Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Kwahiyo mkuu ukapiga kama million 11 ... Je vipi mkuu unamawazo ya siku 1 kuja kuachana na kazi ya uchimbaji kufanya biashara zingine au haujafikiria kuhusu hilo
 
Ahsante mponcha.
Ushawahi kuingia ndani ya fonka?
Mule ni kama umeshajizika tayari.
Usiku wa leo nitakua humo.
 
Mkuu nairoto sikuwahi kurudi tena.
Mshikaji wa kimalawi tulikutana miaka miwili mbele, Mwaja.
Hakunifanya kitu kwasababu Pele Mwaja mimi nilikua na kundi la wauni walio kua wanasumbua pale.
Nilimuahidi kumlipa (kuepusha zogo) lakini sikuwahi kumlipa, na mpaka leo sijui yuko wapi.

Kuhusu wale jamaa, sijui kilicho endelea nyuma, ila mpaka leo Nairoto watu wanachimba, lakini dhahabu hazitoki kama zamani.
 
Hii lugha gani [emoji3][emoji3]
Hiyo ni lugha ya kichimbaji hiyo
Maloja-kujisaidia porin
Kuhila - kupata madini
Duarani - shimo
Moko - sururu
Matufe - udongo unao meguka kwenye kuta za shimo na unaweza kukujeruhi vibaya au kukuuwa kabisa ukikukuta huko chini

Nmepata bahat ya kukaa na wachimbaji sehem tofaut ila naona lugha yao ni moja labda kwakua wanahamahama na wanakutana
 
Sio kwamba baba mkubwa anachimba kisirisiri?
 
huna hata haya kusimulia kutoroka jeshi jinga wewe. kwa hiyo hapo umeridhika kula ugali wa shikamoo mama
ndio nyie tunawaimbaga kwenye chenja mananga wakubwa
Watt wa kishua hao matifu ya kijesh hawayawezi wameshazoea kudekezwa na dady na mamy hata ukimpiga na ukubwa wake wanaenda kukusemea kwa mummyyy
 
Matufe yamenitisha
 
Mkuu Cabo del Gado ni kubwa, ina wilaya 16.
Akina Ali mbabe wanazingua kuanzia wilaya ya Mocimbua, Muedumbe, kisanga na Makumia.

Mimi naenda wilaya ya Montepuez, hii iko mbali kidogo na huko.
Alafu huku mimi ndio huwa nakaa sana, nikitoka ni kwaajili ya mlio.

Hapa Mwatizi ilinileta dhahabu ya Ngorongoza, lakini naona ni pagumu, wacha nikatafute Ruby kwanza.

Kuhusu kudhaniwa ali mbabe, hilo kweli lina tokea, tena Watanzania kibao wako jela za huku kwa kudhaniwa ali mbambe.

Yupo mshikaji wa Dodoma, alisota miaka miwili jela, katoka mwaka jana, nasikia ndugu zake walikuja kumfatilia.

Hilo jimbo si ndo Alshabab wamelitwaa? Utayaweza mazingira ya mchakamchaka na milio ya risasi mara kwa mara?
Angalia tu usije ukahisiwa wewe ni miongoni mwao wakakumaliza askari wa Msumbiji
 
Umesahau fonka-shimo linalochimbwa ndani linaelekea pembeni horizontally kama mwanandani wa pembeni.Hii linatinduliwa kwa poncho na mtindo imara
 
Mkuu hii ni dunia nyingine.
Mara kibao nimejaribu kufanya hivyo lakini nashindwa.
Nikikaa home mwezi tu, nayamiss haya maisha.
Kuna kipindi najiuliza (hasa nikiwa kwenye hali mbaya) hivi nimezaliwa kuishi maporini?
Maana mifano naiona, wapo wazee tunachimba nao.

Mzee anakuhadithia machimbo miaka ya 1980 huko, yani hata sijazaliwa.

Kuna mzee alifuatwa na mwanae arudi home (mwanae ni mkubwa na ana pesa) mzee alikataa kata kata, mpaka yule mtoto akawaomba wazee wenzie (nao ni wachimbaji) wamshauri mzee akubali kurudi home, na mpaka sasa mzee tunae Migodini, sijui yuko poli gani.
Kwa nilivyokusoma naona umeshapata migao mingi sana pesa tena pesa kubwakubwa kwanini usirudi Tz ubadili maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…