Tukio gani ulishawahi kufanya ukahakikisha umemfundisha mtu adabu?

Mungu anisamehe... kuna X alinitenda vbya sana enzi hizo, tumegraduate wote, yeye akawahi kupata mishe, mm bado nasota kitaa... dharau kibao akapata mchizi huko job akampa na mimba akamzalisha... mahusiano yakafa, akazaa nami nikaja kupata mishe......

jamaa alomzalisha akamuacha ... akabaki single mama.... kuna mdogo wake nilipambana nikala, nikahakikisha dada mtu lazima ajue... na akajua alilia na kuumia sana .... hiyo revenge hatokuja kuisahau
 
Unasoma Charambe, unakaa Mbagala Kuu. Mnazi mmoja imefata nini kwenye huu mjadala.
 
Inawezekana siku moja mtakutana na atakuambia ni kwanini alikukimbia, pole sana!
 
😅 😅 aiseeh, sasa konda akikuta hayo matukio yenu, siku nyingine si ndiyo anawagomea kabisa kupanda gari zake?
 
Id inasadifu yaliyomo 2pac shakur🔥
 
Hizo 1 na 2 ni hatari, inahitaji uwe na roho ngumu.
Haya nimekaa kitako nasubiri 3 mpaka 5.
 
Hivi juzi juzi kuna mzee alikua mume wa maza (sio baba yangu mzazi) mizinguo sana, bi mkubwa kila siku analalamika kuhusu yeye. Nilimkuta home kwa bi mkubwa nikampiga bonge la beat mixer kumwambia nisimuone tena pale home, kama anampenda mkewe kweli amhamishe pale kwenye nyumba yetu (kitu ambacho najua alikua uwezo hana). Katika beat langu nikamwambia hapa kwetu uhame, nyumba unayo kakae kwako, usije ukatufia hapa tupewe kesi. Na usipohama nitawapigia simu ndugu zako ntawaambia waje kuchukua mzigo wao.

Kuna mzee mwenzie ambaye tunaelewana akanipigia simu akaniomba nimsamehe yule mzee, nikagoma nikamwambia huyo mpaka ahame kabisa hapo na nisimuone tena akija. Nikaongeza kabla ya kifo chake atakuwa amehema hapo iwe mvua iwe jua, atanijua mimi ni nani.

Akahama. Mwezi mmoja mbele akafariki. Ameenda hospitali siku 3 tu kavuta.

Aisee! Bi mkubwa ananiuliza we umemfanya nini mzee wa watu?
Hata yule mzee aliyeniomba nimsamehe alinipigia akaniambia dah kijana ndio maana tunatakiwa tuwe waangalifu na kauli zetu.....uliniambia kabla hajafa atahama na imekuwa vile vile.

Lakini mimi sijafanya chochote zaidi ya maneno makali ya kusisitiza kweli kweli na akakimbia. Mimi nna ndugu zangu wengine 2 wote wanaume huyo mzee alikua anatuogopa balaa.

Nyumba yetu tumekupa hifadhi unatusumbulia bi mkubwa wetu, why? Kwanza bi mkubwa keshazeeka haitaji hata huyo mume......kwenda huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…