Tukio la Lissu: Dhana 3 za msingi ambazo zinatokana na ‘mchujo’ wa dhana mbalimbali

Haya ndiyo yaleyale ya utanikoma usiku.... tutaona kama kesho utafika.... halafu kweli linatokea la kutokea kwa huyo mtu na muhusika sio wewe. Acha jamii ikuhukumu kwa mdomo wako.
Chunga sana ulimi. Acha uropofu wa kujiona wewe ni mungu mtu.
 
Jana, Septemba 07, 2017, majira ya mchana, zilipatikana taarifa kwamba Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Singida Mashariki, Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani, na Rais wa Chama cha Wanasheria (TLS), amepigwa risasi kadhaa na kujeruhiwa vibaya.

Tukio hilo la kutisha lilitokea jijini Dodoma, wakati Mbunge huyo aliposhuka nyumbani kwake eneo la Area D, inakoelezwa alienda kwa ajili ya kujipatia mlo wa mchana.

Kabla ya kuingia kiundani kwenye makala hii, nitumie fursa hii kutoa salamu za pole kwa Lissu, na kumwombea apone haraka. Salamu za pole pia kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema, chama ambacho Lissu amekuwa akikiwakilisha kwa ufanisi mkubwa.

Pia ni vema nitahadharishe mapema kwamba intelijensia sio sayansi timilifu kwa asilimia 100, kwa kimombo wanasema “intelligence is not an exact science.”

Okey, sasa tuingie mtamboni. Hadi muda huu kuna dhana za msingi tatu ambazo zinatokana na‘mchujo’ wa dhana mbalimbali.

Dhana ya kwanza na ambayo pengine ni maarufu zaidi ya zote ni kwamba jaribio hilo la mauaji ya Lissu lina mkono wa dola. Kwamba sio siri kuwa Lissu amekuwa ‘akiisumbua mno’ serikali, ambapo wafuasi wake wanamwona kama jasiri asiye na uoga wa kusema ukweli, ilhali wapinzani wake wakimwona kama mchochezi.

Yayumkinika kuhitimisha kwamba kama kuna mwanasiasa wa upinzani ambaye amekuwa ‘mwiba mchungu’ kwa serikali ya Rais John Magufuli basi si mwingine bali Lissu.
Na pengine kinachoongeza uzito kwenye dhana hii ni ukweli kwamba Agosti 18 mwaka huu, Lissu aliwaeleza wananchi kwamba anafuatiliwa.

Namnukuu "Naomba kabla sijaanza Mazungumzo yangu nimuombe Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa anaitwa Kipilimba au Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro, wale vijana ambao wamewatuma na kwa wiki tatu mfululizo wananifuata kila nilipo wanaotembea na gari ya Toyota premio namba T460CQV, jana niliwakaba Kanisani St. Peter's.

Kwa upande mwingine serikali ya Magufuli ni kama ilikuwa inatafuta ‘kulaumiwa bure.’ Kwa sababu, Hadi muda huu hakuna sababu moja ya msingi kwa serikali hiyo kuyafanya maisha ya wanasiasa wa upinzani yawe magumu kiasi hiki. Magumu kwa maana ya kuwanyima kila aina ya fursa ya kufanya siasa (political space).

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, zaidi ya viongozi na wafuasi 400 wa Chadema wameshakamatwa tangu Magufuli aingie madarakani. Mtu atayedai kuwa kiongozi huyo ‘anawachukia wapinzani’ hatoonekana mtu wa ajabu japo huenda akatupwa jela.

Katika hotuba zake mbalimbali, Rais Magufuli ameshindwa kuficha hisia zake dhidi ya upinzani na wapinzani. Juni 12 mwaka huu, Rais Magufuli alimweleza Spika Job Ndugai maneno yafuatayo
“Tumia mbinu hiyohiyo ya kuwafanya wasiropokee Bungeni, waropokee nje na kule tutadili nao vizuri kwasababu wanapokua kule ndani wana kinga wanaweza wakatukana chochote, sasa kinga wanayoitumia vibaya bungeni kainyooshe wewe. Wawe wanatoka kule bungeni, ukishamfukuza hata mwezi mzima… atakuja aropokee huku, na mimi nakueleza waache waropokee huku nitadili nao, wala siwatishi lakini hatuwezi kuwa kwenye vita wewe unaanza kugeuka kupiga wale wanaokwenda mbele…. ni nafuu unyamaze ukalale.”

Kwa kuangalia jinsi watendaji wa serikali ngazi za mkoa na wilaya wanavyochuana na polisi kuwanyanyasa wapinzani, hususan wa Chadema, dhana kuwa serikali ina mkono katika jaribio la mauaji ya Lissu ni kama ‘ready-made.’

Hata hivyo, pamoja na ‘dalili zote’ kuashiria uwezekano wa mkono wa serikali katika jaribio la kumuua Lissu, dhana hii inakosa mantiki kiuhalisia. Ni kwamba hakuna tija kwa serikali kumuua Lissu. Sawa, sio siri kuwa uhusiano kati ya serikali na Lissu/ wapinzani sio mzuri, lakini haitokuwa na tija yoyote kwa serikali ya Magufuli kumuua Lissu.

Na hata kama ingekuwa lazima ‘aondoke,’ basi kuna ‘njia mwafaka zaidi’ za mauaji ya watu maarufu (assassination), huku 'kifo cha ajali' ikiwa maarufu na rahisi zaidi.
Halafu kinachotatiza katika tukio la jana, na kinachopunguza zaidi nguvu ya dhana kwamba ‘kuna mkono wa serikali,’ ni jinsi waliofanya shambulio hilo walivyoonekana kama wanahitaji publicity ya kutosha. Kwanini? Jibu lipo kwenye uchambuzi wa dhana ya tatu.

Dhana ya pili ni dhaifu kuliko nyingine mbili. Hii inahusisha mbio za urais mwaka 2020. Kwamba kila siku Lissu amekuwa akijitengenezea mazingira ya mgombea mwafaka wa Chadema/Upinzani katika uchaguzi mkuu ujao, wala halina mjadala. Sio kwamba Lissu amekuwa hodari katika masuala mbalimbali kwa vile anataka urais (hajawahi kutamka nia ya kugombea nafasi hiyo) lakini umahiri wake bungeni na katika masuala ya kisheria na kitaifa kwa ujumla, unamfanya kuwa kipenzi cha takriban kila mfuasi wa Chadema.

Dhana hii dhaifu inasema kuwa jaribio hilo la mauaji ni kazi ya wapinzani wa kisiasa wa Lissu, hususan ndani ya chama chake.

Na kama ilivyokuwa kwenye dhana ya kwanza, hata kama wapinzani wa kisiasa wa Lissu ndani ya chama chake wangekuwa wahusika, kwanini basi tukio hilo lifanyike katika mazingira ya ‘kusaka publicity kwa nguvu’?

Hiyo inatuacha na dhana moja, ya tatu, na ya mwisho. Ya mwisho lakini sio haba katika mantiki. Dhana hii inaeleza kwamba jaribio hilo la mauaji limefanywa makusudi na kile wajuzi wa mambo wanaita ‘rogue elements.’ Hizi zilitusumbua sana katika utawala wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete. Rogue elements hizi zinajumuisha watumishi halali wa vyombo vya dola wanaofanya shughuli zisizo halali. Nani anawatuma? Hiyo ni habari nyingine.

Kuna kitu kinachofahamika kama ‘Deep state.’ Kila nchi ina tafsiri yake kuhusu ‘deep state’ lakini tafsiri nyepesi kwa mazingira yetu ni ushirika wa watu wenye nguvu katika serikali na jamii – mfano vigogo (hususan wa zamani) wa vyombo vya dola, wafanyabiashara wenye uwezo mkubwa na wanasiasa kutoka upande wowote ule, lakini zaidi chama kilichopo madarakani.

Dhana hii inaliona tukio la kujaribu kumuua Lissu kama njia rahisi ya kuichafua serikali ya Rais Magufuli, ambayo kwa bahati mbaya/makusudi ilishajitengenezea mazingira ya kulaumiwa pindi la kutokea likimtokea mwanasiasa wa upinzani kama Lissu. Rais anaposhindwa kudhibiti ‘chuki zake’ dhidi ya wapinzani, anawapa nafasi nzuri ‘wabaya wake’ kutenda kitu kisha ikawa rahisi tu lawama kuelekezwa kwake.

Ndio maana dhana ya kwanza – kwamba kuna mkono wa serikali ya Magufuli kwenye jaribio la kumuua Lissu – inaonekana kama yenye uzito kwa vile "kuna sababu ready-made.”
Dhana hii inapata uzito kutokana na ukweli kwamba Magufuli amejitengenezea maadui wengi, wenye nguvu, na baadhi yao wakiwa viumbe hatari. Kuna watu waliozowea kuishi maisha ya kifalme ambao sasa wanalazimishwa kuishi maisha ya kawaida. Hawa watu wakipata upenyo wa kumdhuru Magufuli, hawatosita kufanya hivyo.

Lakini kwa vile ni ‘vigumu mno’ (angalau kwa wakati huu) kufanikisha jaribio la kumdhuru kiongozi huyo, njia nyepesi inaweza kuwa katika ‘kuua character yake,’ ambayo bahati nzuri kwa ‘wabaya wake,’ sio nzuri sana.

Kumekuwa na malalamiko kadhaa hasa kutoka upande wa upinzani kumtuhumu Magufuli kuwa ni dikteta. Na ukifuatilia mwenendo wa siasa zetu kwa muda huu, sio siri kwamba kuna chembe chembe za udikteta. Kwahiyo, ni rahisi kwa ‘wabaya wa Magufuli’ kutumia mwanya huo kujenga picha ya “serikali ya dikteta yamuua mpinzani wake mkubwa.”

Na hilo linatuleta kwenye suala la publicity. Kwamba jaribio la mauaji hayo liwe na mwangwi wa kutosha ndani na nje ya Tanzania. Mwangwi huo ni wa makusudi ili uakisi taswira inayojengeka kuwa ‘Magufuli ni dikteta. Na madikteta hunyanyasa wapinzani wao, na ikibidi hata kuwaua.’
Kwahiyo, kama kuna funzo kubwa kwa Magufuli katika tukio hili ni kuepuka mazingira yaliyopo ya uhasama mkubwa dhidi ya upinzani hususan Chadema. Kiongozi huyo anatambua fika kwamba kuna watu wapo radhi kufanya lolote lile kumng’oa, na kwa vile ‘njia za kawaida’ sio rahisi, basi inakuwa ‘anything goes,’ liwalo na liwe.

Na dhana hii ya tatu inaleta uhusiano kati ya tukio la jana la jaribio la kumuua Lissu na lile la hivi karibuni la kuchomwa moto kwa ofisi za kampuni ya uwakili wa IMMA. Kama hili la Lissu, tukio la moto nalo lilifanyika katika mazingira ya kuvutia publicity, yaani kama kulikuwa na jitihada za makusudi za kuushawishi umma kwamba “mnaona huyu dikteta Magufuli anakoelekea? Sasa anachoma hadi ofisi wa ‘wabaya’ wake.”

Nihitimishe uchambuzi huu kwa kueleza bayana masuala mawili matatu. Kwanza, lengo la uchambuzi huu mfupi sio kuingilia kazi za vyombo vya dola vinavyoendelea na uchunguzi kuhusu jaribio la kumuua Lissu. Nimefanya uchambuzi huu kama mtu mwenye uelewa wa masuala ya intelijensia na siasa za Tanzania yetu, ikiwa ni pamoja na “yanayojiri nyuma ya pazia.”
Pili, lengo la uchambuzi huu sio kumshawishi mtu yeyote abadili mtazamo wake kuhusu “nani ana/wanahusika.”

Mwisho, kama nilivyotanabaisha awali, tasnia ya intelijensia sio sayansi kamilifu kwa asilimia 100 (intelligence is not an exact science). Kwa maana hiyo, japo uchambuzi huu ni karibu kabisa na hali halisi, sio rahisi sana kufikia hali halisi yenye uhakika wa asilimia 100.

Nimalizie kwa kumtakia afya njema Bwana Lissu huku nikiamini kuwa malaka husika zitafanya kila jitihada kuwanasa wahusika, sio tu kwa minajili ya serikali kujinasua bali ili Bwana Lissu atendewe haki.
 
Good analysis but I still don't discount this scenario as well:
Tundu Lissu made himself a sweet target for quite a number of suspects!:

- Within his party he could already be, to some members, more profitable dead, come the right circumstances, than alive! AND SOME LITTLE DEVILS WON'T HESITATE WHEN THE ATMOSPHERE SIGNALS IT'S TIME TO PIN THE TAIL ON A FALSE MONSTER!
-
-

NB: I FEEL LIKE EVERYONE CHOOSING HIS CONSPIRACY THEORY BASED ON WHICH SIDE OF THE COIN PAYS, WHICH MIGHT EVEN AFFECT THE OUTCOME OF THE CRIMINAL INVESTIGATIONS IN PROGRESS!
 
Uchambuzi mzuri usioegemea upande wowote.
Ila serikali haina pa kujinasua katika hili kwa namna inavyotenda, waswahili tunasema maneno huumba hata kama si kwa kupitia kwenye mikono ya mnenaji.
 
Nimesema humu sana,si rahisi serikali ifanye shambulio la kuvuta attention namna hii 'shambulio la kelele 'na wakati Lissu ameshakuwa mikononi mwa polisi mara kibao si wangeweza hata kumpa sumu ya kummaliza taratibu kama walitaka kumuua.

Hilo walishindwa na wameshashindwa sana tu....

Tatizo ni kuwa, ni ngumu sana kumdhibiti Tundu Lissu akiwa ktk akili zake timamu unless labda wamnunue mke wake anayempikia chakula chake!!

Huyu mtu anazijua sheria karibu zote na hutumia hata huo mwanya wa kukamatwa kamatwa na polisi kuwafundisha sheria haohao polisi...

Sasa leo hawa wamuue kwa njia gani?

Hebu rejea kesi yake ya juzijuzi hapa ya "uchochezi". Hawa polisi pasipo hata kujua wana deal na mtu wa aina gani, wakamtegea mtego wa kitoto kabisa wa kutaka apimwe mkojo huku tuhuma yake ikiwa ni uchochezi!!

Hii ishu ya Lissu imemkalia Magufuli vibaya Sana. Ni ngumu kujisafisha na kisha kujinasua na tuhuma hizi za serikali yake kutaka kumuua huyu bwana kwa mazingira ya kauli na matendo yake mwenyewe aliyoyatengeneza.....

Hata mimi hapa nakataa kabisa kuwa hahusiki na jaribio hili la kutaka kumuua raia wake eti tu kwa sbb anamkosoa kosoa ktk utendaji wake....!!
 
Tumesha shuhudia maneno tata ya viongozi wa juu..kuna mambo hayaitaji sn kufikilia...yamenyooka..Tz sio nchi yenye amani tena..Mungu ibariki Tz mungu mponye Tundu Lissu
Amani iko wapi..kuonyeshewa siraha bastora Nape..
Kuvamiwa mawingu..
Kifo cha Mawazo cha kinyama..
Kupotea kwa Beni saa Nane
Kutekwa kwa msanii Roma..
Hatuja pata report zozote za viombo vya usama..grain of wheat..we dont need this to happen to our motherland Tz.
 
Chahali vip kama theory hii unaidharau? lifanye tukio lionekane very unprofessional lakini lizae matunda? kupoteza maboya kwa wasiofikria vizuri?
 
*Evarist Chahali* anaandika:

Jana, Septemba 07, 2017, majira ya mchana, zilipatikana taarifa kwamba Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Singida Mashariki, Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani, na Rais wa Chama cha Wanasheria (TLS), amepigwa risasi kadhaa na kujeruhiwa vibaya.

Tukio hilo la kutisha lilitokea jijini Dodoma, wakati Mbunge huyo aliposhuka nyumbani kwake eneo la Area D, inakoelezwa alienda kwa ajili ya kujipatia mlo wa mchana.

Kabla ya kuingia kiundani kwenye makala hii, nitumie fursa hii kutoa salamu za pole kwa Lissu, na kumwombea apone haraka. Salamu za pole pia kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema, chama ambacho Lissu amekuwa akikiwakilisha kwa ufanisi mkubwa.

Pia ni vema nitahadharishe mapema kwamba intelijensia sio sayansi timilifu kwa asilimia 100, kwa kimombo wanasema “intelligence is not an exact science.”

Okey, sasa tuingie mtamboni. Hadi muda huu kuna dhana za msingi tatu ambazo zinatokana na‘mchujo’ wa dhana mbalimbali.

Dhana ya kwanza na ambayo pengine ni maarufu zaidi ya zote ni kwamba jaribio hilo la mauaji ya Lissu lina mkono wa dola. Kwamba sio siri kuwa Lissu amekuwa ‘akiisumbua mno’ serikali, ambapo wafuasi wake wanamwona kama jasiri asiye na uoga wa kusema ukweli, ilhali wapinzani wake wakimwona kama mchochezi.

Yayumkinika kuhitimisha kwamba kama kuna mwanasiasa wa upinzani ambaye amekuwa ‘mwiba mchungu’ kwa serikali ya Rais John Magufuli basi si mwingine bali Lissu.

Na pengine kinachoongeza uzito kwenye dhana hii ni ukweli kwamba Agosti 18 mwaka huu, Lissu aliwaeleza wananchi kwamba anafuatiliwa.

Namnukuu "Naomba kabla sijaanza Mazungumzo yangu nimuombe Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa anaitwa Kipilimba au Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro, wale vijana ambao wamewatuma na kwa wiki tatu mfululizo wananifuata kila nilipo wanaotembea na gari ya Toyota premio namba T460CQV, jana niliwakaba Kanisani St. Peter's.”

Kwa upande mwingine serikali ya Magufuli ni kama ilikuwa inatafuta ‘kulaumiwa bure.’ Kwa sababu, Hadi muda huu hakuna sababu moja ya msingi kwa serikali hiyo kuyafanya maisha ya wanasiasa wa upinzani yawe magumu kiasi hiki. Magumu kwa maana ya kuwanyima kila aina ya fursa ya kufanya siasa (political space).

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, zaidi ya viongozi na wafuasi 400 wa Chadema wameshakamatwa tangu Magufuli aingie madarakani. Mtu atayedai kuwa kiongozi huyo ‘anawachukia wapinzani’ hatoonekana mtu wa ajabu japo huenda akatupwa jela.

Katika hotuba zake mbalimbali, Rais Magufuli ameshindwa kuficha hisia zake dhidi ya upinzani na wapinzani. Juni 12 mwaka huu, Rais Magufuli alimweleza Spika Job Ndugai maneno yafuatayo

“Tumia mbinu hiyohiyo ya kuwafanya wasiropokee Bungeni, waropokee nje na kule tutadili nao vizuri kwasababu wanapokua kule ndani wana kinga wanaweza wakatukana chochote, sasa kinga wanayoitumia vibaya bungeni kainyooshe wewe. Wawe wanatoka kule bungeni, ukishamfukuza hata mwezi mzima… atakuja aropokee huku, na mimi nakueleza waache waropokee huku nitadili nao, wala siwatishi lakini hatuwezi kuwa kwenye vita wewe unaanza kugeuka kupiga wale wanaokwenda mbele…. ni nafuu unyamaze ukalale.”

Kwa kuangalia jinsi watendaji wa serikali ngazi za mkoa na wilaya wanavyochuana na polisi kuwanyanyasa wapinzani, hususan wa Chadema, dhana kuwa serikali ina mkono katika jaribio la mauaji ya Lissu ni kama ‘ready-made.’

Hata hivyo, pamoja na ‘dalili zote’ kuashiria uwezekano wa mkono wa serikali katika jaribio la kumuua Lissu, dhana hii inakosa mantiki kiuhalisia. Ni kwamba hakuna tija kwa serikali kumuua Lissu. Sawa, sio siri kuwa uhusiano kati ya serikali na Lissu/ wapinzani sio mzuri, lakini haitokuwa na tija yoyote kwa serikali ya Magufuli kumuua Lissu.

Na hata kama ingekuwa lazima ‘aondoke,’ basi kuna ‘njia mwafaka zaidi’ za mauaji ya watu maarufu (assassination), huku 'kifo cha ajali' ikiwa maarufu na rahisi zaidi.

Halafu kinachotatiza katika tukio la jana, na kinachopunguza zaidi nguvu ya dhana kwamba ‘kuna mkono wa serikali,’ ni jinsi waliofanya shambulio hilo walivyoonekana kama wanahitaji publicity ya kutosha. Kwanini? Jibu lipo kwenye uchambuzi wa dhana ya tatu.

Dhana ya pili ni dhaifu kuliko nyingine mbili. Hii inahusisha mbio za urais mwaka 2020. Kwamba kila siku Lissu amekuwa akijitengenezea mazingira ya mgombea mwafaka wa Chadema/Upinzani katika uchaguzi mkuu ujao, wala halina mjadala. Sio kwamba Lissu amekuwa hodari katika masuala mbalimbali kwa vile anataka urais (hajawahi kutamka nia ya kugombea nafasi hiyo) lakini umahiri wake bungeni na katika masuala ya kisheria na kitaifa kwa ujumla, unamfanya kuwa kipenzi cha takriban kila mfuasi wa Chadema.

Dhana hii dhaifu inasema kuwa jaribio hilo la mauaji ni kazi ya wapinzani wa kisiasa wa Lissu, hususan ndani ya chama chake.

Udhaifu wa dhana hii ni kwamba, kama ambavyo kwenye dhana ya kwanza, hakuna tija katika kumdhuru Lissu hadharani. Kwamba hata kama kungekuwa na lundo la wapinzani wa kisiasa wa Lissu huko kwenye chama chake, kwanini wafanye ‘operesheni’ hiyo waziwazi badala ya kuandaa mkakati wa siri?

Na kama ilivyokuwa kwenye dhana ya kwanza, hata kama wapinzani wa kisiasa wa Lissu ndani ya chama chake wangekuwa wahusika, kwanini basi tukio hilo lifanyike katika mazingira ya ‘kusaka publicity kwa nguvu’?

Hiyo inatuacha na dhana moja, ya tatu, na ya mwisho. Ya mwisho lakini sio haba katika mantiki. Dhana hii inaeleza kwamba jaribio hilo la mauaji limefanywa makusudi na kile wajuzi wa mambo wanaita ‘rogue elements.’ Hizi zilitusumbua sana katika utawala wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete. Rogue elements hizi zinajumuisha watumishi halali wa vyombo vya dola wanaofanya shughuli zisizo halali. Nani anawatuma? Hiyo ni habari nyingine.

Kuna kitu kinachofahamika kama ‘Deep state.’ Kila nchi ina tafsiri yake kuhusu ‘deep state’ lakini tafsiri nyepesi kwa mazingira yetu ni ushirika wa watu wenye nguvu katika serikali na jamii – mfano vigogo (hususan wa zamani) wa vyombo vya dola, wafanyabiashara wenye uwezo mkubwa na wanasiasa kutoka upande wowote ule, lakini zaidi chama kilichopo madarakani.

Dhana hii inaliona tukio la kujaribu kumuua Lissu kama njia rahisi ya kuichafua serikali ya Rais Magufuli, ambayo kwa bahati mbaya/makusudi ilishajitengenezea mazingira ya kulaumiwa pindi la kutokea likimtokea mwanasiasa wa upinzani kama Lissu. Rais anaposhindwa kudhibiti ‘chuki zake’ dhidi ya wapinzani, anawapa nafasi nzuri ‘wabaya wake’ kutenda kitu kisha ikawa rahisi tu lawama kuelekezwa kwake.

Ndio maana dhana ya kwanza – kwamba kuna mkono wa serikali ya Magufuli kwenye jaribio la kumuua Lissu – inaonekana kama yenye uzito kwa vile "kuna sababu ready-made.”

Dhana hii inapata uzito kutokana na ukweli kwamba Magufuli amejitengenezea maadui wengi, wenye nguvu, na baadhi yao wakiwa viumbe hatari. Kuna watu waliozowea kuishi maisha ya kifalme ambao sasa wanalazimishwa kuishi maisha ya kawaida. Hawa watu wakipata upenyo wa kumdhuru Magufuli, hawatosita kufanya hivyo.

Lakini kwa vile ni ‘vigumu mno’ (angalau kwa wakati huu) kufanikisha jaribio la kumdhuru kiongozi huyo, njia nyepesi inaweza kuwa katika ‘kuua character yake,’ ambayo bahati nzuri kwa ‘wabaya wake,’ sio nzuri sana.

Kumekuwa na malalamiko kadhaa hasa kutoka upande wa upinzani kumtuhumu Magufuli kuwa ni dikteta. Na ukifuatilia mwenendo wa siasa zetu kwa muda huu, sio siri kwamba kuna chembe chembe za udikteta. Kwahiyo, ni rahisi kwa ‘wabaya wa Magufuli’ kutumia mwanya huo kujenga picha ya “serikali ya dikteta yamuua mpinzani wake mkubwa.”

Na hilo linatuleta kwenye suala la publicity. Kwamba jaribio la mauaji hayo liwe na mwangwi wa kutosha ndani na nje ya Tanzania. Mwangwi huo ni wa makusudi ili uakisi taswira inayojengeka kuwa ‘Magufuli ni dikteta. Na madikteta hunyanyasa wapinzani wao, na ikibidi hata kuwaua.’

Kwahiyo, kama kuna funzo kubwa kwa Magufuli katika tukio hili ni kuepuka mazingira yaliyopo ya uhasama mkubwa dhidi ya upinzani hususan Chadema. Kiongozi huyo anatambua fika kwamba kuna watu wapo radhi kufanya lolote lile kumng’oa, na kwa vile ‘njia za kawaida’ sio rahisi, basi inakuwa ‘anything goes,’ liwalo na liwe.

Na dhana hii ya tatu inaleta uhusiano kati ya tukio la jana la jaribio la kumuua Lissu na lile la hivi karibuni la kuchomwa moto kwa ofisi za kampuni ya uwakili wa IMMA. Kama hili la Lissu, tukio la moto nalo lilifanyika katika mazingira ya kuvutia publicity, yaani kama kulikuwa na jitihada za makusudi za kuushawishi umma kwamba “mnaona huyu dikteta Magufuli anakoelekea? Sasa anachoma hadi ofisi wa ‘wabaya’ wake.”

Nihitimishe uchambuzi huu kwa kueleza bayana masuala mawili matatu. Kwanza, lengo la uchambuzi huu mfupi sio kuingilia kazi za vyombo vya dola vinavyoendelea na uchunguzi kuhusu jaribio la kumuua Lissu. Nimefanya uchambuzi huu kama mtu mwenye uelewa wa masuala ya intelijensia na siasa za Tanzania yetu, ikiwa ni pamoja na “yanayojiri nyuma ya pazia.”

Pili, lengo la uchambuzi huu sio kumshawishi mtu yeyote abadili mtazamo wake kuhusu “nani ana/wanahusika.”

Mwisho, kama nilivyotanabaisha awali, tasnia ya intelijensia sio sayansi kamilifu kwa asilimia 100 (intelligence is not an exact science). Kwa maana hiyo, japo uchambuzi huu ni karibu kabisa na hali halisi, sio rahisi sana kufikia hali halisi yenye uhakika wa asilimia 100.

Nimalizie kwa kumtakia afya njema Bwana Lissu huku nikiamini kuwa malaka husika zitafanya kila jitihada kuwanasa wahusika, sio tu kwa minajili ya serikali kujinasua bali ili Bwana Lissu atendewe haki.

Nimependa namna ulivyochambua,kama tungekuwa na wachambuzi kumi wa aina yako hakika jibu lingekuwa karibu na kupatikana.
 
Mtanganyika kuna kitu hujaweka sawa na inaweza kuwa pia namna ya jambo hili lilivyopangwa na kufanyika. Pamoja na Jinsi alivyo Rais Maghufuli hawezi tuma watu wakavamie sijui clouds, sijui kurusha bomu kwa shehe, IMMA advocate, sijui saa nane, it doesn't make sense at all vyovyote utakavyofikiria. ila kama ulivyosema kutokana na yeye kuuchukia upinzani na criticism kuna kikundi probably cha dola kikijipa kazi zisizo rasmi na kupata directives not in the formal ways kutoka kwa a senior figure kwa malengo ya kusaidia system aliyopo bila ridhaa na hata kujali hicho akifanyacho kinafaida au hasara kwa serikali. Its also very likely kwamba vyombo vya dola wanapofanya uchungunzi mwisho wa siku hukwama maana mwisho wa siku wanajikuta wanawachunguza jamaa zao (kizungumkuti ). Refer issue ya Roma, Ben saa8.,clouds, nape
 
Nimesema humu sana,si rahisi serikali ifanye shambulio la kuvuta attention namna hii 'shambulio la kelele 'na wakati Lissu ameshakuwa mikononi mwa polisi mara kibao si wangeweza hata kumpa sumu ya kummaliza taratibu kama walitaka kumuua.
Akili ndogo kukuelewa ni kazi sana.
 
Operation haiwezi fanyika bila maagizo toka juu mzee.....let that sink in!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchambuzi nimzuri lakini serikali kwann haitaki kutoa information kuhusu T460CVQ.....na kama wangekua maadui wa serikali,trust me serikali wangewasaka hao watu kwa udi na uvumba.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*Evarist Chahali* anaandika:

Jana, Septemba 07, 2017, majira ya mchana, zilipatikana taarifa kwamba Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Singida Mashariki, Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani, na Rais wa Chama cha Wanasheria (TLS), amepigwa risasi kadhaa na kujeruhiwa vibaya.

Tukio hilo la kutisha lilitokea jijini Dodoma, wakati Mbunge huyo aliposhuka nyumbani kwake eneo la Area D, inakoelezwa alienda kwa ajili ya kujipatia mlo wa mchana.

Kabla ya kuingia kiundani kwenye makala hii, nitumie fursa hii kutoa salamu za pole kwa Lissu, na kumwombea apone haraka. Salamu za pole pia kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema, chama ambacho Lissu amekuwa akikiwakilisha kwa ufanisi mkubwa.

Pia ni vema nitahadharishe mapema kwamba intelijensia sio sayansi timilifu kwa asilimia 100, kwa kimombo wanasema “intelligence is not an exact science.”

Okey, sasa tuingie mtamboni. Hadi muda huu kuna dhana za msingi tatu ambazo zinatokana na‘mchujo’ wa dhana mbalimbali.

Dhana ya kwanza na ambayo pengine ni maarufu zaidi ya zote ni kwamba jaribio hilo la mauaji ya Lissu lina mkono wa dola. Kwamba sio siri kuwa Lissu amekuwa ‘akiisumbua mno’ serikali, ambapo wafuasi wake wanamwona kama jasiri asiye na uoga wa kusema ukweli, ilhali wapinzani wake wakimwona kama mchochezi.

Yayumkinika kuhitimisha kwamba kama kuna mwanasiasa wa upinzani ambaye amekuwa ‘mwiba mchungu’ kwa serikali ya Rais John Magufuli basi si mwingine bali Lissu.

Na pengine kinachoongeza uzito kwenye dhana hii ni ukweli kwamba Agosti 18 mwaka huu, Lissu aliwaeleza wananchi kwamba anafuatiliwa.

Namnukuu "Naomba kabla sijaanza Mazungumzo yangu nimuombe Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa anaitwa Kipilimba au Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro, wale vijana ambao wamewatuma na kwa wiki tatu mfululizo wananifuata kila nilipo wanaotembea na gari ya Toyota premio namba T460CQV, jana niliwakaba Kanisani St. Peter's.”

Kwa upande mwingine serikali ya Magufuli ni kama ilikuwa inatafuta ‘kulaumiwa bure.’ Kwa sababu, Hadi muda huu hakuna sababu moja ya msingi kwa serikali hiyo kuyafanya maisha ya wanasiasa wa upinzani yawe magumu kiasi hiki. Magumu kwa maana ya kuwanyima kila aina ya fursa ya kufanya siasa (political space).

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, zaidi ya viongozi na wafuasi 400 wa Chadema wameshakamatwa tangu Magufuli aingie madarakani. Mtu atayedai kuwa kiongozi huyo ‘anawachukia wapinzani’ hatoonekana mtu wa ajabu japo huenda akatupwa jela.

Katika hotuba zake mbalimbali, Rais Magufuli ameshindwa kuficha hisia zake dhidi ya upinzani na wapinzani. Juni 12 mwaka huu, Rais Magufuli alimweleza Spika Job Ndugai maneno yafuatayo

“Tumia mbinu hiyohiyo ya kuwafanya wasiropokee Bungeni, waropokee nje na kule tutadili nao vizuri kwasababu wanapokua kule ndani wana kinga wanaweza wakatukana chochote, sasa kinga wanayoitumia vibaya bungeni kainyooshe wewe. Wawe wanatoka kule bungeni, ukishamfukuza hata mwezi mzima… atakuja aropokee huku, na mimi nakueleza waache waropokee huku nitadili nao, wala siwatishi lakini hatuwezi kuwa kwenye vita wewe unaanza kugeuka kupiga wale wanaokwenda mbele…. ni nafuu unyamaze ukalale.”

Kwa kuangalia jinsi watendaji wa serikali ngazi za mkoa na wilaya wanavyochuana na polisi kuwanyanyasa wapinzani, hususan wa Chadema, dhana kuwa serikali ina mkono katika jaribio la mauaji ya Lissu ni kama ‘ready-made.’

Hata hivyo, pamoja na ‘dalili zote’ kuashiria uwezekano wa mkono wa serikali katika jaribio la kumuua Lissu, dhana hii inakosa mantiki kiuhalisia. Ni kwamba hakuna tija kwa serikali kumuua Lissu. Sawa, sio siri kuwa uhusiano kati ya serikali na Lissu/ wapinzani sio mzuri, lakini haitokuwa na tija yoyote kwa serikali ya Magufuli kumuua Lissu.

Na hata kama ingekuwa lazima ‘aondoke,’ basi kuna ‘njia mwafaka zaidi’ za mauaji ya watu maarufu (assassination), huku 'kifo cha ajali' ikiwa maarufu na rahisi zaidi.

Halafu kinachotatiza katika tukio la jana, na kinachopunguza zaidi nguvu ya dhana kwamba ‘kuna mkono wa serikali,’ ni jinsi waliofanya shambulio hilo walivyoonekana kama wanahitaji publicity ya kutosha. Kwanini? Jibu lipo kwenye uchambuzi wa dhana ya tatu.

Dhana ya pili ni dhaifu kuliko nyingine mbili. Hii inahusisha mbio za urais mwaka 2020. Kwamba kila siku Lissu amekuwa akijitengenezea mazingira ya mgombea mwafaka wa Chadema/Upinzani katika uchaguzi mkuu ujao, wala halina mjadala. Sio kwamba Lissu amekuwa hodari katika masuala mbalimbali kwa vile anataka urais (hajawahi kutamka nia ya kugombea nafasi hiyo) lakini umahiri wake bungeni na katika masuala ya kisheria na kitaifa kwa ujumla, unamfanya kuwa kipenzi cha takriban kila mfuasi wa Chadema.

Dhana hii dhaifu inasema kuwa jaribio hilo la mauaji ni kazi ya wapinzani wa kisiasa wa Lissu, hususan ndani ya chama chake.

Udhaifu wa dhana hii ni kwamba, kama ambavyo kwenye dhana ya kwanza, hakuna tija katika kumdhuru Lissu hadharani. Kwamba hata kama kungekuwa na lundo la wapinzani wa kisiasa wa Lissu huko kwenye chama chake, kwanini wafanye ‘operesheni’ hiyo waziwazi badala ya kuandaa mkakati wa siri?

Na kama ilivyokuwa kwenye dhana ya kwanza, hata kama wapinzani wa kisiasa wa Lissu ndani ya chama chake wangekuwa wahusika, kwanini basi tukio hilo lifanyike katika mazingira ya ‘kusaka publicity kwa nguvu’?

Hiyo inatuacha na dhana moja, ya tatu, na ya mwisho. Ya mwisho lakini sio haba katika mantiki. Dhana hii inaeleza kwamba jaribio hilo la mauaji limefanywa makusudi na kile wajuzi wa mambo wanaita ‘rogue elements.’ Hizi zilitusumbua sana katika utawala wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete. Rogue elements hizi zinajumuisha watumishi halali wa vyombo vya dola wanaofanya shughuli zisizo halali. Nani anawatuma? Hiyo ni habari nyingine.

Kuna kitu kinachofahamika kama ‘Deep state.’ Kila nchi ina tafsiri yake kuhusu ‘deep state’ lakini tafsiri nyepesi kwa mazingira yetu ni ushirika wa watu wenye nguvu katika serikali na jamii – mfano vigogo (hususan wa zamani) wa vyombo vya dola, wafanyabiashara wenye uwezo mkubwa na wanasiasa kutoka upande wowote ule, lakini zaidi chama kilichopo madarakani.

Dhana hii inaliona tukio la kujaribu kumuua Lissu kama njia rahisi ya kuichafua serikali ya Rais Magufuli, ambayo kwa bahati mbaya/makusudi ilishajitengenezea mazingira ya kulaumiwa pindi la kutokea likimtokea mwanasiasa wa upinzani kama Lissu. Rais anaposhindwa kudhibiti ‘chuki zake’ dhidi ya wapinzani, anawapa nafasi nzuri ‘wabaya wake’ kutenda kitu kisha ikawa rahisi tu lawama kuelekezwa kwake.

Ndio maana dhana ya kwanza – kwamba kuna mkono wa serikali ya Magufuli kwenye jaribio la kumuua Lissu – inaonekana kama yenye uzito kwa vile "kuna sababu ready-made.”

Dhana hii inapata uzito kutokana na ukweli kwamba Magufuli amejitengenezea maadui wengi, wenye nguvu, na baadhi yao wakiwa viumbe hatari. Kuna watu waliozowea kuishi maisha ya kifalme ambao sasa wanalazimishwa kuishi maisha ya kawaida. Hawa watu wakipata upenyo wa kumdhuru Magufuli, hawatosita kufanya hivyo.

Lakini kwa vile ni ‘vigumu mno’ (angalau kwa wakati huu) kufanikisha jaribio la kumdhuru kiongozi huyo, njia nyepesi inaweza kuwa katika ‘kuua character yake,’ ambayo bahati nzuri kwa ‘wabaya wake,’ sio nzuri sana.

Kumekuwa na malalamiko kadhaa hasa kutoka upande wa upinzani kumtuhumu Magufuli kuwa ni dikteta. Na ukifuatilia mwenendo wa siasa zetu kwa muda huu, sio siri kwamba kuna chembe chembe za udikteta. Kwahiyo, ni rahisi kwa ‘wabaya wa Magufuli’ kutumia mwanya huo kujenga picha ya “serikali ya dikteta yamuua mpinzani wake mkubwa.”

Na hilo linatuleta kwenye suala la publicity. Kwamba jaribio la mauaji hayo liwe na mwangwi wa kutosha ndani na nje ya Tanzania. Mwangwi huo ni wa makusudi ili uakisi taswira inayojengeka kuwa ‘Magufuli ni dikteta. Na madikteta hunyanyasa wapinzani wao, na ikibidi hata kuwaua.’

Kwahiyo, kama kuna funzo kubwa kwa Magufuli katika tukio hili ni kuepuka mazingira yaliyopo ya uhasama mkubwa dhidi ya upinzani hususan Chadema. Kiongozi huyo anatambua fika kwamba kuna watu wapo radhi kufanya lolote lile kumng’oa, na kwa vile ‘njia za kawaida’ sio rahisi, basi inakuwa ‘anything goes,’ liwalo na liwe.

Na dhana hii ya tatu inaleta uhusiano kati ya tukio la jana la jaribio la kumuua Lissu na lile la hivi karibuni la kuchomwa moto kwa ofisi za kampuni ya uwakili wa IMMA. Kama hili la Lissu, tukio la moto nalo lilifanyika katika mazingira ya kuvutia publicity, yaani kama kulikuwa na jitihada za makusudi za kuushawishi umma kwamba “mnaona huyu dikteta Magufuli anakoelekea? Sasa anachoma hadi ofisi wa ‘wabaya’ wake.”

Nihitimishe uchambuzi huu kwa kueleza bayana masuala mawili matatu. Kwanza, lengo la uchambuzi huu mfupi sio kuingilia kazi za vyombo vya dola vinavyoendelea na uchunguzi kuhusu jaribio la kumuua Lissu. Nimefanya uchambuzi huu kama mtu mwenye uelewa wa masuala ya intelijensia na siasa za Tanzania yetu, ikiwa ni pamoja na “yanayojiri nyuma ya pazia.”

Pili, lengo la uchambuzi huu sio kumshawishi mtu yeyote abadili mtazamo wake kuhusu “nani ana/wanahusika.”

Mwisho, kama nilivyotanabaisha awali, tasnia ya intelijensia sio sayansi kamilifu kwa asilimia 100 (intelligence is not an exact science). Kwa maana hiyo, japo uchambuzi huu ni karibu kabisa na hali halisi, sio rahisi sana kufikia hali halisi yenye uhakika wa asilimia 100.

Nimalizie kwa kumtakia afya njema Bwana Lissu huku nikiamini kuwa malaka husika zitafanya kila jitihada kuwanasa wahusika, sio tu kwa minajili ya serikali kujinasua bali ili Bwana Lissu atendewe haki.
Usijekuwa ni swahiba unajaribu kumtetea swahiba wako.Mbaya wa umma wa watanzania sote tunamjua ,ni yule anayedanganya umma kwamba ni mtetezi wa wanyonge kumbe ni katili kuliko ubaya wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Exactly what was in my mind isipokuwa dhana ya 'deep state' ambayo kwakweli sikuiwaza kabisa ila nafikiri nayo ina mashiko ya kutosha!
Naungana na wewe Bw. Chahali na asante sana kwa uzi fikirishi
 
Nimesema humu sana,si rahisi serikali ifanye shambulio la kuvuta attention namna hii 'shambulio la kelele 'na wakati Lissu ameshakuwa mikononi mwa polisi mara kibao si wangeweza hata kumpa sumu ya kummaliza taratibu kama walitaka kumuua.
Mkuu,ni rahisi kufikiri hivi kama tu utaruhusu akili yako kufanya uchambuzi wa mambo bila 'ushabiki wa kisiasa'.mara zote ushabiki una tabia ya kufunga macho ya busara na hivyo shabiki atasema tu kile kinachoshibisha njaa ya ushabiki wake
 
Back
Top Bottom