Tukio gani kwenye soka huwezi kulisahau?

Tukio gani kwenye soka huwezi kulisahau?

Goli la mapema baada ya Yanga kufunga hata hawajamaliza kushangilia ulipigwa mpira na chenga za maudhi likaingia goli.

Hii nayo ikae kwenye rekodi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni mchezo wa Fainali ya kombe la dunia, takribani watu bilioni 1 duniani wanafatilia mtanange huo.

Dakika ya 3 ya nyongeza ndani ya dakika 120, ubao ukiwa unasomeka 3-3 kwa Ufaransa na Argentina.

Ndani ya dakika 3 za nyongeza, zikiwa zimebaki sekunde 16 mtanange uishe ili waende penati, huku Leo Messi akijaribu bahati yake ya mwisho ya kutwaa kombe la dunia, ghafla mpira mrefu wa kushtukiza unapigwa kuelekea lango la Argentina.

Kolo Muani, mshambuliaji wa Ufaransa anaupokea mpira ule huku akiwa amebaki yeye na kipa Emiliano Martinez na akijua kabisa akifanikiwa kuweka mpira ule nyavuni anaipa nchi yake goli la 4 na pengine la ushindi.

Kolo Muani anaucha ule mpira unadunda kisha akipiga shuti kati ambalo kipa Martinez anafanikiwa kuzuia na mguu wake na kuinyima Ufaransa nafasi ya ushindi.

Sekunde chache baadae refa anamaliza mpira. Wanaenda mikwaju ya penati na Argentina wanaenda kutwaa ndoo ya dunia mara baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho pale Mexico mwaka 1986.

Hili tukio siwezi kulisahau maana lilibadilisha muelekeo mzima wa mechi, na tukio hili linatajwa kama moja ya save bora kuwahi kufanywa na kipa katika historia ya mashindano ya kombe la dunia.

Wewe ni tukio lipi huwezi kulisahau?

View attachment 2633541
Aguerooo, siku yangu mbaya sana kisoka.
 
Uefa final chelsea vs man u 2008
John tery anakosa penati ya ushindi[emoji17]


Worl cup quarter final uruguay vs ghana 2010
Asamoh gyan anapaisha penati[emoji24]
 
Siwezi kuisahau fainali ya Uefa Champions league 1999 nikiwa darasa la 5, primary....Man U vs Bayern Munchen.....

Chama langu man U tukiwa nyuma kwa goli 1 hadi dk ya 90....(ENZI HIYO YAKIWA MASHETANI MEKUNDU KWELI)...Sio sasa...

Mnyamaaa! Teddy Sheringham ana-equlize! 1-1 kwenye sekunde ya 34 ya dk 3 za nyongeza!!!...

One guner solskjaer (sosha) anapigilia Msumari wa 2 na wa mwisho...kwenye Jeneza la Munchen!

What a Superb Game!....UNBELIEVABLE!
 
Kuna match ujerumani na Italy World Cup 2006......kocha wa ujerumani alikuwa anaandika wapiga penalties dk ya 118 asee nilichokiona kilikuwa ni ukatili wa kibinadamu asee match ilikuwa 0-0
Nimeenda toilet narudi dah nakuta Italy 2-0Germany


Kocha akatafuta kikaratasi🤣🤣
 
Kuna match ujerumani na Italy World Cup 2006......kocha wa ujerumani alikuwa anaandika wapiga penalties dk ya 118 asee nilichokiona kilikuwa ni ukatili wa kibinadamu asee match ilikuwa 0-0
Nimeenda toilet narudi dah nakuta Italy 2-0Germany


Kocha akatafuta kikaratasi🤣🤣
Fabio Grosso mwanaharamu yule,,alifanya binding mmoja wa kijerumani alie sana afu mtangazaji anatangazia sifa.
One of the saddest day in my life
 
Goli la dhahabu la Iniesta dhidi ya Chelsea nusu fainali UCL 2009.

Hilo goli siwezi kulisahau mpaka siku ntakayokufa.
 
Back
Top Bottom