Kafungue na wewe uuze na utoe kodi kama ni rahisi. Kuwa weka watu na kuwa na furaha ya moyon ni zaid ya kodi
Mbona makumbi ya disco wanalipa Kodi.
Yaaani MTU anakibanda anauza katoni moja ya Maji Kwa Siku alipe Kodi halafu MTU anayeuza katoni mia Tano Kwa Siku asilipe Kodi . Afrika Sijui tumelogwa na nani ?
Ni Bora basi Kama angekua anatoa huduma nyingine Kwa jamii kama kujenga mashule ya walemavu Bure , kichimba visima Bure , kujenga mabweni ya watoto Wa Kike n.k. lakini anapata Fedha nyingi za kuinua maisha yake Binafsi kama wafanyabiashara WENGINE wanaolipa Kodi halafu yeye halipi. Anatembelea Magari ya kifahari anajenga mahoteli yake Binafsi Kwa mgongo Wa taasisi ya kidini halafu halipi Kodi. Dini ni taasisi sio biashara ya MTU Binafsi Kwa sababu Ukristo au YESU SIO Mali yake .
Biblia ni kitabu cha Taasisi ya Kikristo huwezi kukitumia Kwa biashara zako Binafsi kitapeli ukaachwa tu.
Brand ya Kristo ilitangazwa Duniani Kwa Jasho na damu za watu ukianzia na ya Kristo Mwenyewe ivyo kuitumia Kwa manufaa Binafsi Badala ya jamii ni Makosa . Walipe Kodi Ili serikali ihudumie wananchi. Kanisa limelala sana ndio Maana Taifa linaangamia kidogo kidogo na serikali nayo isipoona kama Alivyoona Ruto SIO muda mrefu Taifa hili kitapata adhabu kubwa sana .
Ukiangalia watu wamejawa na roho mbaya ya tamaa ya Fedha ,kupitiliza, uaminifu umepungua sana Kwa Wakristo Kwa sababu Wachungaji na manabii wao na maaskofu wamejawa na tamaa kubwa na ubinafsi . YESU amebaki kama biashara ya watu Binafsi na SIO mwokozi Wa roho za watu WOTE kwenye jamii iliyojaa uzinzi,uongo, ulafi,ulevi, Wizi, mauaji, ulawiti , uonevu, na Kila aina ya ubaya lakini Jumapili watu Hao wamejaa makanisani Kununua majai ya upako Badala ya kutubu dhambi na kuziacha Kwa kumaanisha. Watu hawatoi sadaka Kwa ajili ya watumishi na huduma ya Injili Bali wananunua Maji na kuuza Maji.
Kanisa la Kirumi nalo Karne za giza zilizopita Lilifanya utapeli Kama Huo Kwa kuuza Vyeti vya msamaha Wa dhambi . Watu walikimbilia Kanisani kwanye kanisa Katoliki Kwa ajili ya kupata vyeti vya msamaha Wa dhambi.
Wasiokua na vyeti walihesabiwa kuwa ni watu Wenye dhambi na kutengwa.
Hali hiyo ya ukengeufu ilipingwa na Padri mmoja Wa kanisa Katoliki aliyeitwa Martín Luther. Aliupinga utaratibu huo Kwa nguvu zote Hata pale alipotangaziwa kuuawa lakini alisimamia msimamo wake. Baadae walijitokeza waumini WENGINE Kuunga mkono na kuitwa waasi.
Hapo likatokea kanisa la Lutheran na Kanisa Katoliki Kwa kiwango kikubwa likabadili baadhi ya taratibu za kitapeli na kurudi kwenye taasisi ya KIROHO.
Hata hivyo utapeli uliofanywa na Kanisa la Rumi ulifanywa kitaasisi na SIO matakwa ya MTU Kwa manufaa yake. Sasa Leo uuzwaji Wa Maji tiba unaofanywa na Watu Wanaojiita mitume unafanywa Kwa manufaa Binafsi . Ndio Maana kanisa linarithishwa MKE na Watoto wake. Kwa Maana kwamba ni Biashara ya familia kama biashara nyingine zilivyo.