Tukio la Kuungua Moto shule ya Shauritanga 18 June 1994

Tukio la Kuungua Moto shule ya Shauritanga 18 June 1994

Background Check

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2019
Posts
341
Reaction score
498
Habari wakuu!,

Ni muda sasa umepita tangu nipotee katika majukwaa mbalimbali hapa JF.

18 June 1994, Usiku wa manane, wanafunzi katika shule ya wasichana ya Shauritanga wakiwa wamelala, moto mkubwa ulizuka. Mabinti wale walipiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa walinzi hawakufanikiwa hadi wakafa wakiwa wamejikusanya sehemu ya mlango uliokuwa umefungwa na walinzi kwa nje.

Viongozi wa Serikali walikimbia haraka sana, wakatoa kauli nzito za kulaani kilichoonekana kuwa kama hujuma na wakaahidi kwamba tukio hilo halitajirudia tena. Kinachosikitisha ni kwamba miaka 22 baadaye, bado shule zinateketea kwa sababu huenda zinazofanana na tukio la Shauritanga.

Leo nimerudi nina swali ama niseme ninahitaji kufahamu kuhusu kuungua kwa shule ya Shauritanga 18 June 1994, mkoani Kilimanjaro.

Kama kuna mtu yoyote ambaye anamelezo ya kina kuhusu tukio hili, ninaomba anijuze ninahitaji kufahamu mengi kuhusu tukio hili.

Ilikuwaje, chanzo cha moto, walinzi walikuwa wapi kufungua ili wanafunzi watoke.

Lakini pia baada ya uchunguzi uchunguzi ulikuja na majibu gani/Findings kuhusu moto huo

Kesi yake ilifungwaje na ilikuwa ni kesi ya uchunguzi namba ngapi?

I want to know.

Asanteni sana.

Machepele Tanzania.​

shauritanga.jpeg
 
Hili suala ni kuliacha tu kwani lilikuwa na utata sana na kulikuwa na stori nyingi sana wakati huo. Ninaloliona hapa ni kuamsha tu uchungu kwa waliopoteza wapendwa wao ambao walishawasahau kwa muda. Kama kumbu kumbu zangu zipo vizuri ni kuwa aliletwa mpelelezi kutoka Scotland Yard kuchunguza hilo suala lakini ripoti yake sikuwahi kusikia kuwa imewekwa hadharani popote pale.
 
Nahitaji kujua, nina maana yangu kuja kuuliza hapa. Kwa nini sijauliza kuhusu ajali ya MV Bukoba?. Kwa sababu nafahamu ilitolewa report hadharani lakini hii imekuwa Very Classified and Secured kwa nini?.
 
Shauri tanga si ni mixture au ? Si ipo mashati rombo

Maana nilisomaga tution pale kuna kaburi lina ukuta wa simenti wameandika majina sema ilo sikuliona

Sasa sijajua ni hihihii au ziko mbili
 
Back
Top Bottom