelezi. Alihofia maradufu kuona mdomo wa bunduki ukimwelekea.

Aliogopa sana.

Aliona zama ya mtoa roho sasa ipo juu yake.

Akasimama upesi kama alivyoamriwa. Mikono kapeleka kisogoni, akiomba asiuawe.

Alisema,

"Tafadhali usiniue. Nitakupa vyote unavyotaka. Usiniue, nakuomba!"

Mpelelezi akamuuliza bwana huyo yeye ni nani na nini anataka hapo.

Bwana huyo alipotoa maelezo yake ndipo mpelelezi akabaini alikuwa ni yule aliyepokea simu ya awali ya mwanamke huyu aliyekuja kumfuata hapa.

Bwana huyo ni 'boyfriend' wa marehemu.

Kwa maelezo yake, alitoka hapo nyumbani kama nusu saa iliyopita akienda kutoa pesa kwenye ATM.

Mpelelezi alipojihakikishia kuwa bwana huyo ni salama, akashusha bunduki yake na kumtaka asogee karibu.

Akasogea.

Lakini alikuwa anatetemeka.

Baada ya nusu saa, magari ya polisi yakawa yamefika hapo, taarifa ilishatolewa kwenye vyombo hivyo vya usalama na vyombo kadhaa vya habari vimeshawasili kunakili yaliyotokea.

Bwana yule, 'boyfriend' wa Ronelle, alikuwa amejikunyata ndani ya gari la wagonjwa. Mpaka muda wa sasa hakuonekana kuwa sawa.

Alikuwa ameyakodoa macho yake muda wote kama mtu anayeshushudia jambo la kushangaza.

Amejikunyata.

Mwili wake ameufunika shuka zito akiacha kichwa tu.

Alitazama huku na kule lakini akiwa mbali sana kimawazo.

Mpelelezi yeye alikuwa amesimama kwa kando akitazama haya yanayoendelea.

Mvua iliyokuwa imekata kwa sasa, ilimpatia fursa ya kutua koti lake la mvua akalining'iniza begani.

Kidogo, afisa wa polisi akamfuata wakaongea mambo mawili matatu kabla ya afisa huyo kuondoka zake.

Mpelelezi akajiweka kwenye moja ya gari lililokuwepo hapo, akaanza safari.

Lilikuwa ni gari la kukodisha lakini si 'uber'.

Akiwa ameketi nyuma ya gari, akawa anajitafakari. Kidogo akatoa simu mfukoni akaitazama.

Simu hiyo ilikuwa ni ngeni.

Akiwa anaitazama, akakumbuka maneno aliyoteta na bwana yule, mwenza wa marehemu.

Alikumbuka maneno yake akisema,

"Hii simu ni ya Ronelle. Nishakupa 'password' yake. Namba hizo nilizokuambia zitakusaidia kuipata familia unayoitafuta "

Akatoa simu yake na kunakili namba hizo.

Akataka kupiga.

Akasita.

Alikumbuka mawasiliano yake na Ronelle.

Akahisi simu yake si salama tena kwa mawasiliano.

Akazirejesha simu hizo mfukoni kisha akatulia.

Dereva akamuuliza,

"Umesema San Pablo Lytton Casino?"

Mpelelezi akajibu,

"Ndio. Nipeleke hapo "

Aliposema hayo, akajikuta akipitiwa na taswira kichwani ya mwanamke yule mrembo aliyekutana naye katika jengo hilo maarufu la kamari.

Mwanamke aliyekuwa amevalia gauni jekundu.


***
Maana ya kidokezo cha mwisho ni nini
 
Back
Top Bottom