Tukidhani ni Binadamu wenzetu, kumbe ni mashetani! Mtu unaombeaje mwenzako afe kwa Corona? Can't believe this wickedness! Huu sio utu, ni ushetani!

Tukidhani ni Binadamu wenzetu, kumbe ni mashetani! Mtu unaombeaje mwenzako afe kwa Corona? Can't believe this wickedness! Huu sio utu, ni ushetani!

  1. Tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara
  2. Kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi
 
Pascal Mayalla,
Pole sana mkuu Paskali kwa yaliyokupata, Uzuri ni kuwa hufi kwa korona kwavile mtu anataka, Hawa kweli wana mawazo mabaya. nikuambie tu kuwa 'utamaduni' huo haujaanza leo na tumekuwa tukiuchekea tu kwavile ni yule anayesemwa, si mimi.

Kwa mfano, kuna yule aliyetaka mbunge mwenzake auawe kwavile ni msaliti na akapigiwa makofi badala ya kukemewa. kuna na yule aliyesema wapinzani ni korona na ikawa sawa.
Pole ila tusilee tabia hizi za chuki.
 
Kaka yangu Paskali, naelewa uchungu wako. Lakini jiulize kama hiki unachokiona leo (and you have absolutely rightly spoken against it) kingetokea wakati wa miaka 5 ya mwanzo ya utawala wa Kikwete (let alone waliotangulia)?
Who are the culprits? Ilianzishwa wakati wa Kikwete wakati kina Mwigulu wanalipua mabomu na kuua watu wasio na hatia viwanja vya Soweto kwa ajili tu ya kuzuia CHADEMA wasishinde uchaguzi wa marudio wa udiwani. Magufuli alichokifanya ni kuongezea intensity ya tatizo ambalo ni mkakati wa kishetani wa ccm kubaki madarakani (na kumbuka kuwa Kikwete alituambia hadharani kuwa hata ccm kukubaliana na mbinyo wa kuruhusu vyama vingi "ulikuwa ni mkakati wa kuzuia watu wengi zaidi kuichukia ccm kwa kigezo cha kudai vyama vingi maana angalau kipindi hicho ccm ilikuwa inaungwa mkono na 80% ya Watanzania").
Unfortunately kwa ccm, muda huu Watanzania wengi ni waelewa na ccm wanajua kuwa kwenye uchaguzi huru na wa haki ccm LAZIMA itashindwa TU. Ndio maana bingwa wa kuogopa ushindani (Magufuli) anaogopa na kufanya ayafanyayo.

Paskali, naomba nenda ukawaambie watoto wa Azory, ndugu zake Ben Saanane, mke na watoto wa Tundu Lissu (na wengine wote walioumizwa) haya maneno uliyoyaandika leo halafu urudi kutupa feedback.

Sikubaliani na mtu anaemtakia mwenzake kifo, kiwe cha corona au ugonjwa wowote ule, ajali, kurogwa, kupigwa ngumi au risasi. Ila pamoja na hayo, anza kuwaambia watawala watubu kwanza. You can't keep on killing people and expect the victims' relatives to wish you well. Namuomba BWANA YESU WA NAZARETH ANISAMEHE na kutupa wote moyo wa kusamehe.
Hizi pia ni NONDO za uso na nina uhakika mtoa mada amezisoma kwa makini sana!!!!!
 
Ukiona hivyo maana yake watu wameshanyanyasika sana ila hawana cha kufanya wala pa kukimbilia ila sasa wanaona kama nature imetoa majibu kwa wanyonge...ndio wanaomba iwasaidie. Kuna watu huwa wanasema karma is a bitch...sasa tuone kama ni kweli kuwa malipo huwa ni hapa hapa.
 
Pascal Mayalla, Kwa jujuu naungana na wewe. Lakini kwa ndani silikubaliana na wewe. Mayalla ni hivi:
1. Huwezi kupata corona kwa kuombewa, kama vile ambavyo huwezi pona corona kwa maombi. Haijawahi tokea China, haijatokea Saudi, haijatokea Israel na will never never happen Tanzania.

2. Serikali yetu isipotuongoza vizuri kufuata maelekezo ya wataalam tutapata corona. (Sijasema haituongozi vizuri)

3. Ni kawaida siku hizi viongozi wa CCM kutumia vyeo vyao kutaka kuwaumiza wapinzani wao. Mara kadhaa tumeona wabunge wa CCM wakitaka wapinzani wauwawe!!!.

4. Lema anasema amefikishwa polisi zaidi ya mara 100, ni nani anayepanga haya?

5. Utekaji?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sielewi hadi post #334 P kashindwa kuchangia lolote ktk uzi aliouanzisha. Labda backlash imemzidi uwezo wa akili.

Naam!
Chuki ni kuu sana
Ina makali kuwili,
Kali kama pakanga
Inachoma kama fira
Mambo si mambo
Yanatisha

Bazazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyama Pinzani ndo wana tabia hiyo.

Kuna kile kipindi TBC ilisemekana wamepata Corona yaaani watu walikuwa wanashabikia kabisa oooh wakome, wajifunze maneno kibao, tena wakasema bora wapate maana ake Lissu alivyopigwa risasi TBC hawakuripoti.

Kinachoshangaza zaidi mtu anayesema hivyo nae anaenda kwa nyumba ya ibada au kabla ya kuingia kitandani anasali. Pathetic.
Huku hata wakifa wote ni sawa tu,hiyo tv imekaa kusifia tu huwezi wafe tu wote ni heri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utakufa wewe kwanza mjaa lana
Vipi dadangu, mbona unakuja kasi?! Una stress za kuachwa na kwahiyo unatafuta bwana kwa nguvu, au tatizo ni nini hasa?! Kama unatafuta bwana kwa nguvu, then you've a wrong guy cuz you're not my type, and you will never be no matter what.
 
Pascal Mayalla,
Paskali katika maisha yako hujawahi kutana na mtu mwenye uchungu lakini kicheko kinamtoka badala machozi. Hii hali ndio iliyowakumba baadhi ya watanzania katika kipindi hiki.

Sio kwamba wanawaombea wenzao kufa. Wanauchungu wa kuondokewa na jamaa zao kirahisi sana kwa sababu tu ya kauli ya mtu mmoja kwamba tusiwatie wananchi hofu, tuendelee na maisha ya kawaida.
 
Pascal Mayalla,
Bro mayala tatizo liko kwa wenye dhamana nani aliyejali mauaji ya mkuranga rufiji Nani alijali tundu lissu alipopigwa risasi tena wanamajibu ya hovyo sana eti mtu kaenda kwa hawara atarudi kweli Azori Gwanda Simoni Kanguye wote hawakujaliwa.

MwanaCCM anasimama anasema Lissu auwawe mwingine mbunge anataka Zitto auwawe nani aliwakemea braza si kwa mzee wa mafichoni chato wala nn waliona sawa kwasababu tu wana mtizamo tofauti....bro wakanye hao askari wa mbele kabla ya kuwageukia wa nyuma


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta Uzi ungeutendea haki Kama ungerudi nyuma na kutambua chuki hizi kwanini miaka ya karibuni watanzania wameonyesha kuchukia sana.

Mbona watu wa dini au madhehebu tofauti Bado wanapendana lakini wafuasi wa siasa wanachukiana na hasa wanawachukia viongozi wa upande tofauti.

Viongozi wa dini hajaacha kuhimiza upendo kwa waumini wa dini tofauti sio kwa maneno tu Bali kwa vitendo miongoni mwao bila unafiki.

Hii ni tofauti kwenye siasa na iko wazi.

NB siungi mkono kumuombe mtu mabaya


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom