Tukio la Lissu: Dhana 3 za msingi ambazo zinatokana na ‘mchujo’ wa dhana mbalimbali

Toka jana nimesoma maoni ya wengi ...Chahali ndiye aliyechambua hili tukio akiwa na nafsi huru ....[HASHTAG]#prayingforLissu[/HASHTAG]
Ni uchambuzi mzuri sana kuliko mwingine tuliousoma mpaka sasa.
 
Sawa. Lakini kama wahusika ni "deep state", vyombo vya dola vitawapataje?
Hawa kama alivyosema, ni watumishi wa vyombo wa zamani wasio rasmi lakini dola inawajua.
Nadharia hii ya "rogue" inashawishi kwa sababu ndiyo ilitumika kumuondoa Gen. Kombe.

Tumeshuhudia juzi juzi mtu anamtolea bastola Nape Nnauye hadharani. Mpaka leo hatujaambiwa ni nani na alifanywa nini?

Iwavyo, naona kitengo kinamuangusha mkuu. Nashawishika kuamini kuwa kitengo hakikuhusika kumpendekeza na sasa kinamharibia kazi anayetaka kuharibiwa kazi yake. Subiri muda si mrefu watatokea wana kitengo kujilipua na kueleza walivyotumwa.
 
Umeandika vizuri lakini sio Magufuli tu anajitengenezea mazingira mazuri ya kupikiwa lawama na wabaya wake. Vile vile victims wanakuwa wamejijengea mazingira mazuri ya kuwa target. Mfano, Unalalamika kwenye vyombo vya habari kwamba X anataka kukudhuru na huyo X anamaadui wengi ni kuwapa maadui zake idea nini cha kufanya!!
 
Afadhakli Kumbe Bado Kuna watu wanaweza ku reason na kufanya analysis zilizotulia. Most likely dhana ya tatu Ndiyo yenye nguvu zaidi mpaka sasa...of course ukiachilia possibilities nyingine nyingi
 
By the way nimeshangazwa na ukimya wa EL kuhusiana na tukio hili.
Anayetuhumiwa kwenye ishu ya Bensaa 8, kwa kuwasiliana naye wa mwisho; pia ameingizwa humu hakuwepo maskani jana. Inasemekana aliyeenda kuratibu mipango
 
Kuntu
 
Jukwaa la intelijensia huwa lina mambo ambayo huwa yanasaidia sana-ukimsoma THE BOLD unapata na ka-theory kengine kuwa tupo sasa kwenye vita ya uchumi vita ambayo tunaopambana nao wanaona kumuondoa moja kwa moja anaewakatili ni ngumu cha msingi ni kuwagombanisha na kuwapandisha wananchi hasira na kujenga chuki baina ya wenyewe kwa wenyewe ili waje waanza kubondana na utawala uwe mgumu na wenye mirija yao warudi na kuendelea kufyonza upya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najaribu tu kurikiri nje ya box

1. Nani amempiga risasi Lissu?
2. Lengo lilikuwa nini?
A. Ni serkali?
B. Mtu mwingine?

Kama ni serkali basi mambo yanayoweza fikiriwa ni haya;

1. Ilikuwa ni UJINGA WA KARNE kuhamisha ATENSHENI ya Ripoti zilizokuwa zinapokelewa Ikulu jambo lililokuwa muhimu kwao serkali kuliko shambulizi

2. Watuma Unprofessional guys wasiojua wapi wafanyie shambulizi na sehemu gani ya kushambulia muda gani watekeleze adhima yao i.e were STUPID BOYS ON MISSION

3. Lengo ni kujeruhi si Kuua kulingana na namna walivyofanya

KAMA SI SERKALI NI WATU WENGINE Basi lengo, tutajiulizaje?

1. Kutuchanganya waTz hususa kipindi hiki hasa tunapojidai tuna uwezo wa kupandikiza upande wao mtu wetu

2. Kutumia opportunity VIZURI Lissu kama Mwanasiasa na Harakati za kizalendo lkn pia Wakili HURU ili ionekane ukinzania unaodhaniwa upo kati yake kwamba Serkali imehusika hivyo kuhamishia vita ktk viwanja vya nyumbani kutoa kwenye Right Track.

3. Watu walioshambulia huenda watu wenye ushabiki wa SIASA MAJI TAKA wenye u vyama ktk masilai za kitaifa ndio waoweza kujitapa kuwa wako tayari kumuua mTz mwenzao maadamu uko kinyume na chama au wanadhani ni mamluki bila ushahidi wowote.

4. Watu waliomshambulia sio askari WALIOFUNZWA walipiga risasi 5 sehemu zisizo hatarishi HAWA NI WAHUNI FULANI waliotumwa au walioamua kufanya kitu wasicho na Utaalam kabisa.

WAZO LANGU. Tutulie watajulikana nani amefanya haya.

Bwana ataongoza safari
 
Nice work. Amechambua akiwa na mawazo huru
 
hahahhahahahha.ngoja ninyamaze mimi nina starlet ikipigwa risasi kama vile inawaka moto
 
Bahati mbaya hili suala litaishia tu kwa "watu wasiojulikana"
 
nakubaliana kuwa inawezekana serikali haihusikii lakini inakazi pia ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, usalama wetu upo mikononi mwa serikali, Na ukizingatia lisu alilalamika sana kuwa kunawatu wanatafuta maisha yake.
 
By the way nimeshangazwa na ukimya wa EL kuhusiana na tukio hili.
Ulitaka akasemee wapi? Kwani lazima kila kiongozi aite waandishi na kutoa neno?
Lengo lako hukupaswa kulileta kwenye mjadala huu.
 
Ni kweli kabisa, bila hivyo dhana kuwa serikali ya awamu ya tano kuhusishwa haikwepeki
 
Sawa Mkuu!
Nilikutana na kijana wa kitanzania(wa kawaida kabisa) ofisi moja kubwa ya serkali akishughulikia yaliyompata kwa kazi halali aliofanya nje ya nchi. Kwa sababu ya "rogue elements" na haohao "deep state" kijana amewahi kulala ķituo fulani wk kadhaa mtesi wake ambaye ni mfanyabiashara akitembelea kituo kuelekeza! Alifunguliwa mash taka kutaka kudhuru watawala. Ofisi zote walikuwa wana-symphasize na kijana wanaishia kusema tu '...nchi ina we nye we. ...'
Hivi vitu ni mubashara! BTW bastola/bunduki tulizoziona nje nje miezi hii ya karibuni yamefikia wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…