Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

nimerudi tena sasa baada ya kushiba sasa...


pale kibena hospital kumbe nililetwa na wanakijiji tu,kwamba imezoeleka wao wakisikia kelele toka kule msituni basi huwa wanajua lazima ni watu waliopotea pangoni sasa kuonekana kwao huwa kwa style hiyo,na baada ya hapo wengi huwa wanapata kichaa kiasi cha kushindwa kabisa elezea nini waliona kule pangoni...(mimi sikupata nitasema kwanini pia)

....nikiwa bado nauguza kidonda,hapo tayari wafanyakazi wenzangu na ndugu wameshafika,ndugu zangu ni wa njombe na wanajua habari kuhusu msitu,baada ya kuambiwa niliokotwa kule chap wakajua cha kufanya,walikuja na dawa kadhaa na MTAALAMU fulani tokea kijijini kuja kunitoa mkosi na laana zinazopatikana huko(hii huduma ndio aliikosa mangi kwa maelezo ya baadaye) ndio maana aliishia kuwa kichaa...baadae niliambiwa mambo ya mule hayapaswi simuliwa kwahiyo ukifanikiwa kutoka mzima ni aidha ufanyiwe UTAALAMU au uwe kichaa usiwe na kumbukumbu kabisa...

mguu uliendelea kutibiwa na na kuharibika kadri siku zinasonga na ule upele ukawa unazidi na nabadilika kuwa wa kijani mguu wote sasa...madaktari wakashauri unatakiwa kukatwa ili kuoza kusiendelee(hii issue ya matibabu siyo concern yangu haswa)...kwa kifupi ndio wakakata mguu ila with time nilifanikiwa kupata operesheni ya kipande bandia huwezi jua kabisa kuwa sina mguu.

nilikaa pale mwezi mzima ingawa siku za mwanzo zilikua ngumu,kumbukizi ya matukio haikua inakuja full yaani unakumbuka tu habari hadi kipindi fulani halafu hukumbuki nini kilifatia aidha unaishia kusinzia au kupata mawenge...wenge linakuja sababu ile sauti na mwanga vinakua vinaflash upya kichwani,yaani siku za mwanzo ilikua nikifika ile hatua ya mwanga na sauti ya jamaa kule chini kila kitu kinapotea hadi baadae sana ndio ikawa naweza kumbuka kila kitu na kusimulia kama hivi...

sasa turudi kuhusu wale jamaa zangu...hii habari ya jamaa kwakweli sijuagi nini kiliwapata kule,wale wawili wa chini ni mangi alifanikiwa kupata miili yao wengine haikuwahi patikana pamoja na kwamba zilifanyika mila kibao lakini wanachodai ni kwamba mtu akipotelea huko shimoni huwa ni sadaka kwa hiyo wanaita mizimu na hata msihangaike kutafuta ila ukitaka tu mabaki yake ndio kuna mahala wazee huwa wanaenda fata napo ni mifupa na hawaziki kikawaida inazikwa kimila ili kutosambaza wanachoita “tego”

mangi ndani ya ile wiki alifika hospitali na hata alikua na uwezo wa kuongea baada ya kuanza changanyikiwa na nilimuelewa mwanzoni ila kadri siku zinasonga akaacha hata kuwa anatimba kunipa gwala...natoka mimi keshakua chizi

kwa upande wake anasema alichoona kule chini ilikua ni ajabu(mangi alifanikiwa kupanda sababu anasema kwa bahati nzuri kamba yake yule jamaa wa juu alipata akili ya kuifunga kwenye mti kwa juu) kwa hiyo wakati yeye kapigwa mwanga na kuachia kamba bado mangi ilimshika sababu na yeye alikua kajifunga kiunoni akafanikiwa kupanda juu kwa kujivuta kwa ile kamba,anasema yeye alifanikiwa kutoka na pia aliokotwa na wanakijiji na ndio aliyewapa habari hadi ndugu zangu ndio kufanikiwa kunifanyizia dawa...sijui kwa mangi ziligoma labda sababu ya kuwa na damu tofauti na ya wabena,lakini sababu yeye alishawahi kuzama akatoka mzima naona akapuuza.

anasema alipigwa mwanga mkali na aliona kila kitu kule chini,kwa maelezo yake ni aliona masanduku makubwa sana yanaelea lakini sasa huko chini kuna majoka balaa,nyoka ni wengi sana(nahisi ndio hii wanayoita huku uraiani mizimu ya akina MKONGWA)...sasa huwa wanasema ukifika hatua ya kuona hawa ndio lazima ufe au uwe chizi...anasema struggle yake kutoka shimoni haikua rahisi alichoona kuhusu wake jamaa ni kwamba waliyeshuka naye alikamatwa na moja kati ya hao nyoka na kushushwa huko,pia ule mshtuko ulimvuta na aliyekua kamshikia kamba akaangukia humo,sijui kilimtokea nini yule watatu ila naye ilikuja thibitika kwamba alikufa na wazee wa mila...

nitakuja tena..
daah balaa kubwa...
 
Ahsante mkuu, tulishahama ile nyumba.... ule mtaa ulikuwa hauishi vibweka..... watu wenye vichwa vizito wanoona mambo walikuwa hawaishi kuchagawa hata mchana utaskia kelele watu washachagawa wanasema kuna wanga...... mtt yuko poa now ana kama miaka 7 ivi..... na yupo vizuri tu anasoma na muelewa Alhamdulilah. Kuna dada mmoja wa kazi huyo nikikaa nae muda mrefu almost miaka mitano na yeye pia alikuwa anaonaona haya mambo.... kuna siku mida kama 6 usiku ivi mie nishalala nimeshtushwa na kelele kubwa sana.... yule dada analia mie kujua labda kimetokea msiba kapigiwa simu kumbe mume wangu alikuwa na yeye keshashtuka ndio anamtuliza kapandisha majini.....anasema mtt yupo kitandani tunamuona tu pale lkn kiuhalisia kuna watu wamemchkua wapo nae nje kwenye mti pana mti wa bilimbi nje.... bwana weeeee mwili wote ulifanya kama umepatwa na baridi kali.... ikabidi hapo kumsemesha mpk akatulia..... anasema ule mtaa mbaya tena watu majirani tu wana kazi ya kuwachezea wtt kimazingara. Yaani acha tu
hahaah mkuu pole sana sio kwa masaibu hayo..
 
mi binafsi sio muoga na nimekutana na mengi mazito....niliwahi pata pia mtihani wa kupendwa na jini wa kike though mimi hakufanya la maana sababu nafanya ibada na niko karibu na anga za juu kuliko mambo ya kidunia..
Mkuu kila unaponijibu napata swali lingine hopes hutonichoka

Naomba kuuliza, huyo jini aliku approach au wewe ndo ulimtongoza mdada kumbe n jini?
Pia ulijuaje kua ni jini? Na jini akikupenda halafu wewe usimpende vipi anaweza kukidhuru?
 
mi binafsi sio muoga na nimekutana na mengi mazito....niliwahi pata pia mtihani wa kupendwa na jini wa kike though mimi hakufanya la maana sababu nafanya ibada na niko karibu na anga za juu kuliko mambo ya kidunia..
Ww dini gani samahani lakini, nataka kujua dini gani inauwezo wa kupambana na mambo haya au imani yako tu?
 
[emoji23][emoji23][emoji23]

Hata Mimi ninajiuliza swali hilo na amesema kwamba walipo rudi porini walikuwa wakizipekua maiti na kupata madonge ya dhahabu,Sasa hizo dhahabu hazikutosha kuwatajirisha?vinginevyo hii ni hadithi ya kutunga.
Wew hujakaa machimbon naomba ukae kwa kutulia, hamna mchimbaj anaeridhka na pesa ya machimbo maana anajua kesho atapata nyingi zaidi...
 
Mim naamini kwa sasa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimeweka mazingira mazur sana kwa wachimbaji wadogo hapa Afrika, Yaan likitokea tu chimbo tayar wanaweka kituo cha polisi ila zaman ilikuwa ni kama huko msumbij mim nakumbuka mwaka 2012 lilitokea chimbo shinyanga kakora lilikuwa linaitwa nyangarata ilikuwa ni hatar full kuchinjana Mara unakuta Dem kauliwa na chupa imeingizwa kwenye K...
 
Ahsante mkuu, tulishahama ile nyumba.... ule mtaa ulikuwa hauishi vibweka..... watu wenye vichwa vizito wanoona mambo walikuwa hawaishi kuchagawa hata mchana utaskia kelele watu washachagawa wanasema kuna wanga...... mtt yuko poa now ana kama miaka 7 ivi..... na yupo vizuri tu anasoma na muelewa Alhamdulilah. Kuna dada mmoja wa kazi huyo nikikaa nae muda mrefu almost miaka mitano na yeye pia alikuwa anaonaona haya mambo.... kuna siku mida kama 6 usiku ivi mie nishalala nimeshtushwa na kelele kubwa sana.... yule dada analia mie kujua labda kimetokea msiba kapigiwa simu kumbe mume wangu alikuwa na yeye keshashtuka ndio anamtuliza kapandisha majini.....anasema mtt yupo kitandani tunamuona tu pale lkn kiuhalisia kuna watu wamemchkua wapo nae nje kwenye mti pana mti wa bilimbi nje.... bwana weeeee mwili wote ulifanya kama umepatwa na baridi kali.... ikabidi hapo kumsemesha mpk akatulia..... anasema ule mtaa mbaya tena watu majirani tu wana kazi ya kuwachezea wtt kimazingara. Yaani acha tu

duuh aisee hii mbona kali.

yaani sipati picha ningekuwa mimi na mtoto wangu ningejiskiaje!!!
 
Imeandikwa katika Biblia Kitabu cha Hosea 4:11 "Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu."

Ndugu unayesoma ujumbe huu nakuomba ikimbie dhambi ya uzinzi/Uasherati, pamoja na Ulevi (divai) jitenge mbali na dhambi hiyo na usifanye dhambi hiyo tena.
Mpokee YESU KRISTO Mwokozi kwa upya, utubu na utengeneze na MUNGU
Divai ile ile Yesu aliyoitengeneza Harusini??
Au hii Divai ipi?Ya nyanya si zabibu?Hii mnayokunywa kama damu ya Yesu??
Au matone kidogo yana exception ya kuingia Mbinguni?
 
Malizia basi story.
Mkuu najipanga nimalizie, ukiona kimya usidhani ni makusudi bali mambo mengine yanaingiliana, pia wengine si waandishi wazuri wa kupangilia kisa(visa) inahitaji kurecall na kuiweka kisimulizi katika maandishi something different from reciting it verbally. Naahidi kumalizia usiku huu, kifupi kwa kugusa hasa yaliyojiri na ushauri wa juu ya haya mambo yakikutokea ufanye nini bhas.
 
Nilipangiwa kule 2015 kwa " Kutokusoma ni makosa, imezuiliwa" lakini niliipangua baada ya mzee Ngome kufanya mawasiliano na wa intake MMJKT.
Umeisha hiyo babaa
Hahahahaa, 'order' ikitema kuchomoka ni mtiti, labda upate mbanga kama huo. Mi ilintemaga pia kama hivyo ila nkashindwa kuruka kiunzi. Ikabidi nikaripoti Chicago, nlikaa kidogo nkapiganisha kurudi Mgulani
 
Kazakh destroyer kwanini ulimkataa uyo jini??na je ulikutana nae vp?....ebu tupe simulzi mkuu
dah mkuu majini ni viumbe tofauti na sisi wanapaswa kuoana wao kwa wao....hatufanani kwa lolote sema wao wana mapenzi na wivu wa ajabu kwa wanadamu wakikupenda.....iko siku ntahadithia mkuu ila hawezani na mimi yule na kiufupi alitaka nimtimue wife nikae nae yeye akaniletea bla bla za pete sijui na takataka gani na mimi sifananii hayo mambo....
 
Back
Top Bottom