Imekuwa rahisi kwa Ruto, kuja na msimamo huo kwa kuwa yeye mwenyewe ni mkristo mzuri tu, kwa upande wetu itakuwa na changamoto kwani, Rais wetu ni muislam, akijaribu issues za udini zitaamka tu.Nashindwa kuelewa kwanini TRA wanashindwa kuiga kwa Ruto wa Kenya na kuongeza mapato kutoka katika wimbi hili la mitume na manabii walioanzisha biashara ya Maji, chumvi, vitambaa nk wakiviita vya upako na kupata fedha nyingi sana kama biashara isiyo kodi wala cost of production. Msome Rais Ruto alivyoamua.
"Nimeongea na watendaji wa serikali yangu kuhusu baadhi ya wahubiri kucheza na imani za wakenya. Kuanzia sasa yule anataka kuuza maji asajiliwe na mamlaka ya maji, yule anataka kuuza mafuta asajiliwe na food and drugs authority, na yule anataka kuuza mbegu asajiliwe wizara ya kilimo. Watambulike kama wafanyabiashara, na serikali ijue wanauza ngapi kwa siku na walipe kodi. Huku kwa kanisa wabaki wanaoeneza neno la Mungu, sio wafanyabiashara. Hatuwezi kuruhusu imani za wakenya kuchezewa na wakora wachache, wanaotaka kujitajirisha kupitia shida za waumini wetu" William Samoei Ruto, Rais wa Kenya.
Na akikumbuka marehemu JPM alivyohandle issue ya ajali kwenye kongamano la Mwamposa Moshi,hiyo yeye Samia kuwakabili ni lazima itasumbua.