Tukifanya Hivi, Kina Mwamposa na Manabii kuwa Walipa Kodi Wakubwa

Tukifanya Hivi, Kina Mwamposa na Manabii kuwa Walipa Kodi Wakubwa

Ningekutaka uthibitishe ila tutaamsha malumbano yasiyo na maana sababu usingeweza kuthibitisha haya

Ila nimepigwa butwaa kuona ulichoandika hapa maana sijawahi kukutana na kitu kama hicho ktk maisha yangu imani
Yani jamaa katudanganya mchana kweupe utadhani sisi siyo Waumini na hatujui mambo yanavyokwenda
 
Sijawahi kuona Kanisa kwa maana ya Parokia or Jimbo likisema waumini mtatoa kila mmoja mfano laki 3 kwa mwaka.Wewe unachanganya na kupangiwa na Jumuiya unasema ni Parokia/Jimbo.

Kinachofanyika ni huwa Jimbo linapangia kila Parokia ikusanye kiasi flan tuseme kwa ajili ya mavuno.Parokia ikipokea inagawanya kile kiasi ilichopangiwa katika Jumuiya zake na inagawanya kulingana na ukubwa wa Jumuiya mfano Jumuiya ya Mt.Yuda Thadei wanaweza kuambiwa wachangie 2.5M wakati Jumuia ya Mt.Clara wakapangiwa watoe 600K.

Jumuiya zinavyopokea kiasi kilichopangiwa wanakaa chini na kukubaliana sasa kila kaya ya hiyo Jumuiya wachangie kiasi gani? Huwezi kuta mchango huo unalingana.Lakini pia swala la michango ya dhaka,hiyo ni mtu mwenyewe ndiyo anaamua mwaka huu nitachangia kiasi gani,zaka hazilingani pia.

Mnapotuambia Arusha wako tofauti,mna maana Arusha wan Dunia yao peke yao katika utaratibu wa uendeshaji wa Kanisa Catholic nnje ya utaratibu mama unaowekwa na TEC?

Mimi nimemuuliza,ina maana Jimbo la Arusha liko juu ya TEC? Maqna anavyoelezea utadhani Jimbo la Arusha lina utaratibu wake tofauti kabisa na Majimbo mengine yote Tanzania yaliyo chini ya TEC
Mbona kuna parokia nyingi Kila mtu wanampagia Fedha kwa mwaka kwa ajili ya ujenzi?. Ndugu mkuu mimi nimkatolinki, kuna sehemu kuna michango mingi.
Makanisa yote yanahitaji fedha ili yajiendeshe kwa hiyo lazima wajue wanatafuta vipi fedha za uendeshaji.
 
Kodi inatozwa kwenye mapato ya:
1. Business
3. Employment
3. Investment

Sasa tukija kwenye tafsiri business income as per Income Tax Act (ITA) unakuta akina mwamposa and co, wako nje ya wigo wa hiyo tafsiri ( out of scope)

Kodi haitozwi kwa hisia...Kodi inatozwa kwa sheria ambazo ziko challenged mpaka kwenye court of appeals kama kuna mzozo.

Sasa wakati wa utunzi na utafsiri wa sheria ya Kodi words must strictly construed and clearly stated.nje ya hapo hiyo sheria haitafanya kazi.

SASA NIAMBIENI MODALITIES YA HIYO SHERIA ITAKAAJE KIASI KWAMBA ITAMKAMATA MWAMPOSA IACHE SADAKA ZA KAWAIDA KANISANI na Msikitini
Umeambiwa wanauza Maji ,Chumvi na Mafuta. Hizo ni bidhaa Kama bidhaa nyingine zinazolipiwa Kodi.

Sadaka SIO bidhaa ni michango tu kama ilivyo ya harusi na send off . Hakuna kiwango Cha sadaka ni Imani ya MTU na uwezo wake . Tena MTU anayetoa sadaka anakua ameshalipa Kodi zake zote HUKO SERIKALINI Sasa anakwenda kumshukuru Mungu.

Kuuza chupa ya Maji ya nusu Lita Sh. 50,000/- bila Kodi ni Wizi.

YESU mwana Wa Mungu alifanya MUUJIZA Wa Chakula Kwa kuongeza mikate michache ikawa mingi lakini hakuiuza kutibu njaa. Sasa Hawa matapeli wangeweza kuongeza gunia moja la Mchele yawe magunia Elfu Moja kipindi Cha njaa wangeuza Kwa Bei kubwa wasio na Fedha wafe njaa.
Huu nao ni aina ya ushetani utapita mana Maarifa na Ukweli utawaweka watu huru. Watu wanapenda kudanganywa na hawana maarifa ya Neno la Mungu hivyo watadanganywa kuwa mafuta yanatibu lakini watu wanaowadanganya wakiugua wanakwenda kutibiwa na kuchekiwa kwenye MRI iliyotengenezwa na Mwanadamu mwenye maarifa ya kisayansi.
 
Yani jamaa katudanganya mchana kweupe utadhani sisi siyo Waumini na hatujui mambo yanavyokwenda

Nidanganye kwasababu gani mzee?

Dada kanifuata kaomba mchango anadaiwa kanisani (catholic), wewe unakataa nini hasa?

Tena alikuwa desperate sana inaonyesha hiyo pesa inatakiwa kwa haraka.

Mimi ni mtu mzima ninaelewa mambo.
 
Alter wine inatengenezwa Dodoma na huwa inapelekwa moja kwa moja Majimboni na Parokia zote wanakwenda kuchukulia pale Jimboni.Sasa hiyo ya kuuziwa 5lts nani anamuuzia? Pale Jimboni au Parokiani?
Masista wanatengeza katka parokia baadhi na watu hununua wine kwa kunywa.
 
Ningekutaka uthibitishe ila tutaamsha malumbano yasiyo na maana sababu usingeweza kuthibitisha haya

Ila nimepigwa butwaa kuona ulichoandika hapa maana sijawahi kukutana na kitu kama hicho ktk maisha yangu imani

Unamaanisha nini nithibitishe?

Unataka nikamtafuta dada nimlete hapa aseme alikuja kwangu kuomba pesa ili alipie mchango wa kanisa waliompangia?

Unataka nithibitishe nini hasa?
 
Hoja iko hivi?
Kodi hutozwa kwenye mambo matatu tu yaan, business, investment, employment. Chochote nje ya hapo hakitozeki Kodi (out of scope)
Sasa unatakiwa uje na sheria itakayosema na iwe strictly construed ili inmase mwamposa.
No intendment in tax laws, words must clearly be stated.
SASA EBU NISAIDIE HIYO SHERIA ITAKAAKAJE KIASI KWAMBA SADAKA AU MICHANGO kanisan itofautishe na mambo ya mwamposa?
Utaishia kutunga sheria mfu kwan haitaweza kufanya kazi.

Inatakiwa hivi unapowashtaki mwamposas useme ni kivipi arrangement ya transactions zake za maji na mafuta namna ambavyo fall within tax laws na sio kihisia.

Sasa mwamposa si atasena toeni sadaka nitawagawia maji MUNGU alioniruhusu niwagawie...
Wale wa 5,000 watapewa maji , chin ya hapo hatawapo ...hajairuka sheria yeyote
Mwamposa anafanya biashara , yupo ndani ya sheria ya biashara.

Maji anayoyauza kwenye ibada zake huwa huyaoni.

Hapo muhimu ni anazuiwa kuuza hayo maji mpaka apewe leseninya biashara, simple.
 
Sacraments haziuzwi.Utauzaje Sacrament ya Kipaimara ,ubatizo au Komunio? Kama ulimaanisha ile ekarist wanayokula hizo zinatengenezwa Kanisani na masister,huwezi zikuta ziko zinauzwa dukani kama maji,chumvi na mafuta.
Mweleze huku mtu anaweza pokea ekarist hata kama hajatoa sadaka.
 
Mbona kuna parokia nyingi Kila mtu wanampagia Fedha kwa mwaka kwa ajili ya ujenzi?. Ndugu mkuu mimi nimkatolinki, kuna sehemu kuna michango mingi.
Makanisa yote yanahitaji fedha ili yajiendeshe kwa hiyo lazima wajue wanatafuta vipi fedha za uendeshaji.
Michango karibu yote huwa ni Jumuiya ndiyo inapangiwa.Ni kazi kila Jumuiya kukaa na wanajumuiya wake kuona wanapataje hicho kiasi walichopangiwa na kila mchango unapokwenda Kanisani wanachotangaza ni Jumuiya X imetoa kiasi hiki mpaka sasa kati ya lengo walilopangiwa,hawatangazi Mr.Peter ametoa kiasi kadhaa cha ujenzi wa Kanisa.
 
Masista wanatengeza katka parokia baadhi na watu hununua wine kwa kunywa.
Zitakuwa ni sehemu chache sana kama ni hivyo.Lakini nachojua Altar wine yote inatoka Dodoma na huwa wanaletewa kwenye zile drums za blue za ujazo wa 250 ltrs.
 
Mbwa hawa wanaofanya biashara ya kuuzauza mara maji, mara mafuta kanisani walaaniwe kabisa. Injili ya kweli inasema "mmepewa bure, toeni bure" MATHAYO 10:8. Jihadharini na mbwa... WAFILIPI 3:2.
 
Wacheni kupotosha ili kumlinda huyo jamaa yenu.

Makanisa hufanya harambee kwa kuuza vitu kwa lengo la kupata pesa zitakazotumika kwa shughuli fulani hapo kanisani, kama ujenzi, ukarabati wa jengo, hakuna harambee inayofanywa bila sababu.

Kwa mantiki hiyo, sasa hebu tuambie, Mwamposa akiuza maji na mafuta, hizo pesa huwa anazipeleka wapi?na kufanyia kitu gani?
Kwani wew ukifanya harambee hapo kanisani kwako huwa unamuona Mungu ameshuka kuja kuzichukua hizo pesa? Acha kuulizia maswali ya kijinga halafu unajifanya Mkristo
 
Nani alikuuzia mvinyo Kanisani?
Unataka nikutajiae jina au?hii mbona iko wazi,hata leo ikiisha anaenda kununua hukohuko RC,na sio kwamba inauzwa kwa kificho hapana,hata wengine wananunua hapo
 
Unamaanisha nini nithibitishe?

Unataka nikamtafuta dada nimlete hapa aseme alikuja kwangu kuomba pesa ili alipie mchango wa kanisa waliompangia?

Unataka nithibitishe nini hasa?
Ukinisoma pale juu kwa umakini utaona kabisa sikutaka tufike mbali sana kwa sababu isingewezekana kwa wewe kuthibitisha ulichoandika.

Naishi kwenye jamii ya watu wakati mwengine vipo vikao vya michango mbalimbali eg harusi au misiba (imani yangu hata wewe umewahi kushiriki) huwa tunaahidi kiasi fulani cha pesa kulingana na mtu uwezo wako lakini hukuti kuambiwa wewe Saint Anno II lazima uchange Tsh 50,000/= hiyo ni kwa jamii ya kawaida sasa kwa mtu timamu kuamini lipo Kanisa somewhere tena RC lilimlazimisha mtu tena maskini (nasema maskini kwa namna ulivyomtambulisha) atoe Tsh 300,000/= inakuwa na ukakasi sana.
 
Unataka nikutajiae jina au?hii mbona iko wazi,hata leo ikiisha anaenda kununua hukohuko RC,na sio kwamba inauzwa kwa kificho hapana,hata wengine wananunua hapo
Taja Kanisa tujue tufanye uchunguzi na sisi tuamini maneno yako.

Nataka uniambie wewe hiyo wine inauzwa ktk mazingira gani?ndani ya Kanisa au ktk ofisi ya Kanisa?hao wengine wanaonunua hapo obviously walitangaziwa so ni biashara yao waliyoitangaza nitakachofanya nitaitafuta hata mtandaoni niwaulize kama mteja lengo nijue.
 
Yani jamaa katudanganya mchana kweupe utadhani sisi siyo Waumini na hatujui mambo yanavyokwenda
Hawa wasikusumbue mkuu,yupo shehe mmoja uneducated kwa wanaomjua aliishia darasa la nne kwao Mtwara miaka ya 2000 kipindi kile cha mihadhara ya kidini ya wafia dini wasiokuwa na elimu yoyote kuhusu Ukatoliki (wachungaji wa kipentekoste na mashehe ubwabwa) walikuwa wanaparurana mpaka kufika kuliingiza Kanisa Catholic.

So upumbavu aliokuwa anauongea huyo shehe kuhusu RC hao walokole wakashindwa kujibu ilikuwa inaonekana kwake ni ushindi na hii imewajaza ujinga hata waumini wao kuamini kwamba majibu waliyokuwa wanayatoa hao walokole yawe ni ya kweli au ya uwongo ndicho Kanisa linachofundisha.

Nimesahau jina lake ungemsikiliza YouTube ila mimi nimewahi kumsikiliza live pale Manzense Bahakresa akiushambulia Ukatoliki na nyingi ya chuki wanazoandika humu wanafuata kile alichokuwa anakiongea tofauti unakuta muhusika amejifanya yeye ndiyo imemkuta ili kuitia uzito hoja yake.
 
Mishahara yao
Inakatwa kodi hiyo mishahara ya mapadre kanisa katoliki? Na masista na Mabruda na maaskofu katoliki?

Kama haikatwi TRA waende huko kudai kodi ya PAYE

Huu ujinga kukomesha kila mtu alipe kodi wakiwemo mapadre, masista na Mabruda sababu wao ndio wako bitter sana na Mwamposya as if wao huwa hawalipwi chochote kupitia sadaka za waumini hadi wanaanzisha miradi binafsi na kununuliwa magari nk
 
Back
Top Bottom