Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Zamani sana pale jirani na kwa bamkubwa Chamwino kuna kakijiji kanaitwa nzuguni,kuliibuka Chimbo dhahabu inatema mi dogo tu wa 12-14,
nilikua najichanganya sana na maanko wangu alafu walikua watu wa vagi na ubwiii ile mbaya,
sasa walinipenda kwasababu mlinzi wao huko wakipakaza,likianzishwa nzegembe mi nachukua wallet na mali zote zinazohamishika kisha nayeya home.
Machimbo yalipoanza Nzuguni tulienda hawakuniacha bodyguard wao.
Duh kufika kule nilichoka jamaa anachosimulia ni kweli kabisa.
uzinzi,pombe,bangi, kila aina ya uasi unaukuta .ushangae sasa machimbo hata mwezi hayana.
sisi tulikua na kagroup ketu mtu nne wote mayanki tu na tulikua tunachakata vumbi tu lile.
siku kadhaa tukapatapata vimawe viduuchu yani kwenda kuuza tukagawana kahela kadogodogo tu.
Ila mi niliridhika nikasepa nikawaacha maanko maana wao hata ndoto ya kurudi hawana ilikua km wamefika nyumbani,sio hata wachimbaji wao ilikua ni pary pary tu.bangi pombe mabibi na daily wana hela wale jamaa aisee
Ila walikua mafundi malori wazuri sana KAUDO pale na Madereva.
Ule mgodi ulikatika ghafla tu,upo hapo Chamwino pembeni kushoto ukiwa unaenda kwa baba mkubwa.
 
It looks like I should do it ila wacha niendelee hapa hapa kwenye uzi wa mkuu wa mweku mweku ili tusipoteze radha ya maswala yahusuyo dhahabu kwa upana wake.
Sawa basi malizia hapa,

Ila siku ukiwa na muda uanzishe uzi kabisa ili uelezee matukio yote kwa urefu bila kufupisha...

Natumai utaimaliza leo mapema sana hata hivyo mzee wa mweku mweku hana dalili ya kutokea hapa leo, maana mpaka sasa hajaonekana japo kutusalimu tu
 
Mchezo uliishia wapi?
Basi nikazigawanya zile hela mule mule dukani, nikampa dogo laki mbili zingine nikabaki nazo Mimi. Nikamwambia we pita njia yako nami njia yangu hata Kama tunafuatiliwa tusipokonywe yote na usinunue chochote nikukute home. Baada ya makubaliano mi nikashika njia yangu na dogo nae yake, nikaenda duka flani kununua carpet ya manyoya, nikanunua na subwoofer na vitu vingine vidogo dogo vya kupendezesha chumba na nikabakiwa na chenji kazaa nikarudi home.
Usiku tumelala dogo akashtuka kelele mtindo mmoja huku akining'ang'ania mimi, tukakimbia mpaka sebureni. Nyumba nzima watu wakaamka, nami nimejawa na hofu tele huku sijui nini kimempata dogo. Akawa anaulizwa anaweweseka huku akisema kuna mwarabu mzee amekuja akakaa kitandani anataka.....hasemi anaogopa.
Alikua anataka .... Tigo ?
 
Mama na mzee wakasema ameota huyu rudini mkalale. Baada ya kukazimishwa na kuingia room tukapanda kitandani yaani nilikuwa mpaka nausikia moyo wa mdogo wangu ulivyokuwa ukimdunda huku akitetemeka nami nikajawa na hofu kuwa hapa Kuna kitu na si ndoto kama wazazi walivyosema. Dakika kumi nyingi, nikashangaa gafra mdogo wangu kaniruka kuja mwisho wa kitanda ukutani. Ile kuangalia tunapopandia kwenye kitanda kwa macho yangu tena kukiwa na giza nikamwona mtu amevaa kanzu nyeupe akiwa na mandevu kibao akifunua neti like naye apande kitandani...
Aisee kelele nilizopiga hazikuwa na mfano
hahahaahahahahahahahaah nimecheka karibu nikate moto aisee..
 
Pole sana,ila Mungu ni mwema ulivuka
Ni kweli mkuu, hii ishu baadae ilinipelekea niokoke na kumjua Mungu ipasavyo, kutokana na maswahibu ya PETE YA DHAHABU. Naichukia dhahabu mpaka leo, na hata nikioa sitataka kuvaa pete ya ndoa ya dhahabu coz it will be reflecting what I went through by that gold ring.
 
Alikua anataka .... Tigo ?
We jamaa nadhani you're still narrow minded person. Wenzako tunasimulia ishu ambazo zimetusumbua kipindi fulani maishani ili mjifunze we unaleta kilichoujaza moyo wako! Kwani sijasema huko juu yule mzee mwenye ndevu (jini alikuwa anataka nini?)
Umejawa na mawazo potofu, mawazo maovu. Omba Mungu ayabadirishe mawazo yako, jikite kwenye kusoma positive issues something that will help you to be positive minded person na sio kuwa wicked as how you're right now.
 
Sawa basi malizia hapa,

Ila siku ukiwa na muda uanzishe uzi kabisa ili uelezee matukio yote kwa urefu bila kufupisha...

Natumai utaimaliza leo mapema sana hata hivyo mzee wa mweku mweku hana dalili ya kutokea hapa leo, maana mpaka sasa hajaonekana japo kutusalimu tu
Mechi ya Taifa Stars Vs Tunisia imenishika. Naimani tutamaliza, just keep waiting sweetheart
 
Back
Top Bottom