Tukio gani la football liliwahi kukutoa machozi

Simba alipofungwa na stella abdijan bolizozo yule jamaa
 
Daah ile ya asamoa ili niuma mno na ndo mech ya mwsho kucheck kwenye world cup 2010
 
Ila 5 bila ya Simba na Yanga,nililia kwa furaha.OKW ni mtu hatari sana.ningekuwa na hela asingeondoka unyamani
 
Goli la Tambwe la mkono, basi mzee washabiki wakaanza kurusha viti uwanjani, sindio wapenda sifa wakarusha mabomu ya machozi jukwaani, dah machozi yalinitoka bila kupenda, na network ikapotea kabisa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nimecheka sana[emoji23]
 
Kuanguka then kufa uwanjani kwa Marc Vivian Foe
Bingwa wa dimba la chini aliye kuwa anaenda sajiliwa Man United
Wanacheza na Colombia ktk kombe la Federation akaanguka akatolewa uwanjani
Baadae FIFA ikatangza Foe kafariki dunia
Mm nilikuwa namkubali sana huyu mtu
Kiasi kwamba jezi yake ninayo hadi leo
 
Unaikumbuka hii?


 
SIMBA vs ENYIMBA..hadi leo nilishapunguza ushabiki wa mipira ya Bongo,
 
Comment za wengi humu hakika hawakulia zaidi ya kusikitika kimpira tu same pain when you loose big match
 
Nilihuzunishwa sana na matukio yafuatayo katika soka.
  1. Siku United alipofungwa 6-1 na Man City 2011.
  2. Siku ambayo Aguero alipiga goli la tatu dakika ya 92 lililowapa Man City ubingwa wa EPL 2012.
  3. Siku ambayo Sir Alex Ferguson alistaafu kufundisha soka.
  4. Siku ambayo Tanzania ilifungwa na Msumbiji katika mechi ya ku-qualify AFCON 2009.
  5. Msimu uliopita wa VPL ambapo Simba alipigwa nje ndani na Yanga goli mbili kwa kila mchezo.
  6. Siku ambayo United ilipigwa 5-3 na Leicester ambayo ndo kwanza imepanda daraja 2014.
  7. Siku ambayo Suarez alidaka mpira na kuinyima Ghana nafasi ya kupata goli la kuweza kutinga nusu fainali ya kombe la dunia 2010.
 
Ilikuwa 1994 kweli. Yanga alikufa 4-1 Wakati huo George Masatu na Malota Soma aka Ball Juggler walikiwasha balaa. Nilifurahi sana siku hiyo.
 
Didier Drogba alipofunga penalty ya ushindi UEFA final pale Allianz Arena na kutufanya Chelsea kubeba ndoo ya UEFA for the first time in football life. Nilitoa machozi ya furaha siku hiyo.
Kilichonifanya kutoa machozi, kwanza ni kuona mwafrika mwenzetu kaisimamisha Dunia na kuwaonyesha wazungu kua wao si lolote, pili team yetu imepitia uonevu na manyanyaso makubwa kila inapocheza michuano hii. Ile siku haitasahaulika ktk maisha yangu ya kushabikia soka.

DD11
 
Cku ile arsenal anafungwa na man u 8-0.,.cku ile ctaisahau ilinifanya nipoteza hobby ya mpira kabisa Kwa msimu ule...COYG
 
Atletico Madrid vs Real Madrid finali Uefa champions league 2014, Atletico anakufa 4-1 dakika za kulala
 
Senegal Vs Uturuki, Senegal anakufa kwa goli la dhahabu, Uefa Barca vs Chelsea, Chelsea anamtoa Barca na anaenda kuchukua ndoo, Brazil kupigwa 7 na Germany WC 2014, Kifo cha Marc Vivien Foe.....
 
Atletico Madrid vs Real Madrid finali Uefa champions league 2014, Atletico anakufa 4-1 dakika za kulala
Umenikumbusha fainali ya UCL 2016 iliyowakutanisha tena, Atletico akafa kwa matuta 5-3 baada ya kutoka 1-1 dakika 120
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…