Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

usijali mkuu....hapana yeye ndo alikuja na alikosa namna ya kukutana na mimi zaidi ya kupitia kwa mtu akipanda kichwani ananipa ujumbe wake then anatoka {hope umewahi kuona watu wakipandisha mashetani} na alitaka tuonane nikamwambia sina muda huo.

inshort majini wana uwezo wa kupenya kwenye mishipa ya damu na wakatembea na kuingia kwenye mwili wa mwanadamu kisha wanadominate akili na wanashika nafasi ya mtu mpaka watoke ndo anarudishiwa akili yake....so alifanya vitimbi vingi kama kuja kusafisha nyumba, kupika n.k ili wife nimuone mzembe yeye ndo anafaa...then kuhusu madhara yes! kama si mtu wa ibada majini wanaweza kukushughulikia kirahisi sana na hawatumii nguvu nyingi.

Hata ukimkuta mtu anasema sijui haamini hayo mambo ni hayajamkuta tu.....kuhusu ukimkataa ndio unaweza kupata matatizo lakini yanatofautiana unaweza kukosa nguvu za kiume au ukakosa kuoa kama hujaoa au ukawa huna interest na wanawake au ukashindwa kushika mimba kama ni mwanamke.

Nafikiri nimekujibu mkuu wangu..

Mkuu kila unaponijibu napata swali lingine hopes hutonichoka

Naomba kuuliza, huyo jini aliku approach au wewe ndo ulimtongoza mdada kumbe n jini?
Pia ulijuaje kua ni jini? Na jini akikupenda halafu wewe usimpende vipi anaweza kukidhuru?
 
Baba yao umeshindwa jeshi hao wanao si ndio watatoroka siku ya kwanza. maana kilaza huzaa kilaza plus plus
Soma unielewe mkuu jeshini sikushindwa ila kimaisha ama future yangu hakuendena na huko. Jeshi lina masharti mpaka lifestyle. Unamjua askari nakatazwa kuishi nyumba moja na RAIA ama hulijui. Hashauriwi kuoa raia
 
Ww dini gani samahani lakini, nataka kujua dini gani inauwezo wa kupambana na mambo haya au imani yako tu?
Kwa kuwa muwazi mimi ni muislamu ninaefuata muongozo wa mitume kutoka kwa muumba wa mbingu na ardhi.....sisi tumewekewa utaratibu wa kujikinga na shari za ardhini na za mbinguni kwenye kila sekta ya maisha.

Asubuhi kuna maneno maalum tumefundishwa ukiyasoma unapata kinga ya majanga ya aina yote na usiku na wakati wa kulala au wakati wa kuvaa nguo....wakati wa kuingia chooni {maana huishi mashetani huko} wakati wa kula wakati wa kujamiiana na mke/mume inshort kila sehemu kuna maneno maalum ambayo kuyasema ni ibada na effect yake iko accurate kuliko speed ya mwanga....
kuhusu imani nyingine siwezi zungumzia mkuu..
shukran..
 
wilaya ya makete, kata ya matamba, kuna poli pale katika shule ya sekondali ITAMBA linaitwa kisulike, kuna mzungu alikuwa mbishi aliingia na farasi hakutoka mpaka leo

ilo poli ukingia utoki unabaki humo humo ,kuna siku bange zetu zikatutuma tuingie humo ,si unajua watoto wa dar tunaosoma mkoa, tunakua viburi
Nimeishi karibu na hapo unapopataja, ilikuwa mwaka gani mkuu maana kwa sasa kuna miti tu ya kupandwa hakuna pori
 
duuh aisee hii mbona kali.

yaani sipati picha ningekuwa mimi na mtoto wangu ningejiskiaje!!!

Acha tu mkuu, nilikaa kama nilipatwa na ganzi ya mwili wote..:. ukizingatia ni usiku kiasi na nimetoka kwenye mshtuko wa usingizi basi kwa muda nilikaa kama zuzu flani ivi [emoji2], ila kwa siku za mbele tulifanya kisomo kikubwa na kutoa sadaka (hizi sadaka tunazotoa toa tunaona kama ni jambo dogo tu lkn kiukweli mbali na kupata thawabu sadaka pia zinasaidia sana kama kinga, zinatukinga na mambo mengi ya mabalaa)
 
kwa kuwa muwazi mimi ni muislamu ninaefuata muongozo wa mitume kutoka kwa muumba wa mbingu na ardhi.....sisi tumewekewa utaratibu wa kujikinga na shari za ardhini na za mbinguni kwenye kila sekta ya maisha.....asubuhi kuna maneno maalum tumefundishwa ukiyasoma unapata kinga ya majanga ya aina yote na usiku na wakati wa kulala au wakati wa kuvaa nguo....wakati wa kuingia chooni {maana huishi mashetani huko} wakati wa kula wakati wa kujamiiana na mke/mume inshort kila sehemu kuna maneno maalum ambayo kuyasema ni ibada na effect yake iko accurate kuliko speed ya mwanga....
kuhusu imani nyingine siwezi zungumzia mkuu..
shukran..

Naam, ingawa wakati mwengine huwa tunajisahau na hizi duaa za kinga lakn zinasaidia mno mno. Mie nasoma kila siku na kwa wtt wangu wadogo wasoweza kusoma wenyewe huwa nasoma then nawapulizia.
 
Soma unielewe mkuu jeshini sikushindwa ila kimaisha ama future yangu hakuendena na huko. Jeshi lina masharti mpaka lifestyle. Unamjua askari nakatazwa kuishi nyumba moja na RAIA ama hulijui. Hashauriwi kuoa raia
We jamaa acha chai bwana kila siku askari wanaoa raia shida ya jeshi ukitaka kusafiri hata kwenda hapo moro lazima uwe na kibari nje ya nchi ndio kabisaaa mchakato kama unataka kwenda mbinguni
 
nitakua naandika kwa vituo tuvumiliane...nilishawahi andika thread ndefu saaana kipindi fulani simu ikazimaga ghafla kila kitu kikapotea

plan yetu kuingia mwezi wa 12 ilikua sababu ile ni miezi ya kula mavuno kwa wakazi wa Njombe wanajua huu ni msimu wa mvua na watu wengi ndio huwa wanaenda kutambika huko malori kwa magari ya kifahari...hata hao kuku huwa wengi na habari ni kwamba hata mali ndio inakua nyingi,inasemekana huwa inakuja mali na kupotea na ishara ni hao kuku kuwa wengi na kupungua

tulikua watano,1.mimi ,2.mobu (marehemu) ,huyu alikua mkinga alikua ana mishe za kupasua mbao kwa msumeno wa mkono shimoni(waliokaa njombe wanajua hii style ya kupasua mbao) 3.usungilo (marehemu) naye alikua na mishe za kupasua mbao,kwao ni bulongwa makete huko 4.mangi(alitoka mzima) huyu tulifanikiwa kutoka naye ila baada ya kutoka alikaa kama wiki moja akaanza onesha dalili za kuwa kichaa,na akawa kichaa kweli akaondokaga pale njombe hadi leo sijui habari zake (mungu amrehemu huko aliko) 5.mwaikambo (marehemu) jamaa wa mbeya alikua naye kaja kuhangaika na maisha tu Njombe.

Nirudi kwangu mimi kwanza kidogo,by then mimi nilikua mwajiriwa kiwanda cha chai,ajira siyo ya kitaalamu lakini kipato cha kuweza kuwanyanyasa hao jamaa zangu wote kiuchumi...wanangu sana,tunakutana kijiweni tunawa washkaji haswaa...kwenye hii safari mimi ndio nilikua master planer,sababu labda ya kuwa na kauli...mangi ndio alikua kama mwenye maono yote na alikua na njaa sana na hii mali...kwahiyo kupona kwangu mimi ilikua sababu sikua mstari wa mbele kuingia ndani kabisa ya pango kwenye hayo masanduku..

usiku tar 22/12 tukiwa na kila kitu cha kuingia kufungua masanduku tukaenda mdandu...fika tukiwa tushapiga mitungi yetu wanangu wako mbele mbele tukaingilia upande mwingine kabisa wa msitu ambako hata hakuna watu...hakuna kibaya hapo,tunakata majani kwa mapanga na miti midogo kupata njia...tumetembea zaidi ya masaa mawili msituni ili kuja unganisha na njia ya kule wanakoingilia watalii...na sababu tayari tulikua ndani hatukuonekana na wale wazee kule nje pamoja na walinzi wa msitu


wazee...mule ndani ni giza totoro,tochi zetu za mawe zile za kuitwa KURUNZI.,,,betri tatu tatu,tukafika tukaipata ile sasa njia ya ndani kabisa kwenda mapangoni...humu mchana kunatisha saanaaa,sasa imagine usiku inakuaje,hakuna story hapo na kama ni kuitana ni kwa sauti za chini sana,hofu ilikua kubwa na mvua sasa ikawa imeanza kupiga...baridi ni kali sana msituni

tumeendaaaa tukafika sasa kwenye mlango wa pango hapo ndio visa vilipoanzia...kule ndani usiku wanyama ndio wanakua active sababu ya ratiba labda za utalii so usiku pango ndio zinakua na fujo...tukaanza liingia pango bila uoga,mwendo kama wa dakika 30 hivi...huko ni kusikia tu sauti za wadudu na wanyama wadogo..tukamaliza hiyo zone ya zile pango za kitalii sasa tukawa kwenye mwisho ambako watu huwaga hawaruhusiwi kusogea zaidi ya hapo kwa imani kwamba watapotea hawatorudi.

na ndio habari ya vifo vya ndugu zangu watatu,kichaa cha mangi na ulemavu wangu inaanzia hapa...

ulemavu wangu wala usiwape wazo...ni kwamba niliumwa na nyoka huko nikafanikiwa kwa kudra za mungu tu kuokolewa kwa kukatwa mguu wa kushoto..

nitarudi..
Pesa na iheshimiwe na watu wote waseme amina
 
1995-98 mkuu, msitu umekufa ?
da nipe michapo nani aliukata?
Msitunipo shuleni wa miti ya kupandwa na maeneo mengine yote yana mapori lakini sio mapori mazito, niliishi pale 2016 hapakuwa na stori za msitu wenye maajabu ndio maana nadhani unaouzungumzia ulifutika

Mimi nilikuwa naishi jirani kabisa na korongo ambalo ukiibuka unaibukia shule so lazima ningejua
 
Acha kabisa.... Mie niliwahi kutokewa na mauzauza nyumba nilokuwa nakaa mwanzo, usiku nimelala na mtt wangu age kama one year ivi ghafla nikashtuka nimesimamiwa na dada wa kiarabu (namuona mpk leo alivokuwa katusimamia na alivovaa) sema kama kulikuwa na kagiza kdg.... baba wtt kalala chini (si unajua tena mkiwa na wtt wadogo kulala pamoja sio issue) basi nilivoshtuka yule dada akapotea, nikajiuliza mmmh ni ndoto au, jamaa yangu kalala wa juzi habari hana. Nikasema mmh wacha tu niendelee kulala labda waswas tu mana mie nna kaujasiri kdg.. Ile kufumba tu tena macho nikaanza tena kama kuweweseka nashtuka ghafla namuona tena yule dada this time keshainama tayari na mtoto kambeba yaani ile beba ya mikono miwili kwa mbele, niliinuka ghafla akapotea na kila kitu kikarudi kama kilivyo aaah hapo ikabidi nimuamshe mwenzangu kimwambia huku nalia.... yaani ilikuwa kama ndoto lkn ni uhalisia mana kila kitu nilivokionakilikuwa kama kilivyo chumbani na mtt nguo zake za pajamas ni zilezile.... hapo hatukulala tena. Yaani mpk tunahama kile chumba changu mwenyewe nilikua nakiogopa hata mchana mpk nipelekwe mara moja moja ndio najikaza. na huyu mtt ikabidi kumfanyia dawa... tuliambiwa ni kama vile yule jini alimpenda... sasa sijui hata alikuwa anataka kumpeleka wapi
Duuh...

Pole sana ukhty...that was really a havoc....evil spirits are rampant in our houses yaani bora mkautafuta huo msaada

Dua na visomo nyumbani kila baada ya muda kupita ni muhimu.

Wakati wa kulala nyinyi ama hata kids unaweza kuwapaka mafuta ya "misk" kama haiwasumbui(allergies)....

Usiache kutumia MREHANI(kivumbasi) na chumvi ya mawe katika kuoga mara mojamoja...

Nyumbani kwako kama una space panda MKUNAZI...."hawaupendi".
 
Msitunipo shuleni wa miti ya kupandwa na maeneo mengine yote yana mapori lakini sio mapori mazito, niliishi pale 2016 hapakuwa na stori za msitu wenye maajabu ndio maana nadhani unaouzungumzia ulifutika

Mimi nilikuwa naishi jirani kabisa na korongo ambalo ukiibuka unaibukia shule so lazima ningejua
Mi nimesoma pale itamba msitu upo karibu na shamba la shule kule kama unaenda kisaula, shamba la shule unalijua? kule ndio kuna huo msitu haupo karibu na nyumba za watu,

Huo msitu hajawai kuwaka moto hata moto ,uweje, tulikuta story mzungu aliingia na farasi hajatoka mpaka leo

Wawanji wote hawaingii mule ,ndio maana nakushangaa unaposema kuna miti ya kupandwa ,
mule huishia nje wakienda kutambika,
wakiingia hawatoki,

Acha hapo kuna njia ya miguu ukipitia kitekelo kama unaenda chimala,kwenye magofu ya wajerumani mbele kidogo kuna bonde kubwa mule ,kuna mali wajerumani walizitupa, ila mpaka uwe na ramani na uchawi ndio utazipata.

Pale shule wajerumani huwa wanakuja kufundisha mara kwa mara, kuna mmoja anaitwa betina huyu tulizunguka naye mapolini,ila kuna mida anaweza kutuacha sehemu ataondoka peke yake mabondeni, tukimuuliza anadai kuna makaburi ya ndugu zake walikufa kipindi cha ukoloni
 
Back
Top Bottom