Nilitaka niposti kwenye jukwaa la michezo ila kwa hili lililotokea lina kipaumbele cha amani tuliyonayo kutiwa doa kuzidi sheria za mpira,
Kuna timu kutokea Kigoma inaitwa Mashujaa, leo walikuwa wanacheza mechi yao ya mwisho dhidi ya Mbeya City kufuzu kuingia rasmi kwenye ligi kuu, Mechi imechezwa uwanja wa Sokoine Mbeya.
Timu ya mashujaa ilipofunga goli wakati wakiwa wanashangilia wakapita sehemu ya wapinzani wao kushangilia kwa kuwatambia na ni kawaida tumeshazoea, ila ghafla bin vu! kocha wa makipa wa mashujaa akampiga ngumi nzito ya usoni kocha mkuu wa Mbeya city, Jambo hili lilipelekea kocha wa Mbeya city kutoweza kuinuka kwa dakika kadhaa huku akiwa anapewa huduma ya kwanza.
yule kocha wa makipa wa mashujaa kapewa kadi nyekundu tu.
Adhabu ya uwanjani kashapewa ni vema sasa na vyombo vya ulinzi na sheria viingilie kati.
Mapendekezo.
Nchi yetu ni ya amani, vitendo hivi visipewe mwanya wa kuzoeleka, hatua hizi zichukuliwe iwe fundisho wengine wasije kuthubutu.
TFF imfungie miaka mitano kutojihusisha na mpira
Asakwe na kukuwekwa mahabusu
Acharazwe viboko 10
Amlipe faini mhanga.
Kifungo cha miezi 6 Jela
Michezo sio uhasama wala vurugu, Tabia kama hizi zisipewe nafasi ya kuchipuka.
Jamaa kafanya kitu cha kipuuzi sana aisee nimeshangaa mtu mzima kumpiga mtu ngumi vile sijui alifikiri nini yaani michezo imefika huko huyo mtu afungiwe asijihusishe na soka kafanya kitu cha hovyo kweli...
Suala hili lina kipaumbele cha amani kuliko mambo ya kimpira kushuka daraja, timu inaweza kushuka daraja na kupanda lakini mtu kushambuliwa hivi anaweza kupoteza maisha hakuna kufufuka ama kuwa kilema moja kwa moja na jicho lisiweze kuona tena.
Unahitaji elimu ya ziada kwenye sheria.
Kosa la jinai halina cha mpira wala rede.
Ingekuwa wanapigana tungeelewa lakini hii kavamia mtu