Tukio gani uliwahi kufanya ukagundua kweli una stress?

Nikiwa chuo nilikuwa naibu waziri wa michezo,sasa kukawa na event na ikabidi niwe kwenye msafara wa kwenda kutafuta sponsors zunguka sana maofisi ya wadau.Nilivyomaliza nikapita atm kuvuta hela kidogo kwa ajili ya matumizi nimetoa hela atm nikajikuta nimesema asante sitasahahu ile siku that was 2007.
 
kuna mtu niliwahi kumshuhudia anatafuta kitu ambacho amekishika mkononi.
Hiyo mimi juzi,,natoka room naongea na simu,nashuka kwenye ngazi najichek kwenye koti simu haipo,kumbuka bado naongea na simu,naingia room natafuta sioni,,mara pap nakumbuka si ndio hii hapa naongea na mtu,,huyo nikatasamu huku maongezi yanaendelea
 
Stress zisikie tu! Sema acc ikituna unarelax sana
Pale ambapo unakuwa umetoka kutapeliwa kwa maneno mkuu,

Inakua kama utani yaaani ni kama ndoto stress zinakupata dadek unakuwa huelew kabisa ndo apo unamkuta mtu njian unamsalimia za jioni na wakati ni asubuhi
 
Ukilewa Usichati....
 
Mkuu ile ya kuongea huku ubongo wako unakudadisi the way unaongea kama ni sahihi ni lazima uchapie tu aiseee

Kuna mzee nilijikuta badala ya kumsalimia shikamoo nikasema ahsante kwa chakula!!!!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ahahaha nimecheka sasa
 
Hiyo mimi juzi,,natoka room naongea na simu,nashuka kwenye ngazi najichek kwenye koti simu haipo,kumbuka bado naongea na simu,naingia room natafuta sioni,,mara pap nakumbuka si ndio hii hapa naongea na mtu,,huyo nikatasamu huku maongezi yanaendelea
Aisee sio poa mkuu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
mkuu tupe kisa chako kimoja apo
Kuna siku nimeingia tanzania kutokea dubai nilikuwa na matairi ya gari ndogo 4 na tv kubwa, wakati nashuka kwenye ndege nilianza kumuomba Mungu kwa dua ili nisisumbuliwe na TRA.
Cha ajabu nikajikuta naomba msaada wa kupita bila kukaguliwa kwa afisa ambaye nae ni miongoni mwa hao wakaguzi..

Alinionea huruma tu sijui maana nilifanikisha
Kisa kingine

Kipindi hiko nilikua nina kiwanja huko Bagamoyo nikahitaji kujenga nyumba yangu ili nitoke kwenye nyumba za kupanga

Hapo niliikuwa na bajeti ya Milioni 20 tu, nikajikuta namuomba ushauri mwanangu wa darasa la pili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…