Timu zote zina point 86, huku City akiwa na tofauti ya Mabao 63 Man United akiwa na GD ya 55.
City akikipiga na QPR, Man United akigongana na Sunderland.
United alimaliza kwa ushindi wa goli moja, bao la Waza hivyo kufanya kuwa na point 89. City kang'ang'aniwa na QPR, mpaka dakika ya 90, City 1-2 QPR.
Kumbuka hii mechi ni muhimu kwa timu zote mbili. City anapaswa kushinda ili achukue ubingwa na QPR ashinde ili asishuke Daraja.
Sisi Mashabiki wa Manchester United, tupo tunashangalia kombe letu. Mechi imeshaisha tayari.
Zikaongezwa dakika 5 kufidia dakika zilizopotea. Asalaleeeh, dakika ya 92, Dzeko anasawazisha ubao. Sasa ni 2-2.
Bado matumaini kwetu ni makubwa mno. Droo hiyo isingesaidia. Ubingwa ni wetu sisi.
Dakika ya 93, La haula!. Aguero anafunga goli na kufanya kuwa 3-2.
Nilihuzunika mno. Hakika nilipata huzuni iliyo kuu. Mpaka na leo sitosahau. City anatawazwa kuwa bingwa kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo QPR aliponea kushuka baada ya Bolton kutoka sare.
Mungu naomba hili jambo lifutike kwenye kumbukumbu zangu.