Tukio la Kuungua Moto shule ya Shauritanga 18 June 1994

Habari wakuu!,

Ni muda sasa umepita tangu nipotee katika majukwaa mbalimbali hapa JF.

18 June 1994, Usiku wa manane, wanafunzi katika shule ya wasichana ya Shauritanga wakiwa wamelala, moto mkubwa ulizuka. Mabinti wale walipiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa walinzi hawakufanikiwa hadi wakafa wakiwa wamejikusanya sehemu ya mlango uliokuwa umefungwa na walinzi kwa nje.

Viongozi wa Serikali walikimbia haraka sana, wakatoa kauli nzito za kulaani kilichoonekana kuwa kama hujuma na wakaahidi kwamba tukio hilo halitajirudia tena. Kinachosikitisha ni kwamba miaka 22 baadaye, bado shule zinateketea kwa sababu huenda zinazofanana na tukio la Shauritanga.

Leo nimerudi nina swali ama niseme ninahitaji kufahamu kuhusu kuungua kwa shule ya Shauritanga 18 June 1994, mkoani Kilimanjaro.

Kama kuna mtu yoyote ambaye anamelezo ya kina kuhusu tukio hili, ninaomba anijuze ninahitaji kufahamu mengi kuhusu tukio hili.

Ilikuwaje, chanzo cha moto, walinzi walikuwa wapi kufungua ili wanafunzi watoke.

Lakini pia baada ya uchunguzi uchunguzi ulikuja na majibu gani/Findings kuhusu moto huo

Kesi yake ilifungwaje na ilikuwa ni kesi ya uchunguzi namba ngapi?

I want to know.

Asanteni sana.

Machepele Tanzania.​

View attachment 2143146
Mkuu hii shule ni mchanganyiko sio wasichana tu!!!?labda useme bweni la wasichana
 
Nakumbuka lilipotokea lilizusha hofu na taharuki kwa jamii nzima. Ilikuwa ni kipindi ambacho kulikuwa na vugu vugu la matukio mengi yakihusisha pia na maswala ya kidini ... najaribu kurejea:

*Kuchomwa kwa mabucha ya nguruwe
*Kuendelea kwa matukio kama hayo katika shule nyingine
*kupatikana kwa mabomu Mlima kilimanjaro(sijui propaganda)
Moja lilikuwa limeandikwa mistari ya biblia
"Ombeni nany mtapewa, tafteni nany...."
*milipuko ya moto mlima kilimanjaro
*vuguvugu la mihadhara ya kidini kushika kasi

Wenye kumbukumbu zaidi wanaweza leta matukio zaidi

MSRIP.. it was sad indeed
 
Habari wakuu!,

Ni muda sasa umepita tangu nipotee katika majukwaa mbalimbali hapa JF.

18 June 1994, Usiku wa manane, wanafunzi katika shule ya wasichana ya Shauritanga wakiwa wamelala, moto mkubwa ulizuka. Mabinti wale walipiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa walinzi hawakufanikiwa hadi wakafa wakiwa wamejikusanya sehemu ya mlango uliokuwa umefungwa na walinzi kwa nje.

Viongozi wa Serikali walikimbia haraka sana, wakatoa kauli nzito za kulaani kilichoonekana kuwa kama hujuma na wakaahidi kwamba tukio hilo halitajirudia tena. Kinachosikitisha ni kwamba miaka 22 baadaye, bado shule zinateketea kwa sababu huenda zinazofanana na tukio la Shauritanga.

Leo nimerudi nina swali ama niseme ninahitaji kufahamu kuhusu kuungua kwa shule ya Shauritanga 18 June 1994, mkoani Kilimanjaro.

Kama kuna mtu yoyote ambaye anamelezo ya kina kuhusu tukio hili, ninaomba anijuze ninahitaji kufahamu mengi kuhusu tukio hili.

Ilikuwaje, chanzo cha moto, walinzi walikuwa wapi kufungua ili wanafunzi watoke.

Lakini pia baada ya uchunguzi uchunguzi ulikuja na majibu gani/Findings kuhusu moto huo

Kesi yake ilifungwaje na ilikuwa ni kesi ya uchunguzi namba ngapi?

I want to know.

Asanteni sana.

Machepele Tanzania.​

View attachment 2143146
Umenikumbusha mbali sana mkuu maama siku ya mazishi nilikuwepo. Tulianza kutembelea bwenini sehemu walipofia na kisha mazishi. Hii siku ilikuwa ngumu sana yaani msiba mkubwa kama ule ila Rais hakuhudhuria, palikuwa na maelfu ya waombolezaji toka sehemu mbalimbali
 
Nakumbuka tulikuwa tumefunga shule tuliporudi tuliambiwa tuweke funguo za mabweni juu ya loka ili moto ukitokea mtu yeyote afungue mlango.
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu maama siku ya mazishi nilikuwepo. Tulianza kutembelea bwenini sehemu walipofia na kisha mazishi. Hii siku ilikuwa ngumu sana yaani msiba mkubwa kama ule ila Rais hakuhudhuria, palikuwa na maelfu ya waombolezaji toka sehemu mbalimbali
Rais hakuhudhuria 🤔🤔🤔
 
asee kuna watu wakongwe humu, wengine tumekuta history ya darasani na ndo tunaishadadia ila humu kuna watu wamejionea live
 
Back
Top Bottom