Tukifanya Hivi, Kina Mwamposa na Manabii kuwa Walipa Kodi Wakubwa

Unaweza kulifanyia hesabu kanisa katoliki kila senti ukajua inakwenda wapi na inatumika vipi tofauti na hao kina Mwaposya na wa aina hiyo.

Ipo nidhamu ya uendeshaji wa kanisa katoliki ambayo haipo katika makanisa hayo mengine.
Inakwenda kuhudumia kanisa kwa ujumla wake dunia nzima, haibaki yote parokiani.
Ila swali? Watumishi wa kanisa wanalipa PAYE?
Baba zangu wadogo watatu wamejenga nyumba nzuri kijijini kwetu na ni mapadri....hamna padri ambaye hajajenga kwao nakuapia

Mwamposa: Hela inarudi kuendesha huduma na kuwalipa wafanyao kwenye huduma haiendi kwa familia....mwamposa ana hotel mbeya hela za sadaka
 
Uko sahihi kuna watu wanataka kuchokonoa mzinga wa nyuki kwenye haya mambo ya dini

Serikali ikisema haina dini viongoxi wa dini waache kuchokonoana mara ohh yule halipi kodi Serikali nendeni mkamdai

Hayo mambo yatafanya Serikali inogewe na taratibu kuanza kuingilia mambo ya kanisa

Baadaye utakuta TRA hawa hapa wako kwenye mnada wa siku ya mavuno kanisani kuku mmoja anayeuzwa milioni moja mnada wa siku ya mavuno kanisani TRA itataka kodi yake ya mapato

Wivu wa kijinga kuona ohh yule anapata pesa kuliko mimi utaponza makanisa
 
Hayo makanisa ya kisasa ni biashara za watu binafsi huwezi kulinganisha na ukatoliki, angalau kila kinachopatikana kinahesabiwa na kujulikana.

Sikatai uwepo wa ufisadi kanisa katoliki hata hapa mbezi beach St Gasper umekuwepo ufisadi lakini huwezi kulinganisha na hayo yanayofanyika katika makanisa binafsi.

Unawaambia waumini watoe mpaka senti yao ya mwisho halafu wewe askofu unaendesha magari ya bei mbaya! hiyo ni laana mbaya sana.

Na kuna mambo mengi ya kijinga yanayofanyika huko na ni mengi.
 
Mwamposa ana kiwanda chake binafsi ..Maji yake Yana label yake binafsi na waumini wanauziwa hayo maji....uzembe Tu WA Tra...

Hawatakiwi hata kwenda kabisani..
Waende straight kiwandani kwake
 
Sio suala la wivu ukatoliki umekuwepo miaka mingi sana kabla hata hao maaskofu wa makanisa binafsi hawajazaliwa.

Kero ni kuona ongezeko la watu wanaofanywa wajinga kwa sababu ya umaskini wao binafsi, Mungu anatumiwa kibiashara na mtaji na ujinga usiokwisha huko mitaani.
 
Hajakataza hilo mbona.......sio kila muumini atakumbuka au atataka kubeba maji kutoka nyumbani hivyo kawasogezea tu huduma.

Alafu hiyo pia ni sehemu ya sadaka ili kuwezesha huduma yake iendeleee kuwepo.
[emoji3][emoji3][emoji3] sasa kama waumini wa Mwamposa mna tatizo la kusahau, kwanini nabii wenu asiwaombee hilo tatizo liwaishe..
 
[emoji3][emoji3][emoji3] sasa kama waumini wa Mwamposa mna tatizo la kusahau, kwanini nabii wenu asiwaombee hilo tatizo liwaishe..
Tuna mengi ya kufikiri na kukumbuka zaidi ya kutembea na maji.
 
Njoo Arusha,
Arusha ingependeza ungetaja hilo kanisa linalofanya hivyo, lakini kutaja mkoa mzima kwa ujumla, kama jimbo, naamini unakosea, kwasababu sina hakika kama hayo maamuzi yalikuwa makubaliano yaliyohusisha makanisa yote ya jimbo husika..

Kama ndivyo, unamaanisha jimbo la Arusha lina uwezo wa kujiamulia mambo yake lenyewe, tofauti na majimbo mengine, kitu ambacho sikubaliani nacho.
 
Mwamposa ana kiwanda chake binafsi ..Maji yake Yana label yake binafsi na waumini wanauziwa hayo maji....uzembe Tu WA Tra...

Hawatakiwi hata kwenda kabisani..
Waende straight kiwandani kwake
Wew una uhakika kuwa kiwanda hicho hakilipi Kodi au nabwabwaja tuu maneno?
Hapa hakiongelewi kiwanda kinacho jadiliwa ni Yale maji yakisha fika kanisani baada ya kuwa yamesha lipiwa Kodi kiwandani ndipo watu wanataka waumini wakiyachukua Kodi ilipwe tena.
Ni sawa na wew muumini umeamua kupeleka vitu vyako kanisani ili vinadiwe kwajili ya kusaidia huduma halafu anatokea kibwetele fulani anataka ulipe Kodi baaada ya mnada.
 
Itatengenezwa sheria kuenenda na hicho wafanyacho hao "mitume na manabii" wenu.
 
Nimesema wazi hapo ...Tra hawapaswi kwenda makanisani wala misikitini...kama ni maji waende kiwandani....
 
Ruto yuko vizuri! Mama samia punguza tozo kwa wananchi kamua hao manabii fake
 
Woote mwamposa , Catholics ni wafanya biashara wanaotumia mifumo, call them modalities tofauti.
Nimeeleza hapo juu, na hizi modules zao za biashara ni out of our Tax laws scope

Upo sahihi sana. Catholic Church imetengeneza mfumo wake wakupata pesa na Mwamposa naye anatengeneza mfumo wake. Wote ni walewale tu.

Kuna dada mmoja alifika hapa kwangu (Arusha) anaomba nimsaidie mchango anadaiwa kanisani (catholic). Nilimuuliza how much? Akaniambia kiasi alichopangiwa ni karibu laki tatu hivi, na document ya church alinionyesha. Nikasema well nimpatie kiasi, lakini nikajiuliza hii si biashara hii? Huyu dada masikini atapata wapi hii pesa? Si atakuwa anasumbua watu wamchangie?

Jambo lakushangaza yeye mwenyewe anatetea kiasi alichopangiwa nakanisa, ambacho hana.

Mwisho tunarudi palepale Catholics na mwamposa wote macho yao ni kwenye fedha. Kila mtu anatumi mbinu zake.
 
Mwamposa ana kiwanda chake binafsi ..Maji yake Yana label yake binafsi na waumini wanauziwa hayo maji....uzembe Tu WA Tra...

Hawatakiwi hata kwenda kabisani..
Waende straight kiwandani kwake
Asilimia kubwa ya maji anayotumia Mwamposa kwenye mambo yake kiimani ni ya Hill Water, na hicho kiwanda kipo Mapinga, Bagamoyo..

Wewe kama unajua hicho kiwanda chake, weka hapa jina lake, maji anayotengeneza yanaitwaje, na wapi hicho kiwanda kilipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…