Mchimbaji maisha yake anatembea na sururu ndogo tu wanaita MOKO hivyo akiambiwa ahame au Kuna machimbo mapya yanatema dhahabu wala hana cha kubeba zaid ya sururu yake na kusepa, wengi wao hawajarudi nyumban kwao kwa miaka mingi sana maisha yao yamekua ni ya kuhama hama kwenda machimbo mapya sehem anaposikia dhahabu imetema.
Mchimbaji akipata hela huwa anaitumia kwa fujo kunywa pombe, kulala na wanawake tofautitofauti wanaojiuza maeneo ambayo yako pemben na machimbo ambapo huwa wanaanzisha mji wa dharura ambapo panapatikana kila kitu, gesti za mabati,bar za mabati zenye mziki mzito kama upo town kumbe uko porini , na migahawa kwaajili ya chakula maeneo wanapo pata huduma hizo ndo hayo wao wanaita MATANDA .
Ukikuta Hawa jamaa wanakula pesa zao we waache tu wale wanazipata kwa mateso makubwa sana, mfano... Kuna maeneo ya shinyanga watu walifunikwa na udongo wakiwa ndan ya mashimo walikaa siku 42 wakiwa ndan ya ardhi lakin baadhi wengi walifariki na walipona watatu tu baada ya kuchimba kwa siku 41 ndo wakapata maiti na watu wa3 waliokua kwenye Hali mbaya Sana, wao wanasema walikua wanakula mende na baadhi ya wadudu kwa muda huo wote, lakin baadhi ya story inasemekana ilifika hatua wakaanza kula nyama za wenzao waliokufa ili wasife, nafikiri habri ya watu kufukiwa shinyanga ipo hadi YouTube..
Story za machimbo ukiambiwa unaweza kudhani ni movie au unadanganywa ila watu wanapambana sana na maisha