ahahahaha me perfume nilikua hata sijui majina yake nilivoanza kupuliza napuliza mpaka kwenye viatu mpaka mdomoni alooh [emoji1787]
MIaka hiyo kulikuwa na sista mpangaji wetu alikuwa mfamasia akapata kazi JD Pharmacy.
Sasa kule JD pharmacy walikuwa wanauza na unyunyu wakishua. Ila hua wakileta mzigo mpya kuna perfume za sample kwa ajili ya kutest watu wamezipokeaje?
Nilivyomaliza chuo siku ya graduu, akamwomba dogo kuwa anitafutie nguo chakavu zangu kama mbili amabzo sizivai,
Akapewa akachukua box zuri sana.kafunga zile nguo pamoja na ile perfume za sample wanazopewaga JD PHARMACY.
Mwamba wakati wa kufungua zawadi nafungua nylons nakuta nguo zangu nkaona maajabu kwenda kucheki room hazipo kuangaliaa vizuri nkakuta unyunyu na msg yake ya pongezi,
sasa mtoto wa mbwa na unyunyu wapi na wapi?
Basi ule unyunyu nkawa napulizia hovyo hocyo, ila ukipuliza aisee ulikuwa ni balaa. Sasa demu wangu kaja geto kasema unyunyu wako mzuri nkampa.
Yeye akaanza kuutumia, kistarabu sasa siku moja kaenda kwenye sherehe, nduguze wacha wamsifie wacha wampe compliment unanukia balaa umenunua wapi? Jibu ni moja tu kanipa mpenzi wangu.. mwambie atuelekeze,
Sasa siku kaja kunipa zile habari na kuulizia nimenunua wapi, nkasema nilipewa zawadi na mpangaji wetu,. Akaomba nikaulizie bei maana mama yake mkubwa ameupenda,
Mimi nkanyoosha komwe kama nyundo inaenda kugonga msumari kwa mpangaji, kuwa ule unyunyu nimeupenda umenunua wapi? JIBU LAKE ALIKAA KIMYA AKASEMA MIMI NINAO KAMA WAKO SIJAFIKISHA HATA ROBO TATU, NI GHARAMA SANA ULE SIDHANI KAMA UTAWEZA BEI, UPO OFISINI PALE ZIPO PC 3 TU ZILKKUJA 5. Nkamjibu kesho naenda kuchukua niwahi kabla haujaisha. Akasema sawa..
Huyoo kesho yake na komwe kama masai na fimbo yake, nkaenda JD YA MLIMANI PALE, NIMEBEBA SAMPLE YA KOPO,.
weka sample mezani, ni habari yako boss naomba hii pc 1,
Nakumbuka muhindi alinyanyuka akasema karibu ipo na zimekuja brand nzuri zaidi. Hii umeipata wapi? Nkakaa kimya, kwa lugha ya kuogofya nikikjmbuka maneno ya sijui kama utaiwsza bei..
Nkauuliza bei ngapi?
Akanijbu lak 6 ila naweza nkakupunguzia ukichukua mbili... moyo ukalia paaa! Ukamalizia ondoka hapa chap kabla cjaamua kusimama mazima,... jasho jembamba linatoka nkasema kwa sauti ya upole.
Naenda kwenye atm ya crdb nakuja,
Nilichukua sample yangu nkampigia demu wangu nkamwambia kila nilipokuwa najipulizia nilikuwa nachez3a hela bwana hii ngoma 600k...
UShamba huu. Sikujua nimepewa vitu hadimu