Kaka yangu Paskali, naelewa uchungu wako. Lakini jiulize kama hiki unachokiona leo (and you have absolutely rightly spoken against it) kingetokea wakati wa miaka 5 ya mwanzo ya utawala wa Kikwete (let alone waliotangulia)?
Who are the culprits? Ilianzishwa wakati wa Kikwete wakati kina Mwigulu wanalipua mabomu na kuua watu wasio na hatia viwanja vya Soweto kwa ajili tu ya kuzuia CHADEMA wasishinde uchaguzi wa marudio wa udiwani. Magufuli alichokifanya ni kuongezea intensity ya tatizo ambalo ni mkakati wa kishetani wa ccm kubaki madarakani (na kumbuka kuwa Kikwete alituambia hadharani kuwa hata ccm kukubaliana na mbinyo wa kuruhusu vyama vingi "ulikuwa ni mkakati wa kuzuia watu wengi zaidi kuichukia ccm kwa kigezo cha kudai vyama vingi maana angalau kipindi hicho ccm ilikuwa inaungwa mkono na 80% ya Watanzania").
Unfortunately kwa ccm, muda huu Watanzania wengi ni waelewa na ccm wanajua kuwa kwenye uchaguzi huru na wa haki ccm LAZIMA itashindwa TU. Ndio maana bingwa wa kuogopa ushindani (Magufuli) anaogopa na kufanya ayafanyayo.
Paskali, naomba nenda ukawaambie watoto wa Azory, ndugu zake Ben Saanane, mke na watoto wa Tundu Lissu (na wengine wote walioumizwa) haya maneno uliyoyaandika leo halafu urudi kutupa feedback.
Sikubaliani na mtu anaemtakia mwenzake kifo, kiwe cha corona au ugonjwa wowote ule, ajali, kurogwa, kupigwa ngumi au risasi. Ila pamoja na hayo, anza kuwaambia watawala watubu kwanza. You can't keep on killing people and expect the victims' relatives to wish you well. Namuomba BWANA YESU WA NAZARETH ANISAMEHE na kutupa wote moyo wa kusamehe.