Tukiendekeza siasa na udini katika mashindano ya African Football League, hayatadumu

Hoja yako ni nzuri Ila watu wameipokea kwa mtazamo was dini, siasa vitu ambavyo vyote vimekatazwa na FIFA. Saudia Arabia wanatumia nguvu kubwa ya pesa kupenyeza ajenda zao. Pia FIFA imetekwa na Mataifa makubwa Kama USA kuendesha ajenda zao.
 
Watu wana mtindo wanaacha hoja ya msingi iliyoletwa mezani wanakazia eneo ambalo halihusiani na hoja moja kwa moja au mfano ulioambatanisha. Huwa sifahamu wanafanya hivyo kwa kuwa ni mapungufu ya kifikra na uwezo wa kujadili mambo au ni maksudi baada ya kuona hoja ya msingi hawawezi kuipinga.
 
Umeandika sana mkuu.
Kwani leo hii Yanga si yupo top 24?
Msimu uliopita alikuwepo hata top 30?
Unashindwa nini kuelewa kuwa hiyo list itakuwa inabadilika kutokana na perfomance ya CAFCL?
 
Umeandika sana mkuu.
Kwani leo hii Yanga si yupo top 24?
Msimu uliopita alikuwepo hata top 30?
Unashindwa nini kuelewa kuwa hiyo list itakuwa inabadilika kutokana na perfomance ya CAFCL?
Hizo timu zitakazochaguliwa zitakuwa hazibadiliki. Pia kumbuka katika top 24 ya sasa hivi kuna nchi zina timu zaidi ya 2 unadhani zitachukuliwa zote?
 
No, kamsikilize motsepe alikuwa anongea Juzi.
As unaperform ndio utakavyopata nafasi ya kuingia.
Nilimsikiliza vizuri, sikumsikia mahali aliposema timu zitakuwa zinabadilika kila msimu. Amesema katika kuchagua hizo timu 24 wataangalia performance za nyuma na mafanikio ya ndani ya timu ya siku za nyuma siyo za mbele. Na ujue kuongeza timu hadi kuwa 24 ni kutokana na pressure waliyopata otherwise huu mtindo wa timu 8 hizi hizi ulikuwa ufanyike kwa muda.

Tunza uzi huu kwa haya niliyosema.
 
Mjadala unakuzidi kimo

Mkuu, huku bongo hapakufai japo nimeona wakristo wengi tu wanasapoti israel na mauwaji yanayoendelea huko gaza, haijalishi watoto, wazee wao wanashabikia tuu, so Nenda kaishinao hao mayahudi wanaoungwa mkono na mataifa yafuatayo (brazil, india, uingereza, marekani, Germany, france n.k.)
 
VIdeo bado zipo naomba ukarudia kumsikiliza.
 
Bongo hapanifai kisa nimekumbusha madhara ya kuingiza masuala ya dini na siasa kwenye mpira, jambo ambalo CAF na FIFA wamekuwa wanalisisitiza muda mrefu? Nani anastahili kuishi?

Kwa taarifa yako nimekaa mbali kabisa na mijadala na hata news za kinachoendelea huko Mashariki ya Kati. Mada hii nimeileta kwa maslahi ya mpira wa Afrika na AFL siyo kuonyesha hisia zangu binafsi kuhusu masuala ya imani au itikadi za kisiasa.
 
Hao fifa ndo waanzilishi wa siasa michezoni sasa sijui hiyo fifa inayo isemea ni ipi?
 
Ingelikua imeekuuma jinsi wanavyonyanyasika wapalestina, na maelfu kuuawa tena wasio na hatia usingekuja na huu mjadala wa udini

We stand with Palestine 🇵🇸
 
Reactions: Tui
Hao fifa ndo waanzilishi wa siasa michezoni sasa sijui hiyo fifa inayo isemea ni ipi?
Unajua maana ya neno "waanzilishi" au unasema tu ili mradi?
 
Ingelikua imeekuuma jinsi wanavyonyanyasika wapalestina, na maelfu kuuawa tena wasio na hatia usingekuja na huu mjadala wa udini

We stand with Palestine 🇵🇸
Mpira siyo mahali pake. Nimeuliza maswali ya msingi hapa yote mnayakimbia na kwa kauli zenu inaonyesha hamko tayari kusikia au kuona mtu akiwa na maoni tofauti na nyie halafu cha kushangaza ndiyo mnatuhumu wengine kwa ubaguzi. Inashangaza sana.
 
Punguza chuki za kishamba
Maoni kuwa siasa na dini viwekwe mbali na mpira ndiyo chuki? Unajua mara ngapi nimepinga Simba na Yanga kutumika kupenyeza milengo ya kisiasa, nazo zilikuwa chuki? Ushamba ni kudhani wewe pekee ndiyo una haki ya kutoa maoni yako ila mwenzio akitoa ya kwake unataka hata kumdhuru. Huo ndiyo ushamba.
 
Haya maoni umeanza leo?Lete reference ukiitetea Urusi kwa kuondolewa kwenye mashindano yote yanayosimamiwa na FIFA na UEFA nitaamini haukuwa na agenda yako binafsi. Vinginevyo ni kujaribu kuzuia jua kwa ungo.
 
Kuna ambao mnaileta Russia kwenye mada hii wakati ishu hazifananii kabisa, sielewi mnaitaja kwa angle ipi
 
Waarabu ndio wenye pesa kwa sasa, michezo inachohitaji ni pesa tu hata Vatican wakitaka kumiliki timu watu hawana shida kikubwa pesa, official broadcaster wa AFL ni abudhabi sport ndio walioweka mpunga mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…