Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Mama na mzee wakasema ameota huyu rudini mkalale. Baada ya kukazimishwa na kuingia room tukapanda kitandani yaani nilikuwa mpaka nausikia moyo wa mdogo wangu ulivyokuwa ukimdunda huku akitetemeka nami nikajawa na hofu kuwa hapa Kuna kitu na si ndoto kama wazazi walivyosema. Dakika kumi nyingi, nikashangaa gafra mdogo wangu kaniruka kuja mwisho wa kitanda ukutani. Ile kuangalia tunapopandia kwenye kitanda kwa macho yangu tena kukiwa na giza nikamwona mtu amevaa kanzu nyeupe akiwa na mandevu kibao akifunua neti like naye apande kitandani...
Aisee kelele nilizopiga hazikuwa na mfano
hakuwa na mafuta ya mgando au sabuni mkononi?
 
Mkuu hapo mulimpa ulaji huyo muhindi.
Hapo mulikua munauza Pete kama yenyewe, na kidani munge kiuza chenyewe.

Tena hapo, kati ya Pete (dhahabu) na kidani chekundu (Ruby) hicho kidani ndio chenye thamani.

Hicho kidani kikifika points 4 tu ni zaidi ya Milioni moja.
Na jini je?, linauzwa bei gani?
 
Hahaaaaaaa kmmk
Baada ya laana kukithiri polini, Mwenye (chifu) akawatangazia wanakijiji wenzie wawakataze vijana wao wasiingie polini.

Kwakua watu tulikua wengi hakuna alie jua kua wenye kijiji wametususia poli.

Laana iliendelea mpaka ulipo lipuka ule ugonjwa.

****************************************************************************************

Baada ya story hiyo kutapakaa karibu kwa kila mchimbaji, mala majadiliano yalianza.

Kwanza tulijiuliza kama ule ugonjwa ni kweli kipindu pindu mbona tulivyo fika kijijini pale na ugonjwa ulikoma?

Kulikua kuna watu walikua wanaeza habari za mzungu kutia sumu kwenye maji tuliyo kua tunatumia kwenye shughuli zetu mbali mbali.

Lakini swali likaja, kama nikweli sumu, mbona wanaokufa ni wanaume tu? ( na nikweli, kwenye kisanga hichi hakuna mwanamke alie kufa)

Tena ukizingatia walikua wanakufa wengi ni wanunua dhahabu, wafanya biashara wengine, na wanaozunguka na vingwendu.

Kumbuka watu hao wote, machimboni hunywa maji ya dukani.

Jibu likaja kua kuna masharti yamevunjwa.

Watu wakatiana moyo wa kwenda tena polini.
Ikapangwa siku, mwenye kutaka kwenda polini aungane twende.

Nikajifikilia, na mimi nikajipa ujasili wa kuungana na kikundi kitacho rudi tena polini.

Kilicho ni shawishi kikubwa niliamini kuna watu wengi walikua wamekufa na dhahabu mfukoni, hivyo niliamini lazima nirudi na dhahabu.
Pili nilikua nashauku ya kujua kama Wamisunjo alifia pale ama alitoboa mpaka kijijini?

Kulipo kucha safari ilianza.
Safari ilikua ya mtu kama 20+ hivi.

Ila kabla ya safari tulikubaliana hakuna mtu kubeba bange, sigara wala pombe.

Safari ilianza rasmi ya kuelekea polini, njiani tunapishana na maiti, upigi hatua kumi bila kukutana na maiti.

Asikuambie mtu binaadam akifa ananuka balaaa.

Yani ilikua ni mwendo wa kushikapua mpaka unataka kutapika.

Tulitembea mpaka pale tulipo muacha Wamisunjo, nikamkuta jamaa wamemjalia nzi tu, yani hata kumkalibia nilishindwa kwa huzuni.

Safari iliendelea mpaka tunafika matandani.

Tulipo fika matandani, maiti zenyewe hizo! Kama kwenye movies vile.
Kila upande zime jazana maiti tu, kuna harufu mbaya, kama huna moyo wa ujasili lazima utapike.

Tulizunguka polini pale lakini tulishindwa kufanya kazi kutokana na hali halisi.

Tukajadiliana kwamba watu kumi wafuate petrol watu wengine tubaki tukizisomba maiti na kuzi weka sehem moja kisha tuzitie moto.

Kwa wingi wa maiti zile na kuharibika vile ilikua ngumu kuzizika, hivyo wazo wa kuzichoma moto lilikua wazo zuri.

Tukatafuta sehem mbali kidogo na matandani, tukalala.

Hapo uliwashwa moto mkubwa, hapo ni story za kupeana moyo tu husu maisha, kila mtu anaongea lake mpaka asubuhi.

Kulipo kucha wale kumi walielekea kijijini kufuata petrol, na sisi wengine tukaanza kuzisogeza maiti sehem moja (zile zilezo kalibiana.

Mfano fungu moja unakuta maiti tano, fungu lingine watatu kutokana na ukaribu walipo fia.

Nakumbuka mimi na brother mmoja (huyu ni mmalawi) tuliingia ndani ya duka moja hivi, tukamkuta mwenye duka kafa kwenye kiti chake kaa tu.

Tulipekua duka lote (japo kunanuka)mara ya kwanza tuliambulia pesa tu, jamaa nilie nae akania huyu maiti alikua ananunua dhahabu pia hivyo tuwe makini katika kusachi kwetu tusije pishana na dhahabu.

Harakati za kumsachi mfukoni, tukamvua viatu, wapi?
Tukamvua nguo zote (kwa tahadhari ya hali ya juu) hapa tukamkuta na donge la dhahabu kwenye kipochi kidogo cha shingoni, ila marehem alikua kakivaa kiunoni.

Uwezi amini huyu marehem alikufa na biashara yake ikiwa imejaa.

Nakumbuka tulibeba Dragon baadhi ya kasha na kwenda kunywa mbele (hapa tuliapa hakuna mtu kugusa pombe )

Siku ilisha tukizikusanya maiti tu na kuzisachi, mwenye bahati ya kukutana na dhahabu ni ya kwake.

Tulipo gundua kua maiti nyingi zimekufa na dhahabu mikoni, kazi ya kuzikusanya haikua ngumu tena, wala kile kinyaa kikapotea.

Tukaanza kuzigombania maiti kila mtu anataka kusachi, mwisho wa siku tukaingiwa na kama wazimu hivi.

Nakumbuka kuna jamaa walizichapa (nusura wauwane ) wakiigombania maiti moja hivi.
Kuna mmoja kati yao anadai anamfaham malehemu, hivyo yeye ndie mwenye haki ya kuchua dhahabu ya marehem......

Narudi muda si mrefu.
 
Hahaaaa
Haya machimbo ya kuibuka tu wanayaita RUSH..

Yani mzigo ukisoma ndani ya masaa mawili huezi amini kama lilikua pori utakuta Gest, baa, malaya washatimba, mama ntilie, soko, maduka na kila kitu....

Na ndani ya masaa kadhaa pia unaweza kupakuta peupe likiibuka chimbo jipya linalotema.... Watu wa GEITA wanayajua haya mazingira na rush ikidumu miaka minne vijiji vya pembeni kutakua nawatoto wengi balaaaaaa na hawana baba na hawa hua hawaendi shule....
 
huo muda niliousema mkuu ni pale tu jua linapomalizika kuzama mpaka giza rasmi liingie ndo kipindi kimepita....lakini issue ya kufunika vyombo iko wazi maana maradhi yanateremka usiku inashauriwa kufunika vyombo.....kwa case ya kuzuia dawa za usingizi weka chombo specific kwaajili hiyo..
Mkuu fafanua vizuri hili swala...maji na huo muda wa jua kuzama mpaka giza...enhee
 
Back
Top Bottom