Mida ilienda jamaa walirudi kutoka kuzichoma zile maiti na story zikaendelea mpaka asubuhi.
Chaajabu siku hiyo jua lilichelewa kutoka, tukicheki saa ni saa kumi na mbili asbuh (mida tuliyo panga tuanze kazi) lakini hakuna dalili ya kuchomoza jua yani ni kama wingu la alfajir, ila kwa porini kunakua kama kuna ukungu hivi.
Hali ile ya ukungu ilitamba kwa muda mrefu, mpaka mida ya saa 2 asubuhi bado hatujaenda kazini.
Ile hali kila mtu ilimshtua, yani ilikua kila tukitaka kwenda kuanza kazi lakini ile hali inatupa wasi wasi
Mala ghafla mvua ikaanza kunyesha, huwezi amini, mwezi wa nane, lakini mvua utadhani mwezi wa pili vile.
Mvua ilipiga mpaka basi, yani mpaka jioni halijatoka jua, ilikua inapungua tu, muda si mrefu inamwaga tena.
Nakumbuka mvua ilipo kua inapungua ndio muda tulio tumia kujisaidia, yani ikipungua tu utasikia "mwenye gogo akakate ".
Mvua ile tulishinda nayo, tuka kesha nayo mpaka asubuhi.
Mvua haikukata mpaka ikaanza kutujambisha.
Siku ya tatu mvu inakamua tu, kumbuka tuna kalibia kumaliza week polini, lakini hakuna alievuta bange, sigara wala pombe.
Hivyo hali zetu zikaanza kuwa mbaya kutokana na alosto, ukizingatia baridi lake, sio poa.
Nathubutu sema sijawahi kuona mvua iliyo dumu kwa muda mwingi kama hii.
Nakumbuka kuna jamaa aliungua mkono kwa kuukumbatia moto kutokana na baridi.
Siku kama ya tano hivi, ubongo ukanisogea, akili ina niambia nimtoroke mrundi na ile dhahabu, tatizo mvua inayo piga ni kubwa, yani hata mbele uoni.
Tushukuru wengi tulikua na simu wengine saa hiyo ilitusaidia kujua muda, vinginevyo tusingekua tunajua kua huu ni usiku ama mchana?
Tukaanza mashauriano ya kurudi nyumbani, maana hali ishakua sio poa.
Hakuna mwenye uthubutu wakwenda kuchukua sururu na kwenda kuanzisha sonda.
Mashauriano yalidumu siku mzima, kuna watu tunaka turudi (mimi mmoja wapo) na kuna wengine wana fosi tubaki.
Tunao taka turudi tuko wachache, wengi wanataka tubaki, na yule mrundi nae anataka tubaki.
Lakini kati ya tunaodai turudi kuna wengine hata dhahabu hawana, hivyo wengine ilikua wako mguu ndani mguu nje.
Watu wanajiuliza tukirudi na mvua ikaishia na wenzetu wakafanya kazi wakarudi na dhahabu itakuaje?
Pale watu kama saba nane hivi niliona wako serious, na safari ya kurudi kijijini.
Mvua inaendelea kupiga, chaajabu hakuna radi wala umeta, yani ni mwendo wa kulowesha tu.
Akili ikaniambia, mimi ni mwanamme, nime zaliwa siku moja nitakufa siku moja, kufa kulala kaburi tuta.
Nilijipa moyo, kama liwalo na liwe, ila lazima nitoroke na ile dhahabu, kwanza mshikaji anazingua, namuambia tuondoke, yeye ananiambia tukomae, ukizingatia tumejuana kule kule polini.
Mimi na yule mrundi tunaishi camp moja kati ya zile mbili tulizo zijenga hapa karibuni.
Moto mkubwa (porini mvua hata inyeshe vipi, lakini kuni zitawaka tu ) mbele yangu nimenyoosha mikono kuota, huku mawazo yakinirudisha nyumbani, kitambo sijarudi home (Tanzania) muda mrefu sijamuona mkewangu na watoto wangu (hawa wanaishi Nampula).
Moyoni najua kua nilicho nacho (dhahabu) ni cha thamani, uchawi kutoka hapa nilipo tu, nikiingia mjini mimi ni mzungu.
Hapo sijui ni uzito gani, lkn nilisha kadiria kua pesa ya kutamba kwa mama Abuu ninayo.
Nilicheki kisimu changu cha tochi nikagundua ni saa 8 usiku, nikaona huu ni usiku sana, ila ikifika saa 10 alfajir nitoroke.
Kichwani nilijua kua lile kundi lililo apa kuondoka asbuh lazima litanikuta mbele nawasubiri.
Saa kumi alfajir, camp mzima ime lala, mvua kubwa nje inapiga, nikaona hapa sasa mchizi boti wacha nipotelee kizani.
Nikachukua moko yangu (moko ni kifaa cha kazi) tochi yangu, kama naenda kukojoa vile, mbele.
Nitarudi muda si mrefu.