Tukio gani kwenye soka huwezi kulisahau?

Tukio gani kwenye soka huwezi kulisahau?

Hilo la Muani hata yeye mwenyewe kichwani mwake haliwezi kufutika.Pia matukio kama haya hayafutiki kichwani mwangu (1) Gatuso kumkaba Ronaldo, hiyo ilikuwa AC Milan Vs Man utd
(2) Suarez kudaka mpira uliokuwa unaelekea kuwa goli, Uruguay Vs Ghana (3) World cup 2010 German Vs England Lampard anasawazisha lakini refa anakataa goli.Nadhani hiyo ndio iliwafanya waingereza wagundue goal line technology maana mpira aliopiga Lampard ulivuka mstari WA goal na kurudi ndani.
Umenikumbusha mbali sana Gatuso na Ronaldo, Gatuso alikua akimfuata Ronaldo Kila anakoenda hata kama hana Mpira 🤣🤣
 
UEFA 2012
BAYERN MUNICH vs CHELSEA
penalty shout-out
Master wao Bastian Shwaztaiger anakosa tuta afu drogba akamaliza kazi,
What a moment!
Kocha Di Matteo hapo, uwanja wao na bado kombe tukabeba 😂😂
FC BARCA vs MANJESTA YUNAITED
ilipigwa mbungi mpaka babu fergie pete ilitetemeka ikataka kutoka, after match babu alisema "tokea nianze kufundisha mpira sijawahi kutana na timu ya hatari kama barca hii"
Babu alikua mwekundu, miwani ikawa mizito, Big G ikawa chungu

Barcelona ya muda ule ilikua ya kuogopwa mno
 
Ni mchezo wa Fainali ya kombe la dunia, takribani watu bilioni 1 duniani wanafatilia mtanange huo.

Dakika ya 3 ya nyongeza ndani ya dakika 120, ubao ukiwa unasomeka 3-3 kwa Ufaransa na Argentina.

Ndani ya dakika 3 za nyongeza, zikiwa zimebaki sekunde 16 mtanange uishe ili waende penati, huku Leo Messi akijaribu bahati yake ya mwisho ya kutwaa kombe la dunia, ghafla mpira mrefu wa kushtukiza unapigwa kuelekea lango la Argentina.

Kolo Muani, mshambuliaji wa Ufaransa anaupokea mpira ule huku akiwa amebaki yeye na kipa Emiliano Martinez na akijua kabisa akifanikiwa kuweka mpira ule nyavuni anaipa nchi yake goli la 4 na pengine la ushindi.

Kolo Muani anaucha ule mpira unadunda kisha akipiga shuti kati ambalo kipa Martinez anafanikiwa kuzuia na mguu wake na kuinyima Ufaransa nafasi ya ushindi.

Sekunde chache baadae refa anamaliza mpira. Wanaenda mikwaju ya penati na Argentina wanaenda kutwaa ndoo ya dunia mara baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho pale Mexico mwaka 1986.

Hili tukio siwezi kulisahau maana lilibadilisha muelekeo mzima wa mechi, na tukio hili linatajwa kama moja ya save bora kuwahi kufanywa na kipa katika historia ya mashindano ya kombe la dunia.

Wewe ni tukio lipi huwezi kulisahau?

View attachment 2633541
Kolo muani alizingua sana hilo tukio litamtafuna sana,,, wenge lake lilituvunja mioyo sana tuliokuwa tunaisupport ufaransa,,, na sidhani kama kombe la dunia lijalo atakuwa kwenye timu
 
Kolo muani alizingua sana hilo tukio litamtafuna sana,,, wenge lake lilituvunja mioyo sana tuliokuwa tunaisupport ufaransa,,, na sidhani kama kombe la dunia lijalo atakuwa kwenye timu
Yule bwege laiti kama angempa pasi mbape....
 
2005 Liverpool vs Ac milan 3:3 hii ilikua [emoji91].
8 April 2008 Liverpool 4:2 arsenal hii match walcott anawatoka wachezaji sijuii 6 wale ana pass kwa adebayor anatia kamba dk 84 inakuwa 2:2 wenger anaonyesha mikono wachezaji watulie game imeishaaa daah [emoji23][emoji23] dk 86 Liverpool wanapata tuta baadae babel anatia chuma cha 4 .. Arsenal always ni losers [emoji23][emoji23][emoji23]

FA cup final 2005 hii match tunaangalia home ghafla wageni wanakuja kufanya kikao cha harusi ikabidi watu watokee nikabaki chini ya uvungu wa kochi naangalia game huku kikao kinaendelea watu wanataja mahari tu mimi nasikiliza chini huko , Rio anafunga goli linakataliwa niko chini ya uvungu natamani niruke ruke , mwisho kwenye matuta arsenal akabeba baada ya paul scholes kukosa japo game arsenal alikimbizwa mwanzo mwisho
 
Mechi ya madrid na barcelona santiago benabeu....aise dinho alipiga mpira hatari siku hiyo balaa tupu mpaka mashabiki wa madrid wakampigia makofi. Jamaa alikuwa nyoko.

Fa cup semi finl arsenal vs man utd ryan giggs anawachambua mabeki wa arsenal hatari mno.

Mnchester vs real madrid hatari redondo anapiga backheel matata anampita sijui alikuwa henningburg u huku delima anapiga magoli tuu. Beckhama nae akakiwasha.

Trezequet anafunga golden goal dhidi ya toldo fina ya uero 2000. Hatari.

Aisee mpira bwana bonge la burudani.
Heshima kwako mkongwe mwezangu.

Fernando Redondo alimpiga tobo Henning Berg afu akaenda kutoa assist safi kwa Raul. Redondo alikuwa fundi kweli na mguu wake wa dhahabu bahati mbaya majeraha yakaharibu kipaji chake!


Hiyo ya Ufaransa kutwaa taji la Euro 2000 kuna mechi kadhaa za kukumbukwa. Nakumbuka robo fainali walikutana Ufaransa na Ureno nadhani, dakika za lala salama Ufaransa wakapata penati, Zizou akawa anaenda kupiga, Luis Figo akavua jezi na kutoka nje kabla hata Zidane hajaweka mpira kambani na akafunga kweli mechi ikaisha kwa goli la dhahabu.

Figo alivyokuja kuulizwa baadae akasema hakutarajia Zidane kama angekosa hivyo akaona atoke zake mapema😂😂

Wachambuzi wengi wa soka, wanadai michuano ya Uefa Euro 2000 iliyofanyika Ubelgiji na Uholanzi kwa pamoja ni moja kati ya michuano bora kabisa kuwahi kufanyika🫡🫡
 
Coner taken quickly, Origiiiiii

Liverpool 4-0 Barcelona.

Comeback nzito kabisa.
Hii kwangu ndio the best nakumbuka hadi matukio yaliyofanyika banda umiza siku hiyo

Pia kulikuwa na dogo muokota mipira aliyemsaidia Alexander Arnold kuonesha pasi aitupie kwa Origi.

Huyu dogo nimeingia kucheki jina lake nimekuta na taarifa zake ambazo sikuzijua.

1684958457622.png


Dogo anaitwa Oakley Cannonier kumbe alipewa hadi na mkataba kusainiwa na Club kwa kitendo kile cha kuisaidia timu.
 
Sitasahau ile siku Barca amekandamizwa 4-0 pale Anfield kwenye usiku wa UEFA mwaka 2019. Ile ni come-back yangu bora ya muda wote ikifuatiwa na Ile fainali Uefa final match ya AC Milan vs Liverpool 2005.

Sitasahau man city amegongwa mbili na Aston villa afu akashinda tatu sisi liva tulikua tunaombea agongwe tuchukue ligi
 
Back
Top Bottom