Tukibaki Hai, Tutasimulia

Tukibaki Hai, Tutasimulia

TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 16


Na Steve B.S.M




Mpelelezi aliingia ndani ya ukumbi wa San Pablo Lytton Casino.

Macho yake yalitazama hapa na pale. Huku na kule.

Alitazama saa yake ya mkononi. Kweli alikuwa amechelewa.

Alikuwa anailifahamu hilo.

Kutazama kwake saa kulikuwa ni kuangalia tu ni namna gani amekawia.

Alifika kwenye kumbi kubwa, akasimama na kutazama kwa kama dakika mbili hivi.

Hakumwona mlengwa wake.

Mwanamke yule hakuwapo kwenye uwepo wa macho yake.

Waliojaa hapa walikuwa ni wacheza kamari na wala starehe wengine. Walijaa kwelikweli. Lakini si anayemtafuta.

Akashusha pumzi fupi.

Akiwa ametundika koti lake la mvua mkono wake wa kushoto, akasogea mahali pa kujipatia kinywaji.

Alihitaji kitu cha kumpoza kwa siku hii ya leo wakati akitazama kama bado ana nafasi ya kumwona mlengwa wake.

Aliagiza glasi ya whisky, akaegama akinywa taratibu.

Mara kadhaa alikunja sura yake akimeza kitu hii ngumu akiwa anatafakari yaliyotokea leo.

Huku macho yake hayakulala. Bado yaliendelea kutazamatazama kama atabahatika kumwona mtu wake..

Alijiuliza.

Kwanini mwanamke yule hakuona busara kubadilishana namba pale walipoonana kwa mara ya kwanza badala yake akasihi waonane hapa majira kama haya?

Alipoyatafakari ya mwanamke huyo, akahitimisha kwa kukiri ni mwanamke wa kipekee.

Alitabasamu.

Namna alivyocheza naye kamari na kushinda kila mchezo, hili amekuwa akiliwaza sana, kwake ilikuwa ni ajabu mno.

Akashushia na fundo moja la whisky.

Alikunja sura kwa mbali akimeza fundo hilo.

Hivi vitu vigumu huwa anakunywa mara chachechache, siku kama ya leo.

Lakini kwake haijawahi kuwa tabu kamwe.

Si mtu wa pombe sana lakini alibarikiwa kichwa cha kuhimili pombe. Ni nadra sana kumkuta amezidiwa sababu ya ulabu.

Alisafisha koo lake linaloungua alafu akaagiza tena kinywaji.

Akanywa taratibu na kumaliza.

Bado hakufanikiwa kumwona mtu wake.

Kabla hajaagiza tena, akaona aendee mchezo wake aupendao. Mchezo wa kamari.

Aliketi katika mashine moja iliyokuwa pweke, akaweka pesa, mchezo ukaanza.

Alicheza mchezo mmoja baada ya mwingine. Aliweka pesa na kuweka pesa.

Kila alipoweka pesa, ikaliwa.

Kuna muda alibamiza mashine hiyo kiasi majirani zake wakamwangalia kwa taharuki.

Aliona linamfanyia kusudi.

Lakini hilo haikumsaidia kwani alipoweka tena, pesa ikaliwa.

Alihisi kichwa kimekuwa kizito. Ufanisi wake umepungua mno.

Yote hii sababu ya pombe?

Hapana. Alikataa.

Tangu lini?

Lakini kadiri muda ulivyozidi kusonga mbele ndivyo alizidi kuhisi anazidiwa.

Kichwa kinakuwa kizito, kinazungukazunguka.

Akaminya macho yake kwanguvu.

Punde, akahisi mkono kwenye bega lake la kulia. Kutazama, ni yule mwanamke mrembo.

Alikuwa amesimama akitabasamu.

Tabasamu mwanana linalovutia.

Nywele zake leo alikuwa amezilazia bega la kushoto, amevalia gauni la kijani lililoacha mabega yake yote wazi.

Gauni hilo lilimetameta na mwanga wa hapa.

Alilioanisha na kidani cha hereni yake ndefu iliyoning'inia katika sikio lake lenye matundu mawili ya kuvalia hereni.

Tundu la pili katika masikio yake, aliyavalia hereni fupi rangi nyekundu.

Rangi ambayo aliioanisha na mkoba wake mdogo usiokuwa na mkanda.

Mkoba huo alikuwa ameushikilia na mkono wake wa kushoto.

Mpelelezi akasema,

"Aaanh ni wewe!"

Macho yake yalikuwa malegevu.

Akajifaragua kusimama awe sambamba na mgeni wake.

Mwanamke yule akatabasamu akimwangalia.

Akasema,

"Naona umekuja."

Mpelelezi akamjibu,

"Ndio, nimeitikia wito wako "

Mwanamke akamwambia,

"Lakini umechelewa. Nimekuwa hapa kwa muda mrefu sana kukungojea."

Mpelelezi akahamaki akisema,

"Hivyo ulikuwa hapa hata nusu saa iliyopita?"

Mwanamke huyo akatikisa kichwa chake kuridhia.

Akamwambia Mpelelezi kwamba alimwona akifanya yote hayo mpaka kuja kwenye mashine hii ya kamari.

Muda wote huo tangu aingie macho yake yalikuwa pamoja naye.

Alisema,

"Nilitaka kuona uvumilivu wako kama upo sawa na wangu, haswa baada ya kuniweka hapa masaa."

Aliposema hayo, akamuuliza Mpelelezi kama angetaka kucheza naye michezo kadhaa. Mpelelezi akakataa.

Tayari alishapoteza michezo kadhaa hapa, na kichwa chake hakipo sawa.

Hata aliposema hayo, akapata fahamu ya kwamba miguu yake haikuwa na nguvu. Alikuwa anatumia jitihada kubwa sana kujikaza asije akaangukia chini.

Magoti yaligongana.

Yanatetemeka.

Aliomba Mungu wake anayemjua Mwanamke huyu asitambue mapambano yake hayo ya siri lakini alikosa matumaini.

Alihisi anaelekea kushindwa

Aliachana na mazungumzo ya mwanamke huyo akizingatia zaidi mwili wake unaoenda nje ya uwezo.

Jasho jembamba linamchuruza.

Mwanamke yule akamuuliza,

"Upo sawa, bwana?"

Akatikisa kichwa kuridhia. Uso wake ameukunja.

Ghafla, akaona ukumbi unabiduka chini kuwa juu na juu kuwa chini.

Kufumba na kufumbua yuko chini. Hoi!

Anawasikia na kuwaona watu kwa mbali sana. Hamna anachohisi mwilini mwake. Si joto wala baridi. Si maumivu wala furaha.

Haelewi.

Alisikia kwa mbali mwanamke akisema,

"Mungu wangu! Msaada. Nahitaji msaada."

Aliona watu, kwa muono wake hafifu, wakiwa wamesimama wanamtazama.

Wamesimama kama mishumaa.

Wanamwangalia pasipo kufanya lolote lile.

Hakuelewa watu hao walikuwa wanafurahi ama wanasikitika juu yake kwani nyuso zao hazikuonekana vema.

Aliwaona katika ukungu mithili ya kioo kilichoathiriwa na mvuke.

Muda kidogo akasikia mwangwi wa watu wakiangua vicheko huku glasi zikigongana kang-kang, kang-kang.

Kisha hureeeeee!

Akajipotezea fahamu.

***

Brooklyn, New York.

Asubuhi ya saa mbili.


Baada ya mhudumu kuweka mezani kisahani kidogo chenye 'hot ice cream', Richie alinyanyua kijiko chake upesi akajipakulia mdomoni.

Alikuwa amevalia shati pana lenye rangi ya kutu. Masikioni ana 'earphone' zisizotoa sauti. Chini ana jeans nyeusi yenye mkanda mpana uliobana kwanguvu shati lake.

Miguuni raba nyeupe.

Alikuwa na hamu kweli na ice cream.

Uso wake ulieleza namna gani alivyofaidi ladha hii adhimu kila alipoitia mdomoni mwake.

Akiwa anaendelea kufurahia chakula hiki, 'hafla, akasikia mtu akimwita kwa jina lake.

Mtu huyo alikaa kiti kilichomkabala naye, akatabasamu na kumjulia hali.

Alikuwa ni mwanaume mweusi mwenye kunyoa nywele zake kwa mtindo wa panki.

Ana ndevu nyingi zilizochongwa vema kufunika taya na kidevu chake.

Juu amevalia koti la 'jeans', ndani tisheti nyeusi. Chini amevalia suruali ya jeans rangi ya samawati na viatu vikubwa vya kaki aina ya 'Timberland'.

Aliambatana na begi mgongoni. Begi ambalo aliliweka mezani punde alipoketi chini.

Richie akatabasamu.

Huyu ndo' ambaye alikuwa akimngojea hapa.

Alisema,

"Upo ndani ya muda, Jamal. Hiko ndo' nakupendea."

Jamal, mwanaume yule mweusi, akamwambia akiwa anaegeshea mguu wake juu ya mwingine,

"Kwa namna ulivyonisihi, ilibidi niwahi hapa kabla ya kunyookea chuo. Ebu niambie ni kazi gani hiyo?"

Hapa Richie akamshusha presha Jamal.

Alimwambia,

"Ni udadisi wangu tu unanisumbua, bwana. Sijajua kama jambo hili ni kubwa ama lah japo hisia zangu zinanambia hivyo."

Akatoa 'flash drive' rangi nyeupe na kumpatia Jamal.

Akamwambia,

"Nitazamie kazi hizi uniambie nini maana yake."

Jamal akauliza,

"Kazi gani?"

Richie akamsihi,

"Tazama uone."

Jamal akafungua begi lake na kutoa tarakilishi yake ya kisasa chapa ya HP rangi ya fedha.

Akaifungua na kuiwasha kisha akapachika 'flashdrive' alopewa.

Akiwa anangoja, akaagiza kahawa kwa mhudumu. Punde kidogo kahawa yake ikafika ikiwa inafuka moshi.

Akanywa taratibu akibofya tarakilishi yake kwa kidole kimoja cha mkono wa kuume.

Baada ya muda kidogo, akamuuliza Richie,

"Nani amekupa kazi hii?"

Richie akajibu kwa kuuliza,

"Kwani vipi?"

Jamal akaendelea kutazama kazi hiyo akifungua kurasa baada ya kurasa, upesi akirusha macho yake ya kitaalamu.

Richie akajisogeza karibu naye apate kuona.

Alitazama kioo cha tarakilishi asipate kuelewa hata kilichoandikwa.

Akauliza,

"Kuna nini?"

Jamal akamjibu,

"Kuna vitu vingi sana ndani ya data hizi. Kwa haraka hivi sitaweza kujua kila kitu. Yanipasa kuwa na muda."

Richie akauliza,

"Kwani kwa ulivyotazama hapo, hujapata hata wazo tu la juujuu?"

Jamal akatikisa kichwa akisema,

"Si hivyo kama unavyodhani, Richie. Hizi data ni complex na zimewasilishwa kwa kutumia lugha ya kitaalamu ya kemia. Unahitaji muda wa kutosha kuzipitia na kuelewa.

Muda huu wa dakika kumi na tano hautatosha. Hizi fomula za kikemia zs molecular na structural ambazo zimewekwa hapa zina taarifa nyingi za compounds.

Nahitaji kuzichambua ili kupata picha kamili ni nini kinachoongelewa hapa."

Richie akashika kiuno. Akauliza,

"Kwahiyo itachukua muda gani?"

Jamal akamjibu,

"Nipe wiki hivi, n'takujuza hatua niliyofikia."

Richie akastaajabu,

"Hatua? Sio kwamba utakuwa ushajua kila kitu?"

Jamal akaguna.

Akaifunga tarakilishi yake na kuchomoa flash ya Richie.

Akamkabidhi akimwambia,

"Kama una haraka sana, tafuta mtu mwingine. Mimi sitaweza."

Richie akapaswa kuwa mpole.

Alitabasamu akimrudishia bwana huyo flash mkononi mwake akimsihi afanye vile anavyoona bora.

Lakini akaweka neno,

"Tafadhali jitahidi iwe upesi iwezekanavyo."

Jamal akamtoa hofu. Alimwambia atafanya kila kilichopo ndani ya uwezo wake.

Kwasababu ya muda kumtupa mkono, akafungasha vitu vyake aondoke. Hakumalizia hata kahawa yake mezani.

Aliweka begi mgongoni akatokomea akimwacha Richie anamsindikiza kwa macho.

Alipotokomea, ndo' Richie akampigia simu Hilda kumweleza kuwa ameshafika mahala walipokubaliana.

Yu upande wa kaskazini wa mlango wa mgahawa.

Baada ya robo saa, Hilda akawa amewasili eneo hilo.

Alikuwa amevalia kijisweta chepesi kilichokuwa wazi, rangi yake jani la mgomba lililokauka.

Ndani yake anashati jeusi lililofika mpaka mapajani.

Chini ana taiti nyeusi iliyomkaba mpaka kwenye enka za miguu, ikapokelewa na viatu aina ya 'allstars' rangi nyeupe.

Alivutia kutazama.

Watu kadhaa hapa mgahawani walimpatia muda wao kumtazama, haswa Richie ambaye alimtazama mpaka anafika na kuketi mbele yake.

Moyo wake ulikuwa unaenda mbio.

Hakuelewa kwanini hakuwahi kumzoea Hilda.

Kila mwanamke huyo anapotokea mbele ya macho yake basi amekuwa akimkamata mazingatio mithili ya jambo la kushtukiza.

Naye Hilda, kama mtu anayefahamu hilo, akatabasamu akimtazama Richie.

Aliketi.

Akatengeneza nywele zake kwa mkono wa kuume.

"Nimefika."

Richie akatabasamu. Punde mhudumu akaja na kumsikiza mgeni. Ndani ya muda mfupi chakula chepesi cha asubuhi kikawapo mezani.

Chakula hicho kilisindikizwa na soga za hapa na pale, wakitaniana na kuongea mambo ya jumla kabla hawajafika katika mada yao kuu.

Hapa kwa hamu, Hilda akamuuliza Richie juu ya kazi ile.

Alitaka kujua wapi alipofikia katika mkakati wake.

Richie akatabasamu kisha akajikomba kwa kujiamini.

Alimwambia Hilda,

"Kazi ipo mkononi mwa mtaalamu hivi sasa tunavyoongea. Ndani ya wiki hii tutakuwa tushapata kujua haswa kinachoendelea baina ya boss Bryson na mabwana wale."

Lakini Hilda alihofia.

Alikumbuka maagano yale aliyoapa kuhusu kazi hiyo kuwa kila jambo litakuwa siri.

Akamtahadharisha Richie.

Alimwambia laiti kazi hiyo ingelikuwa bado imo mikononi mwake kwa siri, basi katu asingelimhusisha kwa kuhofia kuhatarisha usalama wake.

Lakini katika hilo Richie alipiga kifua chake. Akamtoa hofu na kumjaza matumaini.

Alimwambia,

"Hilda, utafanyaje kazi usiyojua inahusu nini? Na hujakaa ukajiuliza kama boss wako anakulipa fedha kiasi kingi hivyo yeye atakuwa anapata kiasi gani? Kwanini hiyo kazi ina pesa nyingi hivyo?

Tumia akili, Hilda. Hii kazi inaweza ikawa mlango wetu wa mafanikio. Huwezi jua tutaibuka na nini hapa. Hamna mafanikio bila kubeba risk.

Tukubali kulibeba hili. Mbeleni, naona kabisa, kuna tuzo."

Hilda akasema,

"Lakini wewe Richie ndo' ulikuwa wa kwanza kunisihi kuhusu usalama wangu kwenye hii kazi. Mbona umegeuka ghafla hivyo?"

Richie akatumia fursa hii kumweleza Hilda juu ya namna gani alitafakari usiku mzima juu ya swala hili mezani.

Katika tafakari yake hiyo, alijiona yeye pamoja na mwenziwe wanavyoweza kutumia mwanya huu katika kutamatisha uduni wa maisha yao kwa ujumla.

Aliwaza namna gani watakavyoweza kufurahia maisha yao kwa kusafiri huku na kule kuburudisha nafsi zao kwa mandhari nzuri kama zile za Maldives na Copacabana endapo watakapojenga misingi ya pesa.

Lakini zaidi, hili ndani ya nafsi yake asimwambie mtu yeyote, aliona hii inaweza ikawa nafasi ya kujiwezesha kiuchumi katika namna ambayo ataweza kumhudumia mwanamke ampendaye.

Mwanamke huyu aliyeketi mkabala naye.

Hapo alisema na kifua chake pasipo kutumia kinywa na sauti.

Alisema na macho tu Hilda asielewe kitu.

Yeye aliendelea kutafuna, kwa taratibu, akiwaza haya mambo.

Ladha ya chakula aliisikia kwa mbali sana.

Richie alimshika mkono akamsihi amwamini. Kila kitu kitakuwa sawa.

Lakini zaidi akamwomba Hilda kiasi fulani cha pesa.

Kiasi ambacho kilimfanya Hilda aache kutafuna amtazame Richie machoni.

Akamuuliza,

"Dola elfu kumi? Ya nini yote hiyo?"

Richie akamweleza mpango wake.

Laiti wakitumia pesa hiyo, basi watamshawishi bwana Jamal aifanye kazi yao kwa haraka na ufanisi.

Aliamini kufanya kazi hiyo kiridhaa huenda ikapelekea wao kuchelewa malengo.

Hilda akatilia shaka.

Aliona pesa hiyo ni kubwa sana kiasi kwamba itamshtua bwana huyo kuanza kupeleleza nini kipo nyuma yake.

Badala yake alishauri iwe dola alfu mbili.

Hapo wakaridhiana.

Richie akanyanyua simu yake na kumpigia Jamal.

Aliweka 'loudspeaker'.

Bwana huyo alipopokea, akamweleza kuhusu ofa yake.

Jamal aliposikia hiyo ofa akasema kazi hiyo itakuwa tayari ndani ya siku tatu. Lakini kama wakiongeza kidogo basi ndani ya siku moja tu atakuwa ameikamilisha.

Hapo Hilda na Richie wakatazamana.

Richie akaonyesha ishara ya vidole kumi. Hilda akatikisa kichwa kukataa.

Akaonyeshea vidole vitatu.

Basi Richie akasema kwenye simu,

"Dola alfu tatu, kazi kesho iwe tayari."

Jamal akaridhia.

Alisema,

"Tuonane kesho majira ya asubuhi, hapohapo tulipoonana leo."


**
Meli inaenda kuzama[emoji3166]
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 17


Na Steve B.S.M



Brookhaven, New York.

Saa nne asubuhi


Bwana Lambert aliingia ndani ya ofisi akiwa analegeza tai shingoni.

Mkononi alikuwa ameshikilia mkoba mweusi wa ngozi.

Mkoba huo ulikuwa na kifungo cha chuma.

Aliushikilia mkoba huo vema, upo kifuani kwake ameukumbatia na mkono wake wa kuume.

Alipoingia tu ndani akaurejeshea mlango upesi na kwenda moja kwa moja kwenye kiti chake.

Akaketi na kuuweka mkoba wake ndani ya droo ya meza yake.

Kisha akatulia akiskizia.

Moyo wake ulikuwa unapiga kwa kasi.

Aliukua anausikia kabisa kwenye masikio yake makubwa.

Na pumzi yake haikuwa ya kawaida.

Alikuwa anahema kwa kasi japo si kwanguvu.

Alitulia hapo akifikiria.

Akifiria namna alivyotenda mpaka kufika hapo.

Alikumbuka nyendo zake zote alizopitia mpaka kufikia hapo alipoketi.

Akaona kila kitu kipo sawa.

Akashusha pumzi fupi kisha akatua koti lake sasa.

Koti kubwa jeupe

Akalipachika kwenye kiti kisha akawasha tarakilishi yake kwaajili ya kuandika baadhi ya taarifa ambazo zilipaswa kunakiliwa kwenye mafaili.

Akiwa anafanya hivyo, mara mlango ukafunguliwa.

Akarusha macho yake kutazama.

Mlangoni akawaona wanaume wawili waliovalia sare rangi ya bluu iliyokoza

Wamefunika vichwa vyao na kofia aina ya bareti zenye chapa ya ulinzi.

Wanaume hao, mmoja mweupe na mwingine mweusi, walikuwa wamebebelea bunduki mikononi mwao.

Bunduki kubwa mithili ya majangili wanaolenga kuangusha tembo nyikani.

Nyuso zao hazikuwa rafiki.

Macho yao makali yalimtazama Dr. Lambert kana kwamba mwalifu aliyetoka kufanya mauaji.

Naye Dr. Lambert akawatazama kwa kustaajabu.

Aliwatazama kwa macho yasiyoelewa chochote kinachoendelea hapa.

Aliwafahamu mabwana hawa kama wafanyakazi wa ulinzi wa kampuni mpya iliyopata tenda ya kuimarisha ulinzi eneo hili la maabara ya taifa.

Lakini pia aliwafahamu kama wana-ulinzi wa gredi ya pili, juu yao wakiwepo wanausalama.

Mabwana wale wanaovalia suti nyeusi.

Lakini kwanini hawa wako hapa wakiwa wamebebelea silaha?

Alikuwa anaenda kulijua hilo muda si mrefu.

Bwana mmoja kati ya hao walinzi wawili, yule mwanaume mweusi, akamfuata wakati mwingine akiwa amebakia pale mlangoni.

Akamwambia dokta,

"Tunataka kuona ulichokichukua kule maabara."

Dokta akastaajabu.

Alisema,

"Nini hiko? Sijachukua chochote mimi."

Bwana huyo mlinzi akamtazama kwa macho ya kina kirefu cha maji.

Hakuwa na masikhara.

Alitulia kwa kama sekunde tatu akimtazama dokta pasipo kutia neno.

Uso wake uliongea kila kitu.

Dokta akajifaragua akijitetea,

"Sijabeba kitu mimi. Naamini mtakuwa mmekosea au mmenifananisha."

Bwana yule mlinzi, akanyanyua silaha yake na kumwonyeshea.

Dokta akaogopa sana.

Kuona mdomo wa bunduki ukitazama uso wake kulimfanya atetemeke kwa hofu.

Bwana yule akasema,

"Sitarudia tena. Weka mezani kile ulichokichukua maabara."

Kisha akapayuka,

"Upesi!"

Dokta akaruka kwa woga.

Haraka, kwa mikono yake inayotetemeka, akafungua droo na kutoa mkoba mweusi.

Akauweka mezani.

Ulikuwa ni mkoba mweusi wa ngozi wenye kifundo cha chuma.

Punde tu alipouweka mezani, akanyoosha mikono yake juu na kusema huo ndo' mzigo wake alotoka nao maabara.

Wakati huo wenzake wawili walikuwa wameshafika katika eneo la tukio.

Walisimama kule mlangoni wakitazama kwa kurusha macho yao ndani wapate kuona yanayoendelea humo.

Walizuiliwa kuingia ndani na yule mlinzi aloiyesimama hapo.

Mmoja wao alikuwa ni yule bwana mfupi kuliko wote, na mwingine ni yule kijana mwenye umri mdogo kuliko wote humu ofisini.

Mlinzi yule aliyesimama mkabala na dokta, akauchukua huo mkoba mweusi na kuufungua.

Akaupekua.

Kwa kama sekunde kumi hivi alifanya zoezi lake kisha akaurejesha mkoba huo mezani.

Akamtazama mwenzie aliyekuwepo mlangoni na kumpa ishara ya kutikisa kichwa.

Hamna alichopata.

Kumbe ndani ya mkoba kulikuwa na kiasi kidogo cha chakula kwenye kontena na matunda mawili, ndizi mbivu.

Dokta akauliza,

"Ni nini mmeona humo cha ajabu?"

Mabwana wale hawakujibu. Hapa akapata nguvu zaidi ya kuongea.

Aliunyakua mkoba wake akiwatuhumu walinzi wale kwa kuenenda kama wanyama wasiokuwa na akili.

Alisema ya kwamba yeye hubeba chakula chake hata anapokuwa akifanya kazi maabara kwasababu ya matatizo yake ya vidonda vya tumbo.

Hawezi kungoja mpaka muda wa chakula cha mchana ufike.

Anapaswa kufanya hivyo kwani hapa karibuni hali yake ilikuwa mbaya zaidi kiasi cha kutapika damu.

Aliposema hayo, walinzi wakamwomba radhi wakisema walikuwa katika majukumu yao.

Kisha wakaondoka zao na hali ya hapa ikapoa.

Mabwana wale wawili, wenza na dokta, wakaingia na kumpa pole mwenzao huku wakiwarushia tuhuma wanaulinzi hao kwa kutokuwa makini na kusababisha taharuki kali.

Bwana yule kijana alisema,

"Sasa kazi yetu imekuwa kama gereza. Bunduki na risasi zimegeuka kuwa sehemu ya maabara."

Baada ya muda kidogo, hali ikarudi kuwa shwari na shughuli zingine zikaendelea kama kawaida.

Dokta Lambert, akiwa amehakikisha kuwa kila mtu hapa anashughulika na yake, akafungua droo ya pili ya meza yake.

Macho yake yalikuwa na wangalifu mkubwa.

Alifungua droo hiyo kwa utaratibu mno kiasi kwamba hakutengeneza sauti yoyote.

Kisha akaitazama kwa kuibia.

Mkoba wake ulikuwa umekaa kwa kutulia.

Mkoba mweusi wenye fundo la chuma.

Mkoba huu ulikuwa ni wa pili wakati wa kwanza ukiwa kwenye ile droo ya kwanza ya meza..

Droo ambayo aliutoa mkoba ule aliowapatia walinzi kwaajili ya kuukagua.

Akatabasamu kwa mbali.

Mchezo wake ulienda vile alivyokuwa anatarajia.

Mikoba miwili inayofanana kwa kila kitu ilitosha kabisa kumvusha mto yordani.

Akahisi moyo wake umekuwa wa baridi na adhma yake inaenda kutimia.

Akatabasamu tena.

Baadae jioni, majira ya saa kumi, akiwa ameshamaliza kila jambo hapa kazini akaliendea gari lake akiwa na mkoba wake mkononi.

Alilenga kwenda nyumbani moja kwa moja.

Akauweka mkoba wake mahali salama ndani ya gari kisha akatekenya funguo kuwasha chombo.

Kabla hajaondoka, akasikia ngo-ngo-ngo.

Kuna mtu aligonga kioo cha dirisha la upande wake wa kulia.

Moyo ukamlipuka mithili ya guruneti.

Alishtuka kwa hofu kubwa aliyojitahidi kuizuia isionakane lakini uso wake ukafeli.

Macho yake yalijawa na woga.

Alitazama upesi akamwona mwanaume, kwa nje, akiwa anampungia kwa furaha.

Alikuwa ni bwana yule mfupi anayefanya naye kazi katika ofisi moja.

Bwana huyo alikuwa anatabasamu kwa upana akipeperusha kiganja chake.

Akashusha kioo apate kumsikia.

Bwana yule akasema,

"Samahani sana, bwana. Nadhani unaelekea nyumbani. Unaweza ukaniacha hapo mbele kidogo?"

Bwana huyo alitaja mahali aelekeapo lakini Dr. Lambert akamruka kiunzi.

Alimwambia hapiti huko.

Hata na hivyo, bwana huyo akaendelea kusisitiza apewe lifti, atafahamu yeye mwenyewe pa kushukia huko mbele ya safari.

Dr. Lambert akafikiri kidogo.

Alikosa namna ya kumwepuka bwana huyu, hivyo basi, japo kishingo upande, akaridhia kwenda naye.

Akafungua mlango na kuingia ndani kwa furaha.

Akamweleza dokta namna gani anavyopata shida kwenye usafiri baada ya gari lake kupata hitilafu zinazochukua muda kuzitibu huko karakana.

Lakini maelezo yake, dokta hakuyajali. Badala yake alikuwa anawaza kero ya kumpakia bwana huyu kwenye gari yake akifahamu fika ni mtu wa maneno mengi.

Zaidi bwana huyo alikuwa akimpotezea mahesabu yake ya muda kwani alipanga kuongea na Mitchelle punde tu atakaposhika barabara akitoka maabara.

Aongee naye kuhusu mzigo wao kwasababu leo mwanamke huyo alikuwa akiungoja kwa hamu sana ikiwa ndo' siku ya mwisho kati ya zile alizompatia.

Basi aliendesha akiwa ametulia, mawazo mepesi yamemkaa kichwani.

Kuna muda alisahau kama ana mtu pembeni kwa namna alivyokuwa anafikiria mambo yake.

Muda aliomkumbuka akawa haachi kujiuliza bwana huyo atashukia wapi ili apate kuwa huru na shughuli zake.

Kuna muda alitamani kumshusha kwanguvu lakini ndo' hivyo, aliishia tu kutamani kwani asingeweza.

Jambo hilo lisingemjengea picha nzuri.

Gari likazidi kwenda huku mgeni wake haonyeshi dalili yoyote ya kushuka.

Hata alipobadili barabara akitegemea ataambiwa niache hapo, bado hakufanikiwa.

Mgeni alitulia tuli kana kwamba wanaelekea nyumba moja.

Swala hili likaanza kumjengea hofu taratibu.

Alijiuliza bwana huyu anataka nini?

Alianza kufikiria mienendo yake na hapa ndipo akakumbuka sakata lile la chooni.

Alikumbuka siku ile namna alivyotoka chooni kuongea na Mitchelle kisha akakuta mlango upo wazi.

Alipoenda kutazama ofisini hakumkuta bwana huyu mpaka kitambo kidogo aliporejea kutokea kusikojulikana.

Hapa hofu yake ikaongezeka zaidi.

Hajakaa vizuri, simu ikaita.

Hakuelewa ilikuaje, lakini alijikuta anatazamana uso kwa uso na bwana yule.

Akatoa simu mfukoni mwake na kutazama.

Ilikuwa ni namba isiyokuwa na jina lakini moja kwa moja aliishaitambua.

Alikuwa ni Mitchelle.

Akazima sauti kisha akaiweka simu juu ya dashboard ikiwa inatazama chini.

Kukawa na utulivu kidogo.

Lakini haikuchukua muda, simu ikaita tena.

Dokta akaitazama akiwaza. Mwendo wa gari kaupunguza.

Yule bwana wa pembeni akamwambia,

"Si upokee?"

Akamtazama.

Badala yake akaiminya tena simu hiyo na kuendelea na safari kidogo kabla hajaegesha gari pembeni na kumtama bwana yule ashuke.

Alimwambia,

"Nadhani hapa panakutosha. Naomba ushuke, nina safari zangu zingine."

Bwana yule akatabasamu.

Alikuwa ametulia kwenye siti yake kama mtu anayewaza jambo.

Kabla hajafanya kitu, simu ya dokta ikaita tena. Akamtazama dokta na kumwambia,

"Ni yule uliyekuwa unaongea naye chooni, sivyo? Sasa kwanini haupokei?"

Hapo dokta akayakodoa macho.

Akapokea simu ile iliyoita, akasema maneno machache,

"Tafadhali, nakupigia si muda mrefu."

Aliongea akiwa anamtazama mgeni wake. Alipokata, akiwa anatazama kwa walakini, akamuuliza bwana yule,

"Maongezi gani chooni?"

Bwana yule hakujibu. Aliendelea kutabasamu kwa mbali akitazamana na dokta.

Macho yake yalikuwa yanaongea.

Dokta aliyatazama kwa umakini akauona ujumbe wake humo.

Bwana huyo alikuwa anajua JAMBO.

Kumbe siku ile hakukosea kabisa kuwa na mashaka naye pale alipotoka chooni.

Alimuuliza,

"Dr. Jean, niambie ni nini unafahamu?"

Bwana yule akatabasamu sasa akionyesha meno.

Kisha akamwambia Dokta kuwa aliskia kila jambo aliloliongea akiwa chooni.

Lakini pia kama haitoshi, alikuwa anajua kilichotokea leo hii kuhusu mkoba ule mweusi wa ngozi.

Alimwona Dokta akiwa maabara na kupakia baadhi ya vitu kwa siri. Na hata alitambua kuwa mkoba ule aliompa mlinzi kuukagua haukuwa wenyewe.

Mkoba halisi ulikuwepo kwenye droo ya pili. Na huo ndo' mkoba ambao anao hivi sasa kwenye gari.

Alisema,

"Kabla ya walinzi kuja, mimi nilishaona ulichokifanya nikiwa nimesimama dirishani punde baada ya wewe kuingia ofisini.

Niliujua mchezo wote uliokuwa umeupanga, Lambert."

Dokta akakosa cha kusema.

Kwa muda akatulia kitini akijaribu 'kurewind' mambo yote kichwani.

Mbona kila kitu alikiona kipo sawa?

Akajiuliza

Ilikuaje akawa mzembe kiasi hiko?

Maswali hayo yakamnyima fursa ya kumzingatia mgeni wake kwa muda.

Alikuja kurudishwa mchezoni na sauti ya dokta Jean ikisema,

"Sasa naweza nikashuka nikaondoka."

Upesi akamwahi bwana huyo kwa kumshika mkono.

Akamwambia,

"Ngoja kwanza."

Kisha akamuuliza,

"Kuna yeyote umemwambia haya?"

Dokta Jean akajibu,

"Kwa sasa hapana. Sijajua hapo mbeleni."


***
Lah! Hallaullah! Namuonea huruma sana huyu Dr!
 
Kwasasa hapana, sijajua hapo mbele...
Mtu kama huyo unamlambisha sumu akafie mbele kimyakimya amenikera sana sana sana! Dah! Huyu lazima atachafua hali ya hewa huko mbele, lazima!
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 19


Na Steve B.S.M




Jamal akampatia Richie muhtasari wa data ile aliyompatia akaifanyie kazi.

Akamweleza ya kuwa yale yote yaliyomo katika taarifa hiyo yanamhusu binadamu na vijenzi vyake.

Data za muunganiko wa damu ya binadamu, mate ya binadamu na karibia kila kitu kuhusu kemikali zote zilizomo katika mwili hai wa binadamu.

'Chemical composition' za vyakula karibia vyote ambavyo hutumika na binadamu, na pia composition ya karibia kemikali zote ambazo ni sumu kwa matumizi ya binadamu..

'Chemical reactions' karibia zote zinazofanya mwili wa binadamu kufanya kazi kwa ufanisi wake, na athari ya kukosekana kwa kila kemikali ndani ya mwili huo.

Kemikali ambazo zipo tumboni. Kwenye mifupa. Kwenye ubongo.

Kemikali zote zinazozalishwa na ini la binadamu na kazi takribani mia tano za kikemikali zinazofanywa na 'organ' hiyo ndani ya mwili.

Alimwambia Richie,

"Kwa mujibu wa tafiti ya wanasayansi wa chuo cha California waliyoifanya katika mwili wa mwanamke mjamzito, walibaini kuna kemikali takribani mia moja na tisa katika mwili wa binadamu.

Ikiwemo kemikali hamsini na tano ambazo hazikuwahi kuripotiwa popote pale hapo nyuma.

Pia kemikali arobaini na mbili ambazo vyanzo vyake na matumizi yake katika mwili wa binadamu hayafahamiki mpaka leo hii kwa wanasayansi.

Kemikali hizo huitwa 'mystery chemicals'.

Huenda kila mmoja anazo.

Kazi yake mwilini, hakuna anayejua. Chanzo chake mwilini, hakuna anayejua pia.

Lakini ajabu ni kwamba, katika chapisho ulilonipa, zimeanishwa kemikali mia mbili ambazo ni 'mystery'.

Kemikali mpya kabisa, sijapata kuziona wala kujifunza popote pale. Haswa katika mwili wa binadamu.

Kemikali hizo sijajua kazi yake ni nini katika mwili uliotajwa. Na nilishindwa kutafuta majibu zaidi sababu ya masharti uliyonipatia."

Richie akasafisha koo lake kisha akayabandua macho yake kwenye karatasi alilokuwa anasoma.

Akamtazama Jamal usoni.

Mwanaume huyo mweusi alikuwa na macho mekundu. Ni wazi hakupata wasaa wa kutosha wa kulala usiku wa kuamkia siku hii.

Kazi hii ilikuwa kubwa mno.

Wingi wa makaratasi aliyoyashika Richie, ulithibitisha hilo.

Richie akauliza,

"Una uhakika hakuna mtu anayejua kuhusu taarifa hii?"

Jamal akaapa.

Alisema hata mwenzake anayelala naye hakupata kujua ni nini anafanya, hivyo kila kitu kipo salama.

Lakini akamwambia Richie kwamba kemikali hizo ambazo bado hawajazifahamu, huenda angepata taarifa zake kama angemshirikisha profesa wa chuoni kwao.

Alisema,

"Pengine hiko ndo' kinafanya taarifa hii kuwa siri. Huoni hilo?"

Richie akatikisa kichwa.

"Hapana, Jamal. Ni hatari. Naamini kuna taarifa nyingi zijazo, tutakapozipata kwa ukamilifu wake basi tutajua mengi. Acha kwanza nikapitie hizi."

Simu ya Jamal ikaita.

Aliichomoa mfukoni akaitazama. Jina Huncho.

Akaminya sauti kisha akaendelea na maongezi.

Alimtaka Richie ampate pesa yake aondoke kwani yuko nyuma ya muda.

Lakini akasihi chapisho lingine litakapopatikana basi apatiwe maramoja kwani kuna jambo amelihisi na nafsi yake.

Alisema,

"Yawezekana huu ukawa ni mradi wa kutengeneza watu. Sina uhakika lakini ... Sijui ... Nahisi tu."

Richie akamuuliza akiwa ameyakodoa macho yake,

"Kwanini unahisi hivyo?"

Akapandisha mabega yake na kuupinda mdomo.

Akasema,

"Kwa namna taarifa zilivyopangiliwa humo. Taarifa zenyewe zilizowasilishwa. Na usiri wake. Auhisi jambo? ... Ni hisia tu, nilishawahi kusikiasikia haya mambo ... kama nilivyosema hapo mwanzo ... Nahisi tu. Kama si hivyo basi yawezekana ni kuhusu Pharmaceuticals.

Tutapata dira baada ya kupitia kazi zijazo.

Lakini ..."

Hapa akarudi kwenye swali lake la kwanza kabisa alilouliza

"Richie, umetoa wapi hizi data?"

Richie hakuwa tayari na swali hilo. Akasema hayo ni yake na aachiwe mwenyewe.

Kama ilivyo ahadi, akatoa pesa ndani ya begi na kumpatia Jamal.

Jamal akahesabu na kuona ni timilifu. Akashukuru na kuaga.

Muda wote huo simu ya Jamal ilikuwa inaita kwa kutetemeka mfukoni.

Richie akamtazama mwanaume huyo akienda zake.

Alipotoka tu mgahawani, akatoa simu yake na kumpigia Hilda.

Akamweleza yale yote aliyopata kuambiwa na Jamal.

Alisema,

"Kama utapata muda, naomba tuonane."

Hilda akamjibu,

"Sidhani kama itawezekana leo. Kuna kazi kubwa ya boss Bryson nafanya hapa."

Richie akahamaki,

"Kazi nyingine?"

Hilda akamweleza ya kazi hiyo kuwa amepatiwa asubuhi ya siku hii pale alipokutana na Bryson mahali fulani.

Richie akapendekeza wakutane sehemu ili amsaidie kuifanya.

Pendekezo hilo likamfurahisha Hilda.

Alicheka mtu wa pembeni angesikia.

Kwa upande wa Jamal, bwana yule, kijana barobaro, aliyetoka kuongea na Richie muda si mrefu ulopita, aliingia ndani ya basi akaketi pembeni ya dirisha.

Alipoketi tu, akatoa simu yake iliyokuwa inaita mfukoni na kuipokea.

Alikunja sura akisema,

"Huncho, ukipiga mara mbili inatosha kwani nyumba inaungua moto?"

Sauti ya upande wa pili ikazozana naye. Ilikuwa ni sauti ya mwanaume ikikwaruza.

Sauti hiyo ilisema,

"Jamal, ulisema mpaka muda huu utakuwa ushantumia pesa yangu. Naona kimya, vipi?"

Jamal akamwambia yu kwenye basi. Pesa anayo mfukoni.

Punde atakaposhuka basi atamrushia kwenye simu.

Swala hilo likawa gumu kwa Huncho. Hakupenda wazo hilo.

Alitaka pesa yake cash.

Akamwelekeza Jamal mahali alipo kisha akasema anangoja hapo.

Jamal akakata simu.

Akairudisha mfukoni huku akiongea mwenyewe kwa kulalama.

Alisema,

"Madawa yatakuja kumuua huyu mjinga. Yeye anawaza unga tu, hamna kingine."

Baada ya robo saa akashuka toka kwenye basi.

Akaitoa pesa yake na kuitenganisha mfuko kisha akaendelea na safari.

Muda kidogo akawa amekutana na Huncho mahali palipojificha kiasi.

Mwanaume huyo alikuwa mrefu, mweusi, mwenye kuvalia nguo za rangi rangi nyingi.

Nywele zake amezisokota rasta zilizofika mabegani.

Usoni amevalia miwani nyeusi ya jua.

Jamal alimpatia pesa akazihesabu na kukiri zipo sawa kisha akasema,

"Tuonane tena siku nyingine."

Akaondoka zake akimwacha Jamal hapo.


***


New York Police Department, New York.

Saa sita mchana



Mpelelezi alitoka kwenye ofisi ya mkuu wake wa kazi akiwa ameshika kiuno.

Alikuwa amevalia shati jeupe na 'suspender' nyeusi. Suruali ya kitambaa na kiatu kinachong'aa.

Macho yake yalikuwa yamelegea kama mtu aliye na usingizi, kuchoka au vyote kwa pamoja.

Sauti kali iliyotoka kwenye ofisi ya mkuu wake ilifoka,

"Nakwambia unacheza na sharubu za simba. Sitakustahimili tena, afisa. Sitakustahimili tena!"

Mpelelezi akaufunga mlango na kwenda zake.

Uso wake umeparara.

Akiwa anajongea, akasikia mtu anamwita.

Aligeuka akamwona Babyface kwa mbali.

Bwana huyo alikuwa amevalia suti nyeusi nadhifu.

Nywele zake zinang'aa na kulala kama zimelambwa na paka.

Usoni mwake amevaa tabasamu pana linaloonyesha meno yake yote.

Alimpungia mpelelezi mkono, akamwonyesha ishara kuwa anakuja kisha akaenda zake mwelekeo wa ofisi ya mkuu wa upelelezi.

Mpelelezi akamtazama bwana huyo akiwa anatafakari yake kichwani.

Hakukaa hapo, akaelekea kwenye ofisi yake alipojibwaga katika kiti na kushusha pumzi ndefu puani.

Taratibu akiwa anazungusha kiti chake kwenda huku na kule, akawa anatafakari.

Alikuwa na mambo mengi kichwani.

Ni kama vile ujenzi wa ghorofa ulikuwa unaendelea katika ubongo wake.

Alitafakari mambo yanavyokwenda.

Moja baada ya jingine.

Akili yake ikampeleka mbali ...

Siku za nyuma: Majira ya saa nne asubuhi.

Kule San Fransisco, California. Majira ya saa nne asubuhi.


Aliamka kichwa kikiwa kinamuuma.

Alihisi mtu yumo ndani ya fuvu lake akibondabonda na nyundo.

Akiwa ameshika kichwa chake kuugulia maumivu, akakagua mazingira ya hapa alipo.

Palikuwa ni pageni machoni mwake.

Hayakuwa mazingira ya 'lodge' ile aloilipia.

Akaketi kitako akiwaza na kuwazua.

Palikuwa kimya sana hapa.

Hakujua amefikaje.

Aliwaza kama ni hoteli ama nyumbani mwa mtu.

Akatoka kitandani na kuufuata mlango.

Kifua chake kilikuwa wazi, akiwa amevalia suruali pekee.

Chini yuko peku, anauhisi ubaridi wa sakafu.

Kabla hajaufungua mlango, akasikia sauti ya mwanamke ikiwa inaongea huko upande wa pili.

Akatulia tuli, asikie mwanamke huyo anaongea nini.

Kwa dakika moja za kuskiliza, hakuambulia kitu.

Sauti haikusikika vema.

Ni kana kwamba mtu alikuwa anaongea akiwa ndani ya chungu.

Akaufungua mlango na kushika korido.

Alinyookea sebuleni akamkuta mwanamke akiwa ameketi kwenye kochi kubwa, mezani kuna sahani nyeupe yenye bites.

Sebule hii ilikuwa pana lakini yenye uhaba wa samani.

Makochi mawili tu yalikuwapo hapa pamoja na meza ndogo.

Ni bayana mkazi wa hapa alikuwa akipendelea zaidi nafasi kuliko mrundikano wa vitu.

Mwanamke huyo alikuwa anaongea na simu, na punde alipomwona Mpelelezi akakatisha maongezi yake ili apate kumlaki.

Alikuwa ni mwanamke yule wa Casino.

Alikuwa amevalia blauzi fupi rangi ya pink iliyoacha tumbo lake bapa kuwa wazi.

Chini amevalia kibukta kifupi rangi nyeusi chenye michirizi meupe pembeni.

Nywele zake amezibana kwa ustadi mkubwa usidhanie kabisa kama ni ndefu kiasi tunachojua.

Alitabasamu akasema,

"Karibu sana bwana. Naona umeamka."

Mpelelezi akamuuliza imekuaje akafika hapo. Alitaka kujua ni nini kilitokea jana yake usiku.

Mwanamke yule akampoza.

Akamsihi atulie kwanza, atafahamu kila kitu.

Alimuuliza,

"Unajiskiaje?"

Mpelelezi akajibu yuko sawa, lakini mwonekano wake ukiwa kinyume na anachosema.

Kila saa alikuwa anakunja uso wake kwa maumivu ya kichwa na mwenyeji wake akalibaini hilo.

Akamwambia,

"Nilikuandalia supu kwaajili ya hangover. Ni vema ukaipata sasa."

Mwanamke huyo akaenda jikoni na punde akaja na bakuli zuri lenye supu ndani yake.

Akampatia Mpelelezi akimkaribisha.

Lakini kabla Mpelelezi hajatia kitu mdomoni, akauliza,

"Nini kilitokea jana? ... Nataka kujua."

Mwanamke yule akamjibu,

"Nadhani ulikunywa kupita kiasi."

Mpelelezi akapata mashaka.

Hakuwahi kunywa kiasi cha kupoteza kabisa fahamu zake.

Hiyo jana kulitokea nini kiasi cha kushindwa kujimudu?

Ghafla akajipapasa mfukoni mwake.

Hakuhisi kitu.

Mwanamke yule akamwambia,

"Simu zako nilizihifadhi kwaajili ya usalama. Ngoja nikupatie."

Akaenda zake chumbani.

Mpelelezi akiwa hapo sebuleni peke yake, akarusha macho yake huku na kule kufanya ukaguzi wa mazingira ya hapa.

Kichwa bado kilikuwa kinamgonga.

Kuna muda alishindwa kuhimili akakishika kwanguvu.

Punde Mwanamke yule akarejea akiwa na simu mbili mkononi pamoja pia na dawa ya kutuliza maumivu.

Akampatia Mpelelezi.

Mpelelezi akanywa dawa hizo maramoja akisindikizia na maji mengi alopewa.

Akiwa anafanya hivyo, mwanamke yule akawa anamtazama kwa udadisi.

Alimwambia,

"Kunywa sasa supu yako kabla haijapoa."

Mpelelezi akafanya vivyo, lakini kiu yake ya kutaka kujua yanayoendelea hapa ikambana.

Alitaka kuuliza.

Upesi mwanamke yule akamsihi,

"Kula kwanza. Najua una maswali mengi. Nami ninayo pia."

Kisha akatabasamu.

Mpelelezi akazidi kuamini.

Mwanamke huyu alikuwa ni wa ajabu.


***
Nimependa sana taarifa ile ya kisayansi alivyo i present jamal! Ina data nyingi kuliko zilizo kua zimesha gundulika!! Huwezi kupata mahala data hizi popote zaidi ya kusoma
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 22

Na Steve B.S.M


Baada ya kitambo kidogo, hali ilitulia.

Mpelelezi kwa kutumia weledi wake wa kazi, akaanza kujenga mazingira ya kupata kile kilichomfanya afunge safari kutoka New York.

Mwanamke yule mzee, ambaye alikuja kujitambulisha kama mama wa mtoto aliyetangazwa kuuawa, akiwa anashukwa na machozi mengi, akaeleza namna mambo yalivyotokea.

Alivuta mafua mapesi, akatazama chini.

Macho yake yalikuwa mekundu sana. Uso wake umepwaya kama mtu anayejutia jambo au ametingwa na kitu fulani kizito.

Akiwa ametulia vivyo, aonekana kama yu mbali kimawazo, akaeleza namna gani alivyokuwa anampenda mwanaye.

Alikuwa ni kama tunu kwake, haswa ukizingatia hakubahatika kupata mtoto mwingine zaidi ya huyo.

Alisema,

"Alikuwa ndo' dunia yangu ya pekee. Furaha yangu. Sikujihisi mpweke ninapokuwa naye karibu. Alikuwa akinipenda na mimi nilijitahidi kadiri nilivyoweza kuurejesha upendo huo kwake."

Baada ya hapo, akaeleza namna gani swala la mwanaye kujinyonga lilivyomuacha katika bumbuwazi kwani hakuliona likitokea katika siku za usoni.

Alisema,

"Aliondoka kwenda chuo kama ilivyokuwa siku za kawaida. Sikuona ajabu wala dalili yoyote ile. Baadae majira ya saa mbili usiku, nikiwa na mashaka kwa kukawia kwake kurudi nyumbani nikamtafuta rafiki yake, Ronelle, kumuuliza kwasababu simu ya mwanangu haikuwa inapatikana.

Ajabu nilipompigia akasema hakuwa naye na hakumwona kabisa siku hiyo chuoni. Na kwa kudhania labda hajafika chuo, basi akaendelea na mambo yake kama kawaida.

Tukiwa katika hali hiyo ya sintofahamu, mimi na baba yake tukafanya jitihada za kuwasiliana na chuo. Hawakuwa na majibu.

Tulipotaka kupeleka taarifa kwenye vyombo vya usalama, tukaambiwa kiutaratibu ni mpaka pale siku kadhaa, angalau mbili, zitakapopita bila mrejesho wa mhusika basi ndo watalifanyia kazi shauri letu.

Japo tulieleza sababu ya kuwa na hofu, kwamba binti yetu si mtu wa kutoka na kuchangamana na watu, bado hatukuweza kuwashawishi.

Walishikilia msimamo wao.

Sitakuja kusahau, ni kesho yake majira ya asubuhi, nakuja kupata taarifa ya mwanangu kujinyonga.

Mwili wake ulikutwa mbali na chuo, ukiwa umekabwa na kitanzi, unaning'inia bila uhai."

Mama alipofika hapo, akashindwa kuzungumza kwa kama dakika tatu.

Uchungu ulimkaba kooni.

Alihisi kuna donge kubwa linalosugua kwenye shina la shingo yake na kifua.

Mpelelezi akapata kazi ya ziada ya kumtuliza.

Baada ya dakika hizo, sasa akapata kuendelea.

Akamweleza Mpelelezi kwamba aliushuhudia mwili wa mtoto wake ukiwa mochwari. Shingo yake imekuwa nyekundu kwa kubanwa na kamba ngumu.

Walifanya maandalizi ya msiba, lakini waliporejea tena mochwari hawakukuta mwili wa mtoto wao.

Walifanya kila jaribio, kila eneo waliloweza kufika lakini hamna kilichopatikana.

Mwili ulipotea mochwari katika mazingira ya ajabu mno.

Si kamera za hospitali wala walinzi walioweza kutoa majibu ya kueleweka.

Kote huko walisema hamna wanachokijua. Kilichofanyika ni 'attendant' wa zamu pamoja na security kusimamishwa kwaajili ya uchunguzi lakini baadae, baada ya majuma manne, walirejeshwa kazini kama kawaida.

Hivyo walichofanya, wakatengeneza tu kaburi katika mji wa Colma, mji tengefu kwaajili ya shughuli za mazishi ndani ya Jimbo la California.

Kutoka hapa San Fransisco mpaka huko ni takribani maili 3.23.

Walifanya hivyo kwasababu jiji la San Fransisco, tangu mwaka 1900, lilipiga marufuku shughuli za mazishi ndani ya maeneo yake kwasababu ya ukosefu wa sehemu sahihi kwaajili ya ibada hizo.

Ndani ya jiji hilo maarufu, kuna makaburi mawili tu, yale ya kitaifa (ya kiserikali) na yale ya Mission Dolores ambayo yapo chini ya wakatoliki.

Huko, Colma, wakaweka jeneza lisilokuwa na kitu kama sehemu tu ya kumbukumbu ya mtoto wao ambaye hawakupata kuuona mwili wake.

Alisema,

"Tuliona ni sahihi kufanya hilo kwaajili ya kuheshimu na kuonyesha uwepo wake duniani kisha akaondoka kama wapendwa wengine."

Alifuta kwanza machozi kabla hajendelea kunena mengine.

Naye Mpelelezi alikuwa naye sambamba kuhakikisha hamna anachokosa.

Masikio yake na ubongo wake vilikuwa hai kuliko kawaida.

Mwanamke yule akasema ya kwamba hata pale walipojitahidi huku na kule ili wapate kitu, matokeo yake mume wake akaaga dunia katika ajali ya hit-and-run.

Aligongwa kisha gari likatokomea likimuacha anamwagika damu kama fonteini barabarani.

Alichokuja kuambulia ni mwili wa mumewe ukiwa umepasuka kichwa, vipandevipande vya kutosha kabisa kwenye mfuko mdogo wa rambo.

Hapo Mpelelezi akapata taswira halisinya namna gani mwanamke huyu alikuwa anateseka.

Viatu vyake vilikuwa vikubwa mno kuviingia.

Alikuwa na kila sababu ya kulia akaeleweka na dunia nzima.

Hakumaliza, akaendelea akisema hakukoma kutafuta haki yake.

Alikodisha mpelelezi binafsi wa kuchunguza maswahibu haya baada ya kutumia polisi kushindikana, lakini mpelelezi huyo hakufika mbali.

Baada ya majuma mawili tangu ampe kazi hiyo, akapata taarifa kuwa bwana huyo amekutwa amejinyonga katika makazi yake.

Pembeni aliacha ujumbe wa wapi mwili wake upelekwe na kuhifadhiwa lakini hakusema nini kilipelekea maamuzi hayo ya kushtua.

"Kampuni yake ilikuwa katika kilele cha mafanikio," Mwanamke alisema, "ilikuwa ni ajabu kwake kuacha yote hayo na kutamatisha uhai wake."

Baada ya hapo, alikata tamaa ya kuendelea kutafuta tena.

Alipoteza matumaini.

Alijitenga na maisha na maisha yakajitenga na yeye.

Hata sasa anashangaa nini kilichomleta bwana huyu mpelelezi katika kesi hiyo ya miaka iliyopita.

Kesi ambayo alishaambiwa kuwa imefungwa rasmi muda tu.

Aliuliza,

"Kuna kitu mmepata? ... Mmejua nini kilimkuta mwanangu na mume wangu?"

Mpelelezi akashusha kwanza pumzi maana hakujua hata aanzie wapi katika maswali hayo.

Alichofanya ni kumpatia mwanamke huyo matumaini kwamba anaweza akapata kitu katika juhudi zake.

Angalau sasa amepata mwanga wa pa kuendea.

Kufikia hapo alitaka kujua hospitali ambayo mwili wa binti ulipelekwa, tarehe ambayo mwili ulitoweka, jina la ile kampuni binafsi ambayo iliyokuwa inahusika na upelelezi, na jina la mpelelezi huyo aliyefikwa na mauti akiwa anafanya kazi yake.

Alipovipata akashukuru, lakini kabla hajaondoka mwanamke huyo akampatia kijidaftari kidofo chenye jalada la pinki.

Akamwambia,

"Hii ni diary yake niliyopata kumnunulia. Pengine ukitazama unaweza kupata kitu."

Mpelelezi akaichukua.

Diary ambayo ndo' hii anayo mkononi hivi sasa.

Lakini hakuondoka huko bila kupewa onyo na mwanamke yule mzazi wa binti aliyekufa.

Onyo hilo hakuliacha kulisikia hata sasa.

"Kuwa makini na uhai wako."

Katika yote hayo, bado alikuwa na shauri la kurudi San Fransisco, California, siku za karibuni.

Alimini kabisa kuwa kule ndipo njia ilipo ya kufika anapopataka.

Akiwa taratibu anapitiq diary hiyo akitafuta kama kuna lolote anaweza kuambulia, simu yake ya mezani ikaita.

Alipopokea, akasikia sauti ya mkuu wake wa kitengo.

Alimwambia anamuhitaji ofisini maramoja. Akatii agizo.

Akaelekea huko ambapo alimkuta mkuu wake akiwa ameketi kwa kuegemaza mguu wake wa kushoto juu ya wa kulia.

Mezani kulikuwa na kisosi chenye kipisi kidogo cha sigara kinachoishilia moto.

Bwana huyo aliyekuwa amevalia suti rangi ya damu ya mzee, alikuwa ametulia vema ndani ya kiti chake kikubwa na kirefu chenye nyama za kutosha.

Alimtazama Mpelelezi, bila ya kusema jambo lolote, kisha akavuta droo ya meza yake kubwa, akatoa bahasha ya kaki, kimo cha wastani.

Akaiweka bahasha hiyo mezani akisema,

"Nadhani huu ndo' uamuzi sahihi kwa sasa."

Mpelelezi akaidaka bahasha hiyo asijue kinachoendelea.

Kabla hajaifungua, akaambia arejeshe bunduki ya polisi pamoja na beji yake rasmi. Hivyo vitabakia kituoni mpaka pale atakapopewa taarifa rasmi.

Mkuu alitoa angalizo,,

"Kwa sasa hauruhusiwi kujihusisha na kazi yoyote ya polisi. Hauna ithibati hiyo. Umepewa likizo ya lazima wakati tukiwa tunakagua mwenendo wako. Wakati huo wote utakuwa raia wa kawaida na malipo ya mshahara wako yatakuwa nusu ya kawaida."

Mpelelezi alipotaka kujua sababu, akaambiwa kwa ufupi kuwa ni utovu wa nidhamu.

Baada ya hapo, mkuu wake akamtaka aende zake kwani ana shughuli nyingi za kufanya.

Mpelelezi alipotoka, mkuu akawasha sigara kwa kiberiti chake cha gesi alafu akavuta mikupuo mitatu mikubwa.

Mikupuo ambayo aliivuta kwa hisia zote.

Mapafu yake yalipojaa, akautema moshi nje kana kwamba bomba la trekta.

Muda si mrefu, ofisi yake nzima ikajawa na moshi mnene.


****

Brookhaven, New York.

Saa kumi na moja jioni.


Dr. Lambert alifungua kifungo cha kola ya shati lake, kisha akashusha pumzi ndefu ya unafuu.

Sasa alikuwa anahema.

Mbali na uchovu wa kazi alofanya kutwa nzima, bado hakuwa tayari kwenda nyumbani.

Aliketi katika gari lake akingoja jambo. Macho yake yalikuwa yanatazama 'rearview mirror'' (kioo juu ya kichwa cha dereva) kwa umakini ingali akijitahidi kujiweka 'comfortable' kadiri awezavyo.

Mzee huyu alikuwa amevalia shati jeupe la mikono mifupi. Shati lenye mistari midogomidogo ya rangi ya zambarau.

Shati hilo alilichomekea kwenye suruali yake nyeusi ya kitambaa iliyobanwa na mkanda mnene wa kahawia.

Alingojea hapo kwa kama dakika sita ndo akamwona mtu katika kioo.

Alipotazama vema kiooni, akabaini ni mtu aliyekuwa anamngoja, yaani Dr. Jean.

Bwana huyo mfupi alikuwa amevalia shati jeusi lenye nyotanyota ndogo nyeupe zinazometa. Sarawili ya kadeti, rangi ya kahawia ilokoza, na viatu vikubwa vya ngozi.

Bwana huyo alitembea kuja uwelekeo wa gari la Dr. Lambert, lakini alipopiga hatua kadhaa alibadili mwelekeo wake akielekea upande mwingine.

Alifanya hayo akiwa hana utambuzi wowote kama mwenzake yu kwenye gari anamngoja.

Hapo ikampasa Dr. Lambert ashuke upesi kwenye gari lake na kujaribu kumpungia.

Hakuona.

Ikabidi amuite.

Bwana huyo akageuka na kumwona Dr. Lambert akiwa anapunga mkono kumwita. Akapaza sauti,

"Leo sielekei huko. Unaweza kwenda!"

Kisha akaendelea zake kana kwamba hamna kilichotokea.

Alipotembea kidogo simu yake ikaita mfukoni. Alipotoa kutazama, ni Dr. Lambert.

Akapokea.

"Ebu acha ujinga," sauti ya Dr. Lambert ilifoka na kuamrisha, "Njoo kwenye gari langu upesi!"

Alafu simu ikakata.

Bwana huyo akaona isiwe tabu, akaitikia wito.

Aliketi kwenye kiti cha pembeni ya Dr. Lambert alafu akauliza nini sababu ya wito huo.

Lakini akamsihi Dr. Lambert azingatie muda kwani ana mahali anapotakiwa kuwapo si muda mrefu toka sasa.

Dr. Lambert akajikuta anatabasamu.

"Wewe bwana," akasema akisontea kidole kwa mwenziwe. "Umekuwa wa kunipandishia mabega sasa, sio?"

Dr. Jean hakujibu kitu. Lambert akaendelea kumweleza ni namna gani yeye ni mkubwa katika lile 'deal' alilomtambulisha.

Namna gani alivyoanza 'misheni' hiyo na mpaka hapo alipofikia leo, hivyo Jean anapaswa kumsikiza na kumheshimu sana.

Katika hayo yote aliyojinasibu, Jean hakutia neno lolote, badala yake aliuliza,

"Hiko ndo' umeniitia?"

Dr. Lambert akashusha pumzi ya hasira. Alihisi kifua kinataka kupasuka.

Alijitahidi kumudu hasira zake kwa kuhema mara kadhaa, pumzi ndefu, kisha akarejea kwa upole.

Aliuliza,

"Ni nini mlijadili na Mitchelle siku ile kwenye gari? Nataka kujua."

Jean akatabasamu, kisha akajibu,

"Siko tayari kukwambia. Je, una lingine?"

Mbali na jibu hilo, macho yake yalimkera mno Dr. Lambert. Bwana huyo alikuwa anamtazama kwa mboni za dhihaka.

Basi dokta akajikuta akishika usukani kwa hasira.

Hajakaa vema, Dr. Jean akafungua mlango na kwenda zake.


**

Kuna nini kinaendelea kwa Dr. Jean?

Nini alizungumza na Mitchelle kwa siri siku ile alipokutanishwa naye?
Jean mpumbavu sana! Kuna watu wanakuaga vipele makazini ajabu
 
Hahaha.. Mimi nitakumbuka tu kuwa Mitchelle yuko mikononi mwa Dr Lambert kwasasa Hana ujanja tena!! Afanye aje kuimalizia hii kwanza jamani !!
wewe si umeimaliza juzi tu hapa,wengine tulikuwa nae bampa tu bampa
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 23

Na Steve B.S.M

East Hampton, New York.

Saa tano usiku



Gari dogo la wagonjwa, lenye rangi nyeupe na nyekundu, lilikuwa linakimbia katika 'highway likitoa sauti kali ya king'ora.

Juu ya gari hilo, kulikuwa na taa nyekundu na za bluu, zikiwakawawaka kuusindikiza msafara huu wa majanga.

Na kwa sababu ya hiyo, magari yaliyokuwapo barabarani yakawa yanapisha kutoa nafasi kwa gari hilo kuwahi huko linapoelekea.

Likavuka na kuyapita magari mengine kwa kasi.

Mara lilikuwa kushoto na mara kulia ... Kulia na mara tena kushoto.

Dereva, mwanaume mwenye makamo ya miaka arobaini na ushee, alishikilia usukani wake kwanguvu akiwa anatazama barabara kwa umakini mkubwa.

Uso wake mnene ulipambwa na masharubu meusi, kidevu chenye chengachenga za ndevu na macho makubwa ya mduara.

Macho ambayo yalifura kwa ndita, yakikodolea lami asije akaleta maafa.

Mwilini alikuwa na sare nyeusi yenye nembo sawa na gari hili. Nembo ya afya. Kichwani akiwa na kofia nyeusi pia yenye nembo sawasawa.

Pembeni yake, kiti cha pembeni, alikuwa ameketi bwana aliyevalia sawa na yeye, lakini yeye akiwa mchanga zaidi.

Kijana barobaro mwenye mwili mwembamba. Uso wake mrefu, kidevu chake kina ncha kali, masikio yake mapana na macho yake yamejawa na hofu.

Alikuwa anaogopa kasi ya gari hili.

Alitazama mbele kwa kukodoa, mkono wake wa kushoto ukiwa umeshikilia kwanguvu 'handle' juu ya dirisha la mlango wa gari.

Alitamani kusema jambo, lakini asingeweza.

Kwa nyuma yao, baada tu ya kuvuka kigingi kinachotenganisha watu wa mbele ya gari na nyuma ya gari, kulikuwapo na watu wanne.

Mmoja alikuwa ni mke wa Bryson.

Alikiwa amevalia gauni jepesi la kulalia, rangi ya bluu iliyokoza. Miguuni mwake ana viatu vya wazi vyenye manyoya mengi.

Nywele zipo timtim.

Uso ameukunja akimtazama mtoto wake aliyekuwa amejilaza juu ya kitanda kirefu chembamba.

Mtoto Cecy.

Amefunikwa na 'mask' ya kumsaidia kuhema, pembeni yake wakiwa wamesimama wataalamu wawili, mwanaume na mwanamke, wanaohangaikia hiki na kile kuhakikisha uhai unabaki katika mwili wa mtoto huyo.

Wataalamu hao walikuwa wamevalia sare lakini tofauti na wale waliokuwapo mbele ya gari.

Wao walijivalia makoti meupe, mafupi yanayoishia magotini.

Walikuwa wako 'busy' kwelikweli. Mara wamshike mtoto kifuani ... mara watazame mashine iliyokuwa inapiga kelele za ku-bip ... mara waongeze jambo katika mashine ... Mara wajadili.

Wakiwa wanafanya hayo, mama mtoto alikuwa anatazama kwa macho yake mekundu.

Macho yanayovuja machozi.

Macho yanayoonyesha hofu kuu iliyomea ndani yake.

Mikono yake ilikuwa inatetemeka. Kila alivyokaa, hakujihisi 'comfortable' kabisa, hivyo akawa anabadilibadili mikao kila mara.

Jasho, taratibu, linamchuruza kwenye paji lake la uso.

Mkono wake wa kuume ulikuwa umeshikilia simu ambayo ilikuwa hewani muda wote huo.

Upande wa pili wa mawasiliano alikuwamo mumewe akiwa anapashana naye habari juu ya kinachoendelea hapa.

Lakini ni kama dakika nne sasa zimepita, hawajazungumza kitu.

Simu bado ipo hewani ...

Kidogo sauti ya Bryson ikauliza,

"Bado hajaamka?"

Mwanamke, badala ya kujibu, akashikwa na uchungu uliotibuliwa na swali hilo.

Akaukunja uso wake maradufu machozi yakishuka mithili ya mto.

Mafua yakamparamia na kwikwi zikamkaba koo kiasi kwamba ikawa shida hata kuhema.

Kwa hayo tu, mumewe akajua kuwa hali si shwari.

Ilikuwa ipo wazi.

Ikampasa ajivike 'uanaume' kumtia mkewe moyo kuwa yote yatakuwa sawa. Asipoteze tumaini.

Wakati huo naye, bwana Bryson, akiwa katika gari lake binafsi, anajaribu kadiri awezavyo kufukuzia gari hili la wagonjwa.

Katika gari hilo alikuwamo na mtoto wake Cellina, pacha wa yule ambaye yumo katika gari la wagonjwa akiwa hoi, hajitambui.

Bwana huyu, alikanyaga pedeli ya mafuta kwa uzito wa mguu wake akijitahidi kuuweka umakini barabarani kadiri awezavyo.

Kwa mbali kidogo tu, alikuwa analiona gari lile lililombeba mtoto wake pamoja na mkewe.

Kwenye kiti cha pembeni yake, mtoto Cellina alikuwa amekaa kimya kwa kutulia sana.

Alivalia gauni rangi ya pinki lenye mauamaua na vijikatuni kadhaa vinavyochekelea na kufurahi.

Macho yake yalibeba hofu akionekana yu mbali kwa tafakari.

Si bure alikuwa anamuwaza mwenziwe, mama yake au wote kwa pamoja.

Yeye ndo' alikuwa mtu wa kwanza kumwona mwenzie akiwa amedondoka chini ghafla na kupoteza fahamu, wakiwa wanacheza tu chumbani.

Ilikuwa ni swala la kufumba na kufumbua ... anashuhudia mwenzie akiwa anatoka damu kichwani baada ya kujibamiza vibaya.

Sasa picha hiyo haikutoka kichwani mwake.

Alihofia sana japo baba yake alijaribu mno kumtuliza na kumtia matumaini kwa nguvu zote kwani alijua hali hiyo ni mbaya kwa mtoto huyu haswa ukizingatia afya ya moyo wake.

Muda kidogo wakafika hospitali, Cecy akashushwa na kupokelewa na wahudumu ambao walikuwa 'chap' sana.

Wakamhamishia kwenye kitanda chenye magurudumu na kumwingiza moja kwa moja kwenye chumba cha dharura.

Huo ukawa mwisho wa familia yake kumwona, kwani walitakiwa kungoja nje ya chumba ili wawapatie fursa wataalamu kufanya kazi yao huko ndani.

Wakakaa kwenye viti wakingojea kwa kihoro.

Wakiwa hapo wanasali na kuomba yote yawe kheri.

Bryson alimkumbatia mkewe na mwanae, Cellina, akajikuta anashindwa kuzuia chozi kudondoka.

Kama si kuutukuza uanaume wake basi angejikuta chini anagaragara jwa uchungu. Lakini baba akifanya hivyo, wengine itakuaje?

Wakakaa hapo kwa lisaa lizima, ndipo dokta akaja akihitaji kuonana na wahusika.

Alikuwa ni mwanaume mwenye makamo ya miaka thelathini. Mweusi, mrefu, nadhifu na mkakamavu.

Koti lake ni jeupe na shingoni ana kifaa cha kupimia mapigo ya moyo, 'stethoscope'.

Aliomba waelekee ofisini na wahusika wake hawakuwa na hiyana, wakaelekea huko.

Walipofika na kutulia, dokta akachukua maelezo ya wahusika akitaka kujua nini kilitokea na kama swala hilo ni la kawaida kwa mgonjwa.

Baada ya kupata maelezo aliyoyahitaji, ndipo sasa akaeleza kuwa mtoto Cecy ni mhanga mkubwa wa tatizo la moyo.

Kwa kawaida, moyo una valvu nne lakini kwa mtoto Cecy chemba moja haifanyi kazi vema na hiyo ndo' sababu mapigo yake ya moyo yamekuwa si ya kueleweka (irregular beats).

Tatizo hilo ndo' hupelekea mtoto kuvimba miguu, kupata kizunguzungu, kuzirai na kupata uchovu wa mara kwa mara.

Lakini pia mtoto yupo hatarini na ugandaji wa damu, kiharusi, moyo kufeli kabisa na hata kupelekea kifo endapo kama tatizo halitapata ufumbuzi haraka.

Alipoyasema hayo, kwa kutumia taaluma yake akatoa ushauri kwa wazazi hawa kuwa njia bora ya kumnusuru mtoto huyo na matatizo haya makubwa ni kufanya upasuaji mkubwa.

Upasuaji wa kupandikiza kifaa kitakachomsaidia kuongoza moyo wake kuwa na mapigo ya kawaida.

Hiyo ndo' itakuwa tiba pekee ya tatizo hili kwa sasa.

Daktari aliwatoa hofu kwamba mtoto anaendelea vema, lakini bado ataendelea kuwa katika uangalizi wa karibu mpaka pale watakapoona ana ahueni ya kutosha.

Baada ya maelezo hayo, bwana Bryson, maramoja, akaanza kufuatilia taratibu ya upasuaji wa mtoto.

Alitaka kujua gharama na utaratibu wake ili ajue namna gani anaweza kulivaa hili.

Alipopata taarifa za kutosha, akarejea kwa mkewe aliyekuwa ameketi kumngoja muda wote huo.

Hapo akaketi kama mtu aliyetoka kukimbia mbio za ushindani, kwani alishusha pumzi ndefu akifyagia jasho katika paji lake la uso.

Alipoketi akatulia sana akiyatafakari mambo. Huenda alisahau hata mkewe yupo hapo na hajaongea naye juu ya kilichosibu.

Mkewe alipomgusa kumshtua, bwana huyo akakurupuka. Hapo akarejea fahamuni.

Mkewe akamuuliza kinachoendelea naye akamweleza kila kitu.

Gharama za kufanya upasuaji ni kubwa mno, hata mfumo wake wa malipo kwa wale wanaotoa kidogokidogo (installments) bado si rafiki kwa wenye kiasi kidogo cha pesa, kwani muda wa kulipia ni mfupimfupi sana.

Kinachomuumiza zaidi kichwa, ana watoto wawili ambao wote wanahitajika kupata huduma hiyo ya upasuaji.

Fedha hiyo ni nyingi sana kiasi kwamba hata akitumia hati ya eneo lake la kazi kuomba mkopo bado haitatosha kukidhi mahitaji.

Sasa atapatia wapi hiyo pesa?

Alisema,

"Hata lile deal ninalofanya, pesa yake haifikii kiwango hiki, achilia mbali ndo' hiyohiyo ambayo pesa yake nimekuwa nikiitumia kwa muda wote huu."

Hapa pakawa na simanzi mbili.

Moja, ya mahututi ya mtoto na pili, mahututi ya kifedha.

Katika shauri hilo, mke akamshauri Bryson awasiliane na mtu yule anayempatia kazi ili amweleze shida zake. Huenda akamskiza na kumsaidia.

Alisema,

"Bryson, hatuwezi kuacha maisha ya watoto wetu yateketee. Hawa watoto ndo' kitu pekee tulichonacho ... Ndo' kitu pekee nilichonacho ... Kama unavyojua, sina uwezo wa kubeba mimba tena. Vipi nikiwapoteza hawa?"

Bryson akamtazama mwanaye Cellina. Alikuwa ametulia mapajani mwa mama yake, ameshapitiwa na usingizi kitambo.

Akayaangaza macho yake huku na kule. Watu kadha wa kadha wakikatiza na kuteta.

Lakini hamna aliyemzingatia hata mmoja. Mawazo yake yalikuwa mbali sana.

Mbali sana ...

Baada ya muda kidogo, akatoa simu yake mfukoni akatafuta jina Hilda na kupiga.

Alikumbuka kazi alompatia mwanamke huyo.

Zaidi alikumbuka kazi hiyo ina pesa yake taslimu punde itakapomalizika. Japo pesa hiyo si lukuki lakini si haba ... Si sawa na kutokuwa nacho kabisa.

Simu ikaita na kuita mpaka ikakata.

Akapiga tena.

Napo mchezo ukawa uleule ... Simu iliita mpaka ikakata.

Akalalama kwa hasira ...

Wakati upande wa pili, anayempigia akiwa analalama kwa raha tele kitandani.

Mwanamke huyo, yaani Hilda, akiwa hana moja wala mbili, alikuwa anajimwayamwaya katika kitanda chake kikubwa, hapo akiwa na mwanaume aliyekuwa anamkonga moyo.

Si mwingine bali Richie.

Wawili hao walikuwa wamezama katika dimbwi refu la huba kiasi kwamba hawakujali kabisa yanayoendelea duniani.

Kila mmoja alikuwa yuko 'busy' anashindana na mwenzake kuguna kwa raha wanazopeana.

Bryson akapiga simu mpaka akachoka.

Baada ya nusu saa, watu hawa walipomalizana, kila mmoja akiwa ameshusha alichokuwa amebeba, ndipo wakakumbuka simu zao.

Hilda, akiwa ameufunika mwili wake mnene kwa shuka tu, alitazama simu yake akakuta 'missed calls' za kutosha.

Naye Richie pia.

Wote walitafutwa na Bryson kwa muda tofautitofauti.

"Atakuwa anataka nini?" Richie akauliza.

Bwana huyo alikuwa amevalia nguo ya ndani tu. Mwili wake mkangafu wote ukiwa nje.

Hilda pasipo kujibu, akajaribu kumpigia boss wake na kidogo simu ikapokelewa.

Baada ya kulumbana kidogo kwa kutokupokea simu mapema, Bryson akaenda kwenye hoja iliyomfanya apige simu.

Akamuuliza Hilda kama ameshamaliza kazi alompa, naye Hilda akasema kwa upesi kuwa kazi imekwisha.

Kwa maana hiyo basi, Bryson akamtaka aiwasilishe kwake haraka iwezekanavyo.Hilda akasema kesho asubuhi atampatia.

Lakini haraka ya Bryson haikuweza kungoja tena. Alimsihi amtumie muda si mrefu kwa kupitia baruapepe.

Kisha akakata simu.

Akamwacha Hilda katika bumbuwazi.

Upesi akamuuliza Richie,

"Si umeshaimaliza?"

Richie akamwambia bado. Alitarajia ataimaliza mpaka kufikia kesho jioni.

Hilda akashika kichwa.

"Unasemaje, Richie?" Aliuliza akiwa ameyakodoa macho.

Kweli bwana huyo hakuwa amemaliza, na alitoka kumpongeza muda si mrefu kwa kazi alofanya!

Akamsihi upesi wachangake kwani kazi inahitajika iwe imetumwa kwa njia ya barua pepe muda si mrefu.

Kufumba na kufumbua Richie akawasha tarakilishi yake, kazi ikaendelea.

Akawa anachapa huku akiwa uchi wa kufunikwa na nguo ya ndani tu.

Lakini kila alipofanya kazi, muda ukazidi kuyoyoma akiwa bado yuko nyuma.

Kazi ni kubwa.

Wakawa wanangoja muda wowote simu itaita.

Lakini haikuita.

Wakaendelea kufanya kazi kwa haraka wanavyoweza.

Muda ukasonga.

Simu haikuita.

Kazi ikaendelea.

Simu haikuita.

Kidogo, mlango ndo' ukaita.

Ngo! Ngo! Ngo!

Hapa wakajikuta wanatazamana.

Mmoja yu ndani ya shuka na mwingine kwenye nguo ya ndani tu.


**
Duuuh! Mambo ya mua bungala haya! Wanazamisha meli hawa[emoji527][emoji533] , juu napo man down[emoji61][emoji2760]
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 24


Na Steve B.S.M




Kabla hawajakaa vema, kitasa kikasukumwa. Wote wakatazama huko mlangoni.

Lakini kwasababu mlango ulikuwa umefungwa na funguo, haukufunguka. Badala yake ulilalama na kutulia tu.

Hilda akapaza sauti kuuliza ni nani aliyemlangoni huku uso wake wenye mashaka ukimtazama Richie.

Wote walikuwa na wazo moja. Mtu aliyekuwepo mlangoni ni boss Bryson, naye amekuja hapo kwaajili ya kazi alompa Hilda.

Jambo la bwana huyo kukaa kimya wakati aliahidi atawapigia muda si mrefu liliwafanya wakaamini hivyo.

Wakaogopa sana kwani kazi haikuwa imeisha wala hamna dalili ya kufikia kuimaliza masaa ya hivi karibuni.

Hapa hata Hilda akajutia kwanini alimpa Richie penzi lake. Kama muda huo wangekuwa wanafanya kazi basi wangekuwa wamesogeasogea hata kidogo.

Ona sasa ...

Alijilaumu kwa ujinga huo ... Lakini angefanya nini? Alifahamu fika Richie ni mwanaume anayempenda kwa dhati, hivyo kumpatia penzi kungemteka akawa anamfanyia kazi zake bwerere huku yeye akiwa anapokea pesa taslimu toka kwa Bryson.

Sasa, kwa kitambo kidogo, alijutia. Atamweleza nini Bryson?

Hofu ...

Hofu ya bure.

"Mimi Jamal!" Alisema mtu aliyekuwa amesimama mlangoni.

Hakuwa anatania.

Sauti yake ilishuhudia.

Richie anaijua vema hata akishtuliwa usingizini. Bwana huyu amesoma naye kwa miaka kadhaa.

Yeye ndo' akaamka na kwenda mlangoni upesi.

Alivyokuwa anatembea, nguo yake ya ndani ilikuwa inapepea kana kwamba pazia la ufukweni.

Miguu yake membamba ilimfanya aonekane amevaliwa na chupi na siyo yeye kaivaa chupi.

Alifungua mlango akakutana uso kwa uso na Jamal. Bwana huyo alikuwa amevalia tisheti nyeusi yenye maneno meupe: I RUN NEW YORK.

Chini amevalia jeans iliyopauka na raba kali nyeupe, chapa ya New Balance.

Nguo zilikaa katika mwili wake kana kwamba amezitengeneza yeye, ama aliziwekea 'order' kiwandani.

Mgongoni mwake alibebelea begi jeusi lenye mikanda membamba ... Begi lililoonekana tupu kwa kiasi chake kikubwa.

Bwana huyo alistaajabu kumwona Richie katika mavazi yale. Macho yake yakauliza lakini kinywa chake hakikufunguka.

Akakaribishwa sebuleni alipoketi na kuuliza moja kwa moja alipo mwenyeji wa makazi hayo, hapo kidogo akatokea Hilda akiwa amevalia gauni jepesi, usoni amevalia tabasamu changa.

Alimsalimu akamkaribisha.

"Richie ameniambia mengi kuhusu wewe," alisema akimkarimu mgeni huyu, kisha na kuongezea, "lakini nashangaa alikuwa hajui kama unakuja mpaka akanijengea hofu nani anagonga mlango majira haya?"

Baada ya hayo majadiliano mafupi ya nani aliyekuwa mlangoni, huyu akisema hivi na yule akisema vile, na Richie akijitetea kuwa alisahau kabisa kwasababu ya kumezwa na kazi, wakaenda kwenye kile kilichowakutanisha hapa.

Jamal akasema ameitikia wito wa Richie kuja kuibeba kazi kwaajili ya mwendelezo wa pale walipoishia, hivyo kama ipo tayari basi apewe aondoke zake.

"Ngoja kidogo," Richie akamtuliza. "Kazi bado hatujaimaliza. Hata hapa bado tulikuwa tunahangaika nayo kwasabau inatakiwa muda si mrefu."

Alipofikia hapo, Richie akamwomba Jamal kuwa kama itawezekana awasaidie kuongeza nguvu kwenye kuimaliza kazi ile ili wapishe ratiba zingine.

Kidogo Jamal akawa mgumu.

"Lakini haya ni nje ya makubaliano yetu."

Richie akambembeleza akimwomba kama rafiki na sio mwenza wa kikazi sasa. Jamal akaridhia japo kishingo upande.

Alipiga mahesabu kichwani kwake akaona ni vema tu afanye hivyo kwani asipofanya basi hatopata kazi ya kuondoka nayo.

Na asipopata kazi hiyo maana yake hamna pesa.

Pesa anaitaka.

Basi wakiwa watatu wakaishambulia kazi hiyo kwa kasi waliyoimudu, kila mmoja katika uwanja wa tarakilishi ... Richie na Hilda wakitumia tarakilishi mpakato wakati Jamal akitumia ya mezani ilokuwepo hapa sebuleni.

Wakiwa wanafanya hivyo, bado Hilda akawa wa kutazama simu yake mara kwa mara.

Hakuna aliyepiga.

Hakujua kwanini lakini alihisi kuna kitu hakipo sawa.

Shaka hili alisema na moyo wake ...

----

Majira ya saa sita ya usiku ...

Taa za gari zilimulika kwa makali yake wakati gari likikata kona hii ya mwisho ya barabara kabla ya kuingia katika mtaa huu wa makazi.

Baada ya hapo, likatembea kwa kama mita ishirini hivi kisha likasimama na kuzima taa.

Mahali hapa palikuwa na ukimya wa usiku japo watu wachache hawakukosa kuonekana huku na kule wakikatiza mmojammoja, haswa kwa wanaume.

Majengo ya ghorofa yalokuwepo hapa yalikuwa yamewasha taa zake kwenye madirisha lukuki ya vyumba ... ni vyumba vichache tu ndo' vilibakiwa na kiza kwa ndani yake.

Bwana dereva akashuka toka kwenye gari yake na kuendea ghorofa mojawapo kwa mwendo wake wa kasi.

Hatua zake zilikuwa pana na mwendo wake wa ukakamavu kana kwamba mwanajeshi.

Alikwea ngazi na ghorofa ya pili tu, akawa amefika anapoelekea ... Mbele ya mlango, chumba namba 524.

Korido hili lilikuwa na mwanga hafifu. My

Taa ilikuwapo moja tu, japo ilikuwa na mwanga mkali lakini haikutosha kumulika korido yote kwa usawa.

Taa zingine zilishageuka kuwa historia. Ukizitazama unajua tu hazijaaribika leo, jana wala juzi, bali 'mamiezi' yalopita.

Yalishageuka kuwa maskani za buibui.

Bwana akagonga mlango mara moja na kabla hajaitikiwa, akabinua kitasa aufungue mlango.

Mlango haukufunguka.

Akaingiza mkono wake mfukoni na kuutoa ufunguo.

Kabla hajauzamisha ufunguo huo katika kitasa chake, akatazama kwanza kushoto kwa udadisi ... Hapo angalau akaonekana ni nani kwani mwanga ulokuwepo upande huo ulinawirisha uso wake japo kwa udogo.

Alikuwa ni bwana Bryson!

Alouchomeka ufunguo na kutegua kitasa. Mlango ukafunguka akaingia ndani kwa dhamira dhabiti.

Sebule ilikuwa na mwanga wa kutosha lakini hamna mtu hapo.

Ilikuwa ni tupu.

Tarakilishi iliyokuwepo mezani ilikuwa inawaka, na kwenye kochi kulikuwa na tarakilishi ya kupakata ikiwa imefungwa.

Bryson aliifuata tarakilishi hiyo akaishika ... ilikuwa ya moto.

Haikuwa imefungwa muda.

Akaielekea tarakilishi ilokuwepo mezani lakini kabla hajafika, mlango wa chumbani ukafunguka, akatoka Hilda.

Alikuwa amevalia taulo jeupe kifuani. Kichwani ana kiremba cha taulo pia. Uso wake mnene upo uchi bila ya miwani.

Akastaajabu,

"Oh ... Bryson!"

Kisha akaanza kujielezea kwa haya,

"Nilikuwa nangoja simu yako, nilijua utapiga si muda mrefu. Mbona ukawa kimya? ... Ooh ulikuwa unaendesha sio? Usingeweza kupiga simu ..."

Akatabasamu. Wakati huo Bryson aliendelea kutazamatazama huku na kule mara kadhaa kana kwamba kuna kitu anashuku.

Hakuchukua muda, wala kusema mambo mengi, akamwambia Hilda kuwa amefuata kazi hiyo mwenyewe.

Anaihitaji awekewe kwenye 'Flash drive'.

Akaitoa flash hiyo na kumpatia.

"Kwahiyo vipi tena kuhusu barua pepe?" Hilda akauliza, "Umeghairisha? ...." A
Kisha akacheka kidogo tusijue hata ni nini kilochomfurahisha "... Ilikuwa ni kazi kubwa sana, boss. Laiti ningepumzika basi nisingeweza kuimaliza kwa wakati kabisa ..."

Aliendelea kuongea mwenyewe mpaka mchakato wa kuhamisha taarifa ulipomalizika.

Akampatia Bryson flash akisema,

"Lakini boss, kwanini usiku wote huu na ghafla hivi?"

Bryson akamwambia alipata dharura, baada ya hapo akaenda zake.

Hilda akamtazama kwa maswali yaliyoendelea hata baada ya mwanaume huyo kufunga mlango wake.

Akaufuata mlango na kuufunga kwa ufunguo, alipogeuka akakutana na Richie aliyetoka mafichoni.

Kidogo naye Jamal akaungana naye.

"Atakuwa amegundua?" Richie akauliza.

"Sidhani ..." Hilda akajibu akipandisha mabega yake. "Lakini si kawaida yake kutokukaa ..." Akamalizia akiketi kitini.

Macho yamezama kwenye mawazo akijaribu kuelewa kinachoendelea.

"Inaonekama ana haraka sana," Richie akasema na kuongeza, "lakini amewezaje kufungua mlango na uliufunga kwa funguo? ... Ina maana ana ufunguo wako?"

Hilda hakujibu.

Badala yake alinyanyuka akaelekea zake chumbani.

Richie akakubaliana na nafsi yake kwamba hapa kuna kitu kinaendelea.

Kitu fulani asichokijua.

----

Alipojiweka tu kwenye kiti, akaubamiza mlango wa gari kuufunga alafu akatulia hapo kidogo.

Akawa anawaza.

Taratibu akayapitia yale matukio aliyotoka kuyaona kule kwenye makazi ya Hilda, akashindwa kujua nini kinajiri.

Kwanini Hilda aliongopa ametoka kuoga ingali mgongo wae ulionekana kuwa mkavu, haujapata hata tone la maji? ... Ni kifua chake ndicho kilikuwa na matonetone kuonyesha ametoka bafuni.

Kama hakutoka kuoga, kwanini alikawia kuja sebuleni alipofungua mlango? Alikuwa anafanya nini?

Tarakilishi mbili sebuleni zilizokuwa zinafanya kazi, moja ikiwa imezimwa muda si mrefu ... sehemu kubwa ya kiti kikubwa cha sebuleni kubonyea ... Hivi vikampa mashaka.

Kweli Hilda alikuwa mwenyewe?

Kama hakuwa mwenyewe alikuwa na nani? Na huyo mtu anafahamu kuhusu kazi wanayoifanya?

Na kama anaifahamu ...

Hapa akasita ... Aliona panatisha ... akabamiza kichwa chake akilaani anachokiwaza...

Akawasha gari lake na kuondoka upesi.

Akiwa njiani, akajilazimisha sana kuyasahau haya yaliyotokea hapa ili aweze kufikiria namna ya kunusuru afya za watoto wake.

Kwenye hilo, kama alivyokuwa amepanga hapo awali, akawaza hii 'data' alonayo mkononi ahakikishe haitumi kwa namna yoyote ile.

Badala yake ashinikize kuonana na mwanamke yule ili apate fursa ya kumweleza shida zake.

Kwa alivyokiwa anajua, kila anapopewa kazi ya kufanya, basi huchukua siku mbili kabla ya kuanza kuulizwa kama imekamilika au lah.

Hivyo Jua likichomoza, kabla halijafika katikati ya anga, atapokea simu ya kumuuliza hilo, na hiyo itakuwa mara ya kwanza kusema kazi imekwisha.

Tangu amefanya kazi hiyo hajawahi tumia siku mbili tu kuikamilisha.

Na kwasababu hana uwezo wa kuwasiliana na mteja huyo mpaka yeye mwenyewe mteja atakapopiga, basi hiyo itakuwa ni fursa adhimu kwake.

Kwasababu kazi imekwishakukamilika, basi atakata shauri kumwona.

Akaendesha gari njia nzima akiwaza hilo.

Hiyo ndo' ilikuwa njia yake ya pekee ya kupata pesa kubwa anayoitaka.

---

"Unadhani atagundua?" Richie aliuliza.

Hilda alikuwa amesimama kando akiwa ameshika kiuno. Jamal alikuwa ameketi kwenye kochi anawatazama kana kwamba ni 'telemundo' mbele ya macho yake.

Hilda akashusha pumzi fupi. Akatembea hatua nne na kurudi tano. Akatembea tena na kurudi tano.

Kichwani mwake kulikuwa kumejaa.

Mawazo pomoni ...

Alikuwa anajenga ghorofa kichwani mwake kwa mawazo lukuki.

Richie akasema,

"Tatizo alikuja ghafla sana. Hatukuwa na muda wakuhamisha data zote kwa pamoja. Mpaka mlango unachokonolewa na funguo nilikuwa nimeweka data yangu na yako tu, ile ya Jamal sikupata muda kabisa. La sivyo angetukuta hapa!"

Kisha akauliza tena,

"Unadhani atajua kwamba data haijakamilika?"

Akajijibu mwenyewe.

"Hatajua bana ... Enh? Tusiwe na hofu sana, n'na hakika hajui hata kilichomo ndani."

Hilda akamtazama kwa macho makali,

"Serious?" Kisha akauliza.

"Na je, huyo aliyempa hiyo kazi? Yeye hatojua kuwa ni pungufu?"

Swali likawa gumu.




***
Lazima pawake!
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 25




Na Steve B.S.M






Baada ya siku moja ...

Katika sehemu ya siri, majira ya jioni.

Jennifer akiwa amebebelea kikombe kidogo cha udongo kinachofuka moshi, aliufungua mlango mkubwa kukutana na kibaraza cha nje.

Kibaraza hiko kilikuwa kikubwa kwa wastani, kinaning'inia kwenye ghorofa hili, refu la hadhi ya kati.

Ghorofa lenye sakafu kadha wa kadha.

Kwenye kiti kikubwa cha mtindo, katika kibaraza hicho, alikuwa ameketi mwanamke maridadi, Mitchelle.

Mwanamke huyo alikuwa kavalia bukta fupi sana rangi ya manjano na blauzi nyeusi kwa juu. Nywele zake kazibana vema kwa nyuma, uso wake unang'azwa na miale dhaifu ya jua la jioni.

Alikuwa anatazama namna jua linavyozama. Alikuwa anapenda sana jambo hili. Alitulia hapo huku akiwa anatafakari mambo kadhaa kichwani.

Alipenda utulivu huu maana kichwani mwake kulikuwa na vurugu sana.

Pembeni ya kiti hicho kulikuwa na kijistuli kidogo cha kioo. Juu ya stuli hiyo kulikuwa na kijidaftari kidogo kilichofungwa, pembeni kidogo kalamu ndani ya mfuniko wake.

Jennifer akasogeza kijidaftari hiko na kuweka kikombe alichokuja nacho kisha akamkaribisha Mitchelle.

Alimwambia kwa lugha yake ya ishara,

"Nimeona nikutengenezee kahawa yako unayoipenda. Pengine itakupa 'mood' nzuri leo."

Mitchelle akanyanyua kikombe na kukitia mdomoni. Akanywa fundo moja ...

Aaaaahhh ... akajiskia vema. Ni kana kwamba mwili wake ulikuwa unangoja kitu hiki muda wote huo.

Alikunywa tena fundo la pili kisha la tatu ndipo akarejesha kikombe kwenye stuli.

"Ahsante sana, Jenny. Ulijuaje hiki ndo' kitu nahitaji kwa sasa?"

Jennifer akatabasamu kisha akamwambia namna gani anavyomfahamu, na mara zote anapomwona akiwa yuko chini basi humwinua kwa kahawa yake pendwa.

Mitchelle akatabasamu.

Jennifer akamwambia akitumia mikono yake,

"Kwa leo siku nzima ndo' nakuona ukitabasamu kwa mara ya kwanza. Kuna jambo linakutatiza?"

Akatazama kijidaftari kwenye stuli kisha akaongezea,

"Ni mambo yako ya biashara, sio?"

Mitchelle akashusha pumzi fupi kisha akajibebea kikombe chake cha kahawa. Badala ya kujibu, akanywa fundo la kahawa.

"Jipe muda wa kupumzika," Jennifer akaendelea kumuhasa. "Naamini kila jambo litakuwa sawa. Jana na juzi hujalala vema, hakikisha unapata usingizi leo."

Mitchelle akampatia uso wa kumuashiria amemwelewa lakini hakusema jambo na kinywa chake.

Aliendelea kutazama anga jekundu, jua sasa likiwa halionekani.

Jennifer akamtazama kwa kitambo kidogo kisha akakata shauri kwenda zake. Kabla hajafika popote, Jennifer akamuuliza,

"Umeshaniandalia zile nguo zangu za mtoko wa jioni?"

Jennifer akampa ishara kuwa tayari ashafanya vivyo alafu akaenda zake. Akabaki Mitchelle peke yake.

Peke yake katika utulivu aupendao.

Akafungua daftari lake mara moja na kuandika mambo kadhaa kisha akalifunga na kuendelea kunywa kahawa yake.

Kahawa ambayo alizidi kuipatia hamu kadiri anavyoitumia.

Hakuchukua muda mrefu, kahawa ikawa imeisha. Akamwita Jennifer amwongezee. Akiwa anangoja akapiga simu yake mara moja.

Jennifer akiwa anaandaa kahawa, akamsikia 'boss' wake akiwa anateta na simu. Sauti yake ilikuwa kali, anafoka kama mwehu.

Hata yeye akaogopa japo si mhusika.

Alipompeleka kahawa akamkuta akiwa amefura sana. Uso wake karibia wote umekuwa mwekundu.

Kwa hofu kubwa, akaweka chupa ya kahawa kwenye stuli, alafu akachoropoka upesi kwenda zake.

Hata Mitchelle hakumjali.

Alikuwa na mambo yake kichwani yanayomtinga. Mambo mengi kwelikweli.

Alikuwa anatazama daftari lake, akiandikaandika. Akikokotoa na kufunga hesabu.

Alisahau mpaka kahawa yake alomimina kwenye kikombe. Kahawa hiyo ikakaa mpaka ikapoa. Kahawa ilokuwepo kwenye chupa ndo' hakugusa kabisa.

Muda si mrefu alinyanyuka toka hapo akaenda kujiandaa. Baada ya muda mfupi akawa yumo ndani ya gari la kukodi, si 'Uber', akielekea kaskazini mwa eneo analoishi.

Alikuwa amevalia kawaida sana, si kama mtu mwenye mtoko mkubwa, hapa akiwa amejivesha blauzi na jeans tu.

Baada ya dakika kadhaa akawa amefika katika klabu moja ndogo, hapo akajiweka mahali palipotulia, muziki kwa mbali, akawa anakunywa taratibu wine kwa glasi.

Alimaliza glasi ya kwanza, ya pili ikiwa kati, bwana mmoja akaingia katika eneo hilo akiwa anaangazaangaza.

Bwana huyo alikuwa amevalia koti jeusi la ngozi, ndani tisheti nyepesi na chini jeans ikiambatana na raba nyeupe.

Bwana huyo alikuwa ni Bryson.

Alipoangaza upande wake wa kuume, Mitchelle akampungia mkono kumwita. Alisogea hapo na muda si mrefu akaja mhudumu kumsikiliza.

Akaagiza kinywaji laini ambacho hakikuchukua muda kufika. Glasi nyembamba yenye mrija mrefu wa kuvutia.

"Umekuja na kazi yangu?" Mitchelle akauliza.

"Ndio " Bryson akatoa flash kwenye koti lake na kumpatia Mitchelle.

"Ajabu," Mitchelle akasema akitazama flash hiyo, "kazi hii umeifanya kwa upesi sana. Ni kwasababu ya shida yako ama kuna kingine?"

Bryson akatabasamu. Tabasamu lake lilijieleza kuwa hiyo ndo' sababu ... Akanywa fundo moja la kinywaji chake kisha akaelezea ni namna gani alivyokuwa ana uhitaji wa kuonana naye.

Alisema,

"Unajua ni namna gani ilivyo ngumu kuonana na wewe. Niliamini nikifanya kazi hii nikaimaliza kwa haraka basi itakuwa rahisi kukushawishi."

Mitchelle akamtazama bwana huyo kwa macho ya udadisi. Akanywa fundo moja la wine yake alafu akamuuliza akiwa anaendelea kumtazama ... macho ya kupembua,

"Unataka nini, Bryson?"

Bryson kwanza akatulia. Alikuwa anayapanga mambo yake kichwani ... Alitafakari mambo yanayomkabili japo kwa muhtasari kisha akafunguka haja yake.

Alieleza namna gani alivyokuwa na uhitaji mkubwa wa pesa kwani watoto wake wanatakiwa kufanya upasuaji.

Akiwa anaeleza hayo, macho yake yalilenga kwa machozi. Na Mitchelle akajua namna gani bwana huyu alivyokuwa na shida haswa.

Asiseme kitu, akaagiza kinywaji kingine alafu akaulaza mgongo wake kitini.

Kwa ukimya huu wa sekunde chache, muziki laini uliokuwa unapiga hapa ukatawala.

Wimbo wa 'Stuck on You' wa Lionel Richie ulishika hatamu watu wakijifurahisha na vinywaji vyao, wengine wakiimba na wengine wakitikisa miili yao taratibu kuitikia wimbo huo mwanana.

Kwa muda huo Mitchelle, kama kobe aliyejificha ndani ya gamba lake, alikuwa anatunga sheria kichwani.

Kinywaji kilipowasili, akanywa kwanza mafundo mawili alafu ndo' akarejea katika mjadala huu.

Alisema,

"Bryson, pesa kubwa kama hiyo lazima iambatane na makubaliano. Nadhani utakubaliana na mimi katika hilo."

Bryson akasema,

"Bila shaka. Nipo tayari kwa makubaliano yoyote yale alimradi nisaidie watoto wangu."

Mitchelle akatabasamu.

Tabasamu dogo.

Kisha akasema,

"Ok, lakini huenda kuna jambo natakiwa kukusisitizia zaidi, Bryson. Mimi ni mtu 'strict' sana kwenye maagano ninayoyaweka.

Huwa sipindishi wala kupunguza kile ambacho ninaweka nacho maagano, na huo ndo' udhaifu wangu mkubwa. Hivyo nakusihi sana, kuwa makini unapofunga makubaliano na mimi."

Alipofikia hapo, akamkumbusha Bryson makubaliano waliyoyaweka hapo kabla. Alimuuliza kama bado anayaishi makubaliano hayo, naye Bryson akaapa kuwa kila kitu kipo kama vile walivyokubaliana.

"Usiwe na hofu kabisa," alimtoa shaka. "Nasimamia kila tulichokubaliana."

Akiwa anasema haya, akajikuta moyo wake unaenda kasi.

Aliyakumbuka yale mazingira aloyakuta kule kwa Hilda akajikuta anajikaza tu. Alijipa matumaini huenda hamna cha ajabu cha kuhofia kiasi hiko, lakini ... Vipi kama ... Basi tu ...

Aliomba kila jambo liwe kama vile anavyotaraji. Aliupiga moyo wake konde.

Asingeweza kuacha pesa hizi kwani alikuwa ana uhitaji mno.

"Sawa," akasema Mitchelle, "sasa nikuambie maagano yangu kama utayaridhia."

Bryson akasema,

"Niko tayari."

Basi Mitchelle akamweleza yake anayoyataka. Alichukua kama dakika nne kueleza kila agano. Alipomaliza akamwambia Bryson kuwa pesa itaingizwa kesho yake majira ya asubuhi katika akaunti ya benki.

Bryson akafurahi kweli. Hakuamini macho yake.

Alijiona mshindi wa kila vita.

Hakujali makubaliano aliyoyaweka ni makubwa kiasi gani bali ukubwa wa furaha ya kuokoa uhai wa wanae.

Aliondoka hapo akiwa na tabasamu usoni, na alipofika tu nje akampigia simu mkewe kumpatia habari hizi njema.

Naye mkewe akafurahi sana kwani sasa tumaini lilishuka.

Upesi wakatoa taarifa kwenye uongozi wa hospitali na maandalizi ya upasuaji ya watoto wote wawili yakaanza mara moja.

Mama akajawa na tabasamu.

Lakini hakumuuliza mumewe ni maagano gani aliweka kupata pesa hiyo kubwa ... Pengine hilo halikuwa na umuhimu kwake kwa wakati huo.

Cha muhimu ni kuokoa watoto.

Ndani ya klabu Mitchelle, akiwa sasa peke yake, akaagiza tena kinywaji, akaendelea kunywa taratibu akikoshwa na muziki kwa mbali.

Alitazama saa yake, ilikuwa ni saa mbili ya usiku, akaona aendelee kuuvuta muda hapo akingojea saa tatu ifike.

Muda huo alikuwa na ahadi nyingine, hivyo hapa alikuwa na kama lisaa limoja la kukaa. Akautumia muda huo kunywa na huku akitafakari mambo yake ya pesa.

Alinyanyua simu yake akampigia Taiwan, simu ikaita na kupokelewa ndani ya muda mfupi.

Akasema,

"Nitakuja mwenyewe kwenye mnada."

Taiwan akaita,

"Naam!"

Mitchelle akarudia taarifa yake kwamba atahudhuria mwenyewe kwenye mnada.

Taiwan akauliza,

"Ma'am, kuna haja ya wewe kuja huku? Au ni kwasababu ya kudorora kwa biashara hapa karibuni? ... Usijali, nitasimamia kila jambo na kila kitu kitakuwa poa si muda mrefu."

Mitchelle akamwambia kuwa hili jambo atalisimamia yeye. Anataka iwe hivyo.

Aliposema hayo akakata simu.

----

Ni jambo gani Mitchelle amejadiliana na kukubaliana na Bryson?

Shaka la Bryson kwenye usiri wa Hilda litaishia wapi?

Ni mnada gani Mitchelle anataraji kuhudhuria?

Na miadi yake ya saa tatu usiku ni kukutana na nani?


***

Saa nane usiku ...

Mitchelle alipotoka bafuni alikuta kila kitu kikiwa kimeandaliwa mezani, pamoja pia na tarakilishi yake.

Ulikuwa ni usiku mkubwa lakini tayari Jennifer alishafanya kazi yake.

Punde tu Mitchelle aliporejea, aliamka akatimiza wajibu wake huo na sasa alikuwa pembeni akingoja kupakua na kuanua vyombo.

Macho yake yalikuwa mekundu, ameelemewa na usingizi. Japo Mitchelle alimsihi akapumzike lakini bado aliona ni kheri kuwapo hapa.

Alimpakulia Mitchelle chakula chepesi alichokiandaa, supu na 'bites', kisha akaketi kungoja. Mitchelle akawa anakula huku akipapasa tarakilishi yake.

Alichomeka 'flash drive' alopewa na Bryson akawa anatazama kazi yake humo.

Alichokuwa anafanya ni kuwianisha kati ya kazi hiyo na ile aliyoipokea toka kwa Dr. Lambert kuona kama zinarandana.

Taratibu alikula na taratibu akawa anapekua kazi.

Muda si mrefu, akabaini kazi ile haikuwa imetimia.

Takribani karatasi kama kumi na mbili hivi hazikuwapo!

Mapungufu hayo yalikuwa ni makubwa sana kiasi kwamba yalionekana kwa wepesi mno kwenye macho ya Mitchelle.

Akajiuliza, ina maana aliyezichapa hakufahamu upungufu huo?

Akaamini huenda alizichapa kwa haraka ili amletee upesi na amweleze shida yake, hapo akampigia simu Bryson kuhakiki wazo lake.

Akamuuliza kama kuna tatizo lilijiri katika uchapaji wa kazi, bwana huyo akamtoa shaka kuwa kila kitu kilienda sawa.

Alihakikisha hilo kabla hajaweka kazi hiyo kwenye flash drive.

Aliuliza,

"Kwani kuna tatizo?"

Mitchelle akamuuliza idadi ya karatasi zilizoandikwa, hapo Bryson akapatwa na kigugumizi. Alijitetea kuwa alizichapa kwa haraka hivyo hakupata wasaa wa kutazama idadi.

Mitchelle akakata simu.

Maelezo aliyoyapata yakamzalishia mashaka zaidi.

Aliwaza ...

Ina maana Bryson hakufanya kazi ile kwa mikono yake?

Alimpatia nani?

Mbona aliahidi hapo awali kuwa anafuata makubaliano waliyoyaweka?

Hamu ya chakula ikamwisha.

Alisikia damu ikimkimbia kwa kasi mwilini mwake.

"Uko sawa?" Jennifer akamuuliza akitumia mikono yake.

Alimsogelea karibu akimtazama kwa macho ya mashaka.


****
Loooh! Nungwi hapo chombo cha zamaaa!
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 27




Na Steve B.S.M






Basi baada ya kitambo kidogo, ndege ikatua ndani ya jiji la San Fransisco na Mpelelezi akatafuta mahali sawia pa kujipumzisha, ilikuwa ni ndani ya hoteli moja yenye hadhi ya kati, hapo aka-book chumba chenye kujitosheleza alafu akajitupia kitandani akiwa na tarakilishi yake.

Yalikuwa ni majira ya saa nne ya usiku, ndege ilitumia masaa sita na dakika ishirini na kitu kutokea New York mpaka kufika kwenye jiji hili ndani ya jimbo la California.

Taratibu akiwa hapo kitandani, akaanza kupitia kesi zile za maiti kupotea mochwari, moja baada ya nyingine, akizitazama kwa umakini na akijaribu kuzisoma mazingira yake, akaandika kila kilicho cha muhimu katika kesi hizo.

Alikuwa anatafuta ni nini kinachofanana katika kesi zote hizi, na baada ya muda mfupi wa kuzikagua na kuzilinganisha akabaini jambo, watu wote waliouawa walikuwa ni wanafunzi, watatu kati yao walikuwa wanasoma chuo, wawili wakiwa high school.

Swala hili likampa mafikirisho mapya, kwanini wanafunzi? Alijaribu kufuatilia wanafunzi hao kwa tovuti za chuo na shule walizokuwa wanasoma, akagundua ni wanafunzi walokuwa werevu sana kitaaluma, mara kadha wa kadha waliwakilisha taasisi zao katika mashindano mbalimbali ya kitaaluma wakaibuka washindi.

Hapo akajikuta anataka kufahamu jambo, basi upesi akampigia simu mwenzake, afisa yule mnene mwenye kuvalia miwani anayemsaidia kwenye mambo haya ya upembuzi, na baada ya simu kuita kidogo ikapokelewa.

"Hey Travis!" Mpelelezi alisalimu na kuuliza, "Upo wapi?"

Travis akamjibu yu mahali amepumzika anajiburudisha kabla ya kurejea nyumbani, basi akamsihi,

"Kesho utakapokuwa kazini, naomba unitumie anwani za makazi ya wale watu ulioniambia, tafadhali usisahau, ni muhimu."

Travis akamwondoa shaka, atafanya hivyo, na huo ukawa mwisho wa mazungumzo yao, qkafunga mashine yake na kwenda kuoga ili atoke, alidhamiria kwenda Casino akajiburudishe na michezo kadhaa ya kamari, lakini leo akilenga kushinda zaidi kwani alikuwa na njaa na pesa.

Hakujua hapa San Fransisco atakaa kwa muda gani, hivyo kumudu mahitaji yake huku mshahara wake ukiwa nusu, ni lazima atafute njia mbadala ya kupata pesa.

Alitoka chumbani kwake, akashika ngazi kushuka chini. Aliposhuka ngazi kadhaa, akasikia sauti za watu wawili wakizoza huko chini, mmoja mwanamke na mwingine mwanaume.

Sauti ya kike akaitambua ni ya mhudumu, kwani si muda mrefu alizungumza naye kwaajili ya kujipatia hifadhi ya chumba kwahiyo bado anaikumbuka vizuri, lakini hii ya mwanaume hakuwa anaifahamu, alihisi ni ngeni masikioni.

Akashuka ngazi sita akizidi kusikia sauti za watu hao, na saa hii akili yake ikaanza kubishana na nafsi yake kuhusu sauti ile ya kiume.

Alihisi anaijua, hapana, akakataa haijui, mara akahisi anaijua, ila ... hapana, hapana, akasema tena na nafsi yake, siijui sauti hii, kidogo akasema anaijua, na akabaki hapa alipozidi kushuka ngazi.

Kadiri alivyokuwa anaisikia sauti hii ndivyo akili yake ikazidi kumwaminisha kuwa anaijua, na kweli alikuwa anaijua, sauti hii ya kiume ilikuwa ni ya yule mwanaume mlemavu alokutana naye kwenye ndege!

Hakutaka kuamini hili, ila ndo' ulikuwa ukweli wenyewe, ilikuwa ni sauti ya yule bwana mlemavu wa kule kwenye ndege! ... Ina maana yupo hapa?

Sababu hiyo ikamfanya aongeze kasi zaidi katika kushuka ngazi, alitaka kujua hiki anachokiwaza ni kweli au lah.

Alipofika chini hakuamini macho yake, ni kweli kabisa vile alivyokuwa anafikiria, pale mapokezi alikuwapo bwana yule mlemavu katika miwani yake meusi!

Akastajaabu ... Ni namna gani anagumiana na bwana huyu katika mazingira yanayofanana?

Alisimama hapo akitazama, akabaini bwana huyo anataka kuchukua chumba hoteli hiyo, na kweli yule dada wa mapokezi akampatia gharama na bwana huyo akaingia mfukoni kutoa pesa. Alitoa pesa kadhaa na kumpatia huyo dada, naye akapatiwa funguo za chumba nambari 112.

Hiko ni chumba cha pembeni kabisa na kile cha Mpelelezi kwani yeye anakaa chumba nambari 111!

Mpelelezi, akiwa amepigwa na butwaa na akisikia haya yote yanayoendelea hapa, akasimama wima kama mshumaa akiwa ameyatoa macho yake kwa bwana yule mlemavu huku akili yake ikiwa inawaka kwa tafakari.

Alimuwaza sana bwana yule, je alikuwa ni mtu wa kawaida? Hakupata jibu, lakini juu ya yote aliona kuna haja ya dhati ya kumtilia bwana huyu maanani.

Maanani ya karibu.

Mhudumu alimuuliza,

"Ungependa nikusindikize?"

Bwana yule akatabasamu kisha akasema, "itakuwa vema zaidi."

Basi yule dada akatoka katika dawati lake na kuongozana na huyu bwana akimsaidia kumshika, wakaelekea kwenye ngazi, hapo wakapishana na Mpelelezi wao wakipanda juu.

Mpelelezi akawatazama mpaka wakaishilia, alisikia maongezi kidogo kisha akasikia mtu akishuka ngazi upesi, alikuwa ni yule dada wa mapokezi baada ya kumaliza kazi yake, hapo naye akatoka zake hotelini kuelekea nje.

Alipofika huko, hakuchukua muda mrefu kupata taksi, akakwea na kuelekea Casino.

Lakini barabarani alijikuta akimuwaza mtu yule hotelini.

***

"Hapana, inatosha!" Travis alimkatazama mhudumu kuongeza kinywaji kingine mezani kwani alikuwa ametosheka sasa, akalipia 'bill' yake na kunyanyuka akitazamia kueleka nyumbani kwake majira yakiwa ni saa tano ya kuitafuta saa sita ya usiku.

Aliliendea gari lake katika eneo la maegesho, akajiweka ndani na kutikisa kwanza kichwa chake kuona kama kipo sawa, alihisi pombe zimemzidia lakini baada ya kufanya hivyo akajiaminisha yuko sawa, anaweza kuendesha gari na kufika nyumbani salama, basi akatia moto gari yake kwa kutekenya ufinguo, lakini kabla hajaenda popote akastaajabu amekabwa shingo na mikono tokea nyuma!

Mikono minene yenye misuli ya kutosha.

Mikono hiyo ilimkaba kwanguvu kiasi kwamba akayatoa macho yake nje kana kwamba matufe.

Kabla hajafanya chochote, kitambaa cheupe kikafunika pua na mdomo wake, hakuchukua muda akapoteza fahamu, mara punde gari nalo likaondoka lisijulikane wapi linaelekea.

***

Taiwan, Majira ya saa sita usiku ...

Baada ya kutema moshi wa sigara nje, bwana Taiwan alisafisha koo lake kisha akamwambia mwenzake aliyekuwapo kando,

"Inabidi tuibuke na mpango haraka, la sivyo mambo yataharibika kabisa."

Bwana huyu, yaani Taiwan, alikuwa amevalia sweta la mistarimistari lenye kofia juu yake, chini alivalia viatu vyeusi vya wazi.

Pembeni yake, rafiki yake, bwana Yu, alikuwa amevalia shati jeusi, tai nyeusi na suruali nyeusi ya kitambaa iliyomkaa vema, chini ana viatu vyeusi aina ya moka.

Kitu pekee kilichokuwa na rangi tofauti na mavazi yake ilikuwa 'kaua' kadogo kekundu kalichokuwapo upande wake wa kushoto wa kifua, naye bwana huyu alikuwa anavuta sigara kama mwenzake, Taiwan.

"Sasa tutafanyaje?" Bwana Yu akauliza. Macho yao yote yalikuwa yanatazama maji ya bahari yakiwa yanahakisi mwanga wa mataa ya jiji hili, taa hizo za rangi mbalimbali zilifanya eneo hili kupendeza na kuvutia machoni.

Bwana Yu aliuliza tena,

"Kama akigundua Kiellin amefariki, atakuelewa kweli?"

"Hilo halina shaka," Taiwan akamjibu na kuongezea, "nilishajipanga kwaajili ya kitu kama hiko, nitamweleza mtoto alifariki si punde baada yeye kuanza safari ya kuja huku, na kwasababu nilikuwa nikimwambia hali mbaya ya Kiellin, basi haitakuwa ngumu kunielewa."

Akaeleza pia ni namna gani mwili wa Kiellin ulikuwa umetunzwa tangu kifo chake akimpatia daktari maelekezo yote pamoja na fedha nzuri.
Alimhakikishia Yu kuwa Mitchelle hatobaini lolote lile, hata kuhisi kama Kiellin alishafariki masiku kadhaa nyuma.

Alisema,

"Kinachoniumiza kichwa ni kuhusu huu mnada. Lazima tufanye jambo upesi ili tuweze kupata pesa ya maana, na kwa leo nimeonana na Chi gang. Wanataka mzigo ule na wameahidi kutupatia pesa kubwa mno kama tukifanikisha kuwapatia."

Hapo Yu akamtazama Taiwan, macho yake yaliwaka tamaa, akauliza,

"Tutapata kiasi gani?"

Taiwan akamwambia ni mamilioni ya madola, na punde tu watakapozitia kimyani basi hawatakuwa na haja ya kumfanyia kazi mtu yeyote yule mpaka kifo kitakapowakuta uzeeni!

Hakika ofa yao ikamtoa Yu udenda, lakini akili yake haikuwa nyuma kumkumbusha juu ya hatari ya deal hili, akauliza,

"Lakini tutaweza vipi na huku safe ya kutunzia mali ikiwa ina uwezo wa kufunguliwa na mtu mmoja pekee dunia nzima?"

"Ni kweli!" Taiwan akamjibu, kisha kabla hajaongeza neno akavuta kwanza mkupuo mmoja wa sigara na kuutemea moshi puani kama bomba za gari kubwa alafu akasema, "ndo' maana nmekuambia tunahitaji mpangokazi, Yu. Kazi ipo kwetu sasa, kwani uhakika wa pesa toka kwa genge la Chi ni asilimia mia moja na moja!"

Yu alimtazama Taiwan akaona jambo usoni kwake, aliamini bwana huyo ana jambo ameshalipanga kichwani, akataka kulifahamu.

Akauliza,

"Wewe umepanga nini, Taiwan?" Na hapa ndo' akawa amefika mahali ambapo Taiwan alikuwa anangoja, mahali pa kujieleza mawazo yake, bwana huyo akatabasamu kwanza kisha akanyonya sigara yake, moshi huu wa sasa ulikuwa ni muhimu sana kuliko aliouvuta awali kwani aliiona picha fulani kichwani kwake, picha ambayo iliambatana na matumaini makubwa, hivyo moshi huu aliusikia kabisa ukipenya mwilini mwake, na alipoutoa alihisi ahueni kubwa.

Akasema,

"Yu, mpango wangu ni kabambe sana, lakini kutimia nahitaji watu, vipi utanisaidia?"

Aliuliza hivyo akimtazama Yu, Yu naye akatabasamu kama jibu lake, alikuwa radhi kwenye mpango huo, lakini kama ilivyokuwa awali, hakuyaacha mashaka yake nyuma, akauliza,

"Na utammudu vipi, Mitchelle? Kwa namna ulivyokuwa unaniambia kumhusu mtu huyo ni wazi ni mtu hatari. Utafanikiwa kumkabili?"

"Ndo' maana nikakwambia nina mpango kabambe, hukuelewa?" Taiwan akasema akiitupa sigara yake chini, alishamaliza kuinyonya na sasa kimebakia kipisi, akakikanyaga kukizima.

Akaongeza,

"Niamini mimi, Yu. Sema kama nilivyokuambia hapo mwanzo, nahitaji watu, watu, watu."

"Unawahitaji kama wangapi?" Yu akauliza.

"Zaidi ya hamsini." Taiwan akajibu akiweka mkono wake mfukoni, macho yake yanatazama bahari.

Yu akamuahidi ataifanya kazi hiyo, ndani ya siku moja tu kila kitu kitakuwa tayari.

Basi usiku wao ukaisha hivyo, mipango na matumaini mwanana, lakini kwa upande ule wa pili tulipotokea, mambo yakiwa kinyume kabisa.

Katika majira ya asubuhi ya saa mbili hivi, habari zilishamfikia kila mmoja katika ofisi kuu ya polisi jijini New York kuwa mmoja wa maafisa habari wa ofisi hiyo kubwa inayoheshika nchini Marekani, amekutwa akiwa hana uhai katika mazingira ya kutatanisha!

Bwana huyo, kama mbuzi wa kafara, alichinjwa koo lake na kitu chenye ncha kali kisha akatelekezwa katika gari lake maeneo ya Manhattan.

Hapo pamoja naye, ulikutwa ujumbe kwenye kioo cha mbele cha gari, ujumbe ulioandikwa kwa damu iliyoshukiwa kuwa ya marehemu, ukisomeka,

"Suits and tie."


***
Astakafillullah raajun mashetani! Duh!
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 28


Na Steve B.S.M





"Namba unayopiga haipatikani ..."

Ilikuwa ni mara ya tatu sasa Mpelelezi anausikia ujumbe huu lakini bado hakuamini masikio yake, akapiga tena na tena, bado majibu ni yaleyale, namba unayopiga haipatikani kwa sasa.

Akasonya akishika kiuno, majira sasa ni saa tatu asubuhi, amesimama nje ya hoteli alofikia akiwa anatazama barabara kuu inayokatiza hapo, barabara hiyo ilikuwa na wingi wa magari pia na wingi wa watu wanaoenda na kurudi.

Alisimama hapo akiwa anatazama huku na kule, akili yake ipo mbali sana japo macho yake yanaangaza hapa, kichwani alikuwa anatafakari ni nini kimetokea na muda mwingine akiwa anadhani pengine anaota.

Alifungua simu yake akaingia mtandaoni, moja kwa moja akaelekea kwenye tovuti ya kupata habari za jiji la New York, si kwamba hakuingia huko hapo mwanzo, hapana, alishaingia kama mara nane sasa, na si tu sehemu moja, bali tovuti mbalimbali lakini bado hakuwa ameridhika.

Akajaribu tena kupiga simu, yaleyale, simu haipatikani, akang'ata meno yake kwa hasira, kidogo tu akiwa hapohapo, kabla hajafanya kingine, akahisi kitu kimegusa mguu wake wa kushoto, upesi akageuka.

Kumbe ilikuwa ni fimbo, fimbo ya mtu mlemavu asiyeona, fimbo ndefu rangi yake nyeupe.

Kutazama uso, akamwona bwana yule mlemavu ambaye anaishi naye hotelini hapa, bwana huyo alikuwa amevalia suruali nyeusi ya kitambaa, chini ana raba za kawaida sana, hata shati lake la juu halikuwa limenyooshwa, limejikunjakunja kana kwamba limekamuliwa na baunsa, usoni mwake, kama kawaida, alikuwa amevalia miwani meusi.

Bwana huyo alikuwa akitembea akiwa ametanguliza fimbo yake mbele kama macho, lakini alipogusa mtu alihisi kitu akasema upesi,

"Samahani sana, bwana."

Kisha akatabasamu kiwepesi na kuendelea na safari yake kana kwamba hakuna kilichotokea, Mpelelezi akabaki akimtazama bwana huyo namna akienda zake, hakukoma kumtazama mpaka anaishilia akijiuliza mtu huyu ni wa wapi na huku San Fransisco alipokuja hana ndugu kiasi amefikia hotelini? Na kama ni biashara basi ni biashara gani hiyo?

Kwa muda kidogo bwana huyo akawa amemsahaulisha mawazo yake ya awali, mawazo ya kuwaza kifo cha kutatanisha cha Travis, bwana yule alipoishia, akasimamisha taksi iliyokuwa inakatiza, akakwea na safari ikaanza.

Akiwa katika gari hilo, kando ya dirisha, alifungua simu yake akanyookea moja kwa moja kwenye kategoria ya picha, huko akatafuta kidogo na kuangukia kwenye fali alilolutunza kwa jina 'diary'.

Akalifungua na kuanza kutazama ...

Humo kulijaa picha za diary ile alopatiwa na yule mama ambaye mwanaye alifariki, diary ambayo ilikuwa na matukio ya yule mwanamke ambaye picha yake inatumika kwenye kitambulisho cha mtuhumiwa wa mauaji ya The DL.

Mpaka safari inakoma, Mpelelezi alikuwa anasoma diary hiyo kwakupitia picha za simu yake, alikuwa anazipitia kwa umakini kana kwamba anazifanyia mtihani baadae.

Aliposhuka, aliweka simu yake mfukoni akatazama nyumba iliyosimama mbele yake, ilikuwa ni ghorofa ya sakafu kadhaa, rangi yake dhahabu iliyopauka.

Akaingia humo na kunyookea mlango nambari 64, akagonga hapo, sauti ya kike ikaitikia, kidogo mlango ukafunguka akachungulia msichana mwenye makamo ya miaka ishirini hivi, nywele zake ndefu rangi ya bia, macho yake gololi na 'lips' zake nyembamba sana, akamuuliza Mpelelezi,

"Naweza kukusaidia?"

Mpelelezi akaeleza adhma yake. Alionyeshea picha ya kijana fulani katika simu yake kisha akasema anahitaji maongezi machache kuhusu kifo cha mtu huyo.

Alipofanya hivyo, msichana yule akakodoa, uso wake ukapara kwa hofu, akatazama kama Mpelelezi yu na watu wengine, akaona yu mwenyewe, basi upesi akaufunga mlango wake lakini kabla hajafanikiwa, Mpelelezi akauzuia kwa mkono.

"Naomba tuongee tafadhali!"

Msichana yule akakataa katakata, hakutaka kusikia lolote toka kwa Mpelelezi bali kuondoka kwake tu, akalazimisha kufunga mlango kwanguvu zake zote Mpelelezi akimzuia, ilikuwa ni kama igizo la futuhi.

Msichana huyo alipoona hana uwezo wa kumshinda nguvu Mpelelezi, akapaza sauti ya kuomba msaada, sauti yake ilikuwa kali na nyembamba yenye kuumiza sikio, Mpelelezi aliposikia hayo akaachia mlango upesi kutazama mazingira yake ya usalama.

Hakutaka kuleta zengwe hapa, anafahamu fika hakuwa na kitambulisho wala chochote cha kumtambulisha kama yeye ni mwanausalama, hivyo hakuwa na uhalali wowote wa kuwa hapo.

Akatoka hapo haraka akielekea chini lakini wakati huo baadhi ya majirani walishatoka kwenye viota vyao kutazama kinachoendelea, walimtazama Mpelelezi akienda zake na Mpelelezi kama asiyejua kilichoendelea hapa, akatembea kama mtu aliye katikati ya jiji, hakujali watu, ni kama vile hakuwa anawaona, alipofika chini akaitisha taksi na kuketi kitako.

Akiwa ndani ya gari alitazama anwani nyingine ya kuitembelea kisha akampatia dereva maelekezo na gari likaelekea huko.

Njiani akaendelea kusoma ile 'diary' kwenye simu yake, hakutaka kuwaza kitu kingine kabisa, mawazo yake yalikuwa hapo kwa asilimia zote, na kweli baada ya muda mawazo yake yakalipa, kuna jambo akaona humo, jambo la muhimu kuliandika chini, akafanya hivyo katika simu yake hiyohiyo ...

Alitazama orodha ya anwani za kutembelea akaona imesheheni, alikuwa na sehemu nyingi za kwenda na watu wengi wa kuongea nao, kazi ndo' kwanza ilikuwa inaanza, tena katika kipindi chake kibaya kazini.

Alichoomba ni huko kwengine kusilete matata kama hapa alipotoka, la sivyo ... Akatikisa kichwa, lakini alijikuta akitabasamu pale alipokumbuka mkasa wa yule msichana, namna walivyokuwa wanagombania mlango ilikuwa kituko haswa, lakini kila kitu kina sababu, aliamini msichana yule alikuwa na sababu ya kukataa kuongea naye na ni jukumu lake kujua sababu hiyo ni ipi ...

Basi gari likatokomea katika barabara yake ...

***

"Umepata taarifa?" Aliuliza bwana akiwa anaketi chini, mkononi alikuwa amebebelea glasi yenye kinywaji rangi ya dhahabu, glasi inachuruza kwa baridi.

Bwana huyu si mgeni machoni petu, la hasha, alikuwa ni yule mwanaume ambaye alitambulishwa kama mume kwa yule mwanamke ambaye alikutana na Mpelelezi katika uwanja wa kuchezea kamari, yaani Casino.

Mwanaume huyu ambaye tulimwona siku ile akiwa ameukunja uso kumkuta Mpelelezi pamoja na Mwanamke yule ndani, hapa alikuwa na uso wa binadamu wa kawaida kama mimi na wewe, alipoketi alimpatia mtu aliyekaa naye mkabala glasi hiyo alokuja nayo kisha yeye akawa mtupu isipokuwa chupa yake ya maji mezani.

Mtu huyo aliyekuwa naye mkabala si mwingine bali ni yule mwanamke ... mwanamke mrembo mwenye utashi wa kucheza kamari kiasi cha kumshtua Mpelelezi, alikuwa amekaa ndani ya blauzi na pensi fupi ya jeans, uso wake una 'make-up' ya kiasi.

Alikunywa kile alicholetewa kwa fundo moja kisha akaiweka glasi mezani, ndipo akauliza,

"Taarifa gani?"

"Yule bwana yupo San Fransisco," akasema yule mwanaume akiwa anamtazama Mwanamke huyo kwa macho ya mkazo, hata alipokunywa maji yake bado alikuwa anamtazama kwa kumkazia mboni.

"Oooh ..." Mwanamke akaitikia, lakini macho yake hayakuonyesha mshangao wowote kama ilivyokuwa kwenye kauli yake, alikuwa anatazama glasi yake ya kinywaji mezani kama mtu anayefikiria jambo.

Mwanaume akasema,

"Hii ndo' fursa yetu sasa ya kurekebisha makosa."

"Makosa yapi?" Mwanamke akauliza macho yake yakimtazama mwenziwe.

"Hujui makosa yapi?" Mwanaume akastaajabu. "Ulipata nafasi nzuri lakini hukufanya uliyotakiwa kufanya, nilistaajabu kumkuta bwana yule akiwa hai katika nyumba yako!"

"Najua ninachokifanya, Jerry!" Mwanamke akawaka. Aliyatoa macho yake kiasi kuonyesha msisitizo wa anachokisema, Mwanaume akatabasamu, halikuwa tabasamu la furaha.

"Ni kipi hiko? Tulipewa kazi moja tu, moja tu!"

"Na nitaifanya. Sawa?"

"Kama ulilenga hivyo, Evelyn, kwanini ulihitaji msaada wangu siku ile?"

Siku ile ...

Siku ile?

Siku ipi hiyo? ...

Ngoja kidogo,

Ilikuwa ni majuma kadhaa yaliyopita, siku ambayo Mwanamke huyu, Evelyne, alikuwa katika gari majira ya saa tatu usiku akiwa anatazama dirishani.

Hakuwa mwenyewe, pembeni yake alikuwapo huyu mwanaume, Jerry, akiwa ametulia kama chai ndani ya chupa, naye macho yake yalikuwa yanatazama nje, ni bayana kuna kitu walikuwa wanangojea hapa.

Baada ya muda kidogo, Jerry, yaani huyu mwanaume akauliza,

"Una uhakika atakuja hapa?"

Kisha akatazama saa yake ya mkononi.

Mwanamke yule, yaani Evelyne, akiwa anaendelea kutazama nje, akamtoa shaka mwenzake, bado aliamini mtu wake atakuja kama walivyokubaliana hata kama ni kwa kuchelewa.

"Kwa namna nilivyoongea naye mara ya mwisho, naamini kabisa atakuja."

Kweli, haikupita dakika kumi baada ya hiyo kauli, wakamwona mwanaume akiwa anatembea kwa kasi, Jerry alikuwa wa kwanza kumwona, akamnyooshea kidole akiuliza,

"Sio yule?"

Kutazama, ni Mpelelezi, bwana huyo alikuwa ameshuka toka kwenye gari la kukodi si muda, sasa anatazamia kuingia ndani ya Casino.

"Anajua amechelewa, unaweza ukaona tu mwendo wake," alisema Mwanamke ndani ya gari kisha akafungua mlango na kushuka, nyuma yake akifuatiwa na Jerry.

Waliingia ndani, wakasimama kwa mbali walipojihakikishia kumwona Mpelelezi, walikuwa wanamtazama kwa umakini kuhakikisha hapotei machoni mwao, kidogo wakamwona mhudumu akiwa na Mpelelezi, papohapo Evelyne akamtazama Jerry kwa kumpa ishara kisha akafungua pochi yake na kumkabidhi kitu mwanaume huyo, Jerry alipopokea, akaondoka kumfuata yule mhudumu aliyeongea na Mpelelezi, wakati huo Evelyne akiwa anatazama.

Baada ya muda kidogo, Jerry akarejea na kumwambia Evelyne kuwa kazi imekamilika, kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa, Evelyne akampongeza, wakangoja kwa dakika kadhaa wakiwa wanamtazama Mpelelezi kwa mbali, muda ulipowadia, Evelyne akaaga na kwenda moja kwa moja kumfuata Mpelelezi.

Alipokuwepo huko, Jerry alikuwa anatazama kila kitu, macho yake hayakubanduka hata sekunde, aliangalia kila kinachoendelea.

Baada ya muda kidogo, akaona Mpelelezi anadondoka, hapo Evelyne akamtazama na upesi akasogea katika eneo la tukio, akambeba Mpelelezi wakijinasibu wapo naye pamoja kisha wakatoka zao kwenda nje.

Jerry akiwa amembebelea Mpelelezi begani, nyuma yake Evelyne akiwa anatembea kwa upesi, walinyookea kwenye gari lao wakampakia Mpelelezi humo na kuondoka.

Hawakwenda mbali, Jerry akashuka na kumwacha Evelyne peke yake kwenye gari, alimwambia kuna mahali anapaswa kwenda na asubuhi watapata kuonana, basi Mwanamke akiwa katika usukani, akaenda zake akiwa amembebelea Mpelelezi nyuma kana kwamba mzigo.

Lakini akiwa anaenda alikuwa akikaa kumbuka kauli ya Jerry, ya kwamba amtupie mwanaume huyo mahali salama baada ya dakika thelathini kupita kwani hatokuwa na uhai tena.

Kinyume na hapo akanyookea na mwanaume huyo nyumbani akiwa bado ni mzima, anahema japo hana fahamu, huko akamtua na kumpeleka moja kwa moja chumbani.

Kesho yake asubuhi, Jerry alipokuja, anastaajabu kumwona Mpelelezi sebuleni, na alipopata wasaa wa kuzoza na Evelyne kule chumbani aliuliza ni kivipi mwanaume yule alikuwa mzima ingali walimuwekea dawa kali kwenye kinywaji.

Majibu ya Evelyne hayakueleweka, Jerry akahitimisha kuwa dawa ilikuwa imebadilishwa, haikuwa ile waliyoipanga kwani kwa ukali wake uhai wa Mpelelezi ungekuwa historia hivi sasa.

Lakini kwanini Evelyne alifanya hivyo? Hakuna aliyejua bali yeye mwenyewe, sasa anapata nafasi ya pili, nafasi ya sasa hivi, nafasi ya leo hii, Jerry anamsisitiza lakini kama haitoshi simu inaita, anampatia Evelyne aongee nayo, ilikuwa ni simu ya kazi.

Mtu ambaye hakumjua ni nani mpaka pale aliposikia sauti yake.

Mtu huyo akamweleza kuwa hapo alipo yupo nyuma ya gari la kukodi alilomo Mpelelezi, anamfuatilia kwa kitambo sasa, na atakapopata wasaa basi ataimaliza kazi yake upesi bila kusita.

Kabla Evelyne hajaongezea neno, simu ikakatwa, akamtazam Jerry kwa mshangao.

"Hata mimi sikufahamu hilo!" Jerry akajitetea akiwa ameyatoa macho.

Evelyne akasema,

"Kwahyo hapa tuongeapo, kipofu muuaji yupo kazini?"

"Ndio," Jerry akajibu kwa kujiamini, "si umesikia mwenyewe?"

Evelyne akanyanyuka upesi na kwenda zake, hata kinywaji chake hakumaliza, Jerry akajribu kumwita lakini hakufua dafu, mwanamke alienda zake kana kwamba ni kiziwi, hakuna anachosikia.



***.


nini kinaendelea hapa?
Binaadamu ni kiumbe hatari sana kuwahi kuishi kwenye uso wa dunia! Akikudhamiria hakukosi
 
Habari zenu wapendwa? Samahani kwa kuwa kimya kwa kitambo kidogo, sasa narejea na kama nilivyoapa, story hii nitaimalizia hapahapa.

Kuanzia kesho nitarejea kwenye ratiba yangu ya awali.
Daaah afadhali maana sio Kwa kuchungulia huku
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 29




Na Steve B.S.M






Dereva taksi alipoona mtu amepunga mkono, haraka akasogea eneo la tukio kumkwapua mteja, alisimamisha gari kisha mtu akaingia, naye akamtazama kwenye kioo juu ya kichwa chake, rear mirror, na kuuliza,

"Tunaelekea wapi?"

Bwana huyo aliyempakia alikuwa ni Mpelelezi, amebebelea kamkoba kadogo mkononi, ameketi anamtazama, majira yalikuwa ya saa mbili ya usiku.

"La Palma Hotel tafadhali," Mpelelezi alisema kisha dereva akaondosha chombo chake maramoja, kidogo tu wakawa wapo katika msitu wa magari lukuki, barabara imejaa magari yakienda na kurudi, wakati huo Mpelelezi akawa amebanwa na shughuli zake.

Alikuwa yu 'busy' ameweka 'earphone' masikioni anaskiza jambo, na huku kwenye simu yake akiwa anatazama jambo, alikuwa amemezwa kweli, hakuelewa hata safari iliendaje, akili yake yote ilikuwapo pale alipokuwa ameweka mazingatio.

Basi gari likaenda, mara kadhaa likasimama kwasababu ya foleni za hapa na pale lakini halikuchukua muda sana likaendelea zake na safari.

"Muda huu kuna folenifoleni sana," dereva akazungumza, wakati huo gari limesimama kungoja mataa yaruhusu, aliongea akiwa anamtazama Mpelelezi kama atamsikia lakini haikuwa hivyo, bwana huyo hakuwa na habari naye kabisa, yupo peke yake katika ulimwengu wa pekee.

Walipotoka hapo kwenye mataa, dereva akaongea tena kuhusu msongamano wa barabara na magari yake lakini kama alivyoongea hapo mwanzo, hakuna aliyemsikiza, aliongea mwenyewe, naye hakukoma akaendelea kuongea tena na tena.

Safari ikasonga, mara dereva alipopata nafasi akawa anamtazama Mpelelezi kwenye kioo, safari ilipotumia kama dakika kumi na tano hapo ndo' kitu cha kushangaza kikaanza kujiri.

Dereva alimtazama Mpelelezi kwa kioo, kama kawaida akamwona ametingwa, akakata kona toka barabara kuu na kushika njia ndogo, Mpelelezi hakutambua kitu, gari ikaendelea na safari.

Dakika mbili, tatu, nne, tano, kufumba na kufumbua, dereva akafungua mlango na kurukia nje! Ilikuwa ni kama utani lakini kweli. Mpelelezi alistaajabu kumwona dereva akiwa anabiringita chini, kutazama mbele anaona kiti kikiwa kitupu na gari likienda kasi ya kilomita themanini kwa saa, hajafanya kitu chochote, mara anaona gari kubwa kushoto kwake, limewasha taa na linakuja kwa kasi sana, kufumbua na kufumbua gari hilo likabamiza taksi na kulirusha maili na maili mbali!

Liliruka na kujigeuzageuza angani kabla halijatua kwenye jengo kubwa lilipojipondapomda na kuwa mithili ya karatasi lililofinyangwafinyangwa na kiganja cha mkono.

Gari lile kubwa halikubaki abadan, likatokomea lisijulikane limeenda wapi, kasi yake ilikuwa kubwa mno na ukilitazama mbelez huwezi jua kama limekumbana na shurba yoyote.

Kabla watu hawajajaa katika eneo la tukio, gari moja ndogo ikasimama kwa umbali wa mita kadhaa, mtu mmoja akashuka na kusimama akitazama gari lile lililogongwa, mtu huyu hakuwaa anaonekana maana aliposimamia hapakuwa na mwanga wa kutosha, ni baada ya kitambo kidogo ndipo gari likakatiza na kummulika usoni, alikuwa ni yule mwanamke, Evelyne.

Alisimama akiwa ameyatumbua macho yake kana kwamba haamini anachoona au mboni zake zinamdanganya, mkono wake wa kuume alokuwa ameshika nao mlango wa gari ulikuwa unatetemeka vidole, hakukaa hapo muda mrefu, akaingia kwenye gari na kuondoka zake.

Baada ya dakika chache watu wakawa wamejaa hapo kustaajabu ya ajali hiyo mbaya kupata kutokea karibuni, muda si mrefu gari la kubebea wagonjwa na pia polisi kadhaa wakawa wamewasili eneo la tukio, eneo hilo dogo likawa limesongwa kwa kiasi chake, watu wakitaka kushuhudia na huku wengine wakigeuka wasimuliaji kuelezea namna ajali hiyo ilivyotokea.

Punde, kama baada ya dakika mbili tangu watu wasongamane, mtu fulani akaja upesi katika eneo hilo, alikuwa akikimbia kwa kutupa mikupuo mikubwa ya hatua, alipokaribia msongamano wa watu, akapiga kelele akisema,

"Derevaa! Dereva yupo kule, dereva yupo kule! ..."

Kelele zake zilifanya kila mtu amtazame, upesi pasipo kupoteza muda askari mmoja akachoropoka kwenda naye eneo la tukio. Nyuma yake alifuatwa na mtu wa huduma ya kwanza toka kwenye 'ambulance' iliyofikia hapo.

Walipofika huko wakamkuta Dereva akiwa chini, ana majeraha kadhaa na haonekani kujitambua, upesi akachukuliwa na kupelekwa kwenye gari la huduma, haikuwa mbali na mahali ajali ilipotokea, hapo akapewa huduma ya kwanza na si muda akawa amerejea kwenye fahamu zake, hali yake haikuwa mbaya kiasi cha kumkimbiza hospitalini upesi.

Alihojiwa kwa muda chache na polisi kisha gari ndo' likambeba kumpeleka hospitali kwaajili ya matibabu zaidi, pamoja naye akaongozana na polisi mmoja.

Kwa maelezo ya dereva huyo ni kwamba breki zilifeli akiwa katika mwendokasi, na kwasababu ya kunusuru uhai wake akajitupa nje ya chombo, pia kumnusuru mteja wake aliyekuwa amembeba kwenye gari, akamshauri arukie nje kwani hakukuwa na njia mbadala, hata kama angetumia 'handbrake' bado asingefanikiwa kuisimamisha gari upesi kiasi cha kutoikuta barabara kubwa inayokatiza mbele yao.

Baada ya hapo ikabidi mahojiano yahitimishwe kwasababu ya hali ya mtuhumiwa, nafasi itakapopatikana basi yataendelea siku za usoni.

Wakati gari hilo la wagonjwa likiwa linaendelea na safari yake, dereva aliyekuwa amelazwa kitandani, alipata kuuliza kuhusu hali ya yule bwana aliyembeba, alitaka kujua kama amesalimika ama lah. Wakati anauliza macho yake yalikuwa mekundu yaliyojawa maji.

Mhudu akamjibu,

"Kwa hali ile tuliyoiona, hamna anayeweza kubaki na uhai. Gari limeharibika sana kiasi kwamba tumeshindwa kutoa chochote kile. Kama mwili upo ndani, basi ni mpaka gari litakapokatwakatwa, la sivyo haitawezekana kuutoa."

Dereva aliposikia hayo, akachuruza chozi akirejesha kichwa chake kitandani, baada ya hapo pakawa kimya safari ikiendelea.

Mbali na hapo, lile gari kubwa lililosababisha ajali lilisimama mahali baada ya mwendo wake mkali wa madakika kadhaa. Hapo lilipotuama mazingira yalikuwa tulivu na mwanga hafifu lakini bado ubavu wake uling'aa sababu ya maneno yaliyoandikwa hapo yalikuwa ya rangi nyeupe inayometa, yakisomeka;

'RICKY & PAT CLEANING'

Baada ya muda kidogo, ndani ya gari hilo sauti ya kiume ikavuma, sauti iliyoashiria anaongea na simu. Sauti hiyo ilisema,

"Kila kitu kimeenda sawa," kisha kukawa kimya, kidogo akaongezea, "sawa, majira ya saa sita usiku." Baada ya hapo kikafuatia kimya cha muda mrefu, kimya kilichoashiria kuisha kwa maongezi.


... La PALMA Hotel ... Saa sita usiku ...


Baada ya mteja kwenda zake, mhudumu alinakili taarifa kwenye tarakilishi yake ya mezani kisha akainama kuchukua kitu chini ya meza yake kubwa, aliponyanyuka uso kwa uso akakutana na mtu amesimama hapo kama mstimu, akashtuka! Moyo ulimpasua damu ikaenda mbio.

"Aah! Kumbe ni wewe!"

Mbele yake alikuwa amesimama mwanaume mweusi mwenye miwani, mkononi mwake ameshikilia fimbo ya kumsaidia kutembea.

Mhudumu alitabasamu kiuongo sababu ya taaluma yake kisha akashusha pumzi kuiondoa hofu kifuani mwake, alafu akamuuliza bwana huyo amsaidie na nini, bwana akasema,

"Nimekuja kurejesha funguo."

Mhudumu akamuuliza namba ya chumba chake kisha akatazama kwenye tarakilishi yake kuona rekodi, akaona bwana huyo bado alikuwa na siku tatu za makazi hapo, basi akauliza,

"Mbona unasitisha makazi yako, bwana?"

Bwana akamjibu amepata dharura hivyo hatobakia tena hapo, anapaswa kuondoka. Mhudumu akamweleza utaratibu wa fedha kwa wale wasiomaliza muda wao lakini bwana huyo hakujali, alisema yeye amekuja kutoa tu taarifa hana haja na fidia.

Baada ya kuuweka ufunguo mezani, bwana huyo akaenda zake, wakati akienda, dada wa mapokezi akamsindikiza kwa macho mpaka alipotoka, alikuwa anashangaa namna bwana huyo alivyokuwa anatumia fimbo yake kwa ustadi mkubwa, akaishia kutukuza uwezo wa Mungu.

Bwana yule alipofika zake nje, akapanda taksi na kumwambia dereva ampeleke moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege, dereva akatii na kung'oa zake nanga.

Bila shaka bwana huyu alikuwa amelenga kukwea 'Red Eye Flights' - ndege zinazoruka usiku wa manane na kuwasili asubuhi ya mapema.

Muda si mrefu, gari likawa limepotea.


***


Baada ya kuoga, Mitchelle aliketi sebuleni kwa kazi fulani, mwili wake ulikuwa umelowana na hakujali kujikausha.

Alifunika kichwa chake kwa taulo dogo jeupe, taulo kubwa akalitumia kufunikia kiwiliwili chake lakini taulo hilo halikumziba vizuri hivyo sehemu kubwa ya mwili wake ikawa wazi, nalo hakujali, kwani kuna nani wa kumtazama hapa?

Alifungua tarakilishi yake akatazama mambo kadhaa humo, haswa juu ya mnada mkubwa unaotazamiwa kuendeshwa Taiwan siku za karibuni, mnada huo ulikuwa unahusika na mauzo ya vitu na vito vya thamani kubwa.

Baadhi ya mali kwaajili ya mauzo hayo makubwa zilikuwa tayari zishakabidhiwa katika mamlaka husika, na baadhi ya watu wakubwa kiuongozi na kipesa, walikuwa tayari washa-book nafasi zao katika mnada huo adhimu.

Mitchelle alitazama orodha hiyo na akajiridhisha haswa kuwa siku hiyo pesa ipo, tena si ndogo bali ya kutosha, cha muhimu ni kucheza karata zake vema.

Kidogo akiwa katika mafikirio hayo, akakumbuka jambo. Alichukua simu yake akaandika namba fulani toka kichwani kisha akapiga, simu ikaita na kitambo kidogo ikapokelewa na sauti ya kiume, Mitchelle akauliza,

"Vipi?"

Bwana huyo wa upande wa pili akamweleza kuwa kila kitu alichomuagiza amekwishafanikisha, na sasa alikuwa katika zoezi la kumtumia ujumbe kwa njia ya barua pepe.

Baada ya maongezi hayo mafupi, Mitchelle akakata simu kisha akatazama 'inbox' ya email yake, huko akakuta 'messages' mbili, kila moja ikiwa na kichwa chake cha habari, ujumbe wa kwanza uliandikwa RICHIE, wa pili ukaandikwa HILDA, akafungua ujumbe mmoja baada ya mwingine, kwenye kila ujumbe kulikuwa na picha pamoja na maelezo ya anwani ya makazi, akazisoma zote.

Kidogo ujumbe mwingine ukaingia, na mwingine tena ukaingia, jumla zikawa mbili. Akazifungua na kuzisoma, saa hii jumbe hizo zilikuwa zimeambatana na picha za watu wengine mbali na wale wa mwanzo, na picha hizo zikaambatana na anwani zake.

Akazipitia.

Alipomaliza akapiga simu kwenye namba ileile akasema,

"Nimezipata, pesa yako itaingia muda si mrefu." Kisha akakata simu.

Sasa akatulia akifikiria kidogo, mwishowe akajisemea,

"Nitajua ukweli kuhusu kazi yangu, Bryson, kama tupo ndani ya mkataba wetu au lah, bila shaka hatutakuwa maadui."

Alivyosema hayo akajipooza na kahawa yake mezani, kahawa iliyoletwa na Jennifer si punde.


***"
Wamemponza meneja wao kwa kutaka kupekua yasiyo wahusu
 
Kama umenifuatilia vema, mimi huwa naandika filamu sio riwaya.
Filamu na riwaya zina utofauti gani mkuu! Hata riwaya inaweza tengenezewa muvi!!!? Na itakua na tofauti gani na filamu ukiwa unaziangalia
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 30


Na Steve B.S.M





Hilda alitazama nyuma yake, hakukuwa na mtu, alikuwa mpweke katika eneo hili, zaidi ni magari kadha wa kadha yaliyokuwa yemejiegesha kwa mstari mnyoofu, basi akafungua mlango na kuingia ndani ya jengo hili la ghorofa, alikuwa yupo hoi, macho yake ndani ya miwani yalikuwa yamelegea, mwili mchovu na mzito.

Alipandisha ngazi kivivu, akikanyaga kila hatua, mkono wake wa kuume ulikuwa umeshililia kingo ya ngazi hizo akijivuta kana kwamba mzigo.

Akiwa anapandisha ngazi hizo, alilaani kwanini jengo hili halina lifti, alitupa tuhuma zake ingali hakuna aliyemsi

Alipoingia sebuleni, akajitupa kwenye kochi na kushusha pumzi ndefu, pumzi ya uchovu, kisha akatulia hapo tuli kana kwamba anasinzia, muda kidogo simu yake ikaita kwa kunguruma, simu iliita kwa kama dakika moja ndipo akahisi jambo kwani alikuwa yu hoi sana, akaipokea na kuiweka sikioni akiwa amejilaza hapo kwenye kochi.

"Nimefika muda si mrefu ... ndio, niko salama kabisa." Simu ikakata, hakuitoa sikioni yeye akaendelea na usingizi wake hapohapo kochini muda si mrefu akawa amepitiwa na usingizi kabisa kiasi cha kukoroma. Aliuachama mdomo wake wazi akiwa yupo katika ulimwengu mwingine mbali na huu tunaoujua.

Baada ya dakika kadhaa, akiwa amelala hapahapa kochini, mlango ukateguliwa kitasa, hakusikia kitu, kitasa kikaguswa tena kama mara tatu hivi, mlango haukufunguka na Hilda hakugutuka kitu, alikuwa amezama kwenye usingizi mzito shauri ya pombe alizotoka kunywa huko kilabuni pamoja na Richie.

Baada ya majiribio hayo manne ya kufungua mlango kukawa kimya kidogo, ukimya wa sekunde kadhaa kisha ghafla kitasa kikaanza kutoa sauti ya kuchokonolewa na kitu mithili ya waya wa chuma hivi, kidogo tu, kitasa kikafunguka.

Aliyekuwa anachokonoa, akasogeza mlango taratibu, nao mlango ukaitikia amri yake, akatanguliza mguu wake wa kulia ndani, ulikuwa mguu mkubwa wenye kuvalia buti kubwa jeusi, kidogo akauingiza na mguu wake wa pili kisha akaufunga mlango, sasa mwili wake mzima ukawa ndani.

Kwa sekunde tano wana huyo aliyeingia ndani akatulia hapo, alikuwa anayasoma mazingira, kisha akanyanyua mguu wake kuzama ndani zaidi, alimpita Hilda akaenda zake chumbani.

Baada ya muda usiofahamika, Hilda akasikia kitu cha kumshtua, akafungua macho yake. Hakujua ni nini kimemwamsha ila usingizi wake mzito ulikata ghafla, akaangaza huku na kule.

Kuligeuka kuwa patulivu ajabu, hata huko nje hakukuwa na mtu anayekatiza ama kuongea koridoni.

Kidogo akasikia kitu tena, sauti mithili ya mtu anayetembea chumbani, moyo wake ukashtuka na kupasua, alidhani yupo peke yake humu ndani lakini sauti hiyo ikaanza kumfanya ahisi tofauti, pengine kuna mtu mwingine hapa.

Akanyanyuka, akapepesuka, mwili ulikuwa mzito anashindwa kuumudu. Alijitahidi kujikaza mpaka akasimama wima kisha akaelekea chumbani akijivuta.

Aliukuta mlango upo wazi, akausogeza na kuingia, akarusha macho yake huku na kule, hakuona kitu, hakukuwa na mtu wala chochote cha kumtia hofu, akaguna kwa kujishangaa.

"Hizi pombe hizi!" Alisema akitikisa kichwa chake na kuongezea, "kweli nimelewa."

Alikisogelea kitanda chake, akajitupia hapo kama mzigo wa tani mbili, muda si punde akawa anakoroma kama trekta bovu la shamba, hakufahamu chochote kinachoendelea kwani usingizi ulimmeza mzimamzima asibaki hata punje.

Lakini dirisha la mashariki mwa chumba hiki lilikuwa wazi kama vile mlango ulivyokuwa, Hilda hakulitambua hilo, kidogo tu moja ya gari lililokuwepo katika msururu ule wa magari yaliyojiegesha pale nje likatema moshi kwenye bomba lake kuashiria kuwaka kwa injini, punde gari hilo likanguruma na kupotea katika mazingira hayo.

Baada ya hapo mambo yakarudi katika kawaida yake.


***


"Nimewasiliana naye, na kama nilivyokuambia pesa ipo!" Jamal alisema kwa sauti yenye mkazo, macho yake yalikuwa yanamtazama kijana mweusi aliyeketi kwenye kiti, kwa jina Huncho.

Mwanaume huyo mwenye rasta alikuwa amevalia koti kubwa rangi ya manjano na suruali nyembamba rangi ya bluu liyobana miguu yake kisawasawa, chini amevalia raba kubwa rangi nyeupe.

Jamal yeye alikuwa amevalia kaushi nyeupe na pensi nyeusi ya michezo ya kikapu, chini yuko peku nyayo zake zikisabahi sakafu. Hapa walipo ni ndani ya sebule ndogo, pembeni ya meza yenye tarakilishi juu yake, tarakilishi hiyo ilikuwa 'on'.

"Jamal," Huncho akaita na kusema, "ndani ya mwezi huu nataka pesa yangu iwe imekamilika, sawa? Kama kukuvumilia nishavumilia vyakutosha, nadhani ni muda sasa wa kumalizana."

Aliposema hayo akasimama toka kisha akamsogelea Jamal kwa ukaribu usoni, akamwambia hatovumilia tena zaidi ya mwezi huo, kama fadhila ashazifanya kwa kumsaidia kumlipia ada ya chuo kwa semista kadhaa, sasa ni matanga ya kurejesha deni.

"Lakini Huncho, unajua kabisa lengo langu ni nini, sijadhamiria kukwepa deni lako, najua ulinisaidia kipindi cha shida lakini hiyo pesa kwa muda huo ulionipatia sitaweza kuipata, tazama sasa nishabakiwa na majuma mawili tu katika mwezi, majuma hayo nitafanya nini?" Jamal alilalamika, lakini hayo yote hayakuwa na maana kwenye masikio ya Huncho, yeye alichotaka ni pesa yake tu.

Alirudia kauli yake kisha akaenda zake akimwacha Jamal na maswali mengi asiyojua namna ya kuyatatua.

Jamal, mwanafunzi wa mwaka wa nne sasa chuoni akisomea Genomics, ni mwanaume ambaye amezoea kukumbana na changamoto katika maisha yake ya taaluma tangu 'High School' baada ya kuwapoteza wazazi wake wawili kwa ajali mbaya ya ndege, tangu hapo, haswa baada ya kukosa haki kamili za baba yake, amekuwa akitangatanga na kushika hili na lile ili kupata elimu anayoiwazia, elimu anayoitamani tangu enzi na enzi, elimu ya vinasaba, almaarufu The Genomics.

Kwasababu kozi hiyo ni gharama kubwa, amekuwa akihangaika kupata ufadhili kumudu gharama zote, na kwasababu hiyo ilikuwa inampasa kutafuta kazi za hapa na pale kwaajili ya kufidia ada yake lakini pia kumudu maisha ya kila siku, lakini kama ilivyokuwa kwa ndege kuwa sio kila atakapowahi kuamka basi atapata wadudu ndivyo ikawa kwa Jamal pia, si kila mara alipata kazi za kumpatia pesa za kujikidhi hivyo kumpasa akope ili ajisogeze, na mmoja wa watu aliowakopa kiasi kingi cha pesa ni Huncho.

Huncho hakuwa mtu wa kukaukiwa na pesa abadani, biashara yake haramu anayoifanya katika mazingira ya chuo imemfanya kuwa na pesa chafu, pesa za haramu, angeweza kukupatia pesa yoyote unayoihitaji alimradi akuamini, lakini shida huja pale wanaomkopa wanapogeuka kuwa wakaidi, hapo bwana huyu hasiti kutumia njia zake kwenye kukusanya madeni yake, mara nyingi akifanya hivyo huku akiacha mikono yake kuwa safi.

Jamal alikuwa analifahamu hili, yeye si wa kwanza kupewa pesa na bila shaka hatokuwa wa mwisho, anatambua fika ni kadhia gani itamkumba endapo hatopata pesa ya kumlipa bwana huyu na hakutaka kabisa jambo hilo, lakino ataipatia wapi pesa ndani ya muda huo mfupi?

Aliketi akatazama tarakilishi yake, macho yake yakagotea kwenye kazi alokuwa anaifanya, kazi alopewa na bwana Richie pamoja na Hilda, kazi hiyo ilikuwa imebakia nusu kwisha, akimaliza atapata pesa, lakini pesa hiyo atakula kiasi gani, alipie ada kiasi gani? Ni wazi haikuwa inatosha kabisa, pesa ilishaisha kabla hajaishika mkononi.

Akashika kichwa chake akitafakari, lazima apate njia, alisema na nafsi yake, na alipofikiria zaidi akaishia kwenye kazi hii, hakukuwa na mlango wowote wa pesa isipokuwa kazi hii, lakini ataipataje?

Baada ya shauri fulani, akanyanyua simu yake na kupiga. Simu ikaita na kidogo ikapokelewa, akasema,

"Hello, Richie!" Kisha akaongezea, "Naomba tuonane ndugu yangu .... Hata kesho sawa ... Hautapata nafasi siku nzima? ... Ndio, ndugu yangu nina shida sana ... Ni pesa lakini tutafanya makubaliano .... Sio hivyo, ndugu yangu ni ..."

Simu ikakata, akaitazama kama vile haamini kuwa imekatwa, akasema 'hello' mara mbili lakink hakukuwa na kitu, simu ilikatwa, akajaribu kupiga mwenyewe lakini haikuita wala haikusema kitu, zaidi ilipiga beep-beep na kukata yenyewe, hapa bwana huyu akaamini huenda amepigwa kufuli.

Kichwa kikamuwaka moto, sasa akawaza wazo ambalo hakutaka kuliwaza, maamuzi ambayo hakutaka kuyafikia, na akaweka nadhiri endapo njia zingine zikifeli basi hatokuwa na namna isipokuwa kuenenda na hii.

Hii njia ya hatari.

Sasa afanyaje?


***


Maabara, Brookhaven, New York.


Yalikuwa ni majira ya jioni, watu wanatoka kwenye shughuli zao kwaajili ya kwenda majumbani kwa mapumziko, miongoni mwao alikuwa ni Dr. Jean, alikuwa anashuka ngazi akitazama saa yake ndogo ya mkononi. Si kwamba lifti haikuwapo katika jengo hili, la hasha, alipendelea tu kutumia ngazi kwaajili ya mazoezi binafsi.

Basi akiwa anashuka, mara simu yake ikaita, aliitoa mfukoni na kuitazama, namba ngeni, akapokea na kuiweka sikioni.

"Ndio ... Nimeshakamilisha zote, ndio ... Sawa, saa nne usiku."

Simu ikakata, akaiweka mfukoni na kunyookea gari yake, gari mithili ya Ford Ranger rangi yake nyeusi, gari alokuwa anasema ipo kwa fundi ikipata matengenezo sasa ilikuwa isharudi barabarani, akaingia humo na kukanyaga mafuta.

Aliendesha akiwa anaskiza muziki taratibu na huku kichwani kwake akiwa anayapanga mambo makubwa makubwa, mambo ya pesa ndefu, akajikuta anatabasamutabasamu mwenyewe, muda mwingine bila hata ya sababu.

Alipofika kwenye foleni akapata wasaa mdogo, basi akatoa simu yake mfukoni mwake na kutazama akaunti yake ya benki, hakika ilikuwa inapendeza, 'six digits' zilikuwa zinasoma, basi akajiongelesha mwenyewe,

"Mazuri bado yanakuja."

Kisha akatabasamu tena, kidogo mataa yakaruhusu lakini hakuwa na ufahamu, akapigiwa honi lukuki zilizomshtua na kumrejesha kwenye usukani wake, akatimua chombo.

Alipofika nyumbani, hakupoteza muda bali akaanza kujiandaa kwaajili ya miadi yake ya saa nne za usiku, maandalizi haya hayakuwa ya nguo, lah, bali ya mzigo wa kwenda kuukabidhi.

Alichukua lisaa limoja kujiweka sawa kwa kila kitu ndipo sasa akatulia apate kuoga na kuangalia mengine kwani alibakiwa na lisaa limoja mkononi, lakini muda haugandi, si punde muda wa miadi ukafika, ni kama vile muda ulirushwana rimoti, bwana huyu akajiandaa na kuingia ndani ya gari lake kisha akaanza safari akielekea kaskazini.

Alipotembea kwa muda mchache, simu ikaita, kutazama ilikuwa ni namba ngeni lakini alikumbuka ndo' namba ileile aliyoongea nayo hapo kabla, basi akapokea upesi.

"Ndio nipo njiani .... Kama dakika sita tu n'takuwa hapo."

Akairejesha simu mfukoni na safari ikaendelea, kweli baada ya dakika chache akawa amewasili eneo aliloitwa, akatoa simu mfukoni na kupiga.

"Tayari n'shafika."

Alipotoa taarifa hiyo akakaa hapo akitulia, kidogo tu, kama baada ya dakika mbili hivi, akasikia kioo cha dirisha kinagongwa ngo ngo ngo, kabla hajafungua akatabasamu.

Hakujua kuwa hilo ndo' lilikuwa tabasamu lake la mwisho hapa duniani.


****




****
Huku ni kuwindana tu
 
Back
Top Bottom